Wednesday, 10 September 2014

[wanabidii] KWANINI TPN au WANATAALUMA (WAS)ISITUMIKE KUHAMASISHA WATU KUFIKIRI NA KUTENDA MAMBO YA KIMAENDELEO?

TPN imegeuka kuwa uwanja wa siasa uchwara, ubao wa matangazo ya kupongezana pongezi za kihayawani kila kukicha! Watu wamejitoa akili na kupongeza mtu au watu fulani hata kama mtu au watu hao wamekohoa tu achilia mbali kuchemka! Na wakati huohuo TPN imechukuliwa kama mahali pa kulaani na kudhoofisha juhudi zozote zile za kuleta fikra za kimapinduzi na kimaendeleo!

Watu hao hao wanashikilia sehemu mbalimbali na nyeti kiuchumi na kielimu kwa maendeleo ya nchi hii. Ukichungulia CV zao ndio usiseme kwani mtu kama mimi wa elimu ya ngumbaro utaogopa hata kuwasalimu, achilia mbali kuongea chochote mbele yao. 

Lakini hizo sehemu nyeti walizozikalia zimejaa changamoto lukuki kupita maelezo! Ukihoji tu baaaasssii umewakanyaga kwani watakuparura! Watakwambia wewe una matusi, huna nidhamu, u mvivu wa kufikiri, u kipofu kwanini huoni maendeleo yote yaliyokuzunguka!! Unatumiwa na wapinzani! Wewe ni mpinzani, unawaonea wivu, Unazitaka nafasi zao, Wewe ni mtu wa kulalamika tu! Ni hulka ya watanzania kulalamika tu na siyo kutenda! Tukuone wewe basi unayejifanya unaakili sana kama utaleta lolote la maana! n.k, n.k, n.k.

Ukiwaambia wajiuzulu basi ili waingie wengine basi hapo patachimbika!

Ndugu zangu, kuhoji sio kulalamika au kutukana. Ni kuamshana tu. Ukiwa mwenzetu dereva na unatuendesha, hata kama sisi siyo madereva lakini ukisinzia tutajua kwamba hiyo siyo sehemu ya udereva na ni hatari kwamba utapinduka. Hivyo tukikuamsha usikasirike na kudhani kwamba tunakuona kama siyo dereva. Tunakuamsha ili sisi sote pamoja na wewe tufike salama huko tuendako!

Miezi miwili mitatu nyuma Dadaangu Rosemary alihoji hapa kuhusu mwenendo wa TPN kwani inaonekana kutofanya yale yaliyokusudiwa. Akajitokeza ndugu yangu mwingine sijui Alex yule na kujipalia makaa kwa kusema kuwa uongozi uliopo madarakani sasa hivi uliingia kwa lengo la kuinyonga TPN. ASALAAALEEE!!!!

Jambo hilo lilipoozwa na Dada zangu wenye busara na kulisawazisha. Kukatokea majadiliano namna ya kuiamsha tena TPN. Ikapendekezwa pia kama watu wako buzy sana ku-organize meetings basi majadiliano yafanyike hata kwa emails!

Tokea hapo sijajua kama kuna kilichoendelea kwani inawezekana majadiliano yamekuwa hayanifikii! Endapo ni hakuna basi niambieni kama la msingi hapa nini? Tuendelee kuweka maji mdomoni tusiseme au??

Malengo ya TPN ni yapi? Ni kupongeza wanasiasa? Kuwalaani madaktari na waalimu au hata Ukawa hata kama makundi hayo yana hoja za msingi ambazo ningetegemea jukwaa la wanataaluma  kuzichambua hoja hizo na kutoa ushauri unaofaa? Kutangaza michezo ya Simba na Yanga au sijui...?

Wakati uongozi huu ukiomba kupigiwa kura ulimwaga CV za nguvu sana. Rafiki yangu mmoja aitwaye Apollo T.  alitoa maoni positive sana kwa kusema, "...if those CVs are put into use, they are a treasure!

Hivi Uongozi wa TPN, tukisema kwamba your CVs have not been put into use tutakuwa tunawaonea au kuwatukana? au ukweli unauma? Hata hivyo kwa maoni yangu, I see your CVs working against the interest of TPN, and its "real members". Mmeuwa kabisa mioyo ya watu

Ninaungana na Alex kusema kwamba uongozi huu una lengo kinyume na matarajio ya wana TPN halisi. Nasema hivyo kwa sababu CVs (unless zilikuwa ni feki) zinaonyesha uwezo mkubwa wa kiuongozi lakini results ni -ve.

Kama ni kuwa busy na majukumu mengine basi ningetegemea kuwa mngetujulisha kuwa mna changamoto ya kukosa muda kutokana na majukumu mengine na au mngeachia ngazi! Sasa ngazi hamuachii, Ubao wetu mnautumia kwa matangazo yenu wenyewe na binafsi! tuwaeleweje?

Badala ya kulalamika kwamba sisi tunalalamika au tuanwatukana, you should justify your inaction!

Ndugu zangu, ninasema haya si kwa kumaanisha kwamba mimi naweza kuongoza, lahasha. Kama ni suala la uongozi ninahitaji kujifunza kwanza ndipo nije niongoze. lakini nadhani hata ndani ya nyumba kama baba au mama au wote hawawajibiki kwa watoto, watoto wanaweza kuliona hilo na kama hawaogopi kufokewa wanaweza kuwaambia wazazi mapungufu yao. lakini haina maana ya kwamba watoto watakuwa wanataka kuchukua nafasi ya baba au mama.

Nchi yet imefika mahali pabaya sana. Na kama sisi wana TPN tulijibatiza na kujiita wanataaluma wa nchi hii basi tunapaswa kuanza kufikiria na kutenda. Vinginevyo tunatoa taswira mbaya hata nchi za nje. Yanayoendela hapa kwa njia ya mtandao huwa yanaweza yakawafikia hata watu wa mataifa mengine. Fikiria kama TPN ambayo ungetarajia iwe Think Tank lakini ndiyo hiyo inafuka moshi mweusi kama injini iliyonoki, wenzetu watatudharauje?

Nchi nzima inaenda hovyo, inayumba. Uongozi haujui ufanye yepi ya kipaumbele. Ukikosolewa unakuwa on self defense. Majirani zetu au watu wa mbali wakisema jamani mmekaa vibaya inakuwa ayaaa! Mnatutukana, mnatuonea gere, mnatuonea wivu, mtuombe radhi... ayyyiii, jamani! Si tukae chini tukajiuliza kidogo lakini, kwamba kwanini hawa jamaa wanasema tumekaa vibaya? kwanini wanasema serikali yetu ni corrupt?

Tujichunguze tuone kama kweli ni wivu tu au kipo kitu. kama ni wivu lakini pia kuna ukweli, hakuna haja ya kuwajibu watutukanao kwa maneno, ila kwa vitendo, kwa kurekebisha yale madhaifu yetu. Tusipige kelele ila tuamke taratibu na kufanya marekebisho kimya kimya na kuongeza speed ili hata hao wanaotucheka waje siku moja washituke kukuta tumeshawapita.

Wapo watakaosema mimi sina nidhamu au nina mdomo chafu, au mikono michafu sijui! Nakubali mnihukumu vile mtakavyodhirika. Lakini pia nawaomba mtafakari haya niyosema hapa pamoja na waliyokwishasema wenzangu huko nyuma. Hat mjinga akiongea huwa anaweza akabahatisha moja la maana na kumuokoa mwerevu.

Lakini kwa upande mwingine pia, Uongozi wa TPN uko saihihi kusema kuwa sisi ni wakulalamika tu kwani SISI sote tunasemaje? TPN tunasemaje? Tunachukua hatua gani kama kweli nasisi tuna nia ya dhati ya kuleta mabadiliko? tunakubali kupotoshwa? Tutafakari!

Miezi mitatu ilyopita Kakaangu Bubelwa Kaiza alishaleta topic nyeti sana hapa ihusuyo Mikataba ya Madini yakiwemo mafuta na gesi. We didn't say anything about it. I think it is time we should dig it out and discuss. Uzuri wake naamini wapo wanaoweza kutupatia majibu ya kutuelewesha kinachoendelea.

Kwa kumalizia yangu machache, nawaomba msome habari iliyopo hapo chini na tutafakari kimya kimya lakini kwa kushea mawazo.


Vipaumbele kwa mtazamo wangu: 

1. RUSHWA, RUSHWA, RUSHWA, UFISADI, UFISADI UFISADI. Bila kutokomeza hayo basi nchi imeangamia na haitaamka tena. Ufisadi haupigwi vita kwa maneno na porojo au kutishia kutaja majina. Utauangamiza kwa vitendo. ACTION.

1. UWAJIBIKAJI, UWAJIBIKAJI UWAJIBIKAJI. Huyu ni mjombaake Rushwa na ufisadi. Madhara yao hayana tofauti.

1. ELIMU, ELIMU ELIMU. Siyo kwa tu kwa kujenga madarasa. KWA KUWALIPA WALIMU VIZURI. Ukipata walimu wazuri na motivated, hata kama wanafundisha chini ya muembe ujue utapata taifa la nguvu.

1. AFYA, AFYA, AFYA. Watu wakiwa na afya nzuri watakuwa efficient katika mambo yote.


Karibu hapo chini. observe the highlihts.


  US$ 110.54b secured for the Mombasa–Bujumbura highway
 

US$ 110.54b secured for the Mombasa–Bujumbura highway

Highway Mombasa-Bujumbura
A highway: the Mombasa – Bujumbura highway will stretch 1550 – kilometers and will connect the Central Corridor to Tanzania
The African Development Bank (AfDB) has given Kenya a loan worth US$ 110.54b to construct Mombasa–Bujumbura highway that will link Kenya and Rwanda.
Branching off the Northern Corridor at Voi, the Mombasa–Bujumbura highway will stretch 1550 kilometers. The road will also connect the Central Corridor to Tanzania at Moshi. It will also cross Arusha and Singida, on its way to Bujumbura.
The highway will be shorter than the Northern Corridor by 455km. The Northern Corridor will run from Kenya to Burundi, passing through South Sudan, Congo and Rwanda.
The Mombasa–Bujumbura highway will also be shorter than the central corridor by 50 km. The latter runs from Congo to Tanzanian port of Dar es Salaam, through Uganda, Rwanda and Burundi.
The connection of Rwanda to the port of Mombasa through the Mombasa–Bujumbura highway will facilitate quicker transport and movement of commodities, because, according to the Burundi's Chamber of Commerce Secretary–General Christian Nkengurutse, the Mombasa port is more efficient in capacity and clearance than the Dar port. This will make it better than the Central Corridor.
The contractors will be selected by end of November this year since the evaluation process was still ongoing, according to Deusdedit Kakoko, the Tanzania Roads network Agency's Arusha regional manager.

0 comments:

Post a Comment