Saturday 29 December 2012

[wanabidii] Ng'ombe Hanenepi Siku Ya Mnada; Ni wakati wa kuandaa salamu za Mwaka Mpya....!


 Ndugu zangu,

... Najiandaa na salamu za Mwaka Mpya kwa ' Wanakijiji wangu' wa Mjengwablog, Kwanza Jamii na marafiki zangu wa FB. Imekuwa ni utamaduni niliojiwekea tangu mwaka 2006 nilipoanzisha Mjengwablog.

Na salamu za Mwaka Mpya hutolewa mara moja tu kila mwaka, Desemba 31, ni kesho. Ni salamu za mwisho kwa mwaka na zenye kutuvusha kwenda kwenye mwaka mpya. Ni tukio muhimu sana.

Najiandaa vipi? Ni kwa kutembea kwa miguu peke yangu japo kwa saa nzima huku nikitafakari. Kisha nitahitaji kula saladi ya matunda na vikombe vya chai ya rangi bila sukari kabla sijaanza kuyaandika niliyoyafikiri.

Na hata kwa maandalizi hayo haimaanishi kuwa salamu haziwezi kukosa mapungufu, maana, ni kwa vile zinaandikwa na mwanadamu asiyekamilika.

Muhimu ni kutambua, kuwa kwa kila jambo unalotaka kutenda, basi, jitahidi kufanya maandalizi. Na maanandalizi yasifanywe siku ya tukio lenyewe.

Wahenga walisema; ng'ombe hanenepi siku ya mnada!

Maggid Mjengwa,
Iringa.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment