Wednesday, 11 November 2015

[wanabidii] Re: URAIS WA DR. MAGUFULI, NI FUNZO TOSHA KWA WENGINE

Oh dear!

Bw. De kleinson Kim,

Hatuwezi kuzungumzia DEMOKRASIA bila watu, uhuru, katiba n.k

Hivyo, demokrasia ni utawala wa watu katika uhuru na haki katika shughuli kama za uchaguzi na mifumo yote ya maendeleo ya watu. Demokrasia unatambua kwamba kila aliye ADULT katika jamii ana haki ya kuchaguliwa katika jamii kuitumikia jamii.

Malengo makuu ya demokrasia ni kulinda na kudumisha haki za watu wote katika Nyanja zote.

Katiba katika demokrasia ni kwa ajili ya kuweka boundaries (mipaka)ya viongozi na wananchi wote - Katiba in my view ni kama "PLAN OF ACTION" - or "JOB Description kwa kila mhusika. Katiba inatia nguvu - it motivates people to work hard kwa kuwa wanafahamu what is expected of them. Pia inawapa watu nuru wasije wakawa madiktata au mafisadi. Katiba ina-monitor viongozi wa watu.

Uhuru wa kusema na kutenda katika utu na heshima kwa watu wote is the HEART of Demokrasia. Watu wakinyimwa uhuru, basi watakuwa wamenyimwa kila kitu - sawa na nchi iliyovamiwa na magenge ya watu wengine kutoka nchi nyingine na kuwavua utu na heshima yao: km mkoloni alivyofanya hapo nyuma bali wazee wetu wakamwaga damu kujikomboa.

Loss or denial of demokrasi is equivalent to being sentenced to death. Ngumu kwa watanzania!



On Friday, November 6, 2015 at 8:27:37 AM UTC-5, fadhil fadhil wrote:
> Urais wa Dr Magufuli, ni funzo tosha kwa watu wengine
>
> Miezi kama minne iliyopita ni watu wachache sana waliokuwa wakiamini
> kwamba Dr Magufuli atakuja kuwa Rais wa nchi yetu, Hii ilitokana na
> mfumo uliokuwepo huko nyuma wa kuchagua mgombea ku-base zaidi kwenye
> makundi ndani ya Chama na umaarufu wa mgombea.
> Kilichomwibua
> Dr Magufuli ni record yake ya uchapakazi, uadilifu, kutoyumbishwa hovyo
> hovyo kwa sababu ya kusimamia kile anachokiamini kwa manufaa ya wananchi
> na taifa kwa ujumla, Hiyo
> imejidhihirisha zaidi katika wizara zote alizowahi kuziongoza mfano
> Ujenzi na Miundombinu pamoja na Kilimo na ufugaji.
>
> Fundisho tunalopata hapa ni kwamba usingoje mpaka upewe nafasi
> kubwa ya utumishi ndio uanze kuonyesha namna ya kuwatumikia wananchi.
> Piga kazi tu hata kama huna cheo chochote, usingoje mpaka uwe Waziri,
> Mbunge, M /"kiti serikali ya mtaa, nk* WASIPOKUONA BINADAMU MUNGU ATAKUONA NA KUKUINUA TU

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment