Ninaamini kabisa kwamba huenda ni viongozi wa dini kweli walio katiba BMK ndio wameandika waraka huu.
Ninaamini pia kuwa wamekuwa influenced. wamekuwa influenced na nini ni swala la mjadala.
Natamani kuwa kabla ya kuandika au baada ya kuuandika wangeusoma kabla ya kuutuma humu wasingeutuma.
Kwa miaka miwili tume ya kukusanya maoni ilifsanya kazi yake bila kubughudhiwa. Kwa nini bubge linabughudhiwa?
wametaja idadi ya makundi yanayowapinga wabunge wakashindwa kujua kuwa huo ni uwakilishi tosha wa waTanzania wanaopinga mambo yanaqvyokwenda bungeni.
Wameshindwa kujua kuwa rasimu ya pili ya katiba wananchi tunayo kwa hiyo BMK linqapoanza kujadili kitu tofauti wananchi hatuna sababu ya kusubiri fedha zetu ziendelee kuteketea eti tusubiri hatua ya tatu..
Wanashindwa kujua kuwa kama kuna watu wametoka bungeni kupinga jambo. na baada ya hao wabunge hata wangekuwa wawili tu kati ya 600 wanaungwa mkono na utitili wa taasisi mtu yeyote mwenye busara na akili atasomamisha utaratibu na kutafuta maridhiano.
BMK si uchaguzi kuwa upande huu unanadi sera hapana tunahitaji makubaliano.
BMK linajadili jambo la hatari litakalouvunja muungano wetu Muundo wa serikali mbili utakaodumizsha nguvu kubwa ya Zanzibar na kwa hiyo kulifanya taifa kuwa na mataifa mawili tena mataifa mawili ya ajabu Zanzibar na Tanganyika isiyo wazi.
Kama viongozi wetu wa dini hao wana masikio pia basi wayasikie haya na kuyajibu lA SIVYO TUTAENDELEA KUWAHESHIMU.
--------------------------------------------
On Wed, 9/3/14, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] TAARIFA YA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI BMK KUHUSU MWENEND WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, September 3, 2014, 11:26 AM
TAARIFA YA
WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
TOKA WAJUMBE 201 KUHUSU MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM
LA KATIBA
Sisi Wawakilishi
wa Jumuiya na Taasisi za Dini, tuliopendekezwa na Taasisi
zetu na baadaye kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuwa
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na kula kiapo cha
utekelezaji wa jukumu hili kubwa.
Tukiamini
kuandaa Katiba Mpya kwa maridhiano ya Kitaifa kwa wananchi
wote, tulipokea jukumu hili kama wajibu wetu Kitaifa. Aidha
tunaamini kwamba katika kupata maridhiano ya Kitaifa ni
muhimu kuheshimu kila wazo na fikra inayotolewa na
kuunganisha fikra hizo kwa usahihi, kwa njia ya kidemokrasia
kwa kupiga kura na kukubaliana na matokeo ya wengi.
Kama
ilivyoelezwa hapo awali, kabla ya kuanza shughuli za Bunge
Maalum, kila mjumbe alikula kiapo cha kuwa mwaminifu na
mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya
uwezo wake na ufahamu wake, kufanya kazi zinazomhusu, bila
upendeleo na kumuomba Mwenyezi Mungu amsaidie.
Tumeshangazwa na
kusikitishwa sana kuona kwamba mchakato wa kutayarisha
Katiba itakayopendekezwa na Bunge hili kwa wananchi,
unachafuliwa taswira yake. Bunge Maalum la Katiba
linachafuliwa na, shughuli zake kuingiliwa na kupotoshwa na
wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge, Makundi, Taasisi na
Vyombo mbali mbali vya habari, uhalali na ukweli wa shughuli
za BungeMaalum la Katiba unapotoshwa. Wananchi wanaaminishwa
yasiyo na ukweli.
Upotoshwaji huu
umezua mijadala mbali mbali katika jamii ya Watanzania na
bado linaendelezwa kama ifuatavyo:
1. Kwamba Bunge
Maalum la Katiba halina uhalali kwa kuwa hao wajumbe wenzetu
walioondoka wameliondolea uhalali wake kwa vile hwapo,
wakiwepo Bungeni basi uhalalai wake utakuwepo -
utapatikana;
2. Inadaiwa kwamba Kanuni za Bunge Maalum la Katiba
zinavunjwa ovyo ovyo;
3. Inadaiwa pia, kwamba kinachojadiliwa sasa katika Bunge
hili ni Waraka mwingine na si Rasimu iliyotayarishwa na Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, iliyowasilishwa rasmi Bungeni na
kuanza kujadiliwa na wajumbe;
4. Inadaiwa na watu na Taasisi mbali mbali, kwamba viongozi
wa dini, wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na wajumbe wa
Kundi la 201, wanapewa rushwa. Isitoshe Vyombo vya habari
vimeandika tuhuma kama hizi.
5. Inadaiwa pia kwamba wajumbe waliomo katika Bunge hili ni
wachache, ukilinganisha na hao walioko nje ya Bunge
hilo;
6. Bunge hili, kwa tuhuma hizo, lazima lisitishwe au
livunjwe na Mhe. Rais.
Kabla ya kuanza
kuusahihisha upotoshwaji huo, sisi Wawakilishi wa Taasisi za
Dini mbali mbali na Wajumbe wa Kundi la 201 katika Bunge
Maalum la Katiba, tunapenda kufahamisha umma wa Tanzania
mchakato wa kutayarisha Katiba Mpya ulivyo kisheria.
Tunapenda
kuwafahamisha Watanzania wenzetu kwamba mchakato huu una
hatua tatu kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Mpaka hivi sasa ni hatua moja imekamilika. Hatua ya pili
ndiyo inayoendelea, na hatua ya tatu bado haijaanza.
Hatua ya kwanza
ni ile ya uandaaji wa Rasimu. Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83 iliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
chini ya kifungu cha tano cha sheria hiyo. Tume hii ilipewa
jukumu la kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya
Katiba, kuanisha na kuchambua maoni ya wananchi na kisha
kuandaa rasimu ya Katiba. Kazi hiyo ilifanyika kwa kipindi
cha takriban miaka miwili na hatimaye Rasimu ya Katiba
ilikamilika.
Hatua ya pili
ilikuwa ni kuipeleka Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum la
Katiba, ambalo liliundwa kwa shughuli maalum ya kuandika
Katiba inayopendekezwa, ili ifikishwe kwa wananchi ambao
wataamua waikubali au waikatae kwa kuwa wao ndio wenye
maamuzi ya mwisho. Hawa ni Watanzania wote wenye uwezo wa
kupiga kura kwa kutoa maoni yao. Hoja ya Mamlaka ya Bunge
hili hatujazungumzia kwa vile imefikishwa Mahakama Kuu ya
Tanzania ili kupata tafsiri sahihi ya mamlaka ya Bunge hili.
Tunachoweza kusema ni kwamba jukumu kuu la Bunge hili ni
kutengeneza Katiba inayopendekezwa na Bunge ili ifikishwe
kwa wananchi waipigie kura ya maoni. Hatua hii ya pili bado
inaendelea.
Hatua ya tatu ni
pale Bunge Maalum la Katiba tutamkabidhi Mhe. Rais Katiba
inayopendekezwa ambayo itafikishwa kwa wananchi ili
waikubali kama wataridhika nayo au kuikataa kama haikidhi
matarajio yao.
Hatua hii ni ya
mwisho wananchi wakiikubali tunapata Katiba Mpya wakiikataa,
tunaendelea na Katiba tuliyonayo.
Kilichotokea ni
kwamba, wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge hili wameamua
kuukiuka utaratibu uliowekwa kisheria. Badala yake
wamepeleka Rasimu ya Katiba kwa wananchi wakati mchakato wa
kutayarisha Katiba inayopendekezwa bado haujakamilika.
Sisi Wawakilishi
wa Taasisi za Dini, ambao kuuhubiri, kuutangaza na
kuusimamia ukweli ni moja ya majukumu yetu katika jamii,
tumesikitishwa sana na taarifa potofu zinazosambazwa kwa
makusudi na makundi, taasisi na vyombo vya habari mbali
mbali na tukiwa wajumbe wa Bunge hili ambao tunafahamu kwa
kina na tunaridhika na kila hatua ya mchakato huu. Tuna
wajibu wa kusahihisha upotofu huu, unaoendeshwa kwa makusudi
na hivi kuwaeleza Watanzania ukweli na hali halisi inayojiri
hapa Bungeni. Watanzania msifadhaishwe na wala msibabaishwe.
Hali ni shwari. Mchakato unaendelea kwa amani na utulivu.
Katika
kusahihisha upotofu unaozungumzwa kupitia mijadala na
midahalo mbali mbali katika jamii, tunaomba kufafanua hali
ilivyo kama ifuatavyo:-
TUHUMA KWAMBA
BUNGE MAALUM LA KATIBA KUKOSA UHALALI
Jambo hili si kweli hata kidogo kwani kuna wajumbe wa
aina tatu Bungeni ambao wamewekwa na kutambuliwa kisheria.
Hawa ni kama wafuatao:
1. Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
3. Wajumbe 201 walioteuliwa na Mhe. Rais, baada ya
kupendekezwa na Taasisi, Mashirika na makundi mbali mbali
nchini,
Uhalali wa Bunge
unakuwapo wakati wajumbe kutoka makundi hayo matatu wapo
Bungeni, na si Vyama vya Siasa pekee. Iwapo kwa mfano
wajumbe wa 201 wakiamua kutoshiriki katika shughuli za
Bunge, basi sehemu moja muhimu ya Bunge haitakuwapo na
uhalali wa Bunge hautakuwepo.
Hata hivyo,
Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zimeweka idadi ya akidi
ambayo ni nusu ya wajumbe wote wa Bunge Maalum. Akidi hii
ikifikiwa Bunge huendelea na shughuli zake. Akidi hii
hufikiwa kila wakati BungeMaalum linapokutana. Hii
inamaanisha kwamba Bunge Maalum la Katiba linaendesha
shughuli zake kwa misingi ya sheria na taratibu
zilizojiwekea. Bunge lina uhalali wa kufanya shughuli zake
kwa mujibu wa sheria.
TUHUMA KWAMBA
KANUNI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA ZINAVUNJWA
Suala hilo halijawahi kutokea. Kanuni za Bunge Maalum la
Katiba zilipitishwa na wajumbe wote kwa mujibu wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba Sheria Namba 83. Vile vile uendeshaji
wote wa shughuli za Bunge zinafanywa kwa mujibu wa Kanuni za
Bunge Maalum. Kanuni hizo zinatoa fursa ya Bunge Maalum
kuzirekebisha pindi inapobainika ipo haja ya kufanya hivyo
kwa mujibu wa kanuni Namba 87.
WARAKA
MWINGINE UNAJADILIWA NA SI RASIMU YA TUME
Hili nalo si kweli. Tunawahakikishia Watanzania wote kwamba
sisi kama Wawakilishi wa Taasisi za Dini miongoni mwa
wajumbe wa Kundi la 201, kwa ujumla tunasema hii si kweli.
Ni upotoshaji wa makusudi. Tunaijadili Rasimu ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ibara kwa ibara. Ibara nyingi zimeachwa
kama zilivyo. Kuna ibara ambazo zimeboreshwa au
kurekebishwa, kuna ambazo zimeondolewa na kuna nyingine mpya
ambazo zimewekwa ili kuweka mambo ya msingi ambayo Rasimu
haikuyazingatia au haikuyaona.
WAWAKILISHI
WA TAASISI ZA DINI, WAJUMBE WA KUNDI LA 201 WA BUNGE LA
KATIBA KUPEWA AU KUPOKEA RUSHWA
Sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini na Wajumbe wa Kundi la
201 wa Bunge hili tumesikitishwa sana na taarifa hii
iliyosambazwa na baadhi ya watu, na kukaririwa na baadhi ya
vyombo vya habari aidha kupitia kwenye mijadala, midahalo na
makongamano mbali mbali. Baadhi yetu sisi Viongozi wa Kiroho
tumeapishwa viapo vya uadilifu katika uongozi wetu wa kiroho
na tuko mstari wa mbele kuongoza waumini wetu kuepuka dhambi
ya tamaa ya fedha, na kusema uongo. Taarifa kama hizo
hazionyeshi heshima kwa dini au nafasi zetu za kipekee
katika uongozi wa kiroho. Taarifa hizi zinatangazwa kwa
makusudi na watu mbali mbali kupita vyombo vya habari kwa
malengo ya kisiasa na kutudhalilisha sisi Viongozi wa kiroho
mbele ya umma. Tunaomba tabia hii ikomeshwe.
TUHUMA KWAMBA
BUNGE KUWA NA WAJUMBE WACHACHE
Hili nalo si kweli. Wajumbe wanaohudhuria Bunge wanakidhi
akidi inayohitajika kwa mujibu wa kanuni.
HOJA YA
KUSITISHWA AU KUVUNJWA KWA BUNGE MAALUM
Hii ni hoja inayozungumzwa katika mijadala mbali mbali
katika jamii. Msingi wa hoja hiyo ni kutokuueleza umma
ukweli ulioko Bungeni kwa kupeleka taarifa potofu kwa
wananchi kwamba Bunge Maalum limekosa mwelekeo. Hatuoni
sababu za hoja hii kutiliwa maanani kwa kuwa hakuna sababu
za msingi na za kisheria za kufanya hivyo.
HITIMISHO
Kumekuwa na taarifa mbali mbali zenye malengo ya ama
kuingilia shughuli za Bunge hili au kutudhalilisha sisi
wajumbe ambao si Wabunge au Wawakilishi. Wajumbe 201, ambao
mchango wao katika mijadala ya Kamati mbali mbali umekuwa na
uzito wa pekee, hautambuliki katika taarifa hizo ambazo
zimejaa malengo ya kisiasa zaidi kuliko ukamilishaji wa
shughuli za Bunge Maalum.
Kuna taarifa
nyingine zimesambazwa zikiwa na upotoshaji mkubwa, licha ya
kwamba Taasisi zinazosambaza taarifa hizo zina wajumbe wake
katika Bunge Maalum. Wajumbe hao wangeweza kuzielimisha
Taasisi zao ukweli ulipo hapa Bungeni, na hivyo kuwafikishia
wasomaji wao taarifa zilizo za kweli na ili kulijengea Bunge
hili heshima machoni pa umma wa Tanzania na Kimataifa.
Udhalilishaji kama huu unatuumiza hata sisi wajumbe ambao
kwa hiari yetu tuliamua kubaki Bungeni na kuyatimiza hayo
ambayo tulitumwa tuje tuyakamilishe.
Kama tulivyosema
hapo awali ni wajibu wetu kama Viongozi wa Dini na Wajumbe
wa Bunge hili kuutaarifu umma hali halisi katika shughuli za
Bunge Maalum na kuwasihi wapotoshaji kwamba wauheshimu
ukweli na wawaheshimu watanzania kwa kuwaeleza
ukweli.
Ahsanteni
sana.
…………………….
…………………………
SHEIKH HAMID MASOUD JONGO ASKOFU AMOS JOSEPH
MUHAGACHI
BAKWATA KIKRISTO
TAREHE 3
SEPTEMBA, 2014
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment