Saturday 20 February 2016

Re: [wanabidii] JINSI KARUME ALIVYOIUZA ZANZIBAR KWA NYERERE

Kujitambua pande zote mbili ni muhimu sana. Kujua historia yako ni muhimu. Halafu ujithamini usikubali kutumiwa. Kuiacha ZNZ iwe katika utata na kuvunja muungano-bara hatutakaa salama. Kwanza kwani Muunguja au Mpemba ni nani? Katoka wapi? Kafikaje kule? Hebu tuangalie makabila ya TZ hayo 120 plus na historia yao.Kila kabila limekuja hapa limetoka lilikotoka na tuna mchanganyiko wa ajabu. Visiwa vilijitenga na mailand historia inajulikana na imeandikwa. Hii ya kujifanya bara mkae na yenu na ZNZ na yao ni ule ubinafsi wa kutokujitambua. Viongozi na wale wengine wapenda madaraka wasidhanie kuwasikiliza waingereza au wamarekani au waarabu ndio tija kwa misifa na madaraka utakayo. Kwanza hakikisha familia yako ipo mstari wa mbele katika maandamano na mapambano unayoshabikia sio unaihamishia UK halafu hapa unaanzisha zari. Hakikisha hukimbilii Bara kununua ardhi na kujenga unakwenda ZNZ kuanzisha vurugu na maandamano jioni umerudi kwako Bara. kaa huko huko. Karume na Nyerere speech zao zipo. Aliwaona watu wake wakorofi akawapa uhuru kuwa-anayejiona yeye Mwarabu wa Saudia au Oman au wapi-asepe huru aende huko. Anayeamua kubaki atabaki hapa kama Muunguja au Mpemba au Mzanzibari na akawapa muda. Kisha, tunaungana na ndugu zetu-koroga mchanga Mwalimu. Huyu alijua historia ya Utumwa na kujua kule watu mchanganyiko asili yao ni nini? Wengi kwao kwa asili yao ni bara na nchi jirani. Karume alifanya maendeleo makubwa miradi mingine haikukamilishwa hata na huyo Mwanae Karume. Shein kwa muda mfupi kafanya mengi sana. Huduma ya Marehemu Karume kwa wananchi wake ni kama ile ya Gadafi wa Libya. Mabarabara, maghorofa ya kuishi, kuwa na magari ya kuwapeleka na kuwarudisha shamba. Kwa sasa, barabara zimekuwa finyu watu kusogea kujenga kando ya barabara vibanda vya biashara, beach pollution. Wenzetu ZNZ ndio walikuwa wakwanza kuwa na Television kabla ya sisi huku, mfumo ulikuwa British System kiingereza ndio lugha ya kufundishia, maduka yalikuwa yamejaa vitu vya ulaya, India tukitoka bara kwenda kununua TV, baiskeli na vitu vinginevyo. Wapemba ndio walioanzisha mfumo wa Taxi DSM hapa kabla ya vijana wetu kuwa na private taxes nyingi zilikuwa za wapemba na maduka ya jumla na rejareja kariakoo, mtoni, mbagala, Keko mavitu toka ZNZ pia soko ni huku sisi Mchele, nyanya, nyama na Aboud Jumbe alianzisha kituo cha mifugo na kivuko/bandari ndogo ya kusafirishia mifugo kutoka Bara kwenda ZNZ huko Makurunge Bagamoyo ili kupata nyama ZNZ. Nia ya Muungano haikuwa mbaya, udugu wa damu na ukabila upo kuchanganya damu kuwa chotara si hoja. Kuna chotara mweusi kila kona kuliko Mbungwe au Mbulu wa Babati. Obama kawa Rais USA na ni Rais atakayekumbukwa milele kwa upendo wa watu wake na uelewa. Kama kuonewa, ni bara tunaoonewa. Huku wana maduka, investments, makazi lakini wabara walichomewa maduka ZNZ. Bara wanavua, kukata mikoko, kupitisha na kusafirisha mali kimagendo kuja huku kwa faida ya watu binafsi-bado wao wanaona sisi bara ndio tunawaonea. Wameutoa uongozi wa huku kwenye Katiba yao, wana bendera na nyimbo yao ya Kitaifa. Sisi tumemezea-watching it all lakini bado tunaonekana wanoko. Kama muungano utavunjwa-waliohuku wataondoka na kururisha ardhi ya bongoland? Au watabaki huku kama wawekezaji wageni? Au watachukua Uraia wa Bara?

Unataka kunieleza Giriki mwenye kumiliki ardhi Tegeta mbuyuni na kikanisa kile kidogo cha kwao ajione yeye si Mtanzania na aliyekuja huku ni babu wa baba naye hata ugiriki hajafika ajifanye si Mtanzania. Mmakonde aliyefika ZNZ wakati wa Utumwa na baadae alitrace ndugu zake akawapata na anawatembelea akubali kuvunja muungano ajione yeye Muunguja 100% Aliyekuwa Mfalme wa Kilwa anaukoo Mafia na watoto wake walitawala Mijengo ipo KUA na Ras Kisimani. Wapo akina baba na mama waarabu weupe na mchanganyiko, wanamiliki ardhi kubwa sana ila ni watanzania hata huko Uajemi hawajafika. Ukifika baadhi ay maeneo ya Mafia unaona hapa ni Kunduchi kabisa kisiwa kilitoka bara. Na huko ugomvi mkubwa ni wavuvi kutoka Pemba kuingia kuvua ndani na Marine Park mpaka moto uliwaka mpambano 2008 katika kuwaondoa. Halafu -wanaonewa!!
Hao viongozi ving'ang'anisi wa madaraka, wabinafsi, hawajali amnai na maisha ya wenzao kutaka kuanzisha vita kwa mambo yanayoweza kujadiliwa na kukubaliana muafaka. Waiangalie Libya na Iraq na sasa Syria na mifano mingi. Walisahau fadhila na wema wa Kadafi (namfananisha na Marehemu Karume alivyowajengea na kusaidia taifa na watu wake). Wanataka nini hao wanaokwenda kujadiliana na kukutana UK sio hapa TZ walipo. Hutumii mahakama kisheria unatangaza dunia nzima na kutaka usuluhishi nje ya nchi sio ndani kwa mfumo wa kisheria. Unawapa ahadi gani wakikusaidia. Tuna mengi ya kutatua miaka 50+ ya uhuru ili tuendelee sio kuanzisha vita turudi tulikotoka. Vita haitokwisha hata. Itakuwa si ay Kisiasa tu bali ya Kikabila na race na itachanganyika humo humo ya wakulima na ya wafugaji. Ngoma utakuwa umempa mamba atakwenda mpaka mtoni!

Karume hajaiuza ZNZ kwa Nyerere. Nyerere ndio ameiuza Bara kwa Karume kwani wao wapo huru kufanya lolote kwetu sisi hatuna Uhuru huo. Uchao wanatusimbua sisi tumekaa kimya kifarafara tu. Mikoko wanakata, bandari bubu kibao, umeme bili hawalipi, nyama, mchele, nyama tunawashushia kimagendo bila ya kodi. Hatujitambui bendera fuata upepo. Tunaogopa tusiwapa masharti ISIS watapata mwanya na kuja kutumaliza hivyo tunakaa kimya.Baba wa Taifa ameonya mengi na hata kuhusu muungano na ubaguzi. Hakuna alilobakiza katika maono na maonyo yake.

Sielewi na sitaki kuelewesha, wana siwachukii. Nami pia shopping ya wazazi wangu kabla ya uhuru na baada ilikuwa Unguja na Baba ya Mama yangu mzazi alichukuliwa utumwa huko North Kivu akapelekwa Unguja kwa mguu na kukombolewa na meli ya Waingereza wakiwa wanatolewa Unguja baadae kupelekwa kulima Ngazija sijui visiwa gani wapi sikumbuki. Ninawashangaa wasiotambua historia yao na kutumagua!!
--------------------------------------------
On Sun, 21/2/16, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] JINSI KARUME ALIVYOIUZA ZANZIBAR KWA NYERERE
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, 21 February, 2016, 4:01

Binafsi sijawahi
kuelewa ni wapi haswa Hizbu, CUF na SEIF wanataka kuipeleka
ZANZIBAR!!

Hapa kuna nguvu nyingine ya ziada inahitajika. Lakini baada
ya kutumia nguvu shurti kero za muungano zishughulikiwe
mapema. TUSIKUBALI KUVUNJA MUUNGANO, TUTAWAACHA NDUGU ZETU
KWENYE MANYANYASO NA SHIDA.

Ila Hakika haya mambo yatakaa sawa.

Mimi naona ni kujisahau tu!! Tumesahau wapi tumetoka, na
wa-bara wasioijua historia wanapigia debe gari wasilojua
linaelekea wapi.
Sijaandika ili nieleweke…….



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment