Friday, 19 February 2016

Re: [wanabidii] TUMUAMINI WAZIRI UMMY AU DC TEMEKE KUHUSU KIPINDUPINDU?

Happy Katabazi leo nakupongeza sana kwa andiko lako hili japo kuna makosa ya uchapaji (Typing errors) lakini ujumbe wako ni murua sana. Hata mimi nateswa sana na namna wafanyakazi wa Serikali wanavyodhalilishwa sana na watendaji wakuu wa Serikali kwa jinsi wanavyokuwa mistreated mbele ya umma bila kujali kuwa kuna sheria ya kazi na mahusiano kazini ambayo inatoa haki na wajibu kwa mwajiriwa na mwajiri. Utaratibu unaotumika na Serikali yangu hii ya sasa naona umejikita zaidi kumwajibisha mfanyakazi pasipo kufuata taratibu za kazi. Jana nimemwona Waziri mkuu anamhoji meneja/mkurugenzi (Whatever the case) wa bandari ya Tanga kama mtoto mdogo mbele ya hadhara. Sikatai kama kuna makosa ya ubadhilifu wa mali ya umma yanaweza kufanywa na watumishi mbalimbali wa Serikali lakini ni lazima utu wa mtu uthaminiwe kama takwa mojawapo la katiba ya nchi inavyotaka. Kwani kuna tatizo gani kama waziri Mkuu akifanya uchunguzi kwa kutumia mamlaka aliyonayo kupitia vyombo mbalimbali na kwa kufuata taratibu bila kumvunjia mtu heshima na mwisho akachukua hatua kwa kumwajibisha mhusika kwa utaratibu wa kisheria ikiwa imethibitika kweli mtu huyo katenda kosa? Ikumbukwe kwamba kuna kanuni ya kwamba kila mtu anachukuliwa kuwa hajatenda kosa mpaka hapo itakapothibitika vinginevyo : "the innocence principle as per our Constitution" Inakuwaje Waziri Mkuu alyeapa kuilinda katiba yetu amekuwa kinara wa kukiuka sana takwa hili la kikatiba? Kwa kweli utaratibu huu wa kuambush viongozi wengine wa Umma bila kuwapa nafasi ya kusikilizwa ipasavyo si mzuri na ni ishara mbaya kwa nchi inayotazamiwa kufuata utawala bora na utawala wa sheria (Good Governance and Rule of the Law). The Right to be heard, as one of the key indicators of the democratic Society that adheres to the Rule of Law, includes fair hearing, hear the other party. (haki ya kusikilizwa kama ishara mojawapo ya jamii ya kidemokrasia inayozingatia utawala wa sheria, inahusisha  usikilizwaji wa haki, yaani kusikiliza upande mwingine. Fair hearing haiwezi kuwepo ikiwa umemhukumu mtu kabla ya kumsikliza halafu ndo unamwambia aandike barua ya kujieleza ndani ya masaa mawili, 3, 4, 5, 6,7, au hata 24 , 16 , 48 whatever the case. Kuna mantiki gani kisheria na kibinadamu kumwambia mtumishi wa Serikali yako akuandikie barua ya kujieleza baada ya kumshambulia na kumdhalilisha mbele ya hadhara kwa kumtuhumu kuwa kaiba au kakosa? Je, barua atakayoandika ikiwa itakuwa na ukweli kuwa hakuiba na wala hakukosa wewe kama waziri mkuu utafanyaje wakati umeshamdhalilisha mbele ya umma? Ili aonekane mkosaji na ili heshima ya waziri Mkuu iendelee kuwepo machoni pa watu utasikia mtumishi huyo wa Umma katumbuliwa jipu, MISIFA HIYO. Wakati nasoma Tambaza High School miaka kadhaa iliyopita kuna jamaa mmoja tulimpa jina la MISIFA MAKILA KITU. yaani huyu akitaka sifa hasa kutoka kwa wasichana alijipa masifa kibao ikiwa na kjifanya anajua kila kitu. Tukambatiza MISIFA MAKILA KITU. Ndo nionavyo baadhi ya viongozi katika awamu hii. Huwezi kumuumbua kiongozi mwenzako hadharani kwa kumwuliza maswali ya ajabu ajabu mbele ya hadhara halafu umwambie aandike barua ya kujieleza na kesho unamfukuza kazi na kumpeleka mahakamani. Je, huoni kuwa mtu huyo hujamtendea haki kwa kumhukumubila kumsikiliza na baadaye unaweka dhana kwa mahakama kuwa mtu huyo ni mkosaji hasa kwa mahakama zetu hizi ambazo zimeambiwa zikiwatia watuhumiwa hatiani zitapewa bilioni 250? Sisemi lazima Mahakama ifuate kauli hizo za kisiasa ila nashawishika kuamini kuwa baadhi ya mahakimu na majaji ambao wanapatikana kwa mfumo huo huo wa kisiasa wanaweza wakaamua kumfurahisha au kuifurahisha mamalaka iliyowaweka madarakani  kwa kuamua kama utashi wa mamlaka hiyo inavyotaka na hivyo dhana ya uhuru wa mahakama ikapotea kiaina! Mwisho natamka wazi kuwa mimi ni mmojawapo wa wanachama hai na makini wa CCM ambaye siridhishwi na namna wafanyakazi wa serikali wanavyotendewa sasa kwa maana ya kutozingatiwa haki zao kwa mujibu wa Sheria ya kazi na mahusiano kazini na Katiba yetu. Wezi na watumia madaraka vibaya , mafisadi na wengineo kama hao wawajibishwe lakini iwe ni kwa kufuata Sheria za nchi na si kunyemereana wanakofanyiana sasa hivi. Kuna baadhi ya taasisi/watu kazi yao ni umbea. Bila umbea hawana kazi. Ni vizuri kuchuja kila neno litokalo kwa taasisi/au watu hao kwa makini sana dhidi ya watumishi wa serikali ili kuepuka kuhukumu hata wengine ambao hawakutenda makosa wanayotuhumiwa kwayo. Katika dunia hii ya leo iliyojaa hila na chuki kati ya binadamu na binadamu kwa wivu na tamaa za kila aina ni rahisi sana mtumishi wa serikali mwadilifu akatuhumiwa kwa mambo ambayo hata hakuyatenda. Ikiwa hatutakuwa makini serikali inaweza kukosa watumishi wema, waadilifu , wenye weledi mkubwa, taaluma na uzoefu uliotukuka katika maeneo ya kazi kwa mtindo huu wa timuatimua, fukuzafukuza na bomoabomoa kila mahali pa kazi katika jina la kutumbua majipu kwani hata hao wanaotumbua majipu nao pia wanatuhumiwa tuhuma mbalimbali, je nao wafukuzwe fukuzwe tu pasipo kuwapa nafasi ya kusikilizwa ipasavyo? Ni dhahiri kuwa jambo ambalo hupendi kufanyiwa nawe usilifanye kwa mwenzio/ wenzio- the reciprocity principle must be complied with!
Adios,
Ni mimi Leonard Elias Magwayega- Mbeya. 


On Friday, February 19, 2016 8:35 PM, 'Sylvanus Kessy' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Mama Katabazi 
Hebu fafanua unaposema Waziri mkuu ... aliyejidhuru una maana gani. Wewe ni mwanahabari liyebobea wa miaka 16. Tafadhali ujieleze! 
silvanus 



From: Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
To: WANA BIDII <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, February 19, 2016 7:23 PM
Subject: Re: [wanabidii] TUMUAMINI WAZIRI UMMY AU DC TEMEKE KUHUSU KIPINDUPINDU?

Ukumbatiaji tabia za uchafu ni janga kubwa. Hawa watu wanaugua kipindu pindu kila mara. Serikali ishajua tuwavivu kwa kila kitu miaka nenda rudi.
Tulazimishwe usafi tu
On Feb 17, 2016 02:08, "'Happiness Katabazi' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

TUMUAMINI WAZIRI UMMY AU DC TEMEKE KUHUSU KIPINDUPINDU? 

Na Happiness Katabazi

FEBRUALI 15 Mwaka huu,  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu alitoa taarifa ya Wizara hiyo kwa vyombo Vya Habari na vyombo Vya Habari Vya Jana vilimnukuu Akizungumzia mambo mbalimbali ya kiafya ngazi ya Kitaifa ikiwemo Ugonjwa wa Kipindupindu umeibuka upya Dar es Salaam na kwamba tayari wagonjwa sita wakipindupindu wamepatikana katika Wilaya ya Temeke.

Februali 16 Mwaka huu, kupitia Televisheni ya ITV, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema alinukuliwa na Televisheni hiyo akikanusha Kuwa Katika Wilaya yake anayoingoza ya Temeke Hakuna mgonjwa aliyethibitika kuugua ugonjwa wa Kipindupindu.

Kwa mgongano huo wa matamko ya viongozi hao Wawili wa serikali mmoja ambaye ni Waziri(Ummy Mwalimu) na kiongozi mwingine wa serikali ngazi ya Wilaya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke(Mjema).

Watanzania ambao tumefuatilia Habari hii tumebaki na maswali yasiyo na majibu Kwa maana sisi wananchi tumuamini tamko la nani baina ya viongozi ha Wawili wa serikali?

Tunaofikiri sawa sawa Hatuwezi Kusema taarifa ya Wizara kupitia waziri wake Ummy ni ya uongo au ni la kweli au Kanusho la Mkuu wa Wilaya ya Temeke ni la uongo au ni la kweli  hadi pale mamlaka nyingine au Wizara hiyo hiyo au Mkuu  Huyo wa Wilaya mmoja aseme taarifa yake ni ya kweli kwa vielelezo hivi na mwingine akiri amekosea kwa kutoa taarifa tamko lake la Kipindupindu kipo au akipo ni kweli.

Nimepata Mashaka ya kwanini Wizara ya Afya na Wilaya ya Temeke ambazo zote ni Ofisi za umma zitoe taarifa Moja ambayo zinapingana tena hadharani?  Je Katika hili Hakuna Utendaji wa pamoja ?

Kama Wizara ya Afya ilisema imebaini Kipindupindu Kimeibuka upya Wilaya ya Temeke kwanini Kabla ya saa 24 Mkuu wa Wilaya ya Temeke akanushe taarifa hizo za Wizara?Kuna nini hapa ?

Je Waziri Ummy amepotoka kama alivyopotoka Naibu waziri wake Dk.Kigwangala kipindi kile alipovamia Hospitali ya Dk.Mwaka na kumsema hadharani Kuwa Dk.Mwaka Si Daktari, Hana vibali Vya kujitangaza wakati si kweli na ukweli kwamba Dk.Mwaka ni mtabibu anayetambulika na serikali na serikali hiyo hiyo ndiyo iliyompa vibari Vya kuendesha vipindi vyake Vya kitabibu Katika Redio na Televisheni?

Au Mkuu wa Wilaya Mjema naye amepotoka na anaficha ukweli Kuwa Kipindupindu Kuwa hakipo Kwenye Wilaya yake ya Temeke wakati ukweli Kipundupindu kipo Katika Wilaya yake? 

Lakini naye Mkuu wa Wilaya Mjema ni kwanini jana akuona ni busara kwenda Wizarani ya Afya Moja kuomba kuonana na Waziri Ummy kumweleza Ana kwa Ana au kwa maandishi Kuwa taarifa iliyotolewa Juzi na Wizara ya Afya Kuwa kuna Kipindupindu Katika Wilaya yake siyo kweli na kwamba ukweli ni kwamba hakuna wagonjwa wa Kipindupindu Temeke hadi naye Akaamua kutoa taarifa za kukanusha taarifa za Wizara kuwepo wagonjwa wa Kipindupindu Temeke wenye vyombo Vya Habari Hali ambayo imesababisha wananchi wanashindwa   Kushika lipi na kuacha lipi?


Mi ni mtu  wa Kuvuta subira ,naamini ni suala la muda tu ukweli utabainika na tutafahamu Kati ya Taarifa ya Wizara ya Afya iliyotolewa na Waziri Ummy na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke kuwa Hakuna Kipindupindu ipi ni ya ukweli na ipi ni ya uongo.

 Nawaasa  baadhi ya wanasiasa mliobahatika kupata nafasi za Uongozi Katika serikali ya awamu ya tano, punguzeni tabia ya Kupenda kuonekana onekana kila kukicha Kwenye vyombo Vya Habari mkifikiri Kuwa kuonekana kila kukicha Kwenye vyombo Vya Habari mkitoa matamko ,makalipio  kama Manyapara ndiyo Jamii itawaona mnafanya kazi Sanaaa.

Baadhi yenu acheni tabia ya kwenda kuwaondoa madarakani baadhi ya watendaji kwa Fedhea tena Mbele ya vyombo Vya Habari kwa taarifa tu za kusikia 'Hear say evidence'.

Kuna watu ndani ya serikali tangu serikali zilizopita ni wachapakazi,waadilifu na saa 12 asubuhi wameishafika maofisini wanachapa kazi lakini hata siku Moja hawapendi hii tabia ya kwenda kuuza sura 'nyago' Kwenye vyombo Vya Habari  kama baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa hivi sasa ambao nafikiri wanaamini bila sura zao kuonekana Kwenye Televisheni basi aliyewateua sijui atawahesabu hawafanyikazi .

Hivi mlipoteuliwa   kushika hizo nyadhifa Moja ya Kigezo mliambiwa ni lazima muwe mnaonekana Kwenye Televisheni kila kukicha?Naibu waziri Dk.Kigwangala Tulimshuhudia hivi karibuni akijigeuza 'Korokoroni' na suti yake akasimama nje ya geti la Wizara yake akiangalia wachelewaji wakati kazi hiyo siyo yake kabisa tena wakati akifanya Kituko hiki Tayari vyombo Vya Habari asubuhi Kabla ya saa mbili asubuhi vilikuwa vimefika pale vipi piga picha.Sifaa hizi za kijinga .

Kipimo cha uchapaji kazi ,uadilifu serikali siyo kuuza sura kila siku Kwenye vyombo Vya Habari .Muuige mfano kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, Mkuu wa Jeshi la Polisi ,Ernest Mangu,Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju  na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Jaji Eliezer Feleshi.

Viongozi Hao wa umma huwaoni wakibwata bwata ovyo Kwenye vyombo Vya Habari ,ila chini ya Uongozi wao kazi zinafanyika vizuri ,Kisomi na kiu weledi kimya kimya na watendaji wa Taasisi zinazoongozwa na viongozi Hao wafuateni muwaulize shuruba ya kazi bila kuzembea.


Mimi ni mwanahabari kitaaluma wa zaidi ya Miaka 16 nimefanya kazi hiyo, nafahamu Kuwa mwisho wa wanasiasa wanaopenda kufanyakazi kwa kutumia    Sana Vyombo Vya Habari kila wakati hata Katika mambo yasiyo ya Msingi na  lazima  mwisho wao uwa simwema.

Kuna majukumu mengi yanafanywa na waziri ,kuna Ofisa Habari wa Wizara Si yupo anaweza kwenda Katika hiyo kazi akapiga picha,akaandika Habari akatuma Kwenye vyombo Vya Habari basi ujumbe ukafika tena bila kupotoshwa wakati mwingine. 

Hakuna urafiki wa kudumu baina ya waandishi wa Habari Wengi na wanasiasa .Sisi tulifanyakazi na wanasiasa tunalijua hili.

Waziri Mkuu aliyejidhuru Edrward   Lowassa,Rais Jakaya Kikwete ambao walikuwa ni wapenzi wa waandishi wa Habari mkiwafuata wanaweza kuwapa somo Zuri tu kuhusu waandishi wa Habari Na jinsi ya kudili na waandishi wa Habari wakati gani mdili nao na wakati gani msidili nao.


Simaanishi msitoe taarifa kwa umma kupitia vyombo vya Habari toeni ila baadhi yenu punguzeni kidogo huo mchezo .

 Siwalazimishi mfuate ushauri wangu huo ila atakayeona unamfaa auchukue na aufanyie kazi.


Baadhi yenu acheni tabia ya kwenda kuwaondoa madarakani baadhi ya watendaji kwa Fedhea tena Mbele ya vyombo Vya Habari kwa taarifa tu za kusikia 'Hear say evidence ambapo ikitokea siku watu Hao wakishitaki au serikali ikishitakiwa Hamuwezi Kuja mahakamani kutolea ushahidi huo ushahidi ambao mnadai mnao.

Kwasababu siyo Siri hivi sasa baadhi ya watendaji wanafanyakazi kwa uwoga Kwani hawajui uenda wao ni Kesho watashughulikiwa .

Aidha Sidhani kama ni busara kwa kiongozi wa ngazi ya labda Waziri Mkuu kupatiwa taarifa za tuhuma za ubadhirifu ,uzembe,ukwepaji kodi wa Ofisi Fulani wa serikali Kesho yake waziri Mkuu anafunga safari Moja kwa Moja NA Lundo la vyombo Vya Habari na maofisa wengine wa serikali hadi ofisini kwa Ofisa Huyo halafu waziri Mkuu anaanza kumwambia Huyo Ofisa eti anaushahidi unaonyesha amefanya uzembe,uzembe huo umesababisha Hasara ,Mara anataka Ofisa Huyo ifikapo jioni ameletee barua ya kujieleza tena Mbele ya vyombo Vya Habari.Jamani.

Hivi kama kweli umepata taarifa hizo na wewe ni kiongozi wa juu serikalini kwanini uongozane na msafara hadi Katika Ofisi ya Ofisa Huyo ambaye ni Mdogo kwako kimadaraka muanze kutolea Kauli kama mnasutana wakati wote ni Viongozi wa serikali ?

Minaona ingekuwa ni vyema Waziri Mkuu wetu akipata taarifa kama hizo kutoka kwa Vyanzo vyake ambavyo anaviamini sana kama kwamba ushahidi wa taarifa zile Tayari mmeishakubaliwa na Mahakama Kumbe bado, amuite Ofisa Huyo au aagize mamlaka zingine zimuite Ofisa Huyo zimweleze tuhuma zake na zimpe Haki zake za asili ikabainika kuna Haja ya kumsimamisha kazi msimamisheni au mfukuzeni huko ndani kwenu taarifa ije baadaye.

Lakini hii tabia ya Waziri Mkuu Kudai ana taarifa za baadhi ya ubadhirifu ,ukwepaji kodi anaandaa ziara kwanza anaenda eneo la tukio nakuanza kumtunuku Ofisa Huyo hadharani sizani kama ni vyema maana kuna watumishi wengine wa serikali ni wavumilivu na wengine siyo wavumilivu .

Enzi Edward Lowassa akiwa waziri Mkuu naye alikuwa anatumia aina hii kidogo kama waziri Mkuu Majaliwa ya kufika baadhi ya Wilaya anazikataa hotuba za viongozi wa serikali mkoa na Wilaya husika na kuwafokea na kutimua timua watu kazi adharani kitendo kilichotafsiriwa na watu Kuwa ni kuwavunjia heshima watumishi wenzake wa umma.

Siku Moja Lowassa aliendeleza mchezo huo Katika ziara zake mikoani na alimfokea Mkuu mmoja wa Wilaya katika mkoa mmoja wa Kanda ya Ziwa ,Huyo Mkuu wa Wilaya alichomfanyia Lowassa na uwaziri Mkuu Mbele ya hadhara ile Habari ile iliandikwa Kwenye Gazeti la Tanzania Daima hatokaa akisahau hadi Leo na tabia hiyo ilikuwa ikiwakera baadhi ya watu.

Sitetei uzembe,na vitendo vyote vinavyokwamisha maendeleo ya taifa letu ila watumishi wa umma siyo vyema kwenda kujifanya unafanyakazi ziara za kushitukiza Kumbe Tayari wewe una maamuzi yako kichwani unaenda Katika Ofisi za Ofisa Huyo kama formality ukirudi ofisini tu inatangaza kumsimamisha kazi kwanini usimsimamishe kazi bila kufanya hizo ziara mnazodai ni za kushtukiza ambazo Hazina sifa za Kuitwa ni ziara za kushitukiza ?

Kesi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia,Profesa Costa Mahalu binafsi Nilimfuatilia mwanzo mwisho ndani na nje ya Mahakama.Ilinifunza mambo mengi sana.

Kubwa Ilinifunza Kuwa ndani ya serikali kuna baadhi ya watu wana roho za kishetani Kabisa na ni mabingwa wa kuzushia wenzao uongo  mzito na uongo huo unasababisha aliyezushiwa uongo kuondolewa Kazini yaani kusimamishwa kazi na kufunguliwa Kesi ya jinai Mahakamani na kusota sana na kuathirika kiuchumi yeye na familia yake na kudhalilika Mbele ya Jamii na kuonekana ni fisadi wa Fedha za umma.

Lakini kwakuwa Mahakama zetu zinafuata Sheria ushahidi thabiti siyo majungu ,fitna ,Chuki ,uzushi Mahalu alishinda ile Kesi .

Sasa Mimi pia napenda kushauri watendaji wa serikali hii waendelee kutimiza majukumu Yao kwa mujibu wa sheria,hakima busara na  siyo mihemko.

Muelewe Kuwa Hamuwezi kufurahisha watu wote, na watu wanamshangilia Leo Kesho ndiyo Hao Hao watakuwa wakwanza kuwaona hamfai na watasema hamjafanya lolote .

 Hao ndiyo baadhi ya Watanzania walivyo Huwa ni watu wasiyo tabirika na wingine  ni Bendera Fuata upepo.

Na wawe macho sana na taarifa za ubadhirifu dhidi ya watumishi wengine wa umma Kwani kupitia Kesi ya Mahalu nilijifunza Kuwa siyo kila taarifa ya ubadhirifu viongozi wa serikali mnazoletewa zina ukweli asilimia Mia Moja kwasababu kama hamtokuwa makini  hizo taarifa mkaamua kujifanyiakazi mkazitumia kuwadhibu watumishi wenzenu ipo siku watu watumishi Hao watakimbilia mahakamani kupinga maamuzi yenu ya kuwasimamisha kazi,Kuwafukuza kazi.

' Honey moon ' ya serikali ya Rais John Magufuli yaani siku Mia Moja imeisha shikamaneni fanyeni kazi kwa Haki ,maslahi ya taifa letu  na sasa hivi tunaitaji kuona mkituonyesha Ubunifu wenu mpya maana kama timua timua tumeiyona makusanyo ya kodi yameongezeka Tumeyaona hongereni ,Mahakama imepatiwa hela Kabla ya Bunge la Bajeti kuwaidhinishia,Fedha kwa baadhi ya Hospitali zimetengwa.


Nawatakia Afya njema Katika Utendaji kazi wenu kwa taifa hili.Na kila Mara maumbile kumuomba Mungu awaongoze Katika kazi Zenu, awape busara Hekima Katika Utendaji wenu.

Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Afrika 


Chanzo: Facebook: Happy Katabazi

17/2/2016.



Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment