Thursday 11 September 2014

Re: [wanabidii] Viongozi wa UKAWA waibuka na madai mapya tofauti na tamko la TCD!

Naona UKAWA wamekwishashutukia mission, kinachoonekana ni CCM kupitia TCD na mwenyekiti wake Cheyo wanafanya ujanjaujanja wa kuwaingiza kwenye mtego UKAWA na kuuhadaa umma ili kupunguza hasira zetu juu ya fedha zinazoliwa bure na hilo BMK wakati wakijua hakuna katiba wala nini.

Leo nimemsikia Cheyo akiripoti bungeni kwamba UKAWA wasikiuke makubalinao waliyofanya na mheshimiwa rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Hivi huyo Cheyo anaripoti hayo makubaliano kwenye BMK kwa sababu gani? Kwani alitumwa na BMK kuitisha kikao cha makubaliano hayo? Kama hiyo TCD ni taasisi yake ina uhusiano gani na BMK ? Ni UKAWA ipi anayoiambia huko BMK wakati akijua UKAWA hawapo katika ukumbi huo? Kama alikuwa na ushauri kama huo ni  kipi kilimzuia kuutoa siku alipokuwa na hao watu wa UKAWA au akaita press conference nje BMK?

Kimsingi dalili zote zinaonyesha huyu mheshimiwa (Cheyo) anatumiwa kinamna na tangu leo nawashauri UKAWA wajiepushe na huyu mwenyekiti wa TCD. Wakae peke yao na kuangalia mikakati mipya huu walioutengenezewa na Cheyo ni mtego wa panya. Ukimbie kama ukoma. UKAWA Shikiria msimamo wenu kwa umakini mkubwa wapinga dhuluma tuko nyuma yenu

2014-09-11 13:28 GMT+03:00 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>:

Viongozi wa UKAWA waibuka na madai mapya tofauti na tamko la TCD!
Siku mbili kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kufikia Maazimio na Viongozi Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuhusu kulisitisha bunge Maalum la katiba baada ya tarehe 4/10/2014 na kupisha matayarisho ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo ya Mwaka 1977, kikundi kinachojiita umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA kimeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo mara moja na kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4, kwani kufanya hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa za Wananchi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar Es Salaam na Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaounda kikundi cha Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakati wa mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la kujadili maazimio kati ya viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), na Rais Jakaya kikwete uliomalizika Juzi Ikulu ndogo mjini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Mandeleo Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa amesema anamshangaa sana Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa watanzania kwa kuzidi kuliruhusu Bunge hilo kuendelea hadi Oktoba 4 mwaka huu, kwani huko ni kupoteza pesa za watanzania kutokana na yeye Rais Kikwete wakati wa mkutano na Vyama vya hivyo vya Kisiasa alikibuliana nao kwamba Mwenendo wa Bunge hilo hauwezi kuleta Katiba Mpya.

"Mimi namshangaa jinsi Rais Kikwete anavyokubalia pesa za Watanzania zipotee bure kiasi hichi pasipo kuwa na Sababu maana leo hii mpaka octoba 4 ni siku ishirini na ukipiga hesabu za Wajumbe wote waliokuwa Bungeni kwenye Vikao vya Bunge gharama yake ya posho ni zaidi ya Bilioni 3.5 hurafu yeye mwenyewe Kikwete anakubali wazi katiba haitopatikana sasa, huku ni kuchezea pesa za wananchi kabisa maana ukweli huko wazi kabisa ndio maana tunamtaka sisi UKAWA alisitishe sasa bunge hilo ili fedha hizo ziende katika mambo mengine yenye tija"alisema Dokta Slaa,

Dkt. Slaa alizidi kusema anamshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa Watanzania kwani anakubalina na watu 600 kutoka kwenye Bunge la katiba na kuwapuuza watanzania Zaidi ya Milioni 40 ambao hata mlo moja kwa siku ni kazi.

"Huyo ni Rais gani ambaye anashindwa hata kuwaonea huruma Watanzania wanaoteseka tena hata kula mlo moja kwa siku ni kazi, yeye anakubaliana na wajumbe 600 kuteketeza pesa za Wananchi, hivi kweli ndio kiongozi huyu, kwa sababu kiongozi makini ni yule anayeangalia Fedha kwa ajili ya manufaa kwa wananchi wake" alizidi kusema Dkt. Slaa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema wao Ukawa wamepokea kwa moyo wote maamuzi waliyofikia ya kuifanyia marekebisho ya katiba iliyopo na kusema Bunge la katiba litakapoahirishwa, basi wakubaliane kimaandishi ili Rais mpya ajaye aendelee na mchakato huu na asiupuuze.

"Sisi ukawa tunakubaliana na kwa moyo wote maamuzi tuliyofikia katika mkutano na Rais Kikwete. Tunasema wazi tumekubaliana kuahirilisha mchakato huu. Tunataka tukubaliane kimaandishi ili Rais ajaye baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 aendelee na mchakato huu atutaki kabisa kusikia eti Rais anayekuja achukue maamuzi yake mengine. Hatutati kusikia ujinga huo"alisema Mbatia

Mhe. Mbatia ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, aliongeza pia na kusema, wao Ukawa wamefikia uamuzi kwamba, endapo Bunge hilo la katiba litakapoendelea baada ya uchaguzi mkuu, hawatakubali kuongozwa na mwenyekiti wa sasa, Samwel Sitta na kuzidi kusema Mwenyekiti huyo hana sifa ya kuliongoza bunge hilo kutokana na kuendesha siasa za chuki na ubaguzi.

Vilevile naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alisema wanamuomba Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kulikagua Bunge hilo la Katiba kwa madai bunge hilo lilitawaliwa na Ufisadi wa kutisha kutokana mipango yake hiyo.

"Kiukweli namuomba Mkaguzi Mkuu wa Serika alifanyie ukaguzi wa kimahesabu bunge hilo la katiba kutokana na Vikao vyake hivyo kutawaliwa na ufisadi wa kutisha tumeona leo Jinsi kila mjumbe mmoja kwa siku ametengewa bajeti ya chai ya shilingi 10,000 kwa siku tena chai ya asubuhi na jioni na hata bajeti ya vipaza sauti, vyote hivi ni matokeo ya Ufisadi ndio maana tunamtaka alifanyie ukaguzi wa kimahesabu" alisema Prof. Lipumba.

Katika Hatua nyingene Umoja huo wa Katiba wa UKAWA umeitaka tume ya Uchaguzi nchini ilifanyie marekebisho ya haraka Daftari la kudumu la wapiga kura ili liweze kuwaandikisha watanzania ambao hawajapata fursa ya kuandikishwa.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment