Monday, 1 September 2014

Re: [wanabidii] HAPPY BIRTHDAY JWTZ 50 YRS , 2014

Naam nakupongeza nami. Si watu wote hukubali kirahisi makosa. Pia unaweza kuamua kulekebisha au kurekebisha kiswahili
--------------------------------------------
On Mon, 9/1/14, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] HAPPY BIRTHDAY JWTZ 50 YRS , 2014
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, September 1, 2014, 11:18 AM

Asante
Mokili,nitalekebisha.

Sent
from my iPad
On Sep 1, 2014, at
5:00 PM, "'mokili juma' via Wanabidii"
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

Asante
Happy.Umefanya
kazi nzuri katika makala yako, maana umechambua mazuri yote
yalofanywa na "Babu Mnyange" na wenzake wote bila
kumsahau mhe. Dkt Jakaya Kikwete. Pia nimefurahi kupata
habari kuwa wewe Happy ni Afisa Habari wa UB. Ila ndugu
yangu, upande wa lugha bado unahitaji kuongeza bidii zaidi
ili uwe mahiri katika fani yako. Kwa mfano umetumia sana
neno "dhana za kivita" badala ya "zana za
kivita". Aidha, nahisi kutokana na "lugha ya
mama" umetumia herufi "a" pale ambapo
ilihitajika "h". mfano "linaitaji",
"kuakikisha", n.k.Otherwise,
Hongera Happy.Mokili
J.J.

On Monday, September 1, 2014 10:02 AM,
'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:





<photo.JPG>


HAPPY
BIRTHDAY JWTZ  50 YRS,  2014
Na
Happiness KatabaziLEO
Septemba Mosi Mwaka 2014 , Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania ( JWTZ), linaloongozwa na Jenerali Davis
Mwamunyange "Babu Mnyange au Mchuna ngozi'',
limetimiza umri wa Miaka 50  tangu lilipoundwa rasmi
 mwaka 1964.
Namuita
' Babu Mnyange', Mchuna Ngozi' , kwasababu Moja,
mwanangu Queen Mwaijande 'Malkia' akimuona kwenye
Televisheni CDF- Mwamunyange , hawezi kulitamka Jina hilo
kama lilivyo analitamka hivi ' Babu Mnyange
'.
Na
kwakuwa Miaka ya nyuma  kuliibuka matukio ya uchunaji
binadamu ngozi huko Mkoani Mbeya.
Mwamunyange
yeye ni Mnyakyusa toka Wilaya ya Kyela na Mwaijande  yeye
ni Mnyakyusa wa Tukuyu
- Masoko Mkoani Mbeya, hivyo Mimi Huwa nawataniaga wote
hawa ni watu wanaotokea Mkoa wa Mbeya hivyo wote ni  '
Wachuna Ngozi''.
Kabla
ya kwenda Mbali , napenda ni tangaze Kuwa Nina maslahi ya
 JWTZ Kwani wazazi wangu ni watumishi wa Jeshi Hilo na
Familia yetu  inatibiwa Katika Hospitali ya Jeshi Hilo
Lugalo na watoto wote tuliozaliwa Katika Hospitali hiyo na
hadi sasa tukiugua tunatibiwa Katika Hospitali hiyo hivyo
 na mimi binafsi kupitia kazi yangu ya Uandishi wa Habari
nimeripoti habari nyingi za jeshi hilo tangu Mkuu enzi zile
Mkuu wa Jeshi hilo akiwa Jenerali Mstaafu, Wilfred Mboma
hadi sasa JWTZ Inaongozwa na Jenerali Mwamunyange.
Hivyo
haya ninayoyaandika ninayafahamu Kwani mengine
nimeyashuhudia  kwa macho na mengine nimeelezwa na baadhi
ya Wanajeshi ambao ni marafiki zangu na wengine ni mashabiki
wakubwa wa makala zangu ila  siwezi kutaja Majina Yao
kwasababu siyo wasomaji wa Jeshi.
JWTZ
ilizaliwa Mwaka 1964 baada kuchukua  nafasi iliyokuwa
ikishikiliwa na Jeshi  la Kikoloni  la King's African
Rifles (KAR) lilovunjwa  baada ya kutokea kile
kilichoelezwa kuwa ni machafuko  ya Januari 1964.
Leo
wakati  JWTZ  Ikitimiza Miaka 50 tangu kuzaliwa kwake, pia
ndiyo siku aya hitimisho ya maadhimisho ya sherehe hizo
yaliyofanyika kwa zaidi ya wiki moja huko Zanzibar ambapo
tumeongea Michezo mbalimbali imefanywa na Askari wa JWTZ pia
tumeshuhudia maonyesho ya silaha za kivita zilizokuwa
zikionyeshwa na  JWTZ Katika kambi zake mbalimbali na Hilo
limedhiirisha Jeshi letu lipo imara na ina vifaa Vya kisasa
na lipo timamu wakati wowote Kupambana na adui ambaye
atatuchokoza.
Wakati
jeshi letu linatimiza Miaka 50 , wanajeshi wetu wamefanya
mengi licha ya kushiriki kwenye ukombozi wa nchi nyingi za
kusini mwa Afrika, kushiriki shughuli za kulinda amani
" Peace Keeping'  nchi
mbalimbali ikiwemo Kongo, Sudan, Liberia ili kuhakikisha
zinakuwa huru kama ilivyo kwa Tanzania,JWTZ, imekuwa ni
tanuri la kuyapika baadhi ya majeshi mengine ya nchi za
Afrika.
Wananchi
wenzangu waliopata fursa ya kutembelea maonyesho hayo
watakubaliana nami kwamba jeshi letu sasa limekubali
kubadilika na sasa limeanza kufanya kazi Kisayansi na
Kiteknolojia na kwamba limekataa kuendelea kufanya kazi zake
gizani na wasiwasi mithili ya mtu anayeoga
barazani.
Binafsi
Nikiwa mtoto wa Mwanajeshi niliyezaliwa na kuishi  pale
' Area D' Lugalo Block Namba 19,
Dar Es Salaam,  Enzi zile za Miaka 1979  hadi 1989 na
kusoma shule Chekechea Service na kisha darasa la kwanza
hadi la tatu katika Shule ya Msingi Lugalo Dar es Salaam
na  ' Pololo la JWTZ limenikuza' , Kwasababu Baba
yangu Mzazi Thadeo Katabazi alikuwa Mwanajeshi wa JWTZ na
mama yangu Mzazi Oliva hadi sasa bado ni mtumishi raia
kikosi cha 521 KJ.
Natoa
  pongezi kwa wafanyakazi wote wa JWTZ na Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa, chini ya Waziri Dk.Hussein Mwinyi
kwanza kutimiza umri wa Miaka 50.
Pili,
kwa  uamuzi wake wa
kuondokana na fikra za kizamani za kuficha ficha dhana za
kivita kwenye maandaki  kwa kisingizio  kuwa maadui zetu
watafahamu jeshi letu lina zana zipi za kivita.
Kwani
 tangu Jenerali Mwamunyange ateuliwe na Rais Jakaya Kikwete
kuongoza JWTZ, Septemba mwaka 2007, kuongoza jeshi hilo sote
ni mashahidi tumekuwa tukiona JWTZ katika sherehe mbalimbali
ikituma wanajeshi wake kuonyesha dhana zake za kivita,
makomando wa JWTZ  wamekuwa wakitoa 'SHOW' pale
Uwanja wa Taifa katika sherehe mbalimbali
kitaifa. 
Binafsi
napenda sana ' SHOW'
inayotolewaga na Makomando wetu kwani ' SHOW' hizo
zimetufanya tujue kazi ya Komando ni nini na kwamba ni kweli
JWTZ ina makomando hodari na kufahamu kuwa kumbe Komando ni
binadamu kama sisi kwani hapo awali kabla hatujawaona  
Makomandoo  'wakitoa  'SHOW' tulikuwa
 tunajiuliza HIvi Makomandoo ni  watu wa aina gani?Je ni
binadamu Kama sisi? 
Sasa
kupitia SHOW ya Makomandoo hao tumeweza kutambua kuwa
Komando ni binadamu kama binadamu wa kawaida ila tofauti ni
kwamba Komando ana mafunzo makali ya mazoezi ya kumkabili
adui kuliko sisi raia na hata askari wengine ambao si
Makomandoo.
MKuu
wa KIkosi  Cha   521KJ  Lugalo Hospital, Dk.Makele  na
uongozi wa JWTZ  Nawapongeza  kwa kuleta    Mabadiliko
makubwa Katika kikosi hicho ambacho kinaendesha  Hospitali
Kuu ya JWTZ Lugalo  Kwani chini ya uongozi wake   Duka la
Madawa ambalo linahudumia wagonjwa wanaofika hospitalini
kutibiwa kwa kutumia  vitambulisho Vya  Bima ya
Afya.
Kwani
hapo zamani Duka Hilo la kuhudimiwa wagonjwa wanaotibiwa kwa
kutumia vitambulisho vya Bima ya Afya halikuwepo, Hali
iliyokuwa ikileta Usumbufu kwa wagonjwa walikuwa wanaotibiwa
 Kwa kutumia Bima ya Afya kwenda kuchukua dawa maduka ya
madawa nje ya hospitali hiyo.
Chini
ya Uongozi wa CDF- Mwamunyange , Hospitali ya Lugalo  
imeweza kupanuliwa na kuboreshwa na inaendelea kupanuliwa
pia hospitali hiyo hivi sasa ina  Chumba Cha kulaza
wagonjwa mahututi(ICU)  na pia Hospitali Hiyo imepandishwa
 hadhi na kuwa Hospitali ya Rufaa.
Aidha
Katika uongozi wa CDF- Mwamunyange tumeshuhudia wodi ya
watoto iliyokuwa ndani ya eneo la Hospitali ya Jeshi
Lugalo, kuamishiwa katika ndani ya eneo la kombani ya Bendi
ya Jeshi Hilo Mwenge Dar Es Salaam, ambapo wodi hiyo Bado
ipo ndani ya kikosi Cha 521KJ I nafanyakazi saa 24
na huduma zake niza uhakika.
Pia
napongeza manesi,madaktari, wahudumu wa Hospitali ya Lugalo
Kwai wamekuwa na nidhamu ya Hali ya juu kwa kupokea na
kuwahudumia vizuri wagonjwa Ndio mAana hatuzikwi wananchi
wanaofika hospitalini hapo kupata huduma ya matibabu
wakilalamika Kuwa wanapata huduma mbovu na wahudumu
wanawatolea maneno machafu.
Katika
Utawala wa Rais Kikwete tumeona siku ile Kikwete anaenda
kuzindua Makao Makuu ya Kikosi Cha Askari wa Miguu( Land
Force ) , alitangaza kuwaongezea Mbele umri wa Miaka mitatu
ya kustaafu Wanajeshi wetu .
Wakati
Leo JWTZ ikisherehekea Miaka 50 , tumeshuhudia mabadiliko na
kange zako la mishahara na lesheni kwa Wanajeshi wetu na
Wanajeshi wenye shukurani ukikaa nao wanamsifu sana
Mwamunyange wanasema ni kipenzi Cha wanajeshi Kwani
anapigania maslahi Yao na pia wanaiopongeza Rais Kikwete
Kwani Katika Utawala wake ameweza kuijali sana
JWTZ.
Aidha
tumeshuhudia ndani ya Miaka 50 ya JWTZ  ,ujenzi wa nyumba
makazi ya Wanajeshi na familia zao inashika kasi Kwani ndani
ya eneo la Lugalo Hospitali,  ujenzi wa makazi ya wanajeshi
inazidi kushika kasi na majengo mengine
yamekamilika na Tayari Wanajeshi na familia zao
wanaishi.
Septemba
2007 wakati Mwamunyange alivyoapishwa Ikulu na Rais Kikwete
kushika wadhifa huo wa Ukuu wa Majeshi Nilikuwepo, na
Alisema hatawavumilia wanajeshi wake watakaobainika
kuwapigia raia na kwamba ataamuru wafikishwe Katika mahakama
ya kiraia washitakiwe.
Ni
kweli tumeshuhudia baadhi ya Wanajeshi wakifunguliwa Kesi
kati Mahakama za kiraia. Mfano mzuri ni wale Wanajeshi
waliyoshitakiwa kuwa kosa la mauji ya Swethi Fundikila na
Mahakama Kuu Kanda Ya  Dar Es Salaam, ikawakuta na hatia  
na
kuwahukumu Adhabu ya kifo.
Aidha
Mwaka Juzi tulishuhudia zaidi ya Wanajeshi wa tano
wakifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa
la Mauji ambapo walilitenda karibu na Kituo Cha Polisi Kawe
ambapo waliomua raia kwa kipigo.
Pia
Mwaka Juzi tulishuhudia Kanali Ayoub Mwakang'ata ,
Kanali Felix Samilani wakifunguliwa kesi ya matumizi mabaya
ya madaraka Na. 163/2012, Katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Mbele ya Aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo
ambaye kwasasa ameamishiwa   Mkoa wa Kagera, Alocye
Katemana , Aprili 23 Mwaka
huu,   alitoa hukumu ya kuwaachiria Huru maofisa Hao wa
juu wa Jeshi baada ya kuona hawana hatia.
Binafsi
Kesi hii ambayo ilisababisha maofisa wa juu wa ngazi ya Cheo
Cha Brigedia Jenerali kufika mahakamani hapo kutoa ushahidi
wa Kuwatetea maofisa Hao Kuwa hawajatenda makosa
waliyoshitakiwa nayo.
Hata
hivyo tangu kesi hii ilipoanza hadi kumalizika, nilishuhudia
Askari polisi walikuwa waniogopa kuwasogolea wanajeshi Hao
na nilipokuwa nawahoji ni kwanini Polisi hawawalindi  sana
maofisa hao wa JKT  Kwani nao Mbona ni washitakiwa Kama
washitakiwa
wengine.
Polisi
walikuwa wakinijibu wakisema Hao maofisa wa JKT ndiyo wenye
nchi. Nikawa nacheka sana. Na baadhi ya   Wanajeshi wenzao
wakati wote wa Kesi walikuwa wakija kuwasindikiza na
kusikiliza kesi hiyo .
Binafsi
nilipata fursa ya kuiripoti Kesi hiyo tangu ilipofunguliwa
siku ya kwanza hadi ilipomalizika Aprili 23 Mwaka huu. Kesi
hii ilinifundisha Kuwa Wanajeshi wetu wananidhamu ya Hali ya
juu na wanamshikamano.
Kwani
ingelikuwa ni majeshi ya nchi nyingine, siku ile maofisa wa
JWTZ wanafikishwa Katika Mahakama ya Kisutu '
Pangechimbika bila Jembe' , na ndiyo mAana msafara wa
maofisa Hao uliotokeoa Makao Makuu ya Takukuru , Upanga Dar
Es Salaam, ulisindikizwa na Brigedia Jenerali mmoja kwaajili
ya Ulinzi na hata polisi walikuwa hawasogelei Yale Magari
walivyokuwa wamepanda  maofisa Hao.
Sote
ni mashahidi kila kukicha tumekuwa  tukisikia  au kuona
majeshi ya nchi nyingine za Afrika yamekosa mshikamano wake
kweli na hivyo kufikia uamuzi wa baadhi ya wanajeshi wake
kuasi na kuanzisha vikundi vyao haramu vilivyoweka maskani
yake Msituni  na lengo la vikundi hivyo vya waasi limekuwa
ni kupambana na jeshi linaloshika hatamu kwa wakati
huo.
Vikundi
hivyo wa Waasi wa majeshi hayo vinakuwa na Dhamira Kuu  ya
kupindua serikali kisha watwae madaraka, jambo ambalo
limeleta  machafuko   katika nchini nyingi lakini kwa kuwa
Mungu bado anaipenda nchi yetu, JWTZ bado haijafikia hatua
hiyo kwani wanajeshi wake wana mshikamano wa
dhati.
Kwa
wale tunaopenda kutembelea vikosi, makambi ya JWTZ tumekuwa
tukiona zana mbalimbali zikiwamo maghala ya silaha, ndege za
kivita n.k, lakini pindi umuulizapo mwanajeshi hata kama ni
rafiki yako
kwamba ile ni silaha aina gani au komandoo naye anafamilia?
Mwanajeshi ataishia kukujibu kwa mkato "fuata kilicho
kuleta, hizo ni siri za jeshi hutakiwi kujua, umekuja
kutupeleleza na utaruka kichurachura sasa hivi."
Wakati
nikitoa pongezi kwa maadhimisho hayo, nitoe angalizo kwa
jeshi letu kwamba bado wananchi wana imani nalo licha ya
kuwapo kwa baadhi ya vitendo vya utovu wa nidhamu unaofanywa
na baadhi ya askari wa chache, hivyo ambayo wakati mwingine
vitendo hivyo vinalipaka matope jeshi.
Hata
hivyo, hivi sasa jeshi letu limekuwa likitoa ushirikiano
kwa Jeshi la Polisi pindi wanapokamatwa wanajeshi kwenye
matukio ya ujambazi na hatimaye wanafikishwa mahakamani na
mfano mzuri ni Kesi ya mauji maarufu Kama  Kesi ya '
Ubungo Mataa' ambayo inaendelea Katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar Es Salaam, ambayo miongoni mwa washitakiwa ni
Wanajeshi.
Naunga
mkono ombi la CDF- Mwamunyange, katika maadhimisho haya
ambapo katika hotuba zake kila alipokuwa akitembelea kambi
zake pamoja na mambo mengine alikuwa akiwaomba  raia wawe
na uhusiano mwema na jeshi hilo. Lakini napenda kutoa
angalizo kwamba uhusiano mwema kati ya pande hizo mbili uwe
na mipaka na masilahi ya kwa nchi.
Uhusiano
mwema huo usiwe ni ule wa baadhi ya wanajeshi wetu kutumia
mafunzo ya kivita waliyoyapata kwenye vyuo vyao vya kijeshi,
wakaanza kutoa mafunzo hayo kinyemela kwa baadhi ya wananchi
watukutu ili mwisho wa siku waunde magenge ya kihalifu kwa
maana ya mwanajeshi anatoa mafunzo kwa raia, silaha na
kumcholea michoro ya kwenda kufanya ujambazi.
Na
baadhi ya Wanajeshi   ambao nimekuwa nikiwadadisi kuhusu
hali hiyo kila mmoja wao kwa nafasi yake wamekuwa wakinijibu
kwamba Kurugenzi ya Habari ya jeshi haipo huru hivyo na wao
imekuwa ikiwawia vigumu kuwasilisha maombi yetu kwa maafande
wao.
Ni
rai yangu kwa Jenerali Mwamunyange na makamanda wako
mlitazame hili, kwa mtazamo mpana, kwani wananchi wanahitaji
kupata taarifa za jeshi lao ambapo taarifa hizo jeshi
litahakikisha linatoa taarifa ambazo hazimnufaishi adui wa
taifa letu.
Sasa
kwa hali hiyo, tunaona kwamba kuna wananchi wanaopenda
kupata taarifa mbalimbali za jeshi letu, wengine wanapenda
kujiunga na jeshi hilo, kutembelea makumbusho ya jeshi
lakini kwa sababu ya jeshi hili ama kwa kushindwa kuwa
karibu na wananchi ama kwa kuandaa vipindi maalumu katika
televisheni au redio au kuweka taarifa mpya mara kwa mara
katika tovuti ya jeshi hilo ambalo lilizinduliwa
na Luteni Jenerali Abdulahman Shimbo, pale Upanga Mess,
ambapo nami nilikuwa miongoni mwa waandishi wa habari
tuliohudhuria uzinduzi wa tovuti hiyo, kama wanavyofanya
Jeshi la Polisi hivi sasa ndiyo kuna sababisha wananchi
wengi kubaki gizani kuhusu utendaji wa jeshi letu.
Lakini
cha kushangaza kama si cha kustaajabisha, licha ya JWTZ kuwa
na wasomi wa taaluma ya teknolojia ya habari lakini tovuti
ya jeshi hilo imekuwa haina vitu vingi, ama kuweka taarifa
mpya za mara kwa mara na Sioni  Kama wahusika wanafanya
jitihada za kutangaza Website  ya Jeshi Kwani hata lile
Gazeti la Ulinzi hivi sasa  ni Kama limekufa vile Kwani
halionekani mtaani kwa Wingi na kwa wakati Kama zamani.
Mwamunyange " Mchuna Ngozi' Kulikoni  Gazeti la
Ulinzi? 
Mwamunyange
 kama JWTZ haina   fedha za kulipa kiwandani gazeti la
Ulinzi lichapwe, ni kheri utembeze 'Bakuri' na
utangaze  kuwa JWTZ ' limefulia' halina fedha za
kuchapisha gazeti hilo, naamini  makampuni yatajitokeza
kusaidia gharama za uchapaji kuliko kufanya Watanzania wengi
wasilipate gazeti hilo kwa wakati na wasiwe na uhakika wa
kulipata. 
Hata
hivyo Changamoto nyingine inayowakabili Jeshi Hilo ni kwamba
kuna malalamiko ya chini Kwa chini toka kwa baadhi ya
Wanajeshi wake Kuwa ruhusa za kwenda kusoma elimu ya juu
na JWTZ kuwalipia Karo wanajeshi wake imekuwa ni finyu sana
wahitaji Wengi hawapati hitachi Hilo la kusomeshwa na Fedha
za Jeshi.
Niitimishe
kwa Kusema kwamba Hakuna Shaka Kuwa JWTZ inastahili pongezi
Leo ikiwa linatimiza  Miaka 50  kwasabab limepitwa  hatua
 kubwa za kimaendeleo licha bado linaitaji kuongeza kasi ya
kujiletea  maendeleo Kwani hapo zamani Wanajeshi Wengi
walikuwa hawajasoma lakini Leo hii ndani ya majeshi yetu
wasomi ni Wengi na sisi Tunaosoma vyuoni ni mashahidi idadi
ya Wanajeshi kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali ili
kujiendeleza kielimu inaongezeka. Hongereni sana.
Nakupongeza
CDF - Mwamunyange na watangulizi wake na wanajeshi wake kwa
kuakikisha Tanzania inazidi sehemu salama ya kuishi kwani
Leo hii Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano kwasababu bado
haina ingia Kwenye vita licha ya kumekuwepo na baadhi ya
watu wachache ambao wamekuwa wakifanya vitendo Vya
kuhatarisha Usalama wa nchi yetu lakini hata hivyo vyombo
vyetu Vya dola vikiwadhibiti mapema na hatimaye wananchi
tumekuwa tukiishi kwa Amani na wawekezaji wa kigeni wamekuwa
wakija nchini kuwekeza.
Happy
Birthday JWTZ  kutimiza Miaka 50 Mwaka 2014. 
Makala
hii imeandaliwa na :Happiness
KatabaziOfisa
Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB),0716 774494Chanzo:
Facebook: Happy KatabaziBlog:
www:katabazihappy.blogspot.comSeptemba
Mosi Mwaka 2014.



Sent from my
iPad



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment