Monday, 1 September 2014

[wanabidii] Haya aliyanena Zitto Z. Kabwe miaka miwili iliyopita

Haya aliyanena Zitto Z. Kabwe miaka miwili iliyopita:

"Tumegundua kuwepo kwa juhudi za makusudi kutugombanisha CHADEMA.

Hiki ni chama makini, kimezibaini njia hizo na kwa hakika hakiwezi kusambaratishwa.

CHADEMA ndiyo imenipa Umaarufu mimi. Mimi si maarufu kuliko Chama, CHADEMA ni taasisi.

CHADEMA ni chama ambacho kina misingi katika uanzishwaji wake.

Wanasema eti nilishinda kwa umaarufu wangu binafsi. SI KWELI. Niligombea ubunge nikitokea shule. Sikuwa najulikana. Niliikuta 'grassroot network' ya Chama.

Hakikujengwa na mimi. CHADEMA ilijengwa na uongozi uliokuwepo. Nilikuta uongozi intact ( imara). Katika kila kijiji kulikuwa na uongozi na hata katika vitongoji vyote.

Wakati naingia kugombea ubunge kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wenye kadi wanaofika 10,800 katika jimbo zima.

Hawa sikuwatafuta mimi, niliwakuta na ndio waliofanikisha ushindi wangu.

Katika mazingira kama haya utasemaje kuwa mimi ni maarufu kuliko chama wakati chama ndicho kimenipa umaarufu?.

CHADEMA ni Chama ambacho wenyeviti wake wastaafu wanaendelea kuenziwa na kuhudhuria vikao vyote vya Chama. Institutional memory ipo kuliko katika vyama vyote vya upinzani.

Alipohama Dr Aman Walid Kabourou, wengi walidhani ndiyo mwisho wa CHADEMA Kigoma, lakini leo hii CHADEMA ni moto Kigoma kuliko ilivyokuwa awali"..

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment