Habari wote katika jamii! Naomba kufahamu MSINGI wa kuanzisha shirika la kutetea haki za binaadamu! Mwezi huu wenzetu wa Kagera walipatwa na madhara ya kuumia na wengine kufariki. Nini mchango wa wanaharakati wa haki za binaadamu kwa majanga ya aina hii? Au kwa uhalisia wanaharakati wa haki za binaadamu mmefanya nini kwa tukio hilo? Mbona hamsikiki kama ilivyo katika matukio mengine mfano police wakitumia nguvu zaidi kudhibiti mfano waandamaji- mara moja utaona au kusikia mikutano na waandishi wa habari kutoa matamko ya kulaani na nk.
Kwali lingine naomba kuelimishwa, mtu aliekufa ana haki gani kama kifo chake kilitokana na kupigwa au kunyongwa au kupigwa risasi na wahalifu? Hapo je, wanaharakati hakuna kazi ya kufanya? Hili swali linawahusu pia wale wanaopinga adhabu ya kifo. Mfano mdogo tu, janga la tetemeko limeua watu Kagera na wengine wengi wanalala nje na wengine darasani na watoto wanasoma na wahanga wakiendelea kuishi darasanina wengine kuhitaji matibabu na makazi halafu unasikia au kushuhudia mtu au kikundi cha watu wanahujumu michango hiyo ya wahanga! Je huyu si muuaji? kwa nini asiuawe au wasiuawe hawa?
Naomba kuelimishwa!
0 comments:
Post a Comment