Tuesday, 21 April 2015

Re: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - MIGOGORO NDANI YA CHADEMA

Mabadiliko chadema....hili andiko ni la nani?

On 21 Apr 2015 13:23, "MABADILIKO CHADEMA" <mabadilikochadema@gmail.com> wrote:

NAACHANA NA SIASA ZA KIHAFIDHINA ZA CHADEMA

Wakosoaji wangu mara kadhaa wamenitaka kuonyesha upande niliopo kisiasa sijui ni kwanini lakini kwa mwenendo wa comments zao inaonekana ni kwa kutaka kujua namna watakavyokuwa wanajibu hoja zangu. Inaonekana kwao hoja sio issue, issue ni uko upande gani. Mwanzoni sikuona swala hili kama ni la msingi kwa kuwa mimi naamini nchi haijengwi na chama kimoja. Nikawa tayari na bado niko tayari kuunga mkono wazalendo wa kweli kutoka vyama vyote ikiwemo CCM, Chadema, CUF, NCCR, ACT n.k. Nitapinga siasa zote zenye lengo la kufifisha demokrasia, ubinafsi na zisizolenga mabadiliko ya kweli. Hivi karibuni nimejaribu kuungana na wote ambao kwa gharama yoyote ile tulitaka kuona umoja zaidi katika vyama vya upinzani na sio ubaguzi. Juhudi hizi zimekwama kwa kuwa tu eti viongozi wakuu wa Chadema na wafuasi wao hawataki! Mwenendo wa Chadema makao makuu kwa siku za hivi karibuni umegubikwa na sura kuu mbili:

1. Kuzimishwa kwa demokrasia ambayo ndio msingi mkuu wa chama. Lipo genge linalokubaliana nje ya mfumo rasmi wa chama juu ya nani wawe viongozi wakuu wa chama na kuleta kwenye vikao vya chama kama utaratibu tu. Ukitofautiana na genge hili basi utaitwa msaliti. Demokrasia ndani ya chama inataka watu wote kupewa haki sawa katika kugombea uongozi, kuchujwa kwa vigezo na watakaopita mchujo kupigiwa kura. Demokrasia haiwapi haki viongozi wakuu waliopo kukaa pembeni na kukubaliana nani wawe viongozi na kutaka wote tufuate hivyo, hii ni kwa sababu dhana hii inaleta mgongano wa kimaslahi. Kwa mfano Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Wakurugenzi wa makao makuu ni rahisi kumpendelea Mwenyekiti aliyepo (aliyewapendekeza/aliyewateua) kwa kuwa kuchaguliwa kwake ni kujihakikishia kuteuliwa kwao tena. Huku ni kulindana na kunakinyima chama fursa ya kutumia vipaji bora zaidi vilivyopo ambavyo bado vipo nje ya utawala wa uliopo. Pili inaleta hofu na woga kwa wanachama na hivyo wanachama wenye mawazo mbadala hukaa kimya na mawazo yao mwisho wa siku chama kinakuwa na ufinyu wa mawazo.

2. Ajenda ya Mabadiliko ndani ya Chadema haina nguvu tena! Ajenda imekuwa ni fitina dhidi ya mtu au watu, hoja ya USALITI ndio ajenda kuu ya Chadema. Na hapa kuna dhana mbili, ya kwanza ni waraka wa mabadiliko wa akina Kitila Mkumbo unaoitwa mpango wa mapinduzi, wenye akili waliishajibu kuwa hakuna mapinduzi kwenye uchaguzi utakaopigiwa kura. Pili ni propaganda kuwa Zitto Kabwe alinunuliwa na CCM, hili formaly hali exist kwa kuwa hakuna kikao au ngazi yoyote ndani ya Chadema ambapo Zitto aliwahi kutuhumiwa, kushitakiwa au kuhukumiwa juu ya jambo hili, kimsingi halipo kwenye chama. Ni wahuni tu walilianzisha baada ya kuona hoja yao ya waraka wa kimapinduzi haina mashiko.

Mimi naamini demokrasia ya kweli ndani ya chama ni ishara ya kutupa uhakika kuwa hata chama hicho kikishika dola nchi itakuwa na demorasia ya kweli, uhuru na haki za wananchi vitalindwa, uchaguzi huru na wa haki, uwazi katika shughuli za serikali n.k. Kufifisha demokrasia ndani ya chama ni ishara ya wazi kuwa chama hicho kikishika dola kitafifisha pia demokrasia ndani ya nchi.

Wananchi wetu wapo katika hali ngumu, hali ya umasikini wa kipato, hudumu za kijamii bado haziridhishi, safari ya utawala bora bado ni ndefu, n.k. Hoja ya mabadiliko lazima ituonyeshe masuluhisho juu ya masuala hayo niliyoyataja, chama kinapoimba tu mabadiliko kama ngonjera tu bila kutuonyesha mipango ya masuluhisho haitoshi. Labda kikishinda ndio kutakuja na mpango, sawa lakini sasa hii siyo ajenda kuu cha Chadema, ajenda imekuwa ni propaganda juu ya mtu. Huku ni kutoka kwenye hoja iliyokifanya kuwa chama kikuu cha upinzani. Tuelewe lengo sio kushinda uchaguzi eti tu kwa kuwa CCM imechokwa lah! Lengo ni kushinda kwa kuwa chama kina masuluhisho ya matatizo yaliyopo.

Nawatambua makamanda wengi waliovuja jasho kuijenga Chadema na Tanzania kwa dhamira ya kweli, katika masuala ya kujenga nchi bado tupo pamoja kama nilivyo pamoja na wazalendo bila kujali vyama walivyomo. Katika siasa za vyama naachana kabisa na siasa za Chadema, siasa za propaganda, siasa za kukumbatia madaraka kwa hila, siasa za kuua demokrasia, siasa za kificho kificho, siasa za majungu fitina na matusi.

Mwisho, nitamke wazi kuwa tangu sasa nafuatilia kwa karibu siasa za ACT – Wazalendo. Asanteni.



On Wednesday, March 11, 2015 at 7:00:48 PM UTC+3, Abdalah Hamis wrote:
Name:  DSCN4996.JPG  Views: 0  Size:  53.2 KB


Aliyekuwa mlinzi binafsi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. WILBROAD SLAA kwa jina la Khalid Kangezi leo ameibuka na kukanusha taarifa zilizotolea na chama chake kuwa alikuwa anakula njama za kumuua katibu mkuu huyo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma za wazi ndani ya chama hicho.

Akizungumza kwa uchungu ndani ya ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari leo, amesema kuwa kilichotokea hakijui ila anashangaa kuwa chama kimeamua kumtenda na kumpiga sana wakimtuhumu kutaka kumuua kiongozi huyo jambo ambalo amesema kuwa ni la kushangaza na halina ukweli wowote ule.

Name:  DSCN5006.JPG  Views: 0  Size:  43.8 KB


Amesema kutokuelewana kwake na Katibu Mkuu wa chama hicho kulianza pale alipoanza kupishana kwa maneno kati yake na mke wa Dk. Slaa ambapo Slaa alimuamuru aende kwa mke wake akamalize ugomvi wake na mke wake ndipo aendelee na kazi jambo ambalo amesema kuwa alishangaa kuwa hakuwa na ugomvi na mke wa Dk. Slaa na hakuweza kufanya hivyo.

Amesema kuwa siku ya Jumamosi aliitwa Makao Makuu ya chama kwa mualiko kuwa kuna kikao maalum na mwenyekiti wa chama hicho na alipofika aliingizwa chumbani ambapo aliwakuta vijana watano wa chama hicho ambao amewataja kwa majina na bila kumjuza kitu chochote walianza kumpiga mateke, kumtesa, kumvua nguo, kumwagia maji huku wakimtuhumu kuwa amepewa sumu na viongozi wa chama cha CCM ili amuue katibu mkuu dk. Slaa.

Name:  DSCN5015.JPG  Views: 0  Size:  27.6 KB


"Jamani hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uwongo wa hali ya juu na wanataka kunichafua kwa jamii, tena niseme ukweli chama hiki kinataka kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea."

"Ni kwamba mimi nimekuwa mlinzi wa Slaa kwa muda wa miaka mingi sana, tena mimi nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua huo ni unafiki" amesema Kagenzi

Katika Jambo la kushangaza Mlinzi huyo amefichua mipango ya kitesaji na kigaidi inayofanya na CHADEMA huku akisema wameandaa ofisi ya utesaji.

"Jamani hiki chama ambacho kina ndoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia? Maana wameniteka na kunifungia kwenye chumba cha utesaji wanachomiliki wao wamechoma visu na kuweka kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote, eti wakinishinikiza mimi nitaje wanaonituma, jamani nawaambia mimi hanitumi mtu" ameedelea kusema Kagenzi.

Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho huku akisema kwenye mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze hata nguvu za kiume .

Alibanisha kuwa hata alivyokuwa mlinzi wa Dokta Slaa kwa miaka mitano zaidi alikuwa analipwa malipo madogo ya Laki tatu kwa mwezi lakini anasema kuwa hakuandaa mipango ya yoyote ya kumuua,lakini anashangaa kwanini leo wanamsingizia kiasi hicho kwani amedai kuwa kama angekuwa anataka kufanya vitendo vya kukisaliti chama angefanya huko nyuma.

Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa

Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo zinazosemwa kwani hata simu yake haina salio ya pesa na haijawahi kupokea pesa hizo. 

Hatua atakazochukua


Kagenzi amesema hatua iliyobaki sasa hivi ni kwamba tayari ameshahojiwa na jeshi la Polisi na kilichobaki sahivi ni kusubiri kesi mahakamani ili kukishtaki chama hicho kwa Vitendo walivomfanyia navyodai ni vya kiuaji.


On Saturday, November 22, 2014 at 7:22:55 AM UTC-8, Fred Hans Kipamila wrote:
Jabir,
huu si unafiki tu bali ni hofu ya muungano ambao haukutegemewa


From: 'jabir yunus' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com>
To: "wana...@googlegroups.com" <wana...@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, November 18, 2014 11:00 PM
Subject: Re: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - MIGOGORO NDANI YA CHADEMA

Ni walewale - WANAFIKI na WAFITINI.

Unafiki ni mbaya na dhambi kubwa kwa sabb lazima mtu anatumikia watu wengine. Hawa wanatumwa sehemu. Ndo kusema wanakula haramu huko wanakotumwa!

They can go to hell.
 

From: Reginald Miruko <rsmi...@gmail.com>
To: wana...@googlegroups.com
Sent: Tuesday, November 18, 2014 8:28 PM
Subject: Re: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - MIGOGORO NDANI YA CHADEMA

Divide and rule
On Nov 18, 2014 8:25 PM, "MABADILIKO CHADEMA" <mabadili...@gmail.com> wrote:
JUU YA USHIRIKI WAKE KWENYE UCHAGUZI
 
UCHAGUZI MKUU WA 2015 KUPITIA UKAWA
 
 
UTANGULIZI:
 
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni mwamvuli wa kisiasa ulioasisiwa na vyama vitatu ambavyo ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha NCCR Mageuzi. Baadaye chama cha NLD kimejiunga kwenye UKAWA na hivyo kufanya jumla ya vyama vinavyounda umoja huu kufikia vinne. Lengo la awali la mwamvuli huu lilikuwa ni kuwa na sauti ya pamoja katika kutetea na kusimamia Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba kwenye Bunge Maalum la Katiba tarehe 18 Machi 2014. Msukumo wa kutetea Rasimu hiyo umetokana na kubeba matakwa ya CHADEMA na CUF kuhusu muundo wa muungano ambapo Rasimu imependekeza muundo wa Serikali tatu ambao ndio pendekezo la vyama hivi. CHADEMA inaamini kuwa ikiwa muundo wa serikali tatu utapita, itakuwa ni rahisi kushinda uchaguzi wa Tanzania Bara ambako ina wafuasi wengi huku CUF nayo ikiwa na matumaini ya kushinda Zanzibar ambako imeota mizizi kutokana na sababu zinazofahamika. Kwa hali hiyo, hata kama CCM inaweza kushinda uchaguzi wa Muungano, hawatakuwa na mamlaka Zanzibar wala Tanzania Bara na hivyo kuwafanya wapotee kabisa kwenye siasa za Tanzania.
 
 
Baada ya jitihada za kutetea Rasimu hiyo kugonga mwamba kutokana na CCM kutuzidi ujanja na wingi wao bungeni ulitufanya tushindwe kwenye kila hatua ya bunge hilo, CHADEMA tumefanikiwa kubadili mwelekeo wa UKAWA na tumefanikiwa kushawishi vyama washirika kuendelea kubaki ndani ya mwamvuli wakati tukielekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kabla ya uchaguzi Mkuu, kutakuwa na Kura ya Maoni kupitisha Katiba inayopendekezwa ambayo tunaamini kuwa CCM watashinda. Hata hivyo, CHADEMA itaendelea kuwashawishi vyama vingine kuendelea kubaki ndani ya UKAWA kwa madai ya kupiga kampeni ya kura ya HAPANA ilhali CHADEMA ikitumia mwanya huo kujijenga kisiasa.
 
kwenye mchakato wa Katiba Mpya na hapana maoni UKAWA tutashindwa, nguvu kubwa ya CHADEMA kupitia mwamvuli wa UKAWA ni kwenye uchaguzi wa Serikali za
 
Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kwa mujibu wa Makubaliano ya UKAWA ambayo yalisainiwa tarehe 26 Oktoba 2014 kwenye viwanja vya Jangwani Dar es Salaam, vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR na NLD tumekubaliana kusimamisha wagombea wa pamoja kwenye nafasi zote. Mpango wa namna ya kuwapata wagombea ambao kwa kiasi kikubwa umeratibiwa na CHADEMA umekamilika na umesambazwa kwa vyama washirika. Hata hivyo, pamoja na makubaliano hayo, Mkakati wa CHADEMA ni kuhakikisha kuwa inasimamisha wagombea wengi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu kuliko vyama washirika wa UKAWA huku ikihakikisha kuwa nafasi ya mgombea Urais inaangukia kwa CHADEMA.
 

HALI YA KISIASA NDANI YA UKAWA KATIKA KIPINDI CHA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU
 
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika tarehe 14 Desemba 2014 na uchaguzi Mkuu umepangwa kufanyika Oktoba 2015 ambapo CHADEMA imekubaliana na vyama washirika wa UKAWA kusimamisha wagombea wa pamoja. Kikosi Kazi kilichoandaa mkakati huu kimetafakari kwa kina faida na hasara za maamuzi haya kwa CHADEMA kwa kuzingatia mazingira ya sasa na ya baadaye ya kisiasa ndani ya umoja huu. Kwa ujumla mambo yafuatayo yamebainika;
 
1.     Vyama vinavyounda UKAWA ni 'Regional and Tribal Based'. Chama cha NCCR Mageuzi kina wafuasi wengi Mkoa wa Kigoma tu. Hali hii inafanya chama hicho kuwa ni cha Kigoma na baadhi ya watu wanakiita kuwa ni chama cha Waha ijapokuwa kinaongozwa na Mwenyekiti asiye na asili ya Kigoma. Kwetu CHADEMA hii ni advantage kwani tutaweza kukidhibiti chama hicho kuenea katika mikoa mingine. CUF, ni chama kilichoshika hatamu kisiwani Pemba kutokana na sababu za kidini na historia ya Zanzibar. Kwa upande wa Tanzania bara, CUF imejipenyeza kwenye mikoa ambayo ina waumini wengi wa dini ya kiislam kama Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Tabora. Hii pia ni advantage ya CHADEMA kwani ukiondoa mikoa hiyo, CHADEMA ina nafasi ya kusambaa maeneo mengi na UKAWA kuongeza idadi tu ya vyama na kwa vile hawapo kwenye 'vita' ya kugombania
 
wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye chaguzi.
 
2.    Hali ya ndani ya CHADEMA bado haijakaa sawa baada ya maamuzi ya kuwavua uanachama Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba pamoja na maamuzi ya kumvua vyeo vyote ndani ya chama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, ZITTO KABWE ambaye kwa sasa anaonekana kujiimarisha na kujizolea umaarufu kupitia sakata la ''ESCROW ACCOUNT''. Baadhi ya wafuasi wengi wa CHADEMA wamepoteza imani na chama na wengine wameamua kujiunga na chama kipya cha ACT huku wengine wakirejea CCM. Hali hii ni ishara mbaya na ina 'impact' kubwa kisiasa.
 
3.    Aliyekuwa mgombea wa CHADEMA kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, DK WILBROAD SLAA ameendelea kushuka umaarufu kisiasa kutokana na kuwa nje ya majukwaa ya kisiasa kwa muda mrefu. Hali hii inatokana na DK SLAA kutokuwa na nafasi yoyote ya kisiasa nje ya chama na hivyo kukosa fursa ya kushiriki mijadala ya kisiasa kama ile inayotokea bungeni. Aidha, umri wa DK SLAA ni kikwazo kikubwa kwake na kwa CHADEMA tunapoelekea mwaka 2015. Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE licha ya kuwa kwenye uwanja wa siasa kwa muda mrefu kutokana na kuwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hana sifa ya kugombea nafasi ya Urais kutokana na matakwa ya kikatiba hasa juu ya elimu ya mgombea. Suala la elimu limekuwa kikwazo kikubwa kwa MBOWE. Kwa upande Mwingine, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na wa CUF, JAMES MBATIA na PROF IBRAHIM LIPUMBA ni changamoto kubwa kwa chama chetu wakati wa kupendekeza mgombea Urais. Kikwazo kikubwa kipo kwa Lipumba ambaye anaonekana anataka ateuliwe kugombea nafasi ya Urais kupitia UKAWA.
...

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment