Wednesday, 10 September 2014

Re: [wanabidii] Re: GARI LA JWTZ LAPATA AJALI YADAIWA WATU WATATU WAMEKUFA

Kupanga nyumba mstari pande mbili mita chache kutoka barabarani wakati wa vijiji vya ujamaa; watu kusogeza frame za biashara na nyumba barabarani na kuziba mpaka njia za kupita. Nyumba hazipo mita 30-60 kutoka barabara ndogo na kuu jinsi inavyotakiwa. Zamani hakukuwa na magari kama sana. Njia za Mtwara na Lindi mjini na vijijini ni balaa zipo karibu sana na barabara. Kisha, kama vijijini Lindi vijijini unakuta mti au mnazi umeanguka kukatiza barabara unakuwa hauondolewi karne na viongozi wapo hapo. Mtu ambaye hajapita njia hiyo na kuuona anaweza kupata ajali mbaya. Ni uvivu au sijui nini na minazi mwarabu kapanda kama mchicha.
 
Ajali kama hizi zitakuwa nyingi hata mijini bongoland kutonana na sheria ya ardhi kukiukwa hata kule kulikopimwa na wenye nyumba kuwa na hati miliki maeneo ya high na low, medium density kwa sasa ni makorogoro zaidi, kuta ndefu, frame na mabiashara-mbao, garage, mapishi mpaka barabarani. Gari ikiserereka inabeba moto au jiko la mkoaa na kuingia nalo ndani ya nyumba kuchoma nyumba na watu. Viongozi wa kuongea na wananchi wao kama wabunge, madiwani wapo kusaidiana na watumishi wa ugani, serikali za Mtaa kuonya watu kutokuvunja sheria. Pili-anapojenga mtu pasiporuhusiwa kubomolewe mara moja kwa kikosi maalum cha wizara ya ardhi. Awe amepata ruksa rasmi au kwa rushwa mradi tu ramani ya mipango miji inaonyesha asiwepo hapo. Vunja kuta zote zinazoziba feeder road halafu moto ukiwaka hakuna mapito ya gari la zimamoto. Kusogeza waliopangwa barabarani wakati wa vijiji vya ujamaa ni gharama kubwa sana maana resettlement yake inataka fidia kwa bei ya sasa ya gharama za ujenzi kwa vifaa alivyotumia plus mafao mengine mengi ndio umuondoe. Ila, kujihadhari kabla ya hatari ni vema sana.


On Wednesday, 10 September 2014, 18:35, 'Fred Hans Kipamila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Wengine wanasema ni kifaru cha kivita
--------------------------------------------
On Wed, 9/10/14, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: GARI LA JWTZ LAPATA AJALI YADAIWA WATU WATATU WAMEKUFA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, September 10, 2014, 2:19 PM

 

On Wednesday, September 10, 2014 11:03:54 AM UTC+3, Emma
Kaaya wrote:Kutoka Lindi
kuna taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga
kuhusu ajali iliyotokea Mtwara ambayo imehusisha gari la
Jeshi la Wananchi Tanzania(Jwtz)imeripotiwa asubuhi ya leo
na shuhuda wa eneo hilo.
Msafara huo wa Wanajeshi ulikuwa ukitokea Mtwara
kuelekea Nachingwea kwenye camp kubwa ya Jeshi na ajali hiyo
imetokea maeneo ya Mnolela kijijini Lindi,kwa mujibu wa
shuhuda ambaye ametoa taarifa hii kupitia kipindi cha Power
Breakfast kutoka Clouds Fm amesema ajali hiyo imeua
wanajeshi 3 na mwenye nyumba mmoja ambaye ni mwanamke alikua
kalala ndani.Madhara mengine yaliyotokana na
ajali hii ni nyumba mbili kuharibika vibaya,majeruhi wa
ajali hii wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa
Mtwara.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment