Saturday, 3 May 2014

Re: [wanabidii] Umri sahihi wa kutahiri watoto wa kiume!

Atahiriwe akiwa mkubwa kabla ya kufika darasa la 7 yaani akiwa darasa la 4 umri miaka 10, ili auone uchungu, aache jeuri. Kisha apate mafunzo ya usafi na stadi za maisha, mila na desturi za kiafrika. Hii itampa nafasi ya kuwa mpenda jamii, mlinda jamii na mwana maadili.Kuwatahiri wakiwa watoto ndio hawa tuleao digitali, katahiriwa siku chache baada ya kuzaliwa, hakumbuki kunoga kwake/uchungu na huwezi ukamfundisha maana yoyote. Ila watahiriwe hospitali sio porini ili kulinda afya zao. Wale ambao watapata matatizo ya UTI na kuzia mkojo kutokana na ngozi kuziba (kuwa ndefu), basi wasaidiwe mapema. Mafunzo ya kumbi/unyago yaliyoboresha kwa mtaala wa kisasa husaidia sana kuliko ule wa jando na unyago ya zamani.Huu wa sasa madaktari/bwana afya wa zahanati, kituo cha afya, wakunga wa jadi, wazee wa mila, ngariba na somo/kungwi hutumika kufundisha masuala muhimu. Mitaala hiyo ipo imejaribiwa na NGOs kwa kutumia Sera za nchi (Afya ya mwili na usafi wa mazingira, HIV, katiba na masuala ya kimataifa ya haki za Binadamu etc); Mitaala ya In-school and out-of-school youth peer educators ya FHI-AYA; UNFPA (MCHC, Youth); Sera ya Vijana TZ. Kisha wazee wa mila, kungwi, somo hufundisha maadili na vijana kujua kucheza noma za kwao na kushindanisha makundi na kutoka hadharani ili wakubalike kimila na kabila kuwa wapo sawa kama wale waliopitia jando la kisu kavu kavu na mafunzo kamambe kama ya 'Mshitu e nyumbae' (Ona kiambata).
On Saturday, 3 May 2014, 12:35, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:
Baadhi ya vitabu vya dini vinasema mtoto atahiriwe ndani ya siku 14. Na huku wataalam wengine hushauri walau mtoto awe amefikisha miezi mitatu sababu watoto wa kiume mara nyingi huugua sana UTI hasa akianza kutambaa. Mtoto anapotahiriwa akiwa mtoto mdogo anawahi haraka kupona.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment