Saturday, 29 December 2012

Re: [wanabidii] Fw: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo

Sasa Hilda Serikali imepewa mamlaka yote inashindwa nini kuwawajibisha watu wake? Unachekaje na mtu mzembe ambae baadae anakuja kuchafua utendaji wako wakazi na kukushushia credibility kama serikali? 

Majuzi huko huko Lindi na Mtwara tumesikia watu wamebadilishana ardhi na Mwarabu kwa SEMBE kisa kijiji kina njaa. Fikiria jambo kama hili lina tia hasira. Mkuu wa mkoa asieweza kuwabana watu na wakalima mashamba ya kutosha kwa ajili ya chakula na ziada anafaida gani? Mpaka watu wamempa mwarabu ardhi kwa unga karne hii ya 21, tutafika kweli??

Kama hilo halitoshi angalia ngonjera za makazi ya mabondeni serikali inasema bila hatua mathubuti mwisho watu wanakuja kuelea juu ya maji wakati wa mafuriko, why? Kwanini wapinzania nao wasipenyeze agenda zao hapo nakupata popularity?

Mimi naona uzembe wa utendaji wa serikali na usimamizi wa rasilimali ndio utakao leta athali zote hizi, na hata za ukabila na sivingenevyo. Maana unapoacha mwanya ndipo wengine wanapenyeza hata agenda zao za kugawa taifa. Serikali iamuke huko iliko lala ifanye kazi zake.


From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, December 29, 2012 5:02 PM
Subject: Re: [wanabidii] Fw: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo


Ni kweli hata umeme mtumiao Dar wengine wamehamishwa milimali walikokuwa wakila upepo mwanana ili huku DSM na kwingineko mfaidi umeme wao hawana. Nyumba ya Mungu wanaondolewa daima wasihalibu bwawa Nchi ipate umeme. Daraja la Mkapa, Dar Lindi-Msumbiji road inayotegemewa kuunganicha nchi 2 hela zilitoka ktk gas yao?
Hadi nyama -beef huko nyuma 1970s ikitoka Dar kupelekwa kwa ndege Mtwara na lift kuu ilikuwa ndege za JWTZ unapanda bure wakati mto Rufiji umefurika kikomo na Milima ya Lukumburu Songea bus la wahindi la TTCO haliwezi kupita kutokana na tope!! Meli imejaa kikomo, ukiiona ndege ya JWTZ angani-unakimbilia airport. Hiyo ndiyo TZ ya zamani.

Utakaporudi TZ na itakapotokea kazi katika taasisi yako uliyopitia huku TZ-ya kwenda migodini for EIA/SIA utaombewa fursa ili uende ukaone mwenyewe iwe Handeni gold mines, Geita au kupya kokote kule na hata Mererani wapo waliofanya research za dissertation. Ukaone jinsi ardhi ni yao, wanaambiwa wajiunge waunde kampuni ya artisanal miners, mwekezaji anunue anawalipa mamilioni na kisha wanakuwa wabia-kazi hasa na vyombo vya uchimbaji hawana, migodi inawafukia daima wanakufa. Na wakifa watu ndio wanahaha kuingia ndani ardhini kwa pupa eti sasa ndio mapato yataongezeda (sadaka-damu isha mwagika). Kweli sikio la kufa ni la kufa. kati ya wahojiwa 100 utapata 6 tu waliotumia mapato ya madini ktk kujiendeleza economically na socially. Starehe!!

Umoja unakuta haba au hakuna, waliounda huo umoja au kampuni majina ya wenzao hayapo yapo mengine ghost names wamewaacha na kuwadanganya wenzao. Inamfanya mwekezaji apate utata mkubwa ulioje vurugu inazagaa. Lesseni ya kupata eneo lenye bocons na fenced lenye lina madini mbongo atalipa 20,000/= unapanuanua hapo. Ugumu ni nini?
Ni bia ngapi mtu anakunywa na hela nyingi kuhonga changu doa wanaojaa huko migodini? Kila mtu ana kihirizi chake ubinafsi unatawala. Ni vibanda vibana na vileo n.k. inaumiza sana.

Bahati nzuri nimesoma secondary Mtwara na nimefika huko baada ya shule na miaka ya karibuni hadi lindi, nachingwea, Newala. ardhi na misitu si mchezo. Kijana gari alime pamoja na mabonde hayo na mashirika yanayosaidia traditional rice irrigation. kama kila mtu amiliki ardhi atakavyo isiwe ya GVT chini ya Rais-huoni kama tutakuwa kama nchi jirani kuhodhi kiukabila au kwa kipato. Tunaweza kutaua matatizo yaliyopo kama hatutajali kukosa KURA na hasa kama watatenganisha Ajira serikalili na uongozi Kisiasa. yaani-Diwani, Mbunge asiwe mwajiriwa serikalini kushika madaraka kiserikali maana maamuzi muhimu yanazuilika ili usikose KURA na kula.

Kinawazuia nini umoja wa wachimbaji wadogo wadogo mahala-Mererani etc kununua maeneo makubwa? kinawashinda nini matajiri bongoland kuunda kampuni moja kuwa wakaajiri wazungu toka ulaya na maijinia bongoland na vibarua wengine kuzalisha hiyo gas. wakanunua mitambo, wazungu wakafundisha vijana na mwisho kampuni hilo likabobea kuzalisha umeme na kutoa ajira? Vivyo hivyo katika madini-wakaunda kampuni ambayo itachimba huku na kule na kuajiri wabongo? nao wanavijiji wakaacha kuchimba chini kwa chini kuingia kuiba madini kuliko nunuliwa na kampuni? wanafanyiana hivyo hata katika artisanal area. Na ukienda machimbo ya artisanal miners utakuta mmiliki eneo kijadi ndio owner, anawaacha wachimbe, broker ananagharimia chakula wachimbaji magunia yakipatikana anapewa customary owner gunia zake kulingana na makubaliano. Mawe ktk gunia zilizobaki yanakuwa processed. Madini yakipatikana yanauzwa, broker anakata matumizi aliyogharimia kwanza kabla hawajagawana faida iliyobakia. Sasa nani hamiliki ardhi hapa katika mfumo huu uliopo kule ambako watu hawakununua maeneo bali wanachimba katika ardhi ya mtu mwenye eneo-customary owner. Budi kujifunza mifumo iliyopo halafu kupata suluhu.
Nimechangia

--- On Sat, 29/12/12, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] Fw: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 29 December, 2012, 14:43



Wanamabadiliko,
Nafikiri Waziri ametoa hoja nyepesi kutaka kuzima hoja ya watu wa Mtwara.

Waziri akumbuke kua tatizo la watu kutofaidika na raslimari zinazopatikana katika maeneo yao nikubwa sana Tanzania. Hebu jamani fikiria kwa Tanzania haki ya mtu kutumia ardhi inaishia kwenye surface soil (crop cultivation only). Hii inakuja kweli?? Nafikiri kunahaja yakua na tafsiri pana ya haki zinazo ambatana na ardhi ambayo mtu amekua akitumia kwa miaka mingi. Ikiwezekana to borrow definition ya James kua 'Land include much more than just physical soil or substance. It include for instance, building, and any other thing attached permanent to the soil or permanently fastened to anything which is attached to the soil (James 1971)

Kwa Tanzania nitofauti, vitu vyote vilivyochini ya ardhi ni mali ya serikali na mtu aliekua akitumia hiyo ardhi hana haki navyo. Kwahiyo vito vya thamani vikigundulika chini ya ardhi yake mtuhuyo anaondoshwa nakua-compensated kidogo tu na kubadili hao wanaoitwa 'WAWEKEZAJI' badala ya 'WAPORAJI' . Rasilimali hizi zingetumika vema ingekua rahisi sana kwa serikali kujustify, tatizo hilo halijawezekana kwa Tanzania.

Mahali pengine watu wameondoshwa kwanguvu na kuuwawa hovyo, kumbukeni ya Bulyankulu. Chaajabu hao wawekezaji wanaondoka nautajiri mkubwa na watu wa maeneo hayo kubakia masikini 'ndugu zangu tujaribu kuwa fare hata kidogo hivi wewe unaona nihalali wageni watajirikie kwenye ardhi uliokua ukilima, kukusanya kuni, kuchungia mifugo yako huku wewe ukibakia masikini?? Hiyo haikubaliki hata kidogo.

Mahala pengine watu wanaishia kupigwa tena kwa risasi, kuitwa wavamizi kwenye ardhi yao wenyewe, na mbaya zaidi rasilimali zao mhimu kama maji zikiharibiwa na heavy metals nk. Huo ujinga mpaka lini? Niwakati wa Serikali kuangalia kwa upya hizi sera za uwekezaji ambazo kwa sehemu kubwa hazizingatii utu wa mzawa. Hii haiwezi kukubalika.

Utajiri wa vito uliogundulika mahala pengine ungetumika vema TZ, watu wa mtwara wangekua na shule nzuri, hospital nzuri, human resource yakutosha, barabara, maji safi nk. Waziri angeibuka nahoja kua hayayote mnayoyaona Mtwara hayajatokana na Koroshwa tu bali pia na samaki wa Mwanza, Tumbaku ya Tabora, Almasi za Mwadui, Tanzanite ya Merarani, Utalii wa Serengeti nk. ingekua na maana sana. Nahakuna ambae angekua na chembe ya shaka juu ya hoja ya Waziri. But poverty in Southern regions and Tanzania in genral are widespread. Haya mambo mpaka lini jamani??? Nafikiri tuungane na watu wa mtwara kubadilisha sera. Issue ya UZAWA nibora sana ikitumika vema.
Alexander




From: Lemburis Kivuyo <lembu.kivuyo@gmail.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Saturday, December 29, 2012 2:35 PM
Subject: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo

Nimeikuta hii katika gazeti la Mwanachi 29 Desemba  2012 nikaona itasaidia kujadili kwa kina zaidi kuhusu madai ya WanaMtwara kudai Gesi yao

Profesa Muhongo alidai kuwa kuna wakati nchi ilitegemea sana Katani katika kuendesha nchi, hivyo Mtwara nayo ilifaidika na mapato hayo ya katani. Kuna kipindi pia nchi iliendeshwa kwa Kahawa, na Mtwara nayo ilifaidika kwa mapato ya Kahawa. Sasa gesi imegundulika kwao wanataka wafaidi wenyewe. Alidai warudishe hizo pesa kwanza za Katani na Kahawa. Hata hivyo alidai kuwa mkuu wa kaya atatolea ufafanuzi katika salamu zake za kufunga mwaka tarehe 31 Dec 2012


Real Change for Real Development,  

Lemburis Kivuyo
+255654650100/078 7665050/0755646470
Website: www.kivuyo.com,  Skype: lekivuyo, Facebook: http://facebook.com/lemburis.kivuyo, Titter: http://twitter.com/lembu1, Linkedin: http://tz.linkedin.com/in/lembukivuyo, Google+: gplus.to/lembukivuyo
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group, send email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
 
 




--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment