Tuesday, 21 April 2015

Re: [wanabidii] WAFANYABIASHARA ACHENI KUTUMIWA NA WANASIASA KUENDESHA MIGOMO YA KUFUNGA MADUKA

Kama wewe umekwenda shule kweli, kwa nini ubaki na mawazo mgando kwamba mtu asipokubaliana na matakwa yako maana yake ametumiwa na mpinzani wako? Hivi hufahamu binadamu wote wameumbwa na akili. Na wanauwezo wa kuchambua kipi kinafaa na kipi hakifai? Hutambui kuwa mtu anaweza akawa kiongozi, bado wale anaowaongoza wanaona mbali kuliko yeye? Kalaga baho!



On Monday, 20 April 2015, 19:31, 'Sylvanus Kessy' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Tumsamehe jamani. Mimi sisomi tena mambo yake!


--------------------------------------------
On Mon, 4/20/15, 'marcus kabwella' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] WAFANYABIASHARA ACHENI KUTUMIWA NA WANASIASA KUENDESHA MIGOMO YA KUFUNGA MADUKA
To: "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, April 20, 2015, 4:38 PM

Nimeisoma makala ya yako Happines Katabazi.Hii
ya leo na siku zote unazozirusha humu, umegusia mambo mengi
lakini naamini kina unachojivunia nyuma ya pazia au ni kwa
sababu ni wachache wanaingia kwenye mtandao huu na kuona
maneno yako yakukera!Yamkini
mahache yanaweza kuwa na maana.Umemgusia
Shekh Ponda, Dr Ulimboka na wengine wengi waliodhuriwa
ukasema kilichowapata wote tunakijua,  Nikuulize swali
kilichomtesa Ulimboka,Ablosom Kibamba na kumuua Dr. Sengodo
Mvungi unakijua? maana serikali ilikataa katakata kuhusishwa
na wenye ndugu na jamaa zao wameshukuru wewe leo unatokosa
nyoyo zao hivi wewe ungekuwa mke au mtoto wa hao watu
ungejisikiaje mtu anapoandika makala kama hiyo ukiwasifia
waliofanya
  uharamia?
Kumbuka
masikini hana cha kupoteza siku zote kwa udhalimu unaofanywa
siku akisema potelea mbali nchi haitakalika hata kama tuna
jeshi imara kiasi gani. Hivi
ulishafika Mtwara ukaona hasira na mtazamo wa wananchi dhidi
ya serikali?Gesi
imesafirishwa kwa bomba akitokea mtu akamwambia kalipue nina
kiasi cha fedha ataacha kweli?Hakuna
ambae hamuhitaji mwenzake katika ustawi wa taifa hivi
wananchi wakiwaka hasira na serikali ikatuma jeshi likauwa
wote mwisho wa siku wataendabkuomba wapi kura?

Umekuwa
  ukitumia maneno makali na lugha tatanishi ila chezea wooote
waislam achana nao kabisa wale jamaa hawakopeshi
utakavyosema humu unaweza kufikiri umemaliza lakini
wakikuibukia utajuta kuzaliwa.Kila
kinachotokea  mnahusisha wana siasa kwa nini wawe wa
upinzani tu ina maana wa chama tawala wana mtu wao
wanaemtumikia na sio wananchi wa tabaka la chini na
kati. Serikali
ilikuwa inamiliki njia kuu za uchumi ila ufisadi unaopigiwa
kelele haujaanza jana wala juzi ukauwa viwanda makampuni
ikiwemo ya mabasi ya taifa KAMATA huenda ulikuwa hujazaliwa
leo hii kampuni zile zingekuwepo vyama vya ushirika
vingekuwepo na hata shirika la biashara lingekuwepo RTC na
kutoa huduma kwa wananchi kwa weledi migomo ingetoka
wapi?Miaka
y a nyuma wanafunzi wakimaliza shule ya msingi
  hata kama mzazi ana uwezo alikuwa anasubiri matokeo
ikitokea kapangiwa shule ya serikali anaacha ya binafsi
lakini leo baadhi ya watoto na wazazi hawajui hata shule
walizokuwa wamepangiwa na serikali maana hazina umuhimu
kwao. 
Hivi
leo hata shule binafsi zikigoma patatosha? sio ajabu hata
wewe mtoto wako hasomi shule za serikali hivyo ni vema kama
umekubaliana watu wakutolee huduma basi hakikisha walengwa
wanafikiwa kwa usahihi. Kuna
mengi yanaonekana hayaendi mfano serikali inatangaza kila
siku elimu ya msingi ni buree na elimu ya sekondari kutwa ni
20,000 na Bweni ni 70,000 na matibabu kwa watoto wa umri
chini ya miaka 5 na wazee zaidi ya mika 60 watatibiwa
bure.Naomba
wasomaji kama kuna
  anaepata hizo huduma tajwa kwa viwango elekezi kama
nilivyoandika juu aniambie ni shule ipi na hospitali ipi.
Kesho wananchi tukichoka tuakajitoa muhanga tuingie
barabarani mtasema ni wana siasa? Ni
maoni yangu.
Marcus
Kabwella ( mtymishi nisiestahili)0787-905
777
Sent
from Yahoo Mail on Android  From:"'Happiness
Katabazi' via Wanabidii"
  <wanabidii@googlegroups.com>
Date:Mon, Apr 20, 2015 at 12:32
Subject:[wanabidii] WAFANYABIASHARA
ACHENI KUTUMIWA NA WANASIASA KUENDESHA MIGOMO YA KUFUNGA
MADUKA

  WAFANYABIASHARA
ACHENI KUTUMIWA NA WANASIASA KUENDESHA MIGOMO YA KUFUNGA
MADUKA

Na Happiness
Katabazi
KWA zaidi ya miezi nane sasa baadhi
ya wafanyabiashara wenye  maduka katika mikoa mbalimbali
wamekuwa wakigoma kufungua maduka yao kwa madai mapya kila
awamu wanayogoma.

Mgomo wa
kwanza walivyogoma walidai kuwa mashine za EFDS wanauziwa
kwa gharama kubwa na kwamba hawawezi kuzinunua,kodi ni
kubwa.

Mara wafanyabiashara
wakazusha mgomo mwingine ambao wakaja na madai mapya kuwa
hawana elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya mashine ua EFDS
hivyo wanaitaji elimu.

Hivi
sasa wameibuka tena kivingine katika mikoa tofauti eti
wakitaka  Mwenyekiti wa
  Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja  ambaye
Machi 25 mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma
kwasababu alikiuka masharti ya dhamana aliyopewa ikiwemo ya
kutowazuia wafanyabiashara
  kufunga maduka yao wakati kesi yake ikiendelea aachiliwe
huru ndipo watafungua maduka yao.

Akitoa taarifa mbele ya hakimu mkazi wa
mahakama ya Mkoa wa Dodoma, Rebecca Mbilu, Mwendesha
mashtaka wa serikali Rose Shio amesema kuwa upelelezi dhidi
ya kesi hiyo umeshakamilika na kuiomba mahakama kutengua
dhamana ya mshtakiwa kutokana na kukiuka masharti ya dhamana
aliyopewa.
Amesema kuwa pamoja na hilo
Mwenyekiti huyo amekuwa akiendelea kufanya mikutano na
wafanyabiashara kwa ajili ya kuwahamasisha wasiendelee
kulipa kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFDS
kitendo alichosema kuwa ni kukiuka masharti ya dhamana
aliyopewa.

Hata hivyo
wakili wa mshtakiwa, Godfrey Wasonga ameiambia mahakama kuwa
tangu mteja wake apewe dhamana hajawahi kuitisha mikutano na
wafanyabiashara kwani hata juzi hakuwa na mkutano bali
wafanyabiashara waliokuja mjini Dodoma kusikiliza kesi ya
mwenyekiti huyo, waliposikia kuwa yupo Dodoma walikwenda
  kumsalimia baada ya kupata taarifa kuwa yuko katika hoteli
ya Image Hill.

Hata hivyo
hakimu Mbilu alisema kuwa ameridhika na hoja za upande wa
mashtaka na hivyo akatengua dhamana ya Minja na kumtaka
kubaki rumande hadi April Mosi mwaka huu ambapo kesi yake
itakuja kwaajili ya kutajwa.

Watanzania ikumbukwe kuwa Tanzania ni nchi
iliyojiamliwa kuongozwa kwa Katiba na sheria.

Na Ibara ya 107A ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, nanukuu:

" 107A.-(1) Mamlaka ya
utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano
itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara
ya
Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna
chombo cha Serikali
wala cha Bunge au
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar
kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji
haki.
  (2) Katika kutoa uamuzi wa mashauri
ya madai na jinai kwa
kuzingatia sheria,
Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo, yaani:
(a) kutenda haki kwa
  wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzaniaau kiuchumi;
(b)
kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;
(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika
kutokana
na makosa ya watu wengine, na kwa
mujibu wa sheria
mahususi iliyotungwa na
Bunge;
(d) kukuza na kuendeleza usuluhishi
baina ya wahusika na katika migogoro; na
(e)
kutenda haki bila kufungwa kupita kiasi na masharti ya
kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.

Minja amefunguliwa kesi hiyo
ya jinai na kwa makusudi ameamua kukiuka masharti ya dhamana
upande wa jamhuri ukawasilisha ombi la kuomba afutiwe
dhamana kwababu amekiuka masharti na mahakama ikakubaliana
na ombi hilo kwasababu ina mamlaka ya kufanha hivyo.

Sasa haya madai ya
kiuwendawazimu yaani yanayotolewa na  baadhi ya
wafanyabiashara ambao wamedai wameamua kuanzisha mgomo wa
kutofungua maduka eti  kushinikiza Mwenyekiti wao Minja
aachiriwe
  uhuru hayo mamlaka ya kiuwendawazimu lazima watakuwa
wameyapata kwa wendawazimu wenzao ambao ni baadhi ya
wanasiasa wanaowatumia wafanyabiashara hao wa maduka kufanya
vitendo vya uwendawazimu vya kugoma kufungua maduka yao.

Nimelazimika kuwaita hawa
wafanyabiashara wanaogoma wanafanya vitendo vya
kiuwendawazimu na kweli kitendo chao hicho cha kugoma
kufungua maduka kwasababu wanataka Minja aachiriwe huru ni
cha kiuwendawazimu.

Kwababu
mtu mwenye akili timamu ,anateheshimu sheria za nchi na
anayejitambua,mwenye uchungu na taifa lake na asiyekubali
kutumiwa na wanasiasa uchwara kama wanavyotumika hawa
wafanyabiashara uchwara wanaogopa kufungua maduka yao kwa
kutumia njia za kiuni hawezi kufanya hivyo.

Wasomi wa sheria wanamsemo
mmoja usemao ' Haki yako inapoishia ndiyo haki ya
mwenzako inapoanzia'.

Yaani kwa  maana ya msemo huo hapo juu kuwa
wafanyabiashara wana haki ya kupata maslahi na wananchi
wanaotaji
  kupata huduma kutoka kwa wafanyabiashara matokeo yake
hawapati haki hiyo na serikali haipati haki yake ya kupata
mapato.

Sasa hawa
wafanyabiashara uchwara ambao minawaita wafanyabiashara
ucharwa na wanaotumiwa na wanasiasa kwa lengo moja la
kuakikikisha serikali inashindwa kupata mapato kwasababu ya
mgomo huo na matokeo yake serikali itajikuta inakosa fedha
za kuendesha mahospitali,huduma za kijamii muhimu kwasababu
itakuwa haina fedha na mwisho wake wananchi kuichukia
serikali yao na kuanza kuingia barabarani kufanya vurugu
kushinikiza serikali itoke madarakani kwasababu imeshindwa
kuwapatia  huduma muhimu.

Na mpango huo ndiyo ulioratibiwa na baadhi ya
wanaisasa  hapa nchini kwa siri kwa kuwatumia hao
wafanyabiashara uchwara ambao wengi wa wafanyabiashara
wanatokea Mkoa mmoja wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kufanya
migomo hiyo kwa njia dhalimu.

Hata kama wafanyabiashara hao wana madai ya
msingi lakini ni wazi baadhi ya
  wafanyabiashara hao wanatumia njia ambazo hazikubariki
kisheria kudai haki zao.

Haya basi tufanye ni kweli mashine hizo
hawawezi kuzinunua kwasababu bei yake ipo juu,
wamepandishiwa kiwango kikubwa cha kodi na hawawezi
kukimudu.

Nawauliza
wafanyabiashara hawa hivi Mahakamani au kwenye Baraza la
Rufaa la Kodi hawapajui?

Maana huko ndiko sehemu sahihi kwao kwenda
kulalamikia hayo mambo mawili wanayoyapinga matokeo yake
hawajaenda kulalamika huko wameishia kulalamika kwenye
vyombo vya habari,serikalini na kwa hao mabwana zao
wanasiasa wanaowatumia vibaya.

Ibara ya 13(6)(a) ya  Katiba ya nchi
,ninanukuu;

'Wakati
haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji
kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo
kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa
na
haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa
ukamilifu, na
pia haki ya kukata rufaa au
kupata nafuu nyingine ya
kisheria kutokana
na maamuzi
  ya mahakama au
chombo hicho kingenecho
kinachohusika'.

Kwa
lugha nyepesi ibara hiyo nyie wafanyabiashara uchwara ibara
hiyo  inatoa haki ya kukata rufaa katika mahakama ya juu
kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama ya chini kama unaona
una sababu na haki (Locus of stand) ya kukata rufaa katika
Mahakama ya juu.

Kwahiyo
nyie wafanyabiashara uchwara hamna haki ya kukata rufaa
kupinga uamuzi wa mahakama wa kumfutia dhamana Minja ,mwenye
mamlaka hayo ni  Minja mwenyewe na siyo nyie wafanyabiashara
wala wanasiasa uchwara waliopayuka ndani ya bunge akiwemo
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kutaka Minja apewe
dhamana nje ya mahakama na siku zote mahakama inafanyakazi
ndano ya mahakama siyo maneno ya kihuni uhuni yanayotolewa
na wahuni huni nje ya mahakama kutaka apewe dhamana.

Na mtambue uhuni wenu huo wa
shinikizo la kutaka Minja apatiwe dhamana,nyie siyo watu wa
kwanza uufanya, aliiufanya Mwenyekiti wa Chama Cha CUF,
  Professa Ibrahim Lipumba wakati Sheikh Ponda Issa Ponda
alipokamatwa Agosti mwaka 2012 na kufunguliwa kesi ya
uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini alimfungia dhamana kwa mujibu
wa kifungu cha 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
Jinai ya mwaka 2002 na Ponda kweli alikaa gerezani hadi  Mei
8 mwama 2013 alipofungwa kifungo cha mwaka mmoja nje.

Na siyo Lipumba peke yake bali
baadhi ya waislamu wenzake nao walikuwa wakikesha misikitini
na mahakamani kushinikiza aachiwe lakini wapi.

Sasa Minja ninani hadi na yeye
mahakama ipindishe sheria ili impendelee?

Hivi Minja na Ponda nani
mwenye nguvu ya watu na mwenye wafuasi wengi na akiamua
kufanya jambo lake vyombo vya dola vinakesha macho kumsaka
kama siyo Ponda lakini serikali imemdhibiti?

Mbinu yenu hiyo ya kijinga
ndiyo itasababaisha Minja aendelee kusota gerezani.

Ndio maana minashawishika
  kuwafananisha nyie wafanyabiashara mliogoma hivi sasa kwa
sababu eti mnataka Minja aachiriwe huru kwa  sawa  na
wendawazimu kwababu zifuatazo:

Mosi , hamna haki ya kisheria nyie
wafanyabiashara mambumbu wa sheria wa kuilazimisha mahakama
ifanye mnavyotaka nyie.

Pili, mnaingilia majukumu ya kimahakama  ya
kusikiliza na kutolea maamuzi kesi.

Tatu, nyie wafanyabiashara uchwara mliogoma
hamna haki ya kwenda kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya
Dodoma kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma wa
kumfutia dhamana  Minja kwasababu nyie siyo washitakiwa
katika kesi hiyo.

Sasa
kihelehele hiki cha kusema Minja kaonewa wakati hata
usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo haujafanyika  kinatoka
wapi kama siyo ushambenga na ukosefu wa akili na kuipaka
matope mhimili wa mahakama na kuleta fujo katika jamii
yetu?

Watanzania wangapi
wanafutiwa dhamana na  Mahakama mbona hamjawahi kuwa na
umoja kiasi hiki na kufunga
  maduka?

Kwanini Minja tu?
Kwa hiyo ikitokea mahakama isitengue amri yake ya kumfutia
dhamana hadi mwakani ,nyie wafanyabiashara uchwara
mtaendelea hadi mwakani na mgomo wenu  wa kutofungua
madukani yenu hadi atakapopatiwa dhamai hapo mwakani?

Hivi zile leseni za biashara
mlizopewa na serikali kwaajili ya nyie kuendesha biashara
kuna mahali kokote zimeandikwa siku Mwenyekiti wa umoja wa
wafanyabiashara akifutiwa dhamana basi ni ruksa kwa
wafanyabiashara kugoma kufungua maduka?

Hivi hizo leseni za biashara zenu kuna sehemu
yoyote  inaonyesha wafanyabiashara wataruhusiwa kisheria
kugoma kufungua maduka yao kwasababu ya kupinga gharama za
manunuzi ya mashine ya EFDS? Jibu ni hakuna.

Nawauliza nyie wafanyabiashara
uchwara haya mamlaka  ya nyie baadhi ya wafanyabiashara ya
kukaidi kununua mashine hiyo, kushiriki migomo isiyofuata
taratibu za kisheria mmeyapata wapi na kwa mujibu wa sheria
zipi hali inayosababisha
  wananchi kukosa huduma na kulipa kodi kwa serikali yao na
serikali kushindwa kupata mapato?

Halafu tujiulize ni kwanini wafanyabiashara
wenye asili ya Kiarabu na Wahindi hawagomi na wote wapo pale
pale Kariakoo kwa hapa jiji la Dar es Salaam?

Na ni kwanini kila kukicha
mfano Dar es Salaam, wanagoma wafanyabiashara wenye maduka
eneo la Kariakoo tu?

Mbona
wafanyabiashara wenye maduka yenye bidhaa zilizokidhi
viwango kupita bidhaa zinazoouzwa katika maduka ya
wafanyabiashara wagomaji katika maeno ya Posta Mpya,
Sinza,Manzese, Mbezi ,Masaki na Kimara mbona hajuwasikia
wakigoma na kufunga ofisi zao?

Kila kukicha ni wafanyabiashara wa
Kariakoo.Kwanini? Maduka mengi ya Kariakoo inadaiwa
yanamilikiwa  na watu wenye asili ya Kabila la Wachaga na
Wakinga.

Iweje baadhi ya
wafanyabiashara hawa wagomaji wadai hawana feha za kununulia
mashine ya EFDS lakini wafanyabiashara hawa hawa wanamitaji
inayowapa fursa ya
  wenda nchini Uturuki, China ,Kenya na Dubai kwenda kuchukua
  mzigo  na kuuleta Tanzania na kisha kuuza?

Kwanza badhi ya
wafanyabiashara wenye maduka hapo Kariakoo mnatuuzia bidhaa
mbazo hazina ubora .

Lakini
upole Watanzania ndio unawaa kiburi nyie wafanyabiashara
kufanya uhuni we huu lakini mtambue kila jambo lina  mwisho
wake.

Na uchunguzi wangu
nilioufanya kabla sijaandika makala hii unaonyesha kuna
baadhi ya wafanyabiashara wapo tayari kufungua maduka yao
ila wanaogopa kushughulikiwa na wafanyabiashara wenzao ambao
wanaendesha mgomo huo kwa maelekezo ya baadhi ya wanaisasa
toka baadhi ya vyama ya upinzani hapa nchini.

Licha pia kuna baadhi ya
wafanyabiashara wengine hapo Kariakoo wamefunga mlango wa
mbele wa duka hilo anakaa mbele ya hilo duka na endapo
anahisi anayepita mbele yake ni mteja anamuuliza kama
anaitaji huduma na mteja yule akikubali, muuzaji wa duka
hilo anampitishia mlango wa nyuma mteja yule
  na kisha anaenda kumpatia huduma bila kumpatia risiti hali
inayosababisha serikali kuendelea kukosa mapato kutokana na
uhuni huu unaofanywa na wahuni hawa yaani
wafanyabiashara.

Ebu
tujiulize mfanyabiashara wa ukweli na  mweye akili timamu na
tujuavyo sisi wafanyabiashara wengi wanamikopo ya kuendeshea
biashara zao na wanadaiwa kodi za pango, anakubalije kugoma
kufanyabiashara na asiingize fedha  kwa sababu dhaifu kama
hizo?

Nalazimika kuanza
kukubaliana na Mwanasayansi ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB) Dk.Elifuraha Mtaro ambaye kila
siku anasema mitafaruku inayoendelea kuibuka kila kukicha ni
Jiopolitiko Agenda, akiwa anamaanisha mtafuruku inayobuka
kila kukicha ni ajenda chafu za baadi ya mataifa ya kigeni
yasiyotaikia mema Tanzania, wanataka kuakiikisha siku
watanzania tunachinjana  amani yetu inatoweka.

Uenda hawa wanaoendesha mgomo
wa kutofungua maduka tayari wameishapatiwa fedha za uhakika
  na wabaya wa taifa hili ndio maana hata wasipoyafungua
maduka yao hawana hasara kwasababu tayari walishapeww fedha
za kutosha toka kwa  kwa mabwana zao wanaowatuma waanzishe
migomo hiyo kila kukicha.


Maana aingii akilini mfanyaboashara anayeendesha biashara ya
duka lake kwa mkopo ,anatakiwa kila  baada ya muda fulani
akarudishe  marejesho, anadaiwa kodi ya pango akubali
kushiriki mgomo wa kugoma kufungua duka lake.

Maana Tanzania hivi sasa kila
kukicha inaibuka mitafaruku ya kutikisa nchi na kuacha
makovu hali inayosababisha nchi hii hivi sasa ya kuibua na
mitafaruku na siyo furaha tena.

Serikali nayo katika mgogoro huu wa
wafanyabiashafa ,haiwezi kukwepa lawama hii kwamba imekuwa
ikichelewa sana kuchukua maamuzi ya maana ambayo
yangesebabisha hawa wafanyabiashara kurudia kugoma goma.

Nimekuwa nikijiuliza maswali
bila majibu kwamba ni kwanini serikali inabembelezana sana
na wafanyabiashara hawa ambao tangu
  mwanzo wanavunja sheria za nchi na kusababisha wananchi
kukosa huduma na serikali kushindwa kupata mapato?

Je ni kwasababu baadhi ya
viongozi wa serikali nao wanamgongano wa kimaslahi yaani
wanatajwa wao binafsi ,familia zao kumiliki maduka katika
maeneo hayo kama Kariakoo?

Maana aiingii akilini serikali yoyote ambayo
kamwe haipotayari kuona inakoseshwa kupata mapato yake na
wahuni wachache yaani hawa wafanyabiashara halafu iendelee
kuwakumbatia  na kuwa kenulia meno.

Hawa wafanyabiashara wamekuwa na jeuri  kila
wanapojisikia wanagoma  kwasababu uenda  wanadhani  serikali
hii ni 'mhuni' mwenzao haiwezi kuwafanya chochote na
ndio maana hata jana tumeshuudia madereva wa daladala kule
mjini Songea Mkoani Ruvuma nao waligoma utoa huduma kwa
madai kuwa wanaunga mkono mgomo wa wafanyabaishara na
wanashinikiza Minja aachiliwe huru.

Huu  mi nasema ni wazimu unaofanywa  na hao
wenye madaladala na wafanyabiashara kwani
  kadri siku zinavyozidi kusoga mbele ndiyo mnavyodhiirisha
huu siyo mgomo wa wafanyabiashara bali wafanyabiashara hao
na madereva hao wa madaladala wanatekeleza kwa vitendo
maelekezo ya wanasiasa uchwara ambao mara kwa  mara wamekuwa
wakijiapiza nchi haitatawalika na kuiosesha mapato
serikali.

Watu wenye akili
timamu na wachunguzi wa  mambo tumelibaini hili.

Nawashauri wafanyabiashara
mnaogoma  acheni kugoma rudini mfanyekazi na kama kweli
mnafiriki mnamadai ya msingi basi fuateni njia utaratibu wa
kisheria na kiungwana kudai madai yenu na siyo njia hii ya
kihuni na kidhalimu mnayofanya.

Hao wanasiasa  wanaowatumia minawafananishaga
na  Maibilisi kwani nyie siyo watu wa kwanza kuwatumiwa
kutekeleza ajenda zao chafu  ambazo mwisho siku mtaumia nyie
siyo wao.

Kawaulizeni
baadhi ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Madaktari,wakazi wa
Mtwara kuzuia bomba la gesi lisijengwe, baadhi ya  wahitimu
wa JKT .

Wanasiasa
  hao wenye tabia za kishetani waliyatumia makundi kikamilifu
na mwisho wa siku makundi hayo ndiyo yaliyoathirika wale
vinara wa JKT wapo gerezani, yule kinara wa mgomo wa
madaktari kilichomkuta sote tunakifahamu nakilichowakuta
wale baadhi ya wakazi wa Mtwara waliokuwa wakileta vurugu
kuhusu bomba la gesi lisijengwe kilichowafika sote
tunakifahamu na sio wanaisasa hao.

Bila shaka na nyie wafanyabiashara  mnawashwa
mno mnaitaji mmpatiwe dawa ili muache kujikuna huo upelele
unaowawasha hadi unasababaisha mnavunja sheria za nchi kwa
makusudi na mtapatiwa dawa na wenye uchungu na nchi hii kama
msipoacha huo uhuni wenu wa kuikosesha  mapato serikali na
kutusabishia wananchi tukose huduma.

Sasa na nyie wafanyabiashara mnachokitafuta
mtakipata kwasababu ushahidi uliopo wazi mmevuka mipaka sasa
na mna ajenda  chafu nyuma pazi ya mgomo wenu siyo  mashine
ya EFDS na huo ndiyo
  ukweli mchungu
fungueni maduka mfanyebiashara kama biashara
  imewawashinda fungeni maduka ingieni kwenye ulingo wa siasa
tuwajue kuliko kucheza na uchumi wa taifa letu kwa sababu za
kipuuzi tu.

Kama kweli
Tanzania ni taifa linalotaka kupiga  hatua za kimaendeleo
kweli ,minashauri nyie wanasiasa uchwara wetu acheni tabia
zenu chafu za kuingiza siasa zenu chafu katika masuala ya
uchumi,mnaangamiza taifa kiuchumi kwa akili zenu mbovu na
tamaa zenu za madaraka kwa kuuingiza siasa chafu katika
mambo nyeti kama masuala ya uchumi,amani na usalama wa taifa
letu.

Na serikali iache
tabia ya kulealea ushetani huu kwa kuacha madhara yasambae
ndiyo iibuke usingizini ijifanye inaanza kuchukua hatua.Ina
kera sana.

Mungu ibariki
Tanzania

Chanzo: Facebook:
Happy Katabazi
Blogg:
www.katabazihappy.blogspot.com
0716
774494
Aprili Mosi Mwaka
2015.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment