Wednesday, 29 April 2015

[wanabidii] Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania

Wanataaluma,

 

Habari za siku ndugu zangu Wazalendo !

 

Nadhani kila mmoja ameona ambavyo thamani ya fedha yetu ilivyoshuka thamani katika historia ya nchi yetu tangu tupate uhuru.

 

Kushuka kwa thamani ya fedha ya nchi yoyote haina maana ya kuonyesha moja kwa moja kuwa uchumi wa nchi husika umeshuka au umeathirika, hivyo basi  kushuka au kupanda kwa thamani ya fedha kuna faida na hasara kulingana na mfumo na mpangilio wa kiuchumi wa nchi husika. Ziko nchi hufaidika kwa kushusha thamani ya fedha zake makusudi kwa malengo ya kupandisha kiwango cha mauzo ya nje na kuuza zaidi.

 

Mengi yanasemwa kuhusu sababu za kushuka kwa thmani ya fedha yetu dhidi ya dola ya Marekenai sasa nikaribishe michango kama kuna mdau yoyote ndani ya jukwaa hili anaweza kutuelimisha zaidi.

 

Noamba tuchangie mada hii kwa lengo la kuelimishana sababu, faida na hasara na nini kifanyike,  labda kupitia jukwaa hili kuna mambo yanaweza yakachukuliwa na watunga sera wetu ambao baadhi yao ni wanchama wa mtandao huu ili kusaidia kujenga uchumi wetu.

 

Maana taarifa muhimu wananchi wasipoelimishwa vizuri kwa kupewa taarifa sahihi na kwa wakati sahihi inaweza ikasababisha wananchi kupaniki na kuleta athari zaidi kwenye uchumi , mfano ni jinsi uchumi wa dunia ulivyoyumba miaka ya 2008/2009  sababu moja ilichangiwa na wananchi wa Marekani na Uingereza kutopata taarifa sahihi kwa wakati sahihi na ikapelekea wengi wao kufanya maamuzi yasiyo sahihi ya kiuwekezaji/kifedha yaliyosababisha kuyumba kwa uchumi wote wa dunia.

 

Hivyo basi naomba nitoe wito kwa wote tuwe huru kutumia jukwaa hili na majukwaa mengine kwa lengo la kuelimishana na kupashana habari mbali mbali zilizo sahihi kwa faida yetu wote.

 

Wasalaamu.

 

Phares Magesa ,

B.Sc,PGDSE,MBA, IEng.,MIET
----------------------------

Mtaalamu na Mshauri wa TEHAMA, Menejimenti na Uongozi

 

Rais -  Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN)

www.tpntz.org

 

Cell: +255 (0784/0713/0767) 618320

 

E-mail:   magesa@tanzaniaports.com

                pmages@gmail.com

                magesa@hotmail.com

0 comments:

Post a Comment