Sunday, 14 February 2016

Re: [wanabidii]

Lokomai umeizoa wapi hii?? Nadhani ni darasa tosha. Kumbe ndivyo mambo yalivyo?? Hivi walipo hawana mahakama ya kwenda kumbe?? Ya nini kumtaka kumuhangaisha rais wetu wa JMT? Yeye ana haki kumbe kusema atafanya kazi ya kulinda amani mtu asifanye chokochoko. Pia ataiheshimu katiba yao ambayo haiiheshimu kaTIBA YA JAMHURI? Hii hatari. nadhani wakivuka hapa wakiwa na macho yote mawili mawili wakakuwa na akili. Wakipata ushauri watauheshimu.
Dawa waende mahakamani yashindikane washiriki uchaguzi unaotekelezwa kwa mujibu wa Katiba ya Maalim na Karume.
--------------------------------------------
On Sun, 2/14/16, 'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii]
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, February 14, 2016, 7:04 AM

Unafiki na
undumila kuwili kwa sasa umewaumbua. Mlificha magonjwa kwa
unafiki na sasa kifo cha serikali ya umoja wa kitaifa
kinawaumbua.



Mlimtumia Abubakar Khamis Bakary Mwakilishi wa Jimbo la
Mgogoni
kuwasilisha hoja binafsi kulitaka Baraza la Wawakilishi
kufanya
mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu kuanzishwa kwa Mfumo wa
Serikali ya
Umoja wa Kitaifa Zanzibar lakini katika mlengo wa kutaka
kujitenga na
Tanzania Bara. Hoja hiyo, ilikubaliwa na Baraza la
Wawakilishi na
kupelekea kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni Nam 6, 2010.



Mliamua kujifungia kwenye vyumba vya siri bila
kuwashirikisha wananchi
wa Tanzania Bara na mkafikia makubaliano ya kinafiki ya
kubadilisha
katiba yenu kwenye Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza ambayo
kwa sasa
inasema, Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na
nguvu za
kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80
ikiwa sheria
yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo
itayokuwa na
nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho

kinahitilafiana.



Mbaya zaidi, kwa kupitia katiba yenu ya kinafiki
mkatuaminisha kinafiki
kuwa Tume ya Uchaguzi kwa sasa ni huru na inayojitegemea
katika
kutekeleza majukumu yake kupitia Kifungu cha 119 (13) kwa
sababu ina
wajumbe WANNE waliopendekezwa na vyama vya CUF na CCM.
Mjumbe MMOJA
aliyependekezwa na Rais. Jaji MMOJA aliyependekezwa na
Mahakama Kuu na
pia Mwenyekiti aliyeteuliwa na Rais kwa kadri anavyoona
inafaa.



Mkasema wazi katika kifungu cha 119(13) kuwa: "Hakuna
Mahakama yoyote
itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote
lililotendwa na Tume
ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa
masharti ya
Katiba".



Hamkuishia hapo, mkatuambia kupitia Kifungu cha 119(4), kuwa
pindi
Mjumbe wa Tume anapoteuliwa, hakuna mtu/kiongozi mwenye
mamlaka ya
kumuondoa au kumfukuza Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi mpaka
atakapotimiza
miaka mitano tokea kuteuliwa kama Mjumbe wa Tume ya
Uchaguzi.



Tume ya Uchaguzi mkaifanya kama Jini ndani ya chupa, kwa
sasa limetoka
na hamuwezi kulirudisha ndani ya chupa! Mmebaki kulaumiana
kuhusu nani
aliyelitoa jini kwenye chupa!



Mkatuambia mmechoka kufanyiwa maamuzi na watu wa Tanganyika
na kuanzia
sasa vyenu ni vyenu wakati wa raha lakini wakati wa shinda,
vyenu ni
vyetu. Tuliwaambia haiwezekani vyenu viwe ni vyenu pekee
wakati wa raha
lakini wakati wa shida, vyenu viwe vyetu.



Mkasema Watanzania Bara wanachochea mtengane lakini kwa sasa
mmeamua
kushikamana. Tuliwaambia hiyo ndoa yenu haitadumu lakini
mkabisha.
Yamefika wapi?



Unafiki na undumila kuwili kwa sasa unawatafuna!



Maji mliyavulia nguo mkiwa mmejifungia ndani ya chumba cha
siri, hamna budi vile vile kuyaoga.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment