Monday 29 February 2016

[wanabidii] DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA CHUMBA CHA UPASUAJI CHA HOSPITALI YA SANITAS YA MIKOCHENI

Habari za asubuhi,

Tafadhali pokea CODES hapa chini.

Naibu wa  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana  ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo  kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.

"Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara," alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.

Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu  Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.

Dkt. Kigwangalla  alivitaja viwango  vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.

Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.

Tazama MO tv, kuangalia tukio hilo hapa:

Imeandaliwa na Magreth Kinabo, (MAELEZO),  Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv)

Naibu wa  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas,  Bi. Gean Cabral  wakati walipowasilia katika ziara hiyo..

Dk Kigwangalla  akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.

Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.

Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral

Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.

Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..

Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi

Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).

KAWAIDA

Naibu wa  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana  ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo  kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.

"Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara," alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.

Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu  Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.

Dkt. Kigwangalla  alivitaja viwango  vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.

Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.

Tazama MO tv, kuangalia tukio hilo hapa:

Imeandaliwa na Magreth Kinabo, (MAELEZO),  Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv)

dk kigwa

Naibu wa  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas,  Bi. Gean Cabral  wakati walipowasilia katika ziara hiyo..

dk hk 888Dk Kigwangalla  akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.

dk hk55Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.

Kigwangalla akitoa maagizo

Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral

dk hkna

Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.

dk kigwa

Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..

dk hk iio

Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi

dk hk67

Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment