Sidhani kama tunapaswa kuhukumu kwa sababu hatuna uwezo wala mamlaka hayo. Hata hivyo kwa ujumla tunapaswa kujifunza kitu; hatupaswi kuabudu binadamu wenzetu, tunapaswa kumwabudu Mwenyezi Mungu tu. Kwa sababu ya kukata tamaa kwetu, mifadhaiko, matatizo na changamoto mbalimbali za maisha tumeacha njia sahihi na kuchukua njia ya mkato kwa kugeukia binadamu wenzetu na kuwaabudu tukiamini kwamba wana uwezo wa Kimungu! Watu wajanja wanaojiita kila jina (manabii, mitume, wachungaji, nk nk nk) nao wametumia matatizo yetu na kukata tamaa kwetu kama mtaji wao kwa kutuhadaa ili watuvune. Wengine kwa kiburi, wanajipa uwezo wa Kimungu na kujitangaza kila mahali kwamba wanaponya watu, wanafufua waliokufa, nk nk nk!! Hata Yesu Kristu mwenyewe alipofanya maajabu ya kuwaponya na kuwafufua watu aliwaambia wasitangaze neno hilo! Leo tunashuhudia matangazo kila upande ikitangaza uwezo wa miujiza, kuponya na kufufua!! Lakini hao wafu, viwete, vipofu, viziwi tunaowajua kwa uhakika wapo hivyo hivyo. Badala yake watu "anonymous" na "abstract" ndiyo mifano na mashuhuda wa miujiza hiyo! Kuna taarifa zinazoashiria kwamba kuna watu wanaolipwa ili kutoa ushuhuda wa uongo kwamba waliponyeshwa kimiujiza. Tumeona utabiri wa wahubiri maarufu ukienda kombo, ikidhihirisha kwamba wahubiri hao si miungu kama tunavyoamini bali ni binadamu wenzetu tu wanaocheza na akili zetu. Kwa mfano, utabiri wa hivi karibuni juu ya ushindi wa Clinton uliofanywa na TB Joshua ulivyoenda kombo. Kwa mujibu wa BBC, bado waumini wake wakatetea upungufu huo na kudai kwamba TB Joshua hakukosea kwani Clinton alipata kura nyingi za moja kwa moja (popular votes), na hivyo ubashiri ulikuwa sawa!!! Kuna wahubiri kadhaa duniani waliowaongoza wafuasi wao hata kukatisha maisha yao wakiwahadaa kwamba ndiyo njia ya kwenda mbinguni! Kibwetere wa Uganda ni mfano mmoja tu . Jim Jones, kiongozi wa Peoples' Temple aliua wafuasi wake 918 ambao waliamini ni nabii wao! Bila kuingilia imani ya yeyote yule, biashara na hadaa inayoendelea kwa mgongo wa kidini inapaswa kutuamsha na kutufanya tutafakari upya njia zetu za kiimani ili kuchuja nabii yupi ni wa ukweli na yupi wa uongo anayetutumia kama mtaji wa kujitajirisha yeye binafsi huku akitumia matatizo yetu na kukata tamaa kwetu kama daraja la kutuvuna! Ni wakati wa kuamka! Sent from my Samsung mobile |
From: Victor Mwita <victormwita@gmail.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO USIRUDIE TENA KUFANYA USHETANI HUU
Sent: Thu, Nov 24, 2016 1:10:38 PM
Huenda ni watu wengine kujifanya ni watu wa kiroho sana lakini kumbe wakiwa mitaani ni watu kama wengine tu On 24 Nov 2016 16:05, "Telesphor Magobe" <tmagobe@gmail.com> wrote:
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/d/optout. |
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment