Nimekusoma vizuri na mimi pia jana nilimsikia Mzee Cheyo akiongea kuhusu suala hilo. Kwa mawazo yangu, kwa mara nyingine tena, UKAWA au vyama vya upinzania wamefanya kosa. Sina hakika wanapokwenda katika majadiliano haya, huwa wanajipanga namna gani? na sina hakika kama huwa wanapata ushauri wa kitaalamu na mikakati na pia sina hakika huwa wanajaribu kufikiria kilichoko nyuma ya pazia na hasa hidden agenda ya CCM.
Kwanza, ilikuwa ni makosa majadiliano haya kuyafanya chini ya mwamvuli wa TCD hasa ukizingatia kuwa Mwenyekiti wa TCD ni Cheyo. Hivi Cheyo ana chama kweli? Makao makuu ya chama chake yapo wapi? hivi anaweza kuonyhesha ofisi za chama chake angalau japo katika mikoa mitatu? hivi ukiachia yeye na ndugu yake Issac, uogozi mwingine wa UDP ni upi? Kwa hiyo, hapa ni changa la macho, ni wazi kuwa Cheyo anatumika, na hilo Chadema, CUF, na NCCR walitakiwa kulijua. Cheyo anachotaka ni status, heshima na kupata attention katika media tu. He is not a serious man with principles. Hilo ni kosa la kwanza.
Pili, it was a mistake, kukubali kuwa Bunge liendelee hadi October 4. Hili nalo ni kosa. Ilitakiwa msimamo wa UKAWA uwe ni kuwa mchakato usimamishwe immeaditely na hasa Bunge maalumu la katiba. HIvyo basi wangeaangalia ni utaratibu upi ungweze kutumika kulisimamisha Bunge. Na wangekuja na proposala ya kitu chani kifanyike kusimamishe BUnge maalumu la katiba. Na kama CCM wasingekubali, basi majadiliano ingekuwa vyema yakavunjika, na wakatoka bila kukubaliana.
Kutokana na hilo, si kweli kwamba eti katiba mpya ni mpaka 2015, hapana la hasha, hapa pia ni changa la macho. Kilichoahirishwa mpaka 2015 ni kura ya maoni. Hyo maana yake nini? maana yake ni kuwa katiba itapatikana october 4, na Bunge litavunjwa na hakutakuwa na haja tena ya kuwa na Bunge.
Uamauzi wa kuifanyia marekebisho katiba ya 1977 ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki:
Kwanza, huwezi kuwa na uchaguzi huru na wa haki eti kwa kuunda tume huru ya uchaguzi, kuruhusu mgombea binafsi, mshindi kupata zaidi ya 50%, kuruhusu kupinga matokeo ya uchaguzi tu. Haya mambo ni muhimu lakini hayawezi kutupa uchaguzi huru na wa haki. Huwezi kuwa na uchaguzi huru na wa haki bila kufanya mabadiliko makubwa ya kubadilisha mfumo mzima wa utawala ambao hautenganishi chama tawala na serikali. Kwa maneno mengine, serikali ndio chama tawala na chama tawala ndio serikali. Watendaji, watumishi wa serikali, taasisi mbalimbali, vyombo vya usalama, mamalaka za wilaya, mikoa, zote hizi zinahakikisha kuwa mgombea wa chama tawala anashinda. Huwezi kuwa na chaguzi huri katika mazingira ambayo huna taasisi huru na zenye nguvu na madhubuti, huna mahakama huru, huna jeshi la polisi huru, jeshi huru, UWT huru n.k. Huwezi kupata uchaguzi huru katika mazingira haya.
Pili, ni serikali hii ya CCM ndio itakayoandaa muswada na utajadiliwa katika Bunge hili hili ambalo majority ni CCM na bado hawataki kuona hegemony yao inaondoka. Againa watafanya cosmetics changes tu, hatutapata tume huru kama wanayofikiria. hata hayo mengine yanaweza yasipitishwa na tukaingia katika cuaguzi katika mabadiliko ambayo CCM ndio wanayataka.
2015 tutapiga kura ya maoni kwa katiba ambayo itakamilika october 4 ambayo itakuwa imechakachuliwa na wanajua watatumia mbinu na kila hila na hasa huko vijijini kuweza kupata kura za kuipitisha katiba ambayo wao wanaitaka ambayo waliijadili wao wenyewe katika BMK baada ya kuchakachua maoni ya Tume ya Warioba.
Huu ni mchezo na upo well chereogtaphed. Wenye akili wanaona.
Kwa mara nyingine opposition wameingia mkenge, ni monumental blunder.
Date: Thu, 11 Sep 2014 22:13:04 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Viongozi wa UKAWA waibuka na madai mapya tofauti na tamko la TCD!
From: mngonge@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Viongozi wa UKAWA waibuka na madai mapya tofauti na tamko la TCD!
Siku mbili kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kufikia Maazimio na Viongozi Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuhusu kulisitisha bunge Maalum la katiba baada ya tarehe 4/10/2014 na kupisha matayarisho ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo ya Mwaka 1977, kikundi kinachojiita umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA kimeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo mara moja na kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4, kwani kufanya hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa za Wananchi.Hayo yalisemwa jana jijini Dar Es Salaam na Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaounda kikundi cha Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakati wa mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la kujadili maazimio kati ya viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), na Rais Jakaya kikwete uliomalizika Juzi Ikulu ndogo mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Mandeleo Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa amesema anamshangaa sana Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa watanzania kwa kuzidi kuliruhusu Bunge hilo kuendelea hadi Oktoba 4 mwaka huu, kwani huko ni kupoteza pesa za watanzania kutokana na yeye Rais Kikwete wakati wa mkutano na Vyama vya hivyo vya Kisiasa alikibuliana nao kwamba Mwenendo wa Bunge hilo hauwezi kuleta Katiba Mpya.
“Mimi namshangaa jinsi Rais Kikwete anavyokubalia pesa za Watanzania zipotee bure kiasi hichi pasipo kuwa na Sababu maana leo hii mpaka octoba 4 ni siku ishirini na ukipiga hesabu za Wajumbe wote waliokuwa Bungeni kwenye Vikao vya Bunge gharama yake ya posho ni zaidi ya Bilioni 3.5 hurafu yeye mwenyewe Kikwete anakubali wazi katiba haitopatikana sasa, huku ni kuchezea pesa za wananchi kabisa maana ukweli huko wazi kabisa ndio maana tunamtaka sisi UKAWA alisitishe sasa bunge hilo ili fedha hizo ziende katika mambo mengine yenye tija”alisema Dokta Slaa,
Dkt. Slaa alizidi kusema anamshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa Watanzania kwani anakubalina na watu 600 kutoka kwenye Bunge la katiba na kuwapuuza watanzania Zaidi ya Milioni 40 ambao hata mlo moja kwa siku ni kazi.
“Huyo ni Rais gani ambaye anashindwa hata kuwaonea huruma Watanzania wanaoteseka tena hata kula mlo moja kwa siku ni kazi, yeye anakubaliana na wajumbe 600 kuteketeza pesa za Wananchi, hivi kweli ndio kiongozi huyu, kwa sababu kiongozi makini ni yule anayeangalia Fedha kwa ajili ya manufaa kwa wananchi wake” alizidi kusema Dkt. Slaa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema wao Ukawa wamepokea kwa moyo wote maamuzi waliyofikia ya kuifanyia marekebisho ya katiba iliyopo na kusema Bunge la katiba litakapoahirishwa, basi wakubaliane kimaandishi ili Rais mpya ajaye aendelee na mchakato huu na asiupuuze.
“Sisi ukawa tunakubaliana na kwa moyo wote maamuzi tuliyofikia katika mkutano na Rais Kikwete. Tunasema wazi tumekubaliana kuahirilisha mchakato huu. Tunataka tukubaliane kimaandishi ili Rais ajaye baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 aendelee na mchakato huu atutaki kabisa kusikia eti Rais anayekuja achukue maamuzi yake mengine. Hatutati kusikia ujinga huo”alisema Mbatia
Mhe. Mbatia ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, aliongeza pia na kusema, wao Ukawa wamefikia uamuzi kwamba, endapo Bunge hilo la katiba litakapoendelea baada ya uchaguzi mkuu, hawatakubali kuongozwa na mwenyekiti wa sasa, Samwel Sitta na kuzidi kusema Mwenyekiti huyo hana sifa ya kuliongoza bunge hilo kutokana na kuendesha siasa za chuki na ubaguzi.
Vilevile naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alisema wanamuomba Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kulikagua Bunge hilo la Katiba kwa madai bunge hilo lilitawaliwa na Ufisadi wa kutisha kutokana mipango yake hiyo.
“Kiukweli namuomba Mkaguzi Mkuu wa Serika alifanyie ukaguzi wa kimahesabu bunge hilo la katiba kutokana na Vikao vyake hivyo kutawaliwa na ufisadi wa kutisha tumeona leo Jinsi kila mjumbe mmoja kwa siku ametengewa bajeti ya chai ya shilingi 10,000 kwa siku tena chai ya asubuhi na jioni na hata bajeti ya vipaza sauti, vyote hivi ni matokeo ya Ufisadi ndio maana tunamtaka alifanyie ukaguzi wa kimahesabu” alisema Prof. Lipumba.
Katika Hatua nyingene Umoja huo wa Katiba wa UKAWA umeitaka tume ya Uchaguzi nchini ilifanyie marekebisho ya haraka Daftari la kudumu la wapiga kura ili liweze kuwaandikisha watanzania ambao hawajapata fursa ya kuandikishwa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment