Tumejadili na mteja wangu Saed Kubenea,na kukubaliana haya;
1.Tutakatia Rufaa katika Mahakama ya Rufani Tanzania sehemu ya Uamuzi wa Mahakama Kuu katika kipengele cha Mahakama kusema kwamba pamoja na kwamba BMK lina mipaka na linatakiwa kutekeleza mamlaka yake kupitia (on the BASIS OF) Rasimu na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya M.y.K, yenyewe Mahakama haina mamlaka ya kusema nature na extent ya ammendments na improvements za Rasimu.
2. Tutakatia Rufaa pia kwamba baada ya kusema BMK linaweza ku-ammend na ku-improve Rasimu, Mahakama ilitakiwa kusema kwamba ammendments na improvements ni tofauti na kutoa kabisa vifungu kadhaa. Kwamba ni suala la uwazi na clarity.
3. Jumatatu au Jumanne tutawasilisha Notice of Appeal Mahakama ya Rufaa wakati tukisubiri tarehe 7 October kusomewa Hukumu yote kwa urefu na Mahakama ili tuweze kuona reasoning ya Mahakama katika maeneo kama BMK kukusanya maoni. Tulizungumzia hili kule.
4. Tunaangalia pia uwezekano wa kufungua Shauri chini ya Hati ya Haraka katika eneo fulani la Mchakato. Win, lose or draw, tunaamini ni muhimu kuishirikisha Mahakama.
Tunaishukuru Mahakama Kuu kwa kile ilichofanya kwa uwezo wake, na imechangia sana maendeleo ya Sheria na ya Mchakato mzima. Ila bado tuna kiu katika maeneo tuliyoainisha, na tunaona Rufaa ni muhimu.
Kwa nini tunakata Rufaa wakati BMK linaelekea mwisho?; Mchakato hauishi mpaka kumalizika Kura ya Maoni. Anything can happen in between.
Peter Kibatala,
Wakili.
On Thursday, September 25, 2014 4:17:12 AM UTC-7, Jane Mwakalukwa wrote:Mahakama Kuu ya Tanzania iliyokaa chini ya Judges Augustine Mwarija, Aloysius Mujulizi na Dr Fauz Twaib imetoa uamuzi wake leo kufuatia maombi ya Saed Kubenea kama ifuatavyo;
1.Kuna mgongano mkubwa kati ya toleo la Kiswahili na Toleo la Kiingereza la kifungu cha 25 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
2. Kwamba pamoja na mgongano huo, Sheria imekusudia kwamba Madaraka ya Bunge Maalum la Katiba yatatekelezwa kupitia Rasimu ya Tume ya M.y.K kama ilivyowasilishwa kwake.
3. Kwamba mamlaka ya BMK yana mipaka, na kwamba madaraka yake yanaongozwa na na kutekelezwa kupitia Rasimu. BMK linaweza kubadili na kuboresha mapendekezo yaliyomo katika Rasimu mradi tu maboresho yasiende kinyume na misingi iliyowekwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya M.y.K, kama ilivyokuwa pia kwa Tume.
4.Mahakama Kuu haina Mamlaka ya kuamua ni kiwango gani BMK inaweza kuboresha Rasimu kwani hilo ni suala la kisiasa, ingawa BMK inafungwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya M.y.K.
Tumeridhika na maeneo kadhaa, ikiwemo msisitizo wa Rasimu hasa kwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema Rasimu ni "working document tu".
Kuna maeneo hatujaridhika ikiwamo Mahakama kusema haina mamlaka kuamua kiwango cha maboresho ya BMK vs Rasimu.Tutatoa taarifa zaidi baada ya kujadili.
Peter Kibatala,
Wakili wa Saed Kubenea.
On Thursday, September 25, 2014 2:16:31 PM UTC+3, Jane Mwakalukwa wrote:--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment