Thursday, 30 April 2015

Re: [wanabidii] RE: Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania

Kaka Bubelwa nakushukuru kwa uchambuzi wako.
Lakini fahamu kuwa Watanzania-kuanzia sisi wananchi hadi wanaokamata dola --tangu uhuru hadi leo--tumekuwa tukiamini eti ustawi wa nchi yetu na watu wake utapatikana kwa kupokea misaada hasa fedha kutoka nchi tajiri za Ulaya-- kwa vile nchi hizo zilitunyonya kupitia utumwa na ukoloni--kumbe tunajilemaza akili na mwili kwa kudhani kuna cha BURE! Kwa imani kama hii hatuna tofauti kabisa na vile vikundi vya kiimani vilivyojulikana kama 'CARGO CULTS' vilivyoibuka Malanesia miaka ya 1940 hadi 1960 vilivyokuwa vikikesha usiku na kushinda mchana kutwa vikiendesha 'ibada' kwa kuamini kuwa watu wa Malanesia wangepata maendeleo siyo kwa juhudi zao, bali kwa kupokea shehena za mali ambazo zingeshuka kimiujiza kutoka nchi tajiri za Ulaya.

Kwa mfano shilingi yetu itaimarika vipi kama kila anayetafuta kuingia Ikulu, anatafuta kwenda kujitajirisha yeye na familia yake na waliomsaidia --na wakishakamata Ikulu wanatunga sheria za kikoloni--kudhibiti umma na vyombo vya habari --ili waweze kudumu madarakani na kuendelea kujitajirisha wenyewe?

Unadhani ukoloni uliondoka baada ya wakoloni Wazungu kuondolewa? Kwa mtazamo wangu, Afrika --Tanzania ikiwepo tuko kwenye ukoloni mbaya zaidi unaofanywa na watu wetu wenyewe-wanaume na wanawake tunaowapa madaraka ya kuongoza nchi. Tena zaidi ukoloni wa leo utaendelea kukwamisha ustawi wa nchi yetu na watu wake kwa miaka mingi ijayo --maana tunadhani ukoloni umepita na ulikuwa na sura--sura ya Kizungu! Kumbe ukoloni ni matendo--ni watu wachache kukamata dola--kutunga sheria za kikoloni waweze kutawala--ili kujinufaisha huku umma mpana ukifukarishwa kwa kwenda mbele miaka nenda, miaka rudi. Je tutafika?

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 4/30/15, Bubelwa E. Kaiza <bubelwa.kaiza@fordia.org> wrote:

Subject: [wanabidii] RE: Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, April 30, 2015, 10:02 PM




















Hello
tujadili
uchumi wa Tanzania na namna
ya kuuokoa badala ya kuishia kulinganisha tu na mafanikio ya
kiuchumi ya nchi
nyingine. Ni vizuri wachumi wakachukua nafasi yao maana
hisia na mipasho ya
kisiasa haitatusaidia. Let's talk openly.


 

Kwa
taarifa ya wengine,
uchumi wa Kenya umejengewa katika msingi imara wa a strong manufacturing and professional services
industries. Kenya
ni nchi ya tatu kwa Africa kuwa na a very
strong manufacturing industry baada ya Africa Kusini na
Egypt. Bajeti za
kila mwaka za Serikali ya Kenya hutokana na/hutegemea kodi
(hasa kutoka tasnia
ya usindikaji na kilimo) na other
internal pubic financing strategies such as monetary
instruments kwa
asilimia 95. Serikali ya Kenya huachia mashirika ya nje
(BWs) kuchangia
asilimia 5 tu ya bajeti na hii ni baada ya BWs kuomba
kuchangia bajeti ya
Serikali ili wasiwe useless/irrelevant.



 

Nakumbuka
wakati wa
Kibaki BWs walitaka kuleta mambo ya GBS ya hapa kwetu,
kujadili michango yao ya
ku-finance bajeti ya Serikali hadharani, Kibaki aliwaeleza
kuwa Serikali yake
haijadili mambo ya budget financing hadharani, kwamba siyo
utamaduni wa Kenya
na iwapo BWs wangeshindwa kuvumilia utamaduni huo wa Kenya,
Serikali ilikuwa
radhi kutopokea hiyo asilimia 5 yao ya nyongeza katika
bajeti ya Serikali ya Kenya.
BWs waliufyata mpaka leo.


 

Lakini
pia sekta ya fedha
ya Kenya inasimamiwa vilivyo siyo holela kama hapa kwetu.
Huwezi kuona wananchi
waki-transact kwa kutumia dola au euro bali Ksh. Export
component ya Kenya ni
kubwa na nchi ina comprehensive strategy
ya uchumi, mfano tujiulize kiasi cha dola kinachoingizwa
nchini humo kutokana
na travel service export ya KQ. Tujiulize maduka kama ya
NAKUMATI, Mabenki,
manunuzi yanayofanywa na Ofisi za Umoja wa Mataifa
(Giligili?) na kadhalika,
yanayouza bidhaa na/au huduma nje ya Kenya yanaingiza
dola/euro kiasi gani
nchini humo. Kenya ina mkakati mkubwa unaotekelezwa na kila
Mkenya kuhakikisha
uchumi wa nchi unabaki imara.


 

.....
mwaka
2008 Serikali ya Zambia ilifuta mikataba (MDAs) yote ya uchimbaji
madini iliyokuwepo baada ya kuona
nchi yao hainufaiki na mauzo
ya shaba nje ya nchi.
Sheria mpya ya madini ilitungwa
na kuachana na mambo ya MDAs (ushauri wa BWs). Kampuni zinazotaka kuwekeza nchini Zambia hufuata taratibu za kisheria za
kupewa/kununua leseni za uchimbaji
na kuingia kazini. Hakuna misamaa ya kodi
wala ruzuku kwa makampuni ya
wawekezaji kama Tanzania inavyofanya. Zambia inadhibiti mauzo yote ya
shaba nje ya nchi. Leo hii
nilipokwenda kununua ZKwacha hapa Lusaka nimekuta Kwacha 7 zinanunuliwa kwa dola 1.


 

Tunachojifunza
kutoka Zambia ni
kuwa Serikali ikifanya maamuzi sahihi na kuweka
sera sahihi, uchumi wetu unaweza tena
kurudi kwenye reli; hata shilling 5 kununua dola moja
ya Marekani kama ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka
ya 1980.



 

Salam
kwa
MNEC Magesa.


 

Kaiza



 









--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment