Na Mwene Said wa Blog ya Jamii
NAIBU Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, leo amewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kuhoji mamlaka ya Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Said Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwamba maombi hayo ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.
Masaju amewasilisha pingamizi hilo akitoa sababu nne, akiitaka mahakama kutupilia mbali maombi yaliyopo mbele ya jopo la majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Katika pingamizi hilo lililoambatana na hati ya kiapo, AG kupitia naibu wake, amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana dosari ambayo haiwezi kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha sheria kinachoipa nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.
Sababu nyingine, AG anadai kuwa maombi hayo yaliyopo mahakamani hayawezi kuthibitishwa na kwamba hayana mashiko ya kisheria.
Pia, Masaju amedai kuwa maombi yaliyopo mahakamani ni batili kisheria hivyo mahakama iyatupilie mbali.
Jaji Mwarija alisema kesi hiyo itasikilizwa kesho mahakamani hapo.
Katika kesi ya msingi, kesi hiyo namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba chini ya vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011 imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi.
Pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.
Maombi hayo ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo leo chini ya Hati ya Dharura.
Katika kesi hiyo ya msingi anaiomba Mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya masharti ya vifungu hivyo vya sheria hiyo na pia itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.
Kwa mujibu wa hati ya madai, Kubenea anadai kuwa msingi wa kesi hiyo unatokana na uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Desemba Mosi, 2011, lililopitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Anasema sheria hiyo ilikuwa na lengo la kuratibu mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
On Thursday, September 4, 2014 7:41:22 PM UTC+3, Lazaro Limbo wrote:
Tunaomba grounds mkuu!
Sent from my HTC Tilt™ 2, a Windows® phone from AT&T
From: Emma Kaaya <emma...@gmail.com>
Sent: Thursday, September 04, 2014 7:31 PM
To: wana...@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Mahakama kuu kanda ya Dar es salaama imetoa amri ya kusitishwa kwa Bunge Maalum la KatibaLeo tena Historia ya aina yake imeandikwa ambapo Mahakama kuu kanda ya Dar es salaama imetoa amri ya kusitishwa kwa Bunge Maalum la Katiba dhidi ya serikali kupinga Bunge Maalum la Katiba kuendelea. Serikali kupiitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) - iliwawasilisha pingamizi ikipinga maombi ya kutaka Bunge Maalum la Katiba lisitshwe, hata hivyo jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Agustine Mwarija akishirikiana na Dk Fauz Twaib na Aloysius Mujulizi wamesema kwamba kwa mjibu wa Katiba ya JMT ya 1977ibara ya 98 (1) na kwa mujibu wa sheria Na 5 ya 1984 ib 14. ....., ili marekebisho yoyote ya kikatiba yaweze kufanyika ni lazima yaungwe mkono na 2/3 ya wabunge wa Tanganyika na 2/3 ya wanzanzibar na pia ili hii rasimu inayoandaliwa iweze kupata uhalali wa kisheria na kisiasa ni muhimu kuugwa mkono na 2/3 ya wananchi wote wenye uwezo wa kupiga kura ya ndiyo, katika msingi wa uamuzi wao, hali ya kisiasa iliyopo nchini Tz haitaruhusu kupata consensus ya kikatiba kama sheria kuu. Wakili Hon. Pet Kibatali amesema kwamba huu ni uamuzi wa kuokoa kuteketezwa kwa fedha za wananchi ambazo zingesaidia kutatua kero za elimu ya juu, afya na miunddo mbinu. Nakala ya amri hiyo itaambatanishwa kesho saa nane mchana ktk Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment