HAPPY BIRTHDAY JWTZ 50 YRS, 2014
Na Happiness Katabazi
LEO Septemba Mosi Mwaka 2014 , Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ), linaloongozwa na Jenerali Davis Mwamunyange "Babu Mnyange au Mchuna ngozi'', limetimiza umri wa Miaka 50 tangu lilipoundwa rasmi mwaka 1964.
Namuita ' Babu Mnyange', Mchuna Ngozi' , kwasababu Moja, mwanangu Queen Mwaijande 'Malkia' akimuona kwenye Televisheni CDF- Mwamunyange , hawezi kulitamka Jina hilo kama lilivyo analitamka hivi ' Babu Mnyange '.
Na kwakuwa Miaka ya nyuma kuliibuka matukio ya uchunaji binadamu ngozi huko Mkoani Mbeya.
Mwamunyange yeye ni Mnyakyusa toka Wilaya ya Kyela na Mwaijande yeye ni Mnyakyusa wa Tukuyu - Masoko Mkoani Mbeya, hivyo Mimi Huwa nawataniaga wote hawa ni watu wanaotokea Mkoa wa Mbeya hivyo wote ni ' Wachuna Ngozi''.
Kabla ya kwenda Mbali , napenda ni tangaze Kuwa Nina maslahi ya JWTZ Kwani wazazi wangu ni watumishi wa Jeshi Hilo na Familia yetu inatibiwa Katika Hospitali ya Jeshi Hilo Lugalo na watoto wote tuliozaliwa Katika Hospitali hiyo na hadi sasa tukiugua tunatibiwa Katika Hospitali hiyo hivyo na mimi binafsi kupitia kazi yangu ya Uandishi wa Habari nimeripoti habari nyingi za jeshi hilo tangu Mkuu enzi zile Mkuu wa Jeshi hilo akiwa Jenerali Mstaafu, Wilfred Mboma hadi sasa JWTZ Inaongozwa na Jenerali Mwamunyange.
Hivyo haya ninayoyaandika ninayafahamu Kwani mengine nimeyashuhudia kwa macho na mengine nimeelezwa na baadhi ya Wanajeshi ambao ni marafiki zangu na wengine ni mashabiki wakubwa wa makala zangu ila siwezi kutaja Majina Yao kwasababu siyo wasomaji wa Jeshi.
JWTZ ilizaliwa Mwaka 1964 baada kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Jeshi la Kikoloni la King's African Rifles (KAR) lilovunjwa baada ya kutokea kile kilichoelezwa kuwa ni machafuko ya Januari 1964.
Leo wakati JWTZ Ikitimiza Miaka 50 tangu kuzaliwa kwake, pia ndiyo siku aya hitimisho ya maadhimisho ya sherehe hizo yaliyofanyika kwa zaidi ya wiki moja huko Zanzibar ambapo tumeongea Michezo mbalimbali imefanywa na Askari wa JWTZ pia tumeshuhudia maonyesho ya silaha za kivita zilizokuwa zikionyeshwa na JWTZ Katika kambi zake mbalimbali na Hilo limedhiirisha Jeshi letu lipo imara na ina vifaa Vya kisasa na lipo timamu wakati wowote Kupambana na adui ambaye atatuchokoza.
Wakati jeshi letu linatimiza Miaka 50 , wanajeshi wetu wamefanya mengi licha ya kushiriki kwenye ukombozi wa nchi nyingi za kusini mwa Afrika, kushiriki shughuli za kulinda amani " Peace Keeping' nchi mbalimbali ikiwemo Kongo, Sudan, Liberia ili kuhakikisha zinakuwa huru kama ilivyo kwa Tanzania,JWTZ, imekuwa ni tanuri la kuyapika baadhi ya majeshi mengine ya nchi za Afrika.
Wananchi wenzangu waliopata fursa ya kutembelea maonyesho hayo watakubaliana nami kwamba jeshi letu sasa limekubali kubadilika na sasa limeanza kufanya kazi Kisayansi na Kiteknolojia na kwamba limekataa kuendelea kufanya kazi zake gizani na wasiwasi mithili ya mtu anayeoga barazani.
Binafsi Nikiwa mtoto wa Mwanajeshi niliyezaliwa na kuishi pale ' Area D' Lugalo Block Namba 19, Dar Es Salaam, Enzi zile za Miaka 1979 hadi 1989 na kusoma shule Chekechea Service na kisha darasa la kwanza hadi la tatu katika Shule ya Msingi Lugalo Dar es Salaam na ' Pololo la JWTZ limenikuza' , Kwasababu Baba yangu Mzazi Thadeo Katabazi alikuwa Mwanajeshi wa JWTZ na mama yangu Mzazi Oliva hadi sasa bado ni mtumishi raia kikosi cha 521 KJ.
Natoa pongezi kwa wafanyakazi wote wa JWTZ na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, chini ya Waziri Dk.Hussein Mwinyi kwanza kutimiza umri wa Miaka 50.
Pili, kwa uamuzi wake wa kuondokana na fikra za kizamani za kuficha ficha dhana za kivita kwenye maandaki kwa kisingizio kuwa maadui zetu watafahamu jeshi letu lina zana zipi za kivita.
Kwani tangu Jenerali Mwamunyange ateuliwe na Rais Jakaya Kikwete kuongoza JWTZ, Septemba mwaka 2007, kuongoza jeshi hilo sote ni mashahidi tumekuwa tukiona JWTZ katika sherehe mbalimbali ikituma wanajeshi wake kuonyesha dhana zake za kivita, makomando wa JWTZ wamekuwa wakitoa 'SHOW' pale Uwanja wa Taifa katika sherehe mbalimbali kitaifa.
Binafsi napenda sana ' SHOW' inayotolewaga na Makomando wetu kwani ' SHOW' hizo zimetufanya tujue kazi ya Komando ni nini na kwamba ni kweli JWTZ ina makomando hodari na kufahamu kuwa kumbe Komando ni binadamu kama sisi kwani hapo awali kabla hatujawaona Makomandoo 'wakitoa 'SHOW' tulikuwa tunajiuliza HIvi Makomandoo ni watu wa aina gani?Je ni binadamu Kama sisi?
Sasa kupitia SHOW ya Makomandoo hao tumeweza kutambua kuwa Komando ni binadamu kama binadamu wa kawaida ila tofauti ni kwamba Komando ana mafunzo makali ya mazoezi ya kumkabili adui kuliko sisi raia na hata askari wengine ambao si Makomandoo.
MKuu wa KIkosi Cha 521KJ Lugalo Hospital, Dk.Makele na uongozi wa JWTZ Nawapongeza kwa kuleta Mabadiliko makubwa Katika kikosi hicho ambacho kinaendesha Hospitali Kuu ya JWTZ Lugalo Kwani chini ya uongozi wake Duka la Madawa ambalo linahudumia wagonjwa wanaofika hospitalini kutibiwa kwa kutumia vitambulisho Vya Bima ya Afya.
Kwani hapo zamani Duka Hilo la kuhudimiwa wagonjwa wanaotibiwa kwa kutumia vitambulisho vya Bima ya Afya halikuwepo, Hali iliyokuwa ikileta Usumbufu kwa wagonjwa walikuwa wanaotibiwa Kwa kutumia Bima ya Afya kwenda kuchukua dawa maduka ya madawa nje ya hospitali hiyo.
Chini ya Uongozi wa CDF- Mwamunyange , Hospitali ya Lugalo imeweza kupanuliwa na kuboreshwa na inaendelea kupanuliwa pia hospitali hiyo hivi sasa ina Chumba Cha kulaza wagonjwa mahututi(ICU) na pia Hospitali Hiyo imepandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya Rufaa.
Aidha Katika uongozi wa CDF- Mwamunyange tumeshuhudia wodi ya watoto iliyokuwa ndani ya eneo la Hospitali ya Jeshi Lugalo, kuamishiwa katika ndani ya eneo la kombani ya Bendi ya Jeshi Hilo Mwenge Dar Es Salaam, ambapo wodi hiyo Bado ipo ndani ya kikosi Cha 521KJ I nafanyakazi saa 24 na huduma zake niza uhakika.
Pia napongeza manesi,madaktari, wahudumu wa Hospitali ya Lugalo Kwai wamekuwa na nidhamu ya Hali ya juu kwa kupokea na kuwahudumia vizuri wagonjwa Ndio mAana hatuzikwi wananchi wanaofika hospitalini hapo kupata huduma ya matibabu wakilalamika Kuwa wanapata huduma mbovu na wahudumu wanawatolea maneno machafu.
Katika Utawala wa Rais Kikwete tumeona siku ile Kikwete anaenda kuzindua Makao Makuu ya Kikosi Cha Askari wa Miguu( Land Force ) , alitangaza kuwaongezea Mbele umri wa Miaka mitatu ya kustaafu Wanajeshi wetu .
Wakati Leo JWTZ ikisherehekea Miaka 50 , tumeshuhudia mabadiliko na kange zako la mishahara na lesheni kwa Wanajeshi wetu na Wanajeshi wenye shukurani ukikaa nao wanamsifu sana Mwamunyange wanasema ni kipenzi Cha wanajeshi Kwani anapigania maslahi Yao na pia wanaiopongeza Rais Kikwete Kwani Katika Utawala wake ameweza kuijali sana JWTZ.
Aidha tumeshuhudia ndani ya Miaka 50 ya JWTZ ,ujenzi wa nyumba makazi ya Wanajeshi na familia zao inashika kasi Kwani ndani ya eneo la Lugalo Hospitali, ujenzi wa makazi ya wanajeshi inazidi kushika kasi na majengo mengine yamekamilika na Tayari Wanajeshi na familia zao wanaishi.
Septemba 2007 wakati Mwamunyange alivyoapishwa Ikulu na Rais Kikwete kushika wadhifa huo wa Ukuu wa Majeshi Nilikuwepo, na Alisema hatawavumilia wanajeshi wake watakaobainika kuwapigia raia na kwamba ataamuru wafikishwe Katika mahakama ya kiraia washitakiwe.
Ni kweli tumeshuhudia baadhi ya Wanajeshi wakifunguliwa Kesi kati Mahakama za kiraia. Mfano mzuri ni wale Wanajeshi waliyoshitakiwa kuwa kosa la mauji ya Swethi Fundikila na Mahakama Kuu Kanda Ya Dar Es Salaam, ikawakuta na hatia na kuwahukumu Adhabu ya kifo.
Aidha Mwaka Juzi tulishuhudia zaidi ya Wanajeshi wa tano wakifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la Mauji ambapo walilitenda karibu na Kituo Cha Polisi Kawe ambapo waliomua raia kwa kipigo.
Pia Mwaka Juzi tulishuhudia Kanali Ayoub Mwakang'ata , Kanali Felix Samilani wakifunguliwa kesi ya matumizi mabaya ya madaraka Na. 163/2012, Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mbele ya Aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo ambaye kwasasa ameamishiwa Mkoa wa Kagera, Alocye Katemana , Aprili 23 Mwaka huu, alitoa hukumu ya kuwaachiria Huru maofisa Hao wa juu wa Jeshi baada ya kuona hawana hatia.
Binafsi Kesi hii ambayo ilisababisha maofisa wa juu wa ngazi ya Cheo Cha Brigedia Jenerali kufika mahakamani hapo kutoa ushahidi wa Kuwatetea maofisa Hao Kuwa hawajatenda makosa waliyoshitakiwa nayo.
Hata hivyo tangu kesi hii ilipoanza hadi kumalizika, nilishuhudia Askari polisi walikuwa waniogopa kuwasogolea wanajeshi Hao na nilipokuwa nawahoji ni kwanini Polisi hawawalindi sana maofisa hao wa JKT Kwani nao Mbona ni washitakiwa Kama washitakiwa wengine.
Polisi walikuwa wakinijibu wakisema Hao maofisa wa JKT ndiyo wenye nchi. Nikawa nacheka sana. Na baadhi ya Wanajeshi wenzao wakati wote wa Kesi walikuwa wakija kuwasindikiza na kusikiliza kesi hiyo .
Binafsi nilipata fursa ya kuiripoti Kesi hiyo tangu ilipofunguliwa siku ya kwanza hadi ilipomalizika Aprili 23 Mwaka huu. Kesi hii ilinifundisha Kuwa Wanajeshi wetu wananidhamu ya Hali ya juu na wanamshikamano.
Kwani ingelikuwa ni majeshi ya nchi nyingine, siku ile maofisa wa JWTZ wanafikishwa Katika Mahakama ya Kisutu ' Pangechimbika bila Jembe' , na ndiyo mAana msafara wa maofisa Hao uliotokeoa Makao Makuu ya Takukuru , Upanga Dar Es Salaam, ulisindikizwa na Brigedia Jenerali mmoja kwaajili ya Ulinzi na hata polisi walikuwa hawasogelei Yale Magari walivyokuwa wamepanda maofisa Hao.
Sote ni mashahidi kila kukicha tumekuwa tukisikia au kuona majeshi ya nchi nyingine za Afrika yamekosa mshikamano wake kweli na hivyo kufikia uamuzi wa baadhi ya wanajeshi wake kuasi na kuanzisha vikundi vyao haramu vilivyoweka maskani yake Msituni na lengo la vikundi hivyo vya waasi limekuwa ni kupambana na jeshi linaloshika hatamu kwa wakati huo.
Vikundi hivyo wa Waasi wa majeshi hayo vinakuwa na Dhamira Kuu ya kupindua serikali kisha watwae madaraka, jambo ambalo limeleta machafuko katika nchini nyingi lakini kwa kuwa Mungu bado anaipenda nchi yetu, JWTZ bado haijafikia hatua hiyo kwani wanajeshi wake wana mshikamano wa dhati.
Kwa wale tunaopenda kutembelea vikosi, makambi ya JWTZ tumekuwa tukiona zana mbalimbali zikiwamo maghala ya silaha, ndege za kivita n.k, lakini pindi umuulizapo mwanajeshi hata kama ni rafiki yako kwamba ile ni silaha aina gani au komandoo naye anafamilia? Mwanajeshi ataishia kukujibu kwa mkato "fuata kilicho kuleta, hizo ni siri za jeshi hutakiwi kujua, umekuja kutupeleleza na utaruka kichurachura sasa hivi."
Wakati nikitoa pongezi kwa maadhimisho hayo, nitoe angalizo kwa jeshi letu kwamba bado wananchi wana imani nalo licha ya kuwapo kwa baadhi ya vitendo vya utovu wa nidhamu unaofanywa na baadhi ya askari wa chache, hivyo ambayo wakati mwingine vitendo hivyo vinalipaka matope jeshi.
Hata hivyo, hivi sasa jeshi letu limekuwa likitoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi pindi wanapokamatwa wanajeshi kwenye matukio ya ujambazi na hatimaye wanafikishwa mahakamani na mfano mzuri ni Kesi ya mauji maarufu Kama Kesi ya ' Ubungo Mataa' ambayo inaendelea Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, ambayo miongoni mwa washitakiwa ni Wanajeshi.
Naunga mkono ombi la CDF- Mwamunyange, katika maadhimisho haya ambapo katika hotuba zake kila alipokuwa akitembelea kambi zake pamoja na mambo mengine alikuwa akiwaomba raia wawe na uhusiano mwema na jeshi hilo. Lakini napenda kutoa angalizo kwamba uhusiano mwema kati ya pande hizo mbili uwe na mipaka na masilahi ya kwa nchi.
Uhusiano mwema huo usiwe ni ule wa baadhi ya wanajeshi wetu kutumia mafunzo ya kivita waliyoyapata kwenye vyuo vyao vya kijeshi, wakaanza kutoa mafunzo hayo kinyemela kwa baadhi ya wananchi watukutu ili mwisho wa siku waunde magenge ya kihalifu kwa maana ya mwanajeshi anatoa mafunzo kwa raia, silaha na kumcholea michoro ya kwenda kufanya ujambazi.
Na baadhi ya Wanajeshi ambao nimekuwa nikiwadadisi kuhusu hali hiyo kila mmoja wao kwa nafasi yake wamekuwa wakinijibu kwamba Kurugenzi ya Habari ya jeshi haipo huru hivyo na wao imekuwa ikiwawia vigumu kuwasilisha maombi yetu kwa maafande wao.
Ni rai yangu kwa Jenerali Mwamunyange na makamanda wako mlitazame hili, kwa mtazamo mpana, kwani wananchi wanahitaji kupata taarifa za jeshi lao ambapo taarifa hizo jeshi litahakikisha linatoa taarifa ambazo hazimnufaishi adui wa taifa letu.
Sasa kwa hali hiyo, tunaona kwamba kuna wananchi wanaopenda kupata taarifa mbalimbali za jeshi letu, wengine wanapenda kujiunga na jeshi hilo, kutembelea makumbusho ya jeshi lakini kwa sababu ya jeshi hili ama kwa kushindwa kuwa karibu na wananchi ama kwa kuandaa vipindi maalumu katika televisheni au redio au kuweka taarifa mpya mara kwa mara katika tovuti ya jeshi hilo ambalo lilizinduliwa na Luteni Jenerali Abdulahman Shimbo, pale Upanga Mess, ambapo nami nilikuwa miongoni mwa waandishi wa habari tuliohudhuria uzinduzi wa tovuti hiyo, kama wanavyofanya Jeshi la Polisi hivi sasa ndiyo kuna sababisha wananchi wengi kubaki gizani kuhusu utendaji wa jeshi letu.
Lakini cha kushangaza kama si cha kustaajabisha, licha ya JWTZ kuwa na wasomi wa taaluma ya teknolojia ya habari lakini tovuti ya jeshi hilo imekuwa haina vitu vingi, ama kuweka taarifa mpya za mara kwa mara na Sioni Kama wahusika wanafanya jitihada za kutangaza Website ya Jeshi Kwani hata lile Gazeti la Ulinzi hivi sasa ni Kama limekufa vile Kwani halionekani mtaani kwa Wingi na kwa wakati Kama zamani. Mwamunyange " Mchuna Ngozi' Kulikoni Gazeti la Ulinzi?
Mwamunyange kama JWTZ haina fedha za kulipa kiwandani gazeti la Ulinzi lichapwe, ni kheri utembeze 'Bakuri' na utangaze kuwa JWTZ ' limefulia' halina fedha za kuchapisha gazeti hilo, naamini makampuni yatajitokeza kusaidia gharama za uchapaji kuliko kufanya Watanzania wengi wasilipate gazeti hilo kwa wakati na wasiwe na uhakika wa kulipata.
Hata hivyo Changamoto nyingine inayowakabili Jeshi Hilo ni kwamba kuna malalamiko ya chini Kwa chini toka kwa baadhi ya Wanajeshi wake Kuwa ruhusa za kwenda kusoma elimu ya juu na JWTZ kuwalipia Karo wanajeshi wake imekuwa ni finyu sana wahitaji Wengi hawapati hitachi Hilo la kusomeshwa na Fedha za Jeshi.
Niitimishe kwa Kusema kwamba Hakuna Shaka Kuwa JWTZ inastahili pongezi Leo ikiwa linatimiza Miaka 50 kwasabab limepitwa hatua kubwa za kimaendeleo licha bado linaitaji kuongeza kasi ya kujiletea maendeleo Kwani hapo zamani Wanajeshi Wengi walikuwa hawajasoma lakini Leo hii ndani ya majeshi yetu wasomi ni Wengi na sisi Tunaosoma vyuoni ni mashahidi idadi ya Wanajeshi kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali ili kujiendeleza kielimu inaongezeka. Hongereni sana.
Nakupongeza CDF - Mwamunyange na watangulizi wake na wanajeshi wake kwa kuakikisha Tanzania inazidi sehemu salama ya kuishi kwani Leo hii Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano kwasababu bado haina ingia Kwenye vita licha ya kumekuwepo na baadhi ya watu wachache ambao wamekuwa wakifanya vitendo Vya kuhatarisha Usalama wa nchi yetu lakini hata hivyo vyombo vyetu Vya dola vikiwadhibiti mapema na hatimaye wananchi tumekuwa tukiishi kwa Amani na wawekezaji wa kigeni wamekuwa wakija nchini kuwekeza.
Happy Birthday JWTZ kutimiza Miaka 50 Mwaka 2014.
Makala hii imeandaliwa na :
Happiness Katabazi
Ofisa Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB),
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www:katabazihappy.blogspot.com
Septemba Mosi Mwaka 2014.
Sent from my iPad
0 comments:
Post a Comment