Nakuomba sana Happy Katabazi jitahidi kupitia maandishi yako kabla hujayatuma katika sehemu husika! Wewe ni mwandishi wa habari wa siku nyingi, hivyo ninategemea maadishi yako yafuate lugha sahihi ya Kiswahili hata Kiingereza au lugha yoyote ile unayotumia kutoa ujumbe! Nakushukuru sana kwa ushauri ulioutoa katika maada yako ingawa lugha unayoandika si sahihi!! Kazi njema
On 19 Feb 2016 19:35, "'Sylvanus Kessy' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
-- --Mama KatabaziHebu fafanua unaposema Waziri mkuu ... aliyejidhuru una maana gani. Wewe ni mwanahabari liyebobea wa miaka 16. Tafadhali ujieleze!silvanus
From: Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
To: WANA BIDII <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, February 19, 2016 7:23 PM
Subject: Re: [wanabidii] TUMUAMINI WAZIRI UMMY AU DC TEMEKE KUHUSU KIPINDUPINDU?
Ukumbatiaji tabia za uchafu ni janga kubwa. Hawa watu wanaugua kipindu pindu kila mara. Serikali ishajua tuwavivu kwa kila kitu miaka nenda rudi.Tulazimishwe usafi tu--On Feb 17, 2016 02:08, "'Happiness Katabazi' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:--TUMUAMINI WAZIRI UMMY AU DC TEMEKE KUHUSU KIPINDUPINDU?Na Happiness KatabaziFEBRUALI 15 Mwaka huu, Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu alitoa taarifa ya Wizara hiyo kwa vyombo Vya Habari na vyombo Vya Habari Vya Jana vilimnukuu Akizungumzia mambo mbalimbali ya kiafya ngazi ya Kitaifa ikiwemo Ugonjwa wa Kipindupindu umeibuka upya Dar es Salaam na kwamba tayari wagonjwa sita wakipindupindu wamepatikana katika Wilaya ya Temeke.Februali 16 Mwaka huu, kupitia Televisheni ya ITV, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema alinukuliwa na Televisheni hiyo akikanusha Kuwa Katika Wilaya yake anayoingoza ya Temeke Hakuna mgonjwa aliyethibitika kuugua ugonjwa wa Kipindupindu.Kwa mgongano huo wa matamko ya viongozi hao Wawili wa serikali mmoja ambaye ni Waziri(Ummy Mwalimu) na kiongozi mwingine wa serikali ngazi ya Wilaya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke(Mjema).Watanzania ambao tumefuatilia Habari hii tumebaki na maswali yasiyo na majibu Kwa maana sisi wananchi tumuamini tamko la nani baina ya viongozi ha Wawili wa serikali?Tunaofikiri sawa sawa Hatuwezi Kusema taarifa ya Wizara kupitia waziri wake Ummy ni ya uongo au ni la kweli au Kanusho la Mkuu wa Wilaya ya Temeke ni la uongo au ni la kweli hadi pale mamlaka nyingine au Wizara hiyo hiyo au Mkuu Huyo wa Wilaya mmoja aseme taarifa yake ni ya kweli kwa vielelezo hivi na mwingine akiri amekosea kwa kutoa taarifa tamko lake la Kipindupindu kipo au akipo ni kweli.Nimepata Mashaka ya kwanini Wizara ya Afya na Wilaya ya Temeke ambazo zote ni Ofisi za umma zitoe taarifa Moja ambayo zinapingana tena hadharani? Je Katika hili Hakuna Utendaji wa pamoja ?Kama Wizara ya Afya ilisema imebaini Kipindupindu Kimeibuka upya Wilaya ya Temeke kwanini Kabla ya saa 24 Mkuu wa Wilaya ya Temeke akanushe taarifa hizo za Wizara?Kuna nini hapa ?Je Waziri Ummy amepotoka kama alivyopotoka Naibu waziri wake Dk.Kigwangala kipindi kile alipovamia Hospitali ya Dk.Mwaka na kumsema hadharani Kuwa Dk.Mwaka Si Daktari, Hana vibali Vya kujitangaza wakati si kweli na ukweli kwamba Dk.Mwaka ni mtabibu anayetambulika na serikali na serikali hiyo hiyo ndiyo iliyompa vibari Vya kuendesha vipindi vyake Vya kitabibu Katika Redio na Televisheni?Au Mkuu wa Wilaya Mjema naye amepotoka na anaficha ukweli Kuwa Kipindupindu Kuwa hakipo Kwenye Wilaya yake ya Temeke wakati ukweli Kipundupindu kipo Katika Wilaya yake?Lakini naye Mkuu wa Wilaya Mjema ni kwanini jana akuona ni busara kwenda Wizarani ya Afya Moja kuomba kuonana na Waziri Ummy kumweleza Ana kwa Ana au kwa maandishi Kuwa taarifa iliyotolewa Juzi na Wizara ya Afya Kuwa kuna Kipindupindu Katika Wilaya yake siyo kweli na kwamba ukweli ni kwamba hakuna wagonjwa wa Kipindupindu Temeke hadi naye Akaamua kutoa taarifa za kukanusha taarifa za Wizara kuwepo wagonjwa wa Kipindupindu Temeke wenye vyombo Vya Habari Hali ambayo imesababisha wananchi wanashindwa Kushika lipi na kuacha lipi?Mi ni mtu wa Kuvuta subira ,naamini ni suala la muda tu ukweli utabainika na tutafahamu Kati ya Taarifa ya Wizara ya Afya iliyotolewa na Waziri Ummy na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke kuwa Hakuna Kipindupindu ipi ni ya ukweli na ipi ni ya uongo.Nawaasa baadhi ya wanasiasa mliobahatika kupata nafasi za Uongozi Katika serikali ya awamu ya tano, punguzeni tabia ya Kupenda kuonekana onekana kila kukicha Kwenye vyombo Vya Habari mkifikiri Kuwa kuonekana kila kukicha Kwenye vyombo Vya Habari mkitoa matamko ,makalipio kama Manyapara ndiyo Jamii itawaona mnafanya kazi Sanaaa.Baadhi yenu acheni tabia ya kwenda kuwaondoa madarakani baadhi ya watendaji kwa Fedhea tena Mbele ya vyombo Vya Habari kwa taarifa tu za kusikia 'Hear say evidence'.Kuna watu ndani ya serikali tangu serikali zilizopita ni wachapakazi,waadilifu na saa 12 asubuhi wameishafika maofisini wanachapa kazi lakini hata siku Moja hawapendi hii tabia ya kwenda kuuza sura 'nyago' Kwenye vyombo Vya Habari kama baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa hivi sasa ambao nafikiri wanaamini bila sura zao kuonekana Kwenye Televisheni basi aliyewateua sijui atawahesabu hawafanyikazi .Hivi mlipoteuliwa kushika hizo nyadhifa Moja ya Kigezo mliambiwa ni lazima muwe mnaonekana Kwenye Televisheni kila kukicha?Naibu waziri Dk.Kigwangala Tulimshuhudia hivi karibuni akijigeuza 'Korokoroni' na suti yake akasimama nje ya geti la Wizara yake akiangalia wachelewaji wakati kazi hiyo siyo yake kabisa tena wakati akifanya Kituko hiki Tayari vyombo Vya Habari asubuhi Kabla ya saa mbili asubuhi vilikuwa vimefika pale vipi piga picha.Sifaa hizi za kijinga .Kipimo cha uchapaji kazi ,uadilifu serikali siyo kuuza sura kila siku Kwenye vyombo Vya Habari .Muuige mfano kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, Mkuu wa Jeshi la Polisi ,Ernest Mangu,Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Jaji Eliezer Feleshi.Viongozi Hao wa umma huwaoni wakibwata bwata ovyo Kwenye vyombo Vya Habari ,ila chini ya Uongozi wao kazi zinafanyika vizuri ,Kisomi na kiu weledi kimya kimya na watendaji wa Taasisi zinazoongozwa na viongozi Hao wafuateni muwaulize shuruba ya kazi bila kuzembea.Mimi ni mwanahabari kitaaluma wa zaidi ya Miaka 16 nimefanya kazi hiyo, nafahamu Kuwa mwisho wa wanasiasa wanaopenda kufanyakazi kwa kutumia Sana Vyombo Vya Habari kila wakati hata Katika mambo yasiyo ya Msingi na lazima mwisho wao uwa simwema.Kuna majukumu mengi yanafanywa na waziri ,kuna Ofisa Habari wa Wizara Si yupo anaweza kwenda Katika hiyo kazi akapiga picha,akaandika Habari akatuma Kwenye vyombo Vya Habari basi ujumbe ukafika tena bila kupotoshwa wakati mwingine.Hakuna urafiki wa kudumu baina ya waandishi wa Habari Wengi na wanasiasa .Sisi tulifanyakazi na wanasiasa tunalijua hili.Waziri Mkuu aliyejidhuru Edrward Lowassa,Rais Jakaya Kikwete ambao walikuwa ni wapenzi wa waandishi wa Habari mkiwafuata wanaweza kuwapa somo Zuri tu kuhusu waandishi wa Habari Na jinsi ya kudili na waandishi wa Habari wakati gani mdili nao na wakati gani msidili nao.Simaanishi msitoe taarifa kwa umma kupitia vyombo vya Habari toeni ila baadhi yenu punguzeni kidogo huo mchezo .Siwalazimishi mfuate ushauri wangu huo ila atakayeona unamfaa auchukue na aufanyie kazi.Baadhi yenu acheni tabia ya kwenda kuwaondoa madarakani baadhi ya watendaji kwa Fedhea tena Mbele ya vyombo Vya Habari kwa taarifa tu za kusikia 'Hear say evidence ambapo ikitokea siku watu Hao wakishitaki au serikali ikishitakiwa Hamuwezi Kuja mahakamani kutolea ushahidi huo ushahidi ambao mnadai mnao.Kwasababu siyo Siri hivi sasa baadhi ya watendaji wanafanyakazi kwa uwoga Kwani hawajui uenda wao ni Kesho watashughulikiwa .Aidha Sidhani kama ni busara kwa kiongozi wa ngazi ya labda Waziri Mkuu kupatiwa taarifa za tuhuma za ubadhirifu ,uzembe,ukwepaji kodi wa Ofisi Fulani wa serikali Kesho yake waziri Mkuu anafunga safari Moja kwa Moja NA Lundo la vyombo Vya Habari na maofisa wengine wa serikali hadi ofisini kwa Ofisa Huyo halafu waziri Mkuu anaanza kumwambia Huyo Ofisa eti anaushahidi unaonyesha amefanya uzembe,uzembe huo umesababisha Hasara ,Mara anataka Ofisa Huyo ifikapo jioni ameletee barua ya kujieleza tena Mbele ya vyombo Vya Habari.Jamani.Hivi kama kweli umepata taarifa hizo na wewe ni kiongozi wa juu serikalini kwanini uongozane na msafara hadi Katika Ofisi ya Ofisa Huyo ambaye ni Mdogo kwako kimadaraka muanze kutolea Kauli kama mnasutana wakati wote ni Viongozi wa serikali ?Minaona ingekuwa ni vyema Waziri Mkuu wetu akipata taarifa kama hizo kutoka kwa Vyanzo vyake ambavyo anaviamini sana kama kwamba ushahidi wa taarifa zile Tayari mmeishakubaliwa na Mahakama Kumbe bado, amuite Ofisa Huyo au aagize mamlaka zingine zimuite Ofisa Huyo zimweleze tuhuma zake na zimpe Haki zake za asili ikabainika kuna Haja ya kumsimamisha kazi msimamisheni au mfukuzeni huko ndani kwenu taarifa ije baadaye.Lakini hii tabia ya Waziri Mkuu Kudai ana taarifa za baadhi ya ubadhirifu ,ukwepaji kodi anaandaa ziara kwanza anaenda eneo la tukio nakuanza kumtunuku Ofisa Huyo hadharani sizani kama ni vyema maana kuna watumishi wengine wa serikali ni wavumilivu na wengine siyo wavumilivu .Enzi Edward Lowassa akiwa waziri Mkuu naye alikuwa anatumia aina hii kidogo kama waziri Mkuu Majaliwa ya kufika baadhi ya Wilaya anazikataa hotuba za viongozi wa serikali mkoa na Wilaya husika na kuwafokea na kutimua timua watu kazi adharani kitendo kilichotafsiriwa na watu Kuwa ni kuwavunjia heshima watumishi wenzake wa umma.Siku Moja Lowassa aliendeleza mchezo huo Katika ziara zake mikoani na alimfokea Mkuu mmoja wa Wilaya katika mkoa mmoja wa Kanda ya Ziwa ,Huyo Mkuu wa Wilaya alichomfanyia Lowassa na uwaziri Mkuu Mbele ya hadhara ile Habari ile iliandikwa Kwenye Gazeti la Tanzania Daima hatokaa akisahau hadi Leo na tabia hiyo ilikuwa ikiwakera baadhi ya watu.Sitetei uzembe,na vitendo vyote vinavyokwamisha maendeleo ya taifa letu ila watumishi wa umma siyo vyema kwenda kujifanya unafanyakazi ziara za kushitukiza Kumbe Tayari wewe una maamuzi yako kichwani unaenda Katika Ofisi za Ofisa Huyo kama formality ukirudi ofisini tu inatangaza kumsimamisha kazi kwanini usimsimamishe kazi bila kufanya hizo ziara mnazodai ni za kushtukiza ambazo Hazina sifa za Kuitwa ni ziara za kushitukiza ?Kesi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia,Profesa Costa Mahalu binafsi Nilimfuatilia mwanzo mwisho ndani na nje ya Mahakama.Ilinifunza mambo mengi sana.Kubwa Ilinifunza Kuwa ndani ya serikali kuna baadhi ya watu wana roho za kishetani Kabisa na ni mabingwa wa kuzushia wenzao uongo mzito na uongo huo unasababisha aliyezushiwa uongo kuondolewa Kazini yaani kusimamishwa kazi na kufunguliwa Kesi ya jinai Mahakamani na kusota sana na kuathirika kiuchumi yeye na familia yake na kudhalilika Mbele ya Jamii na kuonekana ni fisadi wa Fedha za umma.Lakini kwakuwa Mahakama zetu zinafuata Sheria ushahidi thabiti siyo majungu ,fitna ,Chuki ,uzushi Mahalu alishinda ile Kesi .Sasa Mimi pia napenda kushauri watendaji wa serikali hii waendelee kutimiza majukumu Yao kwa mujibu wa sheria,hakima busara na siyo mihemko.Muelewe Kuwa Hamuwezi kufurahisha watu wote, na watu wanamshangilia Leo Kesho ndiyo Hao Hao watakuwa wakwanza kuwaona hamfai na watasema hamjafanya lolote .Hao ndiyo baadhi ya Watanzania walivyo Huwa ni watu wasiyo tabirika na wingine ni Bendera Fuata upepo.Na wawe macho sana na taarifa za ubadhirifu dhidi ya watumishi wengine wa umma Kwani kupitia Kesi ya Mahalu nilijifunza Kuwa siyo kila taarifa ya ubadhirifu viongozi wa serikali mnazoletewa zina ukweli asilimia Mia Moja kwasababu kama hamtokuwa makini hizo taarifa mkaamua kujifanyiakazi mkazitumia kuwadhibu watumishi wenzenu ipo siku watu watumishi Hao watakimbilia mahakamani kupinga maamuzi yenu ya kuwasimamisha kazi,Kuwafukuza kazi.' Honey moon ' ya serikali ya Rais John Magufuli yaani siku Mia Moja imeisha shikamaneni fanyeni kazi kwa Haki ,maslahi ya taifa letu na sasa hivi tunaitaji kuona mkituonyesha Ubunifu wenu mpya maana kama timua timua tumeiyona makusanyo ya kodi yameongezeka Tumeyaona hongereni ,Mahakama imepatiwa hela Kabla ya Bunge la Bajeti kuwaidhinishia,Fedha kwa baadhi ya Hospitali zimetengwa.Nawatakia Afya njema Katika Utendaji kazi wenu kwa taifa hili.Na kila Mara maumbile kumuomba Mungu awaongoze Katika kazi Zenu, awape busara Hekima Katika Utendaji wenu.Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki AfrikaChanzo: Facebook: Happy Katabazi17/2/2016.
Sent from my iPad
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment