Sunday, 30 December 2012

Re: [wanabidii] Fw: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo


Alexander-ninakujibu kwa urefu kukupa zawadi ya mwaka mpya. Mwingine atakae asome au a-delete.

Lakini mimi ni mdau mwenye uchuku wa maendeleo. Nimtume Bwana Unitume Mimi!! Mimi huchukia sana watu wanapoonewa, kujionea na kuuza utu wao wenyewe na kuuza haki zao, uvivu na uzembe kisha kinywa cha lawama. lakini tu sina uwezo na powers.

Hata ktk familia uonevu na dhuluma zipo. Mtu atateseka hasaidiwi majungu tu ya ndugu huyu na yule ila atakapokufa-michango, kukodi mahema na catering services na maziko ya matarubeta.

Ndio hizi tarumbeta tupigazo daily lakini hatuendi makwetu kuongea na watu wetu kuwasihi wabadike baba asiuze ardhi kwa debe la mahindi. Jiulize kuna NGO ngapi na vyama vya siasa vyenye Volunteer services, vikatafuta hela kuufanya capacity building ya diploma na graduate student wakajitolee kuboresha maisha vijijini kusaidiana na  the few GVT workers-teachers, extension staff na kufuatilia utendaji kazi wao? Tupo mijini na lawama na hata huko FGM inakoendelea hadharani CBO/NGo za haki na usawa wa jinsia zipo. Tufanyeje sisi wabantu ktk kujikwamua tukwamue. Ujambazi, mauaji kishirikina, kuchomeana nyumba na kuibiana mifugo-tutalima sustainably saa ngapi? Ndio tutauza ardhi kwa unga wa dona. Tatizo-hata walikofundishwa na TGNP, TAWLA, WLAC, WAT na NGO nyingine sheria ya ardhi kijijini, baraza za sheria, wilayani kwa kutumia vitabu vya kiswahili poa na kuwapa nakala mpaka ya sheria isemavyo haki za wanawake na aardhi ndiko huko utakuta madudu ya ardhi yafanywayo na kamati hizo zilizopata mafunzo. Wameacha maadili ya mafunzo-wanajali ubinafsi-tumboni street. Hii nayo unasemaje?


Ukiangalia Historical Transect ya UKAME na jinsi watu walivyoukabili utaona maeneo mengine survival strategies walikula nyama pori au ng'ombe/mifugo iliyokufa na ikitoka mafunza; walikula sondo wa ktk miti iliyooza; kula panya; konokono. mafunza ya kipepeo yakaayo ktk miembe na mikorosho. Walichemsha ngozi za mifugo walizokuwa wakilalia kupata mchuzi kunywa; walioza wasichana kwa debe la mahindi; alimtoa mke wake kwa gunia la mahindi; walitegemea kashata ya mahindi na asali etc. Kila ecology ina vitu vyake na survival strategies zake. Wengine walihama toka mbali wakaja kuunda taifa la wahamiaji la Tanzania ya sasa. Baadhi, walifanya vibarua na kupewa kibaba cha unga wa njano (pulenda la mkoloni alipokuwepo); ku-process roots, tubers, yams ambazo ni poisonous na kujua jinsi ya kusafisha mpaka kupata solution sweet iliyoisha sumu na kuweza kuishi na yams hizi zipo zinategemewa kuliwa hadi leo njaa iliwafundisha.  Walikula mabanja ya nzige (matoto yake). Mizizi isiyo na sumu kama ming'oko inaliwa Lindi-Mtwara hadi leo.

Kuna mfungwa ktk historia ya Russia aliachwa afe bila kula lakini alipogundua kuwa mkewe aliyekuwa mjamzito alikuwa amezaa na kunyonyesha mtoto-akamwomba anyonye ziwa-akawa mama huyo  anakwenda kumuona na kumnyonyesha kisiri akadumu. Askari magereza na mahakama ikaona yule ni Saint (mtakatifu)-ameishi muda mrefu bila kula akafunguliwa awe huru. Kumbe akinyonya titi na kupata nutrients akasurvive.

Hii ya kuuza ardhi kwa debe au madebe ya unga Lindi-Mtwara kwa sasa-ni survival strategy. wameona wana ardhi kubwa/nyingi .

Tuna makabila hapa TZ kwa sasa pamoja na elimu ya haki za jinsia nao kuhusishwa bado yanamtoa msichana age 10 yanachukua uhamisho shule lakini anahamia kwa mume yeye anapata ng'ombe 2 au zaidi au laki au zaidi hela ambazo hazidumu lakini ameshaharibu maisha ya mtoto. Mwingine anaoza kilabuni kwa vikimbo vya ulanzi, kangara, kindi na mtoto anapelekwa kwa anayempa pombe hiyo daily. Hii unaisemaje na wakishitakiwa wanahonga sana hela kesi inaishia mpaka wanaharakati wanachoka wenyewe!!

Katika kipindi hicho usemacho watu wanakufa njaa maeneo hayo nimeona mengi nikiwa project coordinator wa mradi unaohisaniwa na tajiri mmoja na mkewe waishio Michigan akiwahurumia wa-Lindi.

Nilitumia pesa binafsi zangu kununua mbegu za mahindi, ufuta, mtama., kunde na kupeleka Lindi vijijini shule mbili za msingi na chekechea mpya ikiansaliwa kujengwa. Niliwaomba walime mashamba ya shule ili wawe wanalisha wanafunzi bila ya kununua chakula, wazingatie kilimo bora wamshirikishe afisa kilimo kata na walimu wafundishao masuala ya science na kilimo, geography, ujasiriamali etc ili wapate mazao bora kwa kutumia conservation agriculture. Mzungu akija atatoa hela zaidi kwa kuona juhudi yao. Walikuwa wakiangua minasi ya shule michache iliyopo na kununua unga wa uji hela zikisha basi.
Waliomba power tiller wakatetewa ilikwenda pamoja na mzungu kusema no masuala ya teknologia-trekta, gari etc not sustainable tukanunua kiubabe kutumia hela zake maana ni priority ya walengwa ili wazalishe. Mafunzo yakatolewa vijana 2 ili walime mashamba posho shule na wanakijiji watapanga. Mabonde mazuri, waliomao hupata mahindi, mtaalamu wa Aga khan Foundation yupo hapo kijijini maana tarafa ina kilimo ya umwagiliaji cha mpunga mifereji asili maji kutoka mto. Mabonde MAZURI, sana unapenda uhamie huko ila huwezi kuwa mahali pote.

Nenda Mkuranga nako ukayaone mabonde, kayaone Mtwara na Rufiji ama penye Miti hakuna wajenzi.

Kilichoendelea ni waliopata mafunzo ya power tiller kulala mbele. Pamoja na maelezo ya masharti ya mafunzo na kazi bado walidhania eti wataajiriwa na mradi  badala ya kuwa watumishi wa kijiji. Power tiller toka ipelekwe (waliyoomba wenyewe kwa kilio) haikujengewa kajumba ka stoo ya kuhifadhi iliachwa nje robo mwaka watoto wakachezea na kuchana viti, kubomoa taa zake. Shamba la mtelemko halikupigwa makinga maji. Mbolea mifugo iliyosaidiwa na NGO-CONCERN kibao haikubebwa kupelekwa shamba.

Baadhi ya mashamba ni zero distance kutoka majengo ya shule na umwagaji mbolea ya bure, ufukiaji nyasi kwa mboji-NIL. Uwajibikaji tatizo kubwa. Pamoja na kukubaliana misingi ya kazi majungu yalitawala hadi Mwl Mkuu ikabidi kutumia hela za shule kwa vibarua kuchimbua visiki  na wanafunzi kulima badala ya powertiller na wazazi kushiriki.
Kila ukienda kuna uswahili mpya sio yale mliyokubaliana. Hii hukatisha tamaa hata watumishi wa ugani ambao hubaki kufanya miradi yao ya kilimo na biashara nyingine maana wananchi wapo ktk kupika majungu kudhaniana hili au lile.

Mashamba mengine ya chekechea inayojengwa na mhisani hayakulimwa eti mpaka jengo likamilike!! Makubaliano ni kulima, kuuza na kuweka hela bank shule ikianza zitalipa mlinzi, kununua vifaa etc; ila mwaka shule ikianza chakula kitalisha watoto ambao hawasomi kutokana na umbali wa makazi. hela ya kufungua account, kupiga picha na nauli ya kwenda (Mjini 62 km away)-toka mfukoni kwangu 85,000/=. Quarterly visit unakwenda-story mpya.
Sasa jengo limekwisha kontrakta kamaliza kujenga account haina hela hawakulima-Uswahili na kulalama wakati mtendaji ni wewe kutwa upo barazani unafaidi story na kuunda majungu mapya-viboko vya mjerumani virudi. Tabia hizi za kipuuzi ndio hata kama nchi ichukuliwe na chama kingine, bila ya kutamka suala la uwajibikaji na utendaji kazi (badala ya huduma ya bure eti nchi ina hela, madini, mbuga, gas etc) hayatapatikana maendeleo. Tusiahidi kubweteka, tuahidi kazi, kila mmoja tutamtaka alime, achangie inapobidi.  Turudie kukagua mashamba nani kalima nani hana la cash and food crop, nani hana choo-ajenge kinguvu etc.

Ardhi Bwerere-Ardhi ipo lakini tutajimaliza wenyewe na kuwa watumwa ndani ya nchi yetu tusipoangalia. Na kwa vile nyingi-msukuma na mmasai analima kwake mifugo anapeleka Kilosa, Lindi, Rufiji eti huko mahindi ni majani ya kulisha mifugo. lakini hata akilima huko Rufiji msukuma halishii shambani kwake bali kwa mzaramo. Akiulizwa whyMsukuna na Mmasai unafanya hivyo-eti anapandisha mori, kulia uonevu!! Mbona Magu, Bunda, Maswa, Tarime, Engerosambu, Kitwai, Naitolia, Nyamuswa etc unalima hulishii shambani kwako? Why Kilombero, Ihombwe, madizini, Mabwerebwere? Lioboisirret 10km toka tarangine national park unalima kwa trekta game conservation area, NCA ndani kwa plough mbona mahindi mabichi shambani si lishe ya mfugo umezungusha miti ya miba na nkuifukuzia mbali isipite shambani. Ardi kubwa, ya umma, tunahaki kwenda popote pale bila ya kuvunja sheria. Ni nyingi na ndio maana wanauza kwa unga wa kula. Chief wa Kilwa huko aliuza Kilwa Kisiwani kwa kitambaa cha mita 40 kwa Persian akafukuzwa aondoke. Chief Pazi aliwaahidi wanyamwezi kitambaa cha bafta mita 10 wakiwafukuza wakamba maendeo ya bagamoyo walimtia mimba bintie na wakiwinda Paa kuwauzia wasambaa. Kitambaa hana akawapa ardhi wakae na wanaitwa-Wadoe (Wadoezi) wapo kati ya bagamoyo na Tanga. Historia ya mahindi na ardhi inajirudia.

KTK mradi nilioutaja Lindi Vijijini Shule mpya ya Chekechea ya kujengwa kitongoji cha kijiji kilicho mbali 5+km kutoka kati ya kijiji ilipewa ekari 100 customary land na wazee 2 ili shule ekari 6, shamba 4 jumla 10 na 90 wazazi walio mbali wasogee wajenge karibu ili watoto 3-6 yers wasome baadae kuwe na shule ya msingi maana hata age 10 haendi shule zipo 5+km away. Ila kulima wakalime to mbali ktk mashamba yao.

Unafikiri hao wazee wana ekari ngapi kama wametoa 50 each kuipa serikali-Lindi Rural na Kijiji wajengewe shule na mhisani?

Kijiji kikatoa 50 acres kwa kundi la vijana tuliohamasisha CBO yao jumla vijana wana ekari karibu 500 walizopewa ktk vijiji 5 vya Kata. Ndio maana wanakijiji wanaweza kuuza Ardhi kwa unga, sigara, litre ya tembo-pombe au chochote kile-wanayo hawajafirisika.

Huu mpango wa serikali kupimia viwanja vijana, watu wa mabwepande na wengineo walioathirika-hautofanikiwa bila ya sheria kali na kupiga muhuri Hati ya plot hizo kuwa hakiuzwi not transferable ili kulinda haki ardhi ya waliopewa na kulinda wasiuze kianasa. Watu wanauza ardhi waliyopewa kiurahisi kusaidiwa-anahamia barabarani au kwingine na kuweka msongamano usiotakiwa. Ni sawa hili suala la kufuga na kuhahamaha au kula matunda lakini ukiwa na njaa unapewa unga na kuomba msaada wa mahindi. Why mla matunda usilime na miti inakufa na fungus matunda na mizizi hakuna. Funga nyuki kisasa uuze asali na lima kiasi. Punguza mifugo fuga kisaa nhybrid cows uendelee. walihama ulaya wakabadilika faida ya kupoteza mifugo over 50% kutokana na ukame, kuuana, kupigana kutaisha utaleta maendeleo yako. tatizo ni SIASA kuogopa kukosa KURA utakapowahamasisha na kushuritisha upunguzaji mifugo for sustainable env and livestock keeping. Huitumii SUA vizuri na ipo kwa ajili yako.

Mabondeni-Vijiji bora zamani ardhi cutomary vikawa vijiji nje ya miji sasa ni squatters kwa desturi hii mpaka vingine Waziri wa ardhi anataka vipangwe upya (makongo). Changanyikeni msongamano hovyo, Goba pia wameuza ardhi msongamano barabarani hata moto ukiwaka zimamoto haina pa kupita. Makongo ndio balaa gari likisepetuka limo ndani ya majumba. Vichwa vyetu vina nini?

Bonde la Msimbazi-Jangwani- Kigogo. Ramani ya City 1979 inakuonyesha ni hazardous area na ndio maana nyumba hata za mkoloni-quarters za vigae za eneo la Kigogo; Nyumba za vymva 6 na zile nyingine ndogo-hazikujengwa mabondeni. Za Kinondoni hazikujengwa bondeni Hannanasif, au mwananyamala bondeni au jangwani. Za magomeni ziliishia round about ya magomeni mapipa sio Sunna walikozamishwa na maji. Kwani Serikali ni Kichaa? Mbona majengo ya Muhimbili na Jangwani Secondary school hayakushuhwa bondeni Jangwani Mto Msimbazi-Jiulize? Ule upole wa GVT na kuwaacha wananchi kwa muda mrefu wabomoe kwa hiari yao ili wachukue vifaa wapewe usafiri wakajenge huko waliko na ubinadamu wake wa kiafrika GVT ndio unaacha ujenzi uendelee.Kwa vile ni Vipofu na Viziwe hatujifunzi jinsi tulivyopoteza mali nan uhai wa watoto/ndugu eti tunarudi tena pale pale. Mtoto akililia wembe-mpe. Hata ulaya hugomea onyo la hali ya hewa na tunawaona wakielea kupitia TV. Ubishi na tabia ya binadamu, sheria kali ikitumika polisi na wahusika wataviziwa na kuuawa mitaani ndio tunaogopa. Kwani polisi na maafisa tunaishi nao huko mbananoni mitaani. Mokoloni aliwaweka mbali kambi na majumba maalum. Kuiacha hii wapo pasipo ulinzi inaleta utata ktk kutekeleza sheria kali.

Mradi wa UNDP-ILO Assist umeboresha Hannanasif-wameuza nyumba zao, wakaaza kukusanya takataka na kufugia mto msimbazi kujenga. Hii ni pamoja na kuwekewa mifereji ya kutupa maji, kuwekewa SACCOS na kupata mikopo ya biashara ndogondogo, kuboresha hapo kuna zahanati. Na sasa wamefanya kinyume, vyoo wameunganisha katika mifereji wazi (kinyume) na mafuriko yakawaelekeza maisha kwa kukiuka mradi walioufiku kuwakomboa na maisha na mafuriko-Vichwa pumba? Kuna Cassino, bar, bar, lodges, saluni za kumasaji watu vindevu-serikali ikutendee nini uione inakupenda? Wewe unaisaidiaje ili usaidike vizuri. Mbembe punda hadi mtoni hutoweza kumfungua kinywa anywe maji hadi atake mwenyewe. Hatubebeki. Hata uzoaji takataka upo decentralized. Hatawaki kuchanga hata 500/= kwa wiki baadhi ni 10,000/= kwa mwezi na wana lodges, magenge kuzalisha takataka bali kutupa usiku barabarani na kumwaga kinyesi ktk open stormwater drainage system. Wanasogeza na kung'oa mawe ya Mh Mangufuli na kujenga barabarani. Greda likienda kubomoa-maandamano. Lori likiparamia nyumba na moto kuwaka kuua watu-serikali mbaya. Wanapofunga kuta mtaa mzima hakuna pa kupita-tuseme ajali za moto hatuzioni? Ni sawa na mwendesha bodaboda ambaye anaona wenzake walivyokufa, kukatika miguu-anaendesha bodaboda kavaa ndala, kufia kaegesha mgongoni, kapakia watu 3 anaovertake hovyo, na hao 3 hawanakofia na wala hawathamini uhai wao-Serikali iongeze sheria ya bodaboda iwe kali. nanyi mmepanda 3 kwa huyo mwenye ndala. Hamuwezi kususia msiipande mpaka awe na kofia na amevaa rubber shoes hata kama ni mtumba wa 500/=. Mikanda ya ndala ikinasa ktk pedeli si mtaanguka?

Usimamizi raslimali na uzembe wa GVT-Tenganisha ajira ya mtumishi wa umma na Siasa. Fukuza mzembe. Mtu anauza customary land yake anaondoka Lindi anahamia Rufiji kwa mjomba ambaye ana over 100 acres. Hela anachezea hafanyi maendeleo yoyote. lakini uuzaji usingatie sheria. Viongozi kijijini wasimamie hilo. tatizo tunaogopana na ndio maana hata Warundi wanajaa na mifugo na tumewapa ardhi wenyewe, kuwaoza watoto wetu kisha tunalaumu GVT lakini viongozi na wenye customary land wamewaweka kwa mafao yao binafsi pamoja na wahusika wengine. Ulinzi shirikishi, majeshi ya mila, wazee wa mila wapo wapi kuwaasa wanaopotoka-Serikali!! kamati ya Ulinzi na Usalama Kijijini kulikoni. Hata wazee wa mila kumuonya kiongozi au mzee/mtu atoaye ardhi kwa wageni kinyume sha sheria NILI? wakakata miti msituni-wanawaajiri kubeba mbao au kukata na kubeba kunia za mkaa au wanawauzia mkaa wanapata hela za kugharimia vita vyao kwao na kununua mifugo zaidi. Mmelala?

Uzembe wetu wote tuisaidie serikali. Mnakaa kikao kijijini mnaandika ghost names, mnatia sahihi kwamba walikuwepo hao wananchi ambao hawakuwepo, inakwenda wilayani imesainiwa kijiji, Kata, Tarafa, mwekezaji anaipeleka wilayani, TIC anapewa eneo-kumbe mmepeana visenti mmetumia udanganyifu. Huko juu wanajua njia rasmi kisheria imetumika lakini mmemshauri mwombaji atoe hela mharakishe kumbe ulani wenu. Wageni wengine tunawafundisha uovu sisi hata jinsi ya kuwaunganishia mita za umeme ili wasilipe mamilioni Tanesco badala yake laki 3 uwe unapewa wewe kila mwezi Tanesco analipwa laki badala ya mamilioni. Kwa jinsi hiyo wageni wamepanga NHC houses wamekupa wewe millioni 50 ukahama kaingia anaishi humo wamejazana humo wengi kukala kwa zamu vyoo vinafurika  wanatiririshia nje maana hawezi kufika DAWASA-NHC kuomba huduma hawamjui wataomba na passport na hati ya uhamiaji. Tupo nasi kuhujumu nchi yetu na wanatucheka ujinga hao tuwawekao iwe sisi na uhamiaji wote manzamane. Uzembe wetu wote kwani serikali ni nani kama sio uongozi na watu wake. hata katika familia wapo watu wasomi na akili zao wanadhulumu mali ya marehemu kumnyang'anya mke/mama mfiwa watoto na haki zake-kisingizio MILA kumbe ni uroho binafsi.

Hata kudumu kwa ukeketaji-MILA. Lakini wanaume wakisema 'NO' tutaona wasiokeketa sio wanaokeketwa FGM itakwisha tu. Mbona hamsemi ndio kwanza ubinafsi unatumika kusingizia mila.

Mwaka mpya 2013 uje utufumbue macho wote ktk majukumu yetu tuwe na mtazamo chanja tuache uharakati wa kisiasa na dira ya mapato binafsi ya kuzima njaa bali ya maendeleo yetu na nchi yetu.

Pamoja na kusema haya-sio kila eneo la TZ linanuka uozo. yapo maeneo yanafanyakazi vema na ni vijiji au wilaya za kuigwa. Tujifunze pia kutoka humu humu sio toka nje tu ambapo mifumo yake ni tofauti na yetu. Tunaweza, tukiamua kujibadilisha, itawezekana.


--- On Sat, 29/12/12, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Fw: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 29 December, 2012, 16:26

Sasa Hilda Serikali imepewa mamlaka yote inashindwa nini kuwawajibisha watu wake? Unachekaje na mtu mzembe ambae baadae anakuja kuchafua utendaji wako wakazi na kukushushia credibility kama serikali? 

Majuzi huko huko Lindi na Mtwara tumesikia watu wamebadilishana ardhi na Mwarabu kwa SEMBE kisa kijiji kina njaa. Fikiria jambo kama hili lina tia hasira. Mkuu wa mkoa asieweza kuwabana watu na wakalima mashamba ya kutosha kwa ajili ya chakula na ziada anafaida gani? Mpaka watu wamempa mwarabu ardhi kwa unga karne hii ya 21, tutafika kweli??

Kama hilo halitoshi angalia ngonjera za makazi ya mabondeni serikali inasema bila hatua mathubuti mwisho watu wanakuja kuelea juu ya maji wakati wa mafuriko, why? Kwanini wapinzania nao wasipenyeze agenda zao hapo nakupata popularity?

Mimi naona uzembe wa utendaji wa serikali na usimamizi wa rasilimali ndio utakao leta athali zote hizi, na hata za ukabila na sivingenevyo. Maana unapoacha mwanya ndipo wengine wanapenyeza hata agenda zao za kugawa taifa. Serikali iamuke huko iliko lala ifanye kazi zake.


From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, December 29, 2012 5:02 PM
Subject: Re: [wanabidii] Fw: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo


Ni kweli hata umeme mtumiao Dar wengine wamehamishwa milimali walikokuwa wakila upepo mwanana ili huku DSM na kwingineko mfaidi umeme wao hawana. Nyumba ya Mungu wanaondolewa daima wasihalibu bwawa Nchi ipate umeme. Daraja la Mkapa, Dar Lindi-Msumbiji road inayotegemewa kuunganicha nchi 2 hela zilitoka ktk gas yao?
Hadi nyama -beef huko nyuma 1970s ikitoka Dar kupelekwa kwa ndege Mtwara na lift kuu ilikuwa ndege za JWTZ unapanda bure wakati mto Rufiji umefurika kikomo na Milima ya Lukumburu Songea bus la wahindi la TTCO haliwezi kupita kutokana na tope!! Meli imejaa kikomo, ukiiona ndege ya JWTZ angani-unakimbilia airport. Hiyo ndiyo TZ ya zamani.

Utakaporudi TZ na itakapotokea kazi katika taasisi yako uliyopitia huku TZ-ya kwenda migodini for EIA/SIA utaombewa fursa ili uende ukaone mwenyewe iwe Handeni gold mines, Geita au kupya kokote kule na hata Mererani wapo waliofanya research za dissertation. Ukaone jinsi ardhi ni yao, wanaambiwa wajiunge waunde kampuni ya artisanal miners, mwekezaji anunue anawalipa mamilioni na kisha wanakuwa wabia-kazi hasa na vyombo vya uchimbaji hawana, migodi inawafukia daima wanakufa. Na wakifa watu ndio wanahaha kuingia ndani ardhini kwa pupa eti sasa ndio mapato yataongezeda (sadaka-damu isha mwagika). Kweli sikio la kufa ni la kufa. kati ya wahojiwa 100 utapata 6 tu waliotumia mapato ya madini ktk kujiendeleza economically na socially. Starehe!!

Umoja unakuta haba au hakuna, waliounda huo umoja au kampuni majina ya wenzao hayapo yapo mengine ghost names wamewaacha na kuwadanganya wenzao. Inamfanya mwekezaji apate utata mkubwa ulioje vurugu inazagaa. Lesseni ya kupata eneo lenye bocons na fenced lenye lina madini mbongo atalipa 20,000/= unapanuanua hapo. Ugumu ni nini?
Ni bia ngapi mtu anakunywa na hela nyingi kuhonga changu doa wanaojaa huko migodini? Kila mtu ana kihirizi chake ubinafsi unatawala. Ni vibanda vibana na vileo n.k. inaumiza sana.

Bahati nzuri nimesoma secondary Mtwara na nimefika huko baada ya shule na miaka ya karibuni hadi lindi, nachingwea, Newala. ardhi na misitu si mchezo. Kijana gari alime pamoja na mabonde hayo na mashirika yanayosaidia traditional rice irrigation. kama kila mtu amiliki ardhi atakavyo isiwe ya GVT chini ya Rais-huoni kama tutakuwa kama nchi jirani kuhodhi kiukabila au kwa kipato. Tunaweza kutaua matatizo yaliyopo kama hatutajali kukosa KURA na hasa kama watatenganisha Ajira serikalili na uongozi Kisiasa. yaani-Diwani, Mbunge asiwe mwajiriwa serikalini kushika madaraka kiserikali maana maamuzi muhimu yanazuilika ili usikose KURA na kula.

Kinawazuia nini umoja wa wachimbaji wadogo wadogo mahala-Mererani etc kununua maeneo makubwa? kinawashinda nini matajiri bongoland kuunda kampuni moja kuwa wakaajiri wazungu toka ulaya na maijinia bongoland na vibarua wengine kuzalisha hiyo gas. wakanunua mitambo, wazungu wakafundisha vijana na mwisho kampuni hilo likabobea kuzalisha umeme na kutoa ajira? Vivyo hivyo katika madini-wakaunda kampuni ambayo itachimba huku na kule na kuajiri wabongo? nao wanavijiji wakaacha kuchimba chini kwa chini kuingia kuiba madini kuliko nunuliwa na kampuni? wanafanyiana hivyo hata katika artisanal area. Na ukienda machimbo ya artisanal miners utakuta mmiliki eneo kijadi ndio owner, anawaacha wachimbe, broker ananagharimia chakula wachimbaji magunia yakipatikana anapewa customary owner gunia zake kulingana na makubaliano. Mawe ktk gunia zilizobaki yanakuwa processed. Madini yakipatikana yanauzwa, broker anakata matumizi aliyogharimia kwanza kabla hawajagawana faida iliyobakia. Sasa nani hamiliki ardhi hapa katika mfumo huu uliopo kule ambako watu hawakununua maeneo bali wanachimba katika ardhi ya mtu mwenye eneo-customary owner. Budi kujifunza mifumo iliyopo halafu kupata suluhu.
Nimechangia

--- On Sat, 29/12/12, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] Fw: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 29 December, 2012, 14:43



Wanamabadiliko,
Nafikiri Waziri ametoa hoja nyepesi kutaka kuzima hoja ya watu wa Mtwara.

Waziri akumbuke kua tatizo la watu kutofaidika na raslimari zinazopatikana katika maeneo yao nikubwa sana Tanzania. Hebu jamani fikiria kwa Tanzania haki ya mtu kutumia ardhi inaishia kwenye surface soil (crop cultivation only). Hii inakuja kweli?? Nafikiri kunahaja yakua na tafsiri pana ya haki zinazo ambatana na ardhi ambayo mtu amekua akitumia kwa miaka mingi. Ikiwezekana to borrow definition ya James kua 'Land include much more than just physical soil or substance. It include for instance, building, and any other thing attached permanent to the soil or permanently fastened to anything which is attached to the soil (James 1971)

Kwa Tanzania nitofauti, vitu vyote vilivyochini ya ardhi ni mali ya serikali na mtu aliekua akitumia hiyo ardhi hana haki navyo. Kwahiyo vito vya thamani vikigundulika chini ya ardhi yake mtuhuyo anaondoshwa nakua-compensated kidogo tu na kubadili hao wanaoitwa 'WAWEKEZAJI' badala ya 'WAPORAJI' . Rasilimali hizi zingetumika vema ingekua rahisi sana kwa serikali kujustify, tatizo hilo halijawezekana kwa Tanzania.

Mahali pengine watu wameondoshwa kwanguvu na kuuwawa hovyo, kumbukeni ya Bulyankulu. Chaajabu hao wawekezaji wanaondoka nautajiri mkubwa na watu wa maeneo hayo kubakia masikini 'ndugu zangu tujaribu kuwa fare hata kidogo hivi wewe unaona nihalali wageni watajirikie kwenye ardhi uliokua ukilima, kukusanya kuni, kuchungia mifugo yako huku wewe ukibakia masikini?? Hiyo haikubaliki hata kidogo.

Mahala pengine watu wanaishia kupigwa tena kwa risasi, kuitwa wavamizi kwenye ardhi yao wenyewe, na mbaya zaidi rasilimali zao mhimu kama maji zikiharibiwa na heavy metals nk. Huo ujinga mpaka lini? Niwakati wa Serikali kuangalia kwa upya hizi sera za uwekezaji ambazo kwa sehemu kubwa hazizingatii utu wa mzawa. Hii haiwezi kukubalika.

Utajiri wa vito uliogundulika mahala pengine ungetumika vema TZ, watu wa mtwara wangekua na shule nzuri, hospital nzuri, human resource yakutosha, barabara, maji safi nk. Waziri angeibuka nahoja kua hayayote mnayoyaona Mtwara hayajatokana na Koroshwa tu bali pia na samaki wa Mwanza, Tumbaku ya Tabora, Almasi za Mwadui, Tanzanite ya Merarani, Utalii wa Serengeti nk. ingekua na maana sana. Nahakuna ambae angekua na chembe ya shaka juu ya hoja ya Waziri. But poverty in Southern regions and Tanzania in genral are widespread. Haya mambo mpaka lini jamani??? Nafikiri tuungane na watu wa mtwara kubadilisha sera. Issue ya UZAWA nibora sana ikitumika vema.
Alexander




From: Lemburis Kivuyo <lembu.kivuyo@gmail.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Saturday, December 29, 2012 2:35 PM
Subject: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo

Nimeikuta hii katika gazeti la Mwanachi 29 Desemba  2012 nikaona itasaidia kujadili kwa kina zaidi kuhusu madai ya WanaMtwara kudai Gesi yao

Profesa Muhongo alidai kuwa kuna wakati nchi ilitegemea sana Katani katika kuendesha nchi, hivyo Mtwara nayo ilifaidika na mapato hayo ya katani. Kuna kipindi pia nchi iliendeshwa kwa Kahawa, na Mtwara nayo ilifaidika kwa mapato ya Kahawa. Sasa gesi imegundulika kwao wanataka wafaidi wenyewe. Alidai warudishe hizo pesa kwanza za Katani na Kahawa. Hata hivyo alidai kuwa mkuu wa kaya atatolea ufafanuzi katika salamu zake za kufunga mwaka tarehe 31 Dec 2012


Real Change for Real Development,  

Lemburis Kivuyo
+255654650100/078 7665050/0755646470
Website: www.kivuyo.com,  Skype: lekivuyo, Facebook: http://facebook.com/lemburis.kivuyo, Titter: http://twitter.com/lembu1, Linkedin: http://tz.linkedin.com/in/lembukivuyo, Google+: gplus.to/lembukivuyo
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group, send email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
 
 




--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment