Saturday, 29 December 2012

[wanabidii] Re: [PK] VYAKULA VYA GMO MADUKANI KWETU

Waheshimiwa,
Wiki iliyopita kabla ya Christmas, nilialikwa kuwa mgeni rasmi huko visiwa vya Komoro kwa kujadili masuala haya ya vyakula kutoka pande za ulaya ambavyo vimepigwa marufuku huku Ulaya kwaajili ya madhara mbali mbali.
Katika mijadala hiyo ambayo ilikuwa kwenye semina na workshops mbali mbali mbali za wiki 2 tulijaribu kutiliya mkazao vyakula vyetu vya Kiswahili ambavyo Wazee wetu walikuwa wakivitumiya kwa karne nyingi.
Katika semina hiyo, tulikuwa na wataalamu mbali mbali kama Professor Bakri Othman from U.S.A. ambawo wameonesha kitaalamu kuwa nchi nyingi za Kiaafrrika zinatumiwa kuwa jaa la vitu vilivyooza huku Ulaya.
Kwa hivyo sijastaajabu kuona mjadala huu, hapa kwenye mtandawo, na itabidi serikali zetu watiye mkazo kutumiya local products zetu zaidi katika mikahawa yetu,  madukani na nyumbani pia. Ni muhimu sana kuwasomesha watoto wetu kupenda vyakula vyetu vya jaddi ambavyo vina siha zaidi kuliko hivi vyakula vya ulaya.
Katika vitabu vingi vyangu vya mapishi ambavyo vinapatikana kwenye Amazon.com, nimeonesha ule ustaarabu tulikouwa nawo miaka mingi iliyopita, ya vyakula, na ustaarabu huu unapoteya.
 
From: Yona Maro
Sent: Saturday, December 29, 2012 6:45 PM
Subject: [PK] VYAKULA VYA GMO MADUKANI KWETU
 

Ndugu zangu


Nilikuwa natafuta vyakula Fulani Fulani vya watoto na moja ya kitu nilichokuwa naangalia kwenye kila bidhaa ni kama vyakula hivyo vina nembo zenye kuonyesha kama ni GMO au la , Nilipata bidhaa kama 3 hivi zilizokuwa na chapa inayosema NON GMO kwa zile bidhaa zinazotoka nje ya nchi haswa Ulaya Na Marekani .


Bidhaa hizi nimezikuta katika duka la shoprite mlimani city ,hii imekuwa ishara nzuri maana tumejadili mara kadhaa kuhusu bidhaa kuwekwa nembo kama ni GMO au la hii nimeiona kwa mara ya kwanza hapo Shoprite .


Hili sio Tangazo la biashara ila ni kuleta mjadala huu mpana zaidi kuhusu bidhaa zinazotokana na GMO haswa vyakula ambavyo inasemekana vipo nchini na watu wanatumia na tumekuwa tukisikia au kusoma kuhusu madhara ya bidhaa hizi sehemu mbalimbali duniani .


Kama una ushuhuda wowote kuhusu GMO kwa kanda ya afrika mashariki au popote ulipo tunaweza kutupa kutumia mtiririko wa mjadala huu au tuma kwenda wanabidii@googlegroups.com kama wewe sio mwanachama wa Wanabidii na wengine wataweza kusoma mchango wako .


Karibu tuendelee kujadiliana huku tukijenga nchi zetu .


Unaweza kusoma au kujifunza zaidi kuhusu GMO kwa kutembelea


http://www.raiamwema.co.tz/chembe-hai-za-ng%E2%80%99ombe-nge-zachanganywa-kutengeneza-ng%E2%80%99ombe-mpya


http://en.wikipedia.org/wiki/Genetically_modified_organism


http://www.whfoods.com/genpage.php?tname=george&dbid=207



--
*************************************************************************************************
Geniuses Training and Business Services
Certificate and Diploma in Teaching, Training, Business Management & Entepreneurship, Legal Studies, Social Media & Marketing, Project Management, Multimedia Development, English and Literature Studies, Children Studies, Psychology, ICT Foundation Course
Call 0705297307 or 0786695083 or Email to: info@geniusesltd.com
 
*************************************************************************************************
TO ADVERTISE HERE: email: amosogal @ gmail.com
*************************************************************************************************
To subscribe:progressive-kenyans+subscribe@googlegroups.com:
Unsubscribe:progressive-kenyans+unsubscribe@googlegroups.com
 
 

0 comments:

Post a Comment