Hawa ni viongozi wa dini zipi,taarifa yao mbona haina kichwa wala miguu,waache upotoshaji,hayo wanayoyabadilisha wameyafanyia utafiti lini,mbona viongozi wa TEC,CCT,PCT wanaona tofauti na wao,shida hapa taarifa ya kutetea posho na si katiba,hii inaumiza mioyo yetu kuona katiba hata haijamilizika kutungwa ilshakataliwa tayari na wasomi,wanasiasa,Watanganyika na hata wazanzibar,wakumbuke historia inakwenda kuwahukumu.
'godfred mbanyi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
>Mmmh! Very interesting Utopian tale!
>
>--------------------------------------------
>On Wed, 9/3/14, 'Hamisi Nkuluzi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI BMK KUHUSU MWENEND WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "oldmoshi@gmail.com" <oldmoshi@gmail.com>
> Date: Wednesday, September 3, 2014, 10:05 PM
>
> Ukweli ni aibu kwa
> viongozi wetu wa madhehebu wala hawana maana kabisa , wapo
> kwa masilahi yao , kama walifuatilia midahalo kabla ya
> kuanza BMK wala hawangekuwa wanaendelea kuhudhuria. Pili
> hawa wanaojiita wakristo hivi wanapewa mamlaka na kutoka
> biblia ipi maana hawaruhusiwi kuapa lakini kwa kuogopa
> kaisari walikula kiapo ,wamesahau Daniel na wenzake
> walivyokuwa watii kwa sheria ya Mungu wa Israel hata kufa.
> Suala la kuapa halipo kuanzia kitabu cha mwanzo hadi ufunuo
> huwezi kulisoma. Wanisaidie hawa viongozi wa Dini ya
> Kikristo.kwa nini isiendelee tu katiba ya zamani kwani hata
> ingekuwa Tanganyika bado inahitaji viongozi waaminifu na
> waadilifu siku hizi waliopo madarakani ndio matajiri.
> Nadhani kama viongozi wanamuogopa Mungu aliyehai wangeacha
> kuendelea kula hela ya
> wanyonge
>
>
>
> On Wednesday,
> September 3, 2014 9:46 PM, 'Jovi kamuntu' via
> Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
>
> Ni aibu kuweka liwaya
> kama hii hapa. Soma mwisho
> BAKWATA KIKRISTO
> maana yake nini. Kutumiwa kubaya
> sana. Jovin
> Bifabusha
>
>
>
> DIRECTOR
>
> KWFF LTD
>
> P. O. Box 313
>
> Skype: jovin.bifabusha
>
> Karagwe, Tanzania
>
> +255 784 709200
>
>
> On Wednesday, September 3, 2014 9:26
> PM, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
>
>
> TAARIFA YA WAWAKILISHI WA
> TAASISI ZA DINI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA TOKA WAJUMBE 201
> KUHUSU MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA
>
> Sisi Wawakilishi wa Jumuiya
> na Taasisi za Dini, tuliopendekezwa na Taasisi zetu na
> baadaye kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
> Tanzania, baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuwa
> Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na kula kiapo cha
> utekelezaji wa jukumu hili kubwa.
> Tukiamini kuandaa Katiba Mpya
> kwa maridhiano ya Kitaifa kwa wananchi
> wote, tulipokea jukumu hili kama wajibu wetu Kitaifa. Aidha
> tunaamini kwamba katika kupata maridhiano ya Kitaifa ni
> muhimu kuheshimu kila wazo na fikra inayotolewa na
> kuunganisha fikra hizo kwa usahihi, kwa njia ya kidemokrasia
> kwa kupiga kura na kukubaliana na matokeo ya wengi.
>
> Kama ilivyoelezwa hapo awali,
> kabla ya kuanza shughuli za Bunge Maalum, kila mjumbe
> alikula kiapo cha kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya
> Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo wake na ufahamu
> wake, kufanya kazi zinazomhusu, bila upendeleo na kumuomba
> Mwenyezi Mungu amsaidie.
>
> Tumeshangazwa na kusikitishwa
> sana kuona kwamba mchakato wa kutayarisha Katiba
> itakayopendekezwa na Bunge hili kwa wananchi, unachafuliwa
> taswira yake. Bunge Maalum la Katiba linachafuliwa na,
> shughuli zake kuingiliwa na kupotoshwa na wajumbe wenzetu
> walio nje ya Bunge, Makundi, Taasisi na Vyombo mbali mbali
> vya habari, uhalali na ukweli wa shughuli za BungeMaalum la
> Katiba unapotoshwa. Wananchi wanaaminishwa yasiyo na
> ukweli.
>
> Upotoshwaji huu umezua
> mijadala mbali mbali katika jamii ya Watanzania na bado
> linaendelezwa kama ifuatavyo:
>
> 1. Kwamba Bunge Maalum la
> Katiba halina uhalali kwa kuwa hao wajumbe wenzetu
> walioondoka wameliondolea uhalali wake kwa vile hwapo,
> wakiwepo Bungeni basi uhalalai wake utakuwepo -
> utapatikana;
> 2. Inadaiwa kwamba Kanuni za
> Bunge Maalum la Katiba zinavunjwa ovyo ovyo;
> 3. Inadaiwa pia, kwamba kinachojadiliwa sasa
> katika
> Bunge hili ni Waraka mwingine na si Rasimu iliyotayarishwa
> na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyowasilishwa rasmi
> Bungeni na kuanza kujadiliwa na wajumbe;
> 4.
> Inadaiwa na watu na Taasisi mbali mbali, kwamba viongozi wa
> dini, wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na wajumbe wa Kundi
> la 201, wanapewa rushwa. Isitoshe Vyombo vya habari
> vimeandika tuhuma kama hizi.
> 5. Inadaiwa pia
> kwamba wajumbe waliomo katika Bunge hili ni wachache,
> ukilinganisha na hao walioko nje ya Bunge hilo;
> 6. Bunge hili, kwa tuhuma hizo, lazima
> lisitishwe au livunjwe na Mhe. Rais.
>
> Kabla ya kuanza kuusahihisha
> upotoshwaji huo, sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini mbali
> mbali na Wajumbe wa Kundi la 201 katika Bunge Maalum la
> Katiba, tunapenda kufahamisha umma wa Tanzania mchakato wa
> kutayarisha Katiba Mpya ulivyo kisheria.
>
> Tunapenda kuwafahamisha
> Watanzania wenzetu kwamba mchakato huu una hatua tatu kwa
> mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Mpaka hivi sasa ni
> hatua moja imekamilika. Hatua ya pili ndiyo inayoendelea, na
> hatua ya tatu bado haijaanza.
>
> Hatua ya kwanza ni ile ya
> uandaaji wa Rasimu. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya
> 83 iliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya kifungu
> cha tano cha sheria hiyo. Tume hii ilipewa jukumu la
> kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba,
> kuanisha na kuchambua maoni ya wananchi na kisha kuandaa
> rasimu ya Katiba. Kazi hiyo ilifanyika kwa kipindi cha
> takriban miaka miwili na hatimaye Rasimu ya Katiba
> ilikamilika.
>
> Hatua ya pili ilikuwa ni
> kuipeleka Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum la Katiba,
> ambalo liliundwa kwa shughuli maalum ya kuandika Katiba
> inayopendekezwa, ili ifikishwe kwa wananchi ambao wataamua
> waikubali au waikatae kwa kuwa wao ndio wenye maamuzi ya
> mwisho. Hawa ni Watanzania wote wenye uwezo wa kupiga kura
> kwa kutoa maoni yao. Hoja ya Mamlaka ya Bunge hili
> hatujazungumzia kwa vile imefikishwa Mahakama Kuu ya
> Tanzania ili kupata tafsiri sahihi ya mamlaka ya Bunge hili.
> Tunachoweza kusema ni kwamba jukumu kuu la Bunge hili ni
> kutengeneza Katiba inayopendekezwa na Bunge ili ifikishwe
> kwa wananchi waipigie kura ya maoni. Hatua hii ya pili bado
> inaendelea.
>
> Hatua ya tatu ni pale Bunge
> Maalum la Katiba tutamkabidhi Mhe. Rais Katiba
> inayopendekezwa ambayo itafikishwa kwa wananchi ili
> waikubali kama wataridhika nayo au kuikataa kama haikidhi
> matarajio yao.
>
> Hatua hii ni ya mwisho
> wananchi wakiikubali tunapata Katiba Mpya wakiikataa,
> tunaendelea na Katiba tuliyonayo.
>
> Kilichotokea ni kwamba,
> wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge hili wameamua kuukiuka
> utaratibu uliowekwa kisheria. Badala yake wamepeleka Rasimu
> ya Katiba kwa wananchi wakati mchakato wa kutayarisha Katiba
> inayopendekezwa bado haujakamilika.
>
> Sisi Wawakilishi wa Taasisi
> za Dini, ambao kuuhubiri, kuutangaza na kuusimamia ukweli ni
> moja ya majukumu yetu katika jamii, tumesikitishwa sana na
> taarifa potofu zinazosambazwa kwa
> makusudi na makundi, taasisi na vyombo vya habari mbali
> mbali na tukiwa wajumbe wa Bunge hili ambao tunafahamu kwa
> kina na tunaridhika na kila hatua ya mchakato huu. Tuna
> wajibu wa kusahihisha upotofu huu, unaoendeshwa kwa makusudi
> na hivi kuwaeleza Watanzania ukweli na hali halisi inayojiri
> hapa Bungeni. Watanzania msifadhaishwe na wala msibabaishwe.
> Hali ni shwari. Mchakato unaendelea kwa amani na utulivu.
>
> Katika kusahihisha upotofu
> unaozungumzwa kupitia mijadala na midahalo mbali mbali
> katika jamii, tunaomba kufafanua hali ilivyo kama
> ifuatavyo:-
>
> TUHUMA KWAMBA BUNGE MAALUM
> LA KATIBA KUKOSA UHALALI
> Jambo hili si
> kweli hata kidogo kwani kuna wajumbe wa aina tatu Bungeni
> ambao wamewekwa na kutambuliwa kisheria. Hawa ni kama
> wafuatao:
> 1. Wabunge
> wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
> 2. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
> Zanzibar.
> 3. Wajumbe 201 walioteuliwa na
> Mhe. Rais, baada ya kupendekezwa na Taasisi, Mashirika na
> makundi mbali mbali nchini,
> Uhalali wa Bunge unakuwapo
> wakati wajumbe kutoka makundi hayo matatu wapo Bungeni, na
> si Vyama vya Siasa pekee. Iwapo kwa mfano wajumbe wa 201
> wakiamua kutoshiriki katika shughuli za Bunge, basi sehemu
> moja muhimu ya Bunge haitakuwapo na uhalali wa Bunge
> hautakuwepo.
> Hata hivyo, Kanuni za Bunge
> Maalum la Katiba zimeweka idadi ya akidi ambayo ni nusu ya
> wajumbe wote wa Bunge Maalum. Akidi hii ikifikiwa Bunge
> huendelea na shughuli zake. Akidi hii hufikiwa kila wakati
> BungeMaalum linapokutana. Hii inamaanisha kwamba Bunge
> Maalum la Katiba linaendesha shughuli zake kwa misingi ya
> sheria na taratibu zilizojiwekea. Bunge lina uhalali wa
> kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria.
>
>
> TUHUMA KWAMBA KANUNI ZA
> BUNGE MAALUM LA KATIBA ZINAVUNJWA
> Suala
> hilo halijawahi kutokea. Kanuni za Bunge Maalum la Katiba
> zilipitishwa na wajumbe wote kwa mujibu
> wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sheria Namba 83. Vile
> vile uendeshaji wote wa shughuli za Bunge zinafanywa kwa
> mujibu wa Kanuni za Bunge Maalum. Kanuni hizo zinatoa fursa
> ya Bunge Maalum kuzirekebisha pindi inapobainika ipo haja ya
> kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni Namba 87.
>
>
> WARAKA MWINGINE
> UNAJADILIWA NA SI RASIMU YA TUME
> Hili
> nalo si kweli. Tunawahakikishia Watanzania wote kwamba sisi
> kama Wawakilishi wa Taasisi za Dini miongoni mwa wajumbe wa
> Kundi la 201, kwa ujumla tunasema hii si kweli. Ni
> upotoshaji wa makusudi. Tunaijadili Rasimu ya Tume ya
> Mabadiliko ya Katiba ibara
> kwa ibara. Ibara nyingi zimeachwa kama zilivyo. Kuna ibara
> ambazo zimeboreshwa au kurekebishwa, kuna ambazo
> zimeondolewa na kuna nyingine mpya ambazo zimewekwa ili
> kuweka mambo ya msingi ambayo Rasimu haikuyazingatia au
> haikuyaona.
>
>
> WAWAKILISHI WA TAASISI ZA
> DINI, WAJUMBE WA KUNDI LA 201 WA BUNGE LA KATIBA KUPEWA AU
> KUPOKEA RUSHWA
> Sisi Wawakilishi wa
> Taasisi za Dini na Wajumbe wa Kundi la 201 wa Bunge hili
> tumesikitishwa sana na taarifa hii iliyosambazwa na baadhi
> ya watu, na kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari aidha
> kupitia kwenye mijadala, midahalo na makongamano mbali
> mbali.
> Baadhi yetu sisi Viongozi wa Kiroho tumeapishwa viapo vya
> uadilifu katika uongozi wetu wa kiroho na tuko mstari wa
> mbele kuongoza waumini wetu kuepuka dhambi ya tamaa ya
> fedha, na kusema uongo. Taarifa kama hizo hazionyeshi
> heshima kwa dini au nafasi zetu za kipekee katika uongozi wa
> kiroho. Taarifa hizi zinatangazwa kwa makusudi na watu mbali
> mbali kupita vyombo vya habari kwa malengo ya kisiasa na
> kutudhalilisha sisi Viongozi wa kiroho mbele ya umma.
> Tunaomba tabia hii ikomeshwe.
>
>
> TUHUMA KWAMBA BUNGE KUWA
> NA WAJUMBE WACHACHE
> Hili nalo si kweli.
> Wajumbe wanaohudhuria Bunge wanakidhi
> akidi inayohitajika kwa mujibu wa kanuni.
>
>
> HOJA YA KUSITISHWA AU
> KUVUNJWA KWA BUNGE MAALUM
> Hii ni hoja
> inayozungumzwa katika mijadala mbali mbali katika jamii.
> Msingi wa hoja hiyo ni kutokuueleza umma ukweli ulioko
> Bungeni kwa kupeleka taarifa potofu kwa wananchi kwamba
> Bunge Maalum limekosa mwelekeo. Hatuoni sababu za hoja hii
> kutiliwa maanani kwa kuwa hakuna sababu za msingi na za
> kisheria za kufanya hivyo.
>
> HITIMISHO
> Kumekuwa na taarifa mbali mbali zenye malengo
> ya ama kuingilia shughuli za Bunge hili au kutudhalilisha
> sisi wajumbe ambao si Wabunge au Wawakilishi. Wajumbe 201,
> ambao mchango wao katika mijadala ya Kamati mbali mbali
> umekuwa na uzito wa pekee, hautambuliki katika taarifa hizo
> ambazo zimejaa malengo ya kisiasa zaidi kuliko ukamilishaji
> wa shughuli za Bunge Maalum.
> Kuna taarifa nyingine
> zimesambazwa zikiwa na upotoshaji mkubwa, licha ya kwamba
> Taasisi zinazosambaza taarifa hizo zina wajumbe wake katika
> Bunge Maalum. Wajumbe hao wangeweza kuzielimisha Taasisi zao
> ukweli ulipo hapa Bungeni, na hivyo kuwafikishia wasomaji
> wao taarifa zilizo za kweli na ili kulijengea Bunge hili
> heshima machoni pa umma wa Tanzania na Kimataifa.
> Udhalilishaji kama huu unatuumiza hata sisi wajumbe ambao
> kwa hiari yetu tuliamua kubaki Bungeni na kuyatimiza hayo
> ambayo tulitumwa tuje tuyakamilishe.
> Kama tulivyosema hapo awali
> ni
> wajibu wetu
> kama Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Bunge hili kuutaarifu
> umma hali halisi katika shughuli za Bunge Maalum na kuwasihi
> wapotoshaji kwamba wauheshimu ukweli na wawaheshimu
> watanzania kwa kuwaeleza ukweli.
> Ahsanteni
> sana.
> …………………….
> …………………………
> SHEIKH HAMID
> MASOUD JONGO ASKOFU AMOS JOSEPH MUHAGACHI
> BAKWATA KIKRISTO
> TAREHE 3 SEPTEMBA,
> 2014
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
> Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
> Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
> Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment