Mzee Mzindakaya Nusura akamatwe na Takukuru....
* Takukuru waahidi kuwa mbongo kwa sasa...
Katika hali isiyotarajiwa Mzee Chrisant Mzindakaya (Mbunge mstafu) amejikuta akiponyoka mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) baada ya maofisa wa taasisi hiyo kupata taarifa za mzee huyo kugawa rushwa kwa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi...
"Mzee Mzindakaya, tokea juzi, jumapili tulipata taarifa kwamba anagawa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ili wamchague Pinda kuwa mgombea wa chama hicho kitendo ambacho ni kinyume na sheria No. 11/2007 kifungu cha 15 Pcca" amesikika mmoja wa afisa wa taasisi hiyo. Ingawa mpaka sasa bado tunafanyia kazi taarifa hizo za awali na muda wowote tutatoa taarifa rasmi...
Taarifa hizo pia zilizothibitishwa na baadhi ya wajumbe wa chama hicho ambapo walisema tokea juzi Mzindakaya amekuwa na utaratibu wa kuwaita wajumbe wa mkutano mkuu kutoka mkoa wa Rukwa kwa makundi (Wilaya) nyumbani kwake na kisha kuwahonga Tsh. 100,000/= (kwa kila mjumbe) na kuwambia wamchague Mizengo Pinda kuwa mgombea wa chama cha Mapinduzi....
"Hii siyo mara ya kwanza kufanya hivi, nakumbuka mwezi wa pili alituita sisi wa Rukwa, Katavi na Tabora na kupewa kiasi cha Tsh. 150, 000/= kila mmoja" mjumbe kutoka Sumbawanga mjini amesikika akisema...
Mzindakaya amekuwa na kashfa mbali mbali katika mkoa wake na Taifa kwa ujumla. Mpaka sasa haijulikani kama zile fedha billion 9 alizokopa serikalini baada ya kughushi nyaraka kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa hata baada ya kugundulika kuwa alighushi nyaraka...
Pia katika wilaya yake Mzee Mzindakaya alipora ardhi kwa wananchi zaidi ya ekari 4,000 mpaka sasa wananchi wamelia kwa muda mrefu bila kupata majibu, yawezekana kabisa hii ni kutokana na Pinda kuwa nyuma yake, na sasa kumuweka kama kampeni meneja wake kanda ya Magharibi
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment