Saturday, 27 September 2014

Re: [wanabidii] WAISLAMU NA WAKRISTO WAIKATAA KATIBA YA CCM

Ngapula.

Nadhani tuachane na hii mada,maana naona hatuwezi kuelewana

Rgrds
Magora

On Sep 27, 2014 6:48 PM, "Ngupula GW" <ngupula@yahoo.co.uk> wrote:
Ndugu yangu Magora,maisha hayaendi hivyo...mbona tunachokiongea ni cha kawaida kabisa na ni sawa?kwa nini wewe huelewi?naamini waislam wengi wanaofuatilia tunayoyaongea wanajua ni ukweli tupo na wanakubaliana nasi....sasa mtu akisema,ndugu zangu waislam,tusiipinge katiba ya sasa kwa msingi wa kukosekana mahakama ya kadhi kwani hata rasimu haikuwa na mahakama hiyo...bali tutafute hoja za msingi za kusimamia zitazounganisha watz...tatizo liko wapi ndugu yangu Magora?....ndugu yangu,badilisha jinsi ya kufikiri na jiepushe na mambo yanayokumiza moyo wako,la sivyo utajikuta uko al shabab somalia...huwa wanaanza hivyohivyo......leo tatizo ni wakoloni,sijui ulitaka hali iweje? Mi nafikiri ni jambo la kushukuru sana kuwa Tanganyika ilitawaliwa na watu wastaarabu kiasi fulani,la sivyo pengine ukristo baran ungekuwa 95% kama ulivyo uislam zanzibar...

Magora Hassan <magorah15@gmail.com> wrote:

Ngapula

Ni bora waislam tuipinge katiba hii kwa msingi wa kukosekana mahakama ya kadhi ili na ninyi Wakristo muikubali ili unafiki ujulikane wazi,matamko mengi yametolewa kulitaka BMK kusitishwa eti tu hakuna maridhiano,leo hii kwa kuwa waislam wataamua kuipinga katiba hii eti yale matamko ya kupinga BMK yatabatilishwa na kuwa sehemu ya kuikubali katiba hiyo. Ni jambo lililo wazi kuwa Wakristo wanaona kama wana hati miliki ya nchi hii na ndio wenye haki ya kuamua kwa niaba ya waislam.Hii ndio sababu leo Ngapula anaongea haya anayoongea. Hakuna shaka juu ya hilo kwa nguvu hii mlonayo leo haikuja kwa bahati mbaya,kwani iliandaliwa na Wakoloni na leo inaendelezwa na warithi wao kwani waliandaliwa kwa zaidi ya karne na haya ni matokeo yake.
Pamoja na yote haya sisi kama waislam hatuwezi kuacha kutetea dini yetu eti tu Ngapula na wenzake hawapendi,la hasha,tutasimamia tunachoona kinafaa hata kama sauti zetu zutapuuzwa lakini ipo siku umuhimu wetu utaonekana na haki itapatikana tu.

Rgrds
Magora

On Sep 26, 2014 5:53 AM, "'Ngupula GW' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Napenda waislam kama mkiamua kuipinga katiba hii basi iwe kwa kuangalia maslahi mapana ya nchii hii na sio kukosekana mahakama ya kadhi...mkiaza kampeni hizo mtajenga mazingira ya wakristo kuikubali katiba hii kwa kuwa tu haijazingatia suala mahakama ya kadhi.....wakristo wengi hatupendi kwa namna yeyote ile masuala ya dini yaingizwe kwenye katiba...ngupula

'Gikaro Ryoba' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Ni jambo lisilopingika kwamba CCM wamejipanga kisawasawa kuhakikisha akidi ya wajumbe inatimia bungeni ili katiba yao ipite bila kikwazo chochote. Hili suala liko wazi hasa ukizingatia kwamba CCM wamependekeza kwamba wajumbe watakaokuwa nje ya nchi wapige kura wakiwa hukohuko waliko. Sababu ya kutumia mbinu hii ni kutaka kuchakachua kura….hii mbinu ni nzuri sana kwa kuwa itawawezesha kuchokmekea kura za maruhani ili hatimaye akidi itimie na katiba ipigiwe kura za NDIYO bungeni kabla ya kuileta kwa wananchi.
 
Sababu ya pili itakayoifanya katiba hii ipite ni ukweli kwamba CCM wamekuwa wakitumia fedha nyingi sana kuwarubuni wajumbe wa kundi la 201 ili wawasaidie kupitisha katiba mpya, ijapokuwa kuna baadhi ya 201 ambao hawatetereshwi na hila za CCM.
 
Hili sio jambo la kushangaza kwani CCM wamejizatiti vizuri kuhakikisha kwamba hiyo mbinu yao ya kilaghai inafanikiwa. Ila kitakachonisikitisha sana ni ikiwa wakristo na waislamu waliopo uraiani wataipigia kura ya NDIYO katiba iliyopendekezwa. Hii hasa inatokana na sababu zifuatazo:
 
1.      Mahakama ya Kadhi yamezikwa na CCM waziwazi na hawataki hata kuyazungumzia. CCM wamefanya hivi kwa kuwa wanajiamin

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment