Prof. Shivji ana ajenja ya siri au ametumwa na watu fulani aongee kwa maslahi yao. Rasmu ya sasa ilivyo ndiyo msimamo wa Shivji ulivyo. Ukisoma maabdiko mengi ya Prof. Shivji huko nyuma anaushangaa muundo wa muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar (kwa mfano, The Legal Foundation of the Union). Watu hawa wanabadili ajenda iliko mezani ya kujadili rasmu ya katiba wanatangaza utengano. Hii ni mbinu mpya ya kubadili maada ili wananchi wawaone wenzao wanataka kuvunja muungano.
Nimeshangazwa na kauli za katibu wa CCM kule Zanzibar, anasema maalimu Sefu ajiuzuru nyadhifa zake kama hataki muundo wa serikali mbili! Ni jambo la kushangaza kusikia maneno haya toka kwa kiongozi mkuu wa chama tawala, anamwambia Sefu amwandike barua rais wa Zanzibar kuomba kujiuzuru. Sefu kawekwa na katiba ya Zanzibar na si kwa huruma ya CCM wala Shein. Anachotakiwa kufanya Kinana kama kweli anao ubavu ni kuwaambia Wazanzibar katiba yenu haifai tuichane maana inawaweka madarakani wapinzani wa CCM.
Huyu mtu hana jipya na ziara zake ni za kupoteza muda tu kama si kwa ajili ya posho. Ndiyo maana alipowaita mawaziri walioteuliwa na Mwenyekiti wake ni mizigo, Mwenyekiti hakumjali wala kumjibu alimpuuza tu. Kama yeye aliamini katika alichokisema ziarani ambacho mwenyekiti wake alikipuuza alistahili kujiuzuru, lakini hawezi kwa vile anazihitaji posho zaidi kuliko kukijenga chama.
Maalimu Sefu yupo pale kwa mujibu wa katiba ambayo imeiondoa Zanzibar chini ya mamlaka ya Muungano, huwezi kumwambia Sefu jiuzuru bila kwanza kuifuta katiba yenyewe. Hakuna mwenye ubavu wa kumwondoa Maalimu madarakani pasi kuivunja katiba ya Zanzibar kwanza. Tujadili hoja iliyoletwa mezani ambayo ni rasmu ya katiba tusibadili hoja kwa manufaa ya matumbo yetu. Wala hakuna sababu ya kuzungumzia juu ya katiba ya Zanzibar, tuliwaona wakiitengeneza kwa umakini na kwa mshikamano wa ahli ya juu, wakajiwekea wigo wa kutulizwa na mtu juu ya mambo yao tukanyamaza. Hata alipotokea mwendawazimu kutuonyesha njia kwamba wamejiondoa kimya kimya tukasema mwendawazimu huyo tusimsikilize. Leo kinana anataka kujitia madaraka juu ya mambo ya Zanzibar amechelewa.
--------------------------------------------
On Sun, 5/11/14, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] UKAWA wanapigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar?
To: hamisznz@gmail.com, wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, May 11, 2014, 12:07 PM
Mimi sioni kama ukawa wanapigania
uzanzibari na utanganyika ila wanataka bunge la katiba
lijadili rasimu iliyoletwa kwao na tume. Hisia ya
utanganyika hazikuletwa na tume bali tume ilizikuta kwetu.
Zimekolezwa na katiba ya sasa ya zanzibar ambayo kimsingi
ilivunja muungano kwa kukinzana na katiba ya muungano. Hii
ndiyo inafanya watu makini kumshangaa shivji. Inakuwaje
asielewe tume. Marekebisho ktk mapendekezo ya tume nje ya
mfumo wa shirikisho ni kuibembeleza zanziba ikubali kurudi
kwenye serikali isiyo kama ya sasa ila kama ya 1964 na ya
Tanganyika iwe vile. Hii itaimarisha muungano. Kinyume chake
serikali 2 ni sawa kuufutilia mbali muungano.
----------
Sent from my Nokia Phone
------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, May 10, 2014 4:46:47 PM GMT-0700
Subject: [wanabidii] UKAWA wanapigania uhuru wa Tanganyika
na Zanzibar?
KATIKA mada aliyoitoa Machi 31, mwaka huu wa 2014 kwa vijana
wa vyuo vikuu
jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, Profesa Issa
Shivji
alionyesha wasiwasi kuwa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko
ya Katiba kuhusu
muundo wa Muungano wa Serikali tatu yangeibua hisia za
utaifa wa Tanganyika
na Zanzibar.
Maoni haya ya Profesa Shivji yalipingwa na Tume yenyewe
pamoja na watu
kadhaa, tena kwa maneno makali yaliyomshambulia Profesa
Shivji binafsi na
kuachana na hoja zake. Wakosoaji wa Profesa Shivji walienda
mbali zaidi na
hata kumtuhumu kwamba amenunuliwa na Chama cha Mapinduzi
(CCM).
Utamaduni wa kutuhumu watu kununuliwa umeanza kuota mizizi
na kugeuka kuwa
ugonjwa wa kitaifa katika nchi hii. Kwamba kila mtu asiye
mwanachama wa CCM
anapaswa kutoa maoni yasiyofanana na msimamo wa CCM. Ole
wako utoe maoni
yako ambayo kwa bahati nzuri au mbaya yakaendana na maoni na
msimamo wa CCM
basi unaingizwa kwenye orodha ya watu walionunuliwa na chama
hiki. Huu ni
udhaifu mkubwa sana katika ujenzi wa hoja. Hata hivyo, hii
si hoja yangu
kwa leo.
Hoja yangu ya leo ni kwamba kile kilichoonekana kwamba ni
hofu ya Profesa
Shivji sio hofu tena bali ni jambo halisi na la kweli
kabisa. Tayari hisia
za utaifa wa Tanganyika na Zanzibar zimekwishaanza
kujitokeza waziwazi.
Sasa watu wanavaa fulana za Tanganyika na katika mitandao ya
kijamii watu
wanajivunia utanganyika na sio utanzania tena.
Pengine hizi mbwembwe za kuvaa fulana na kujipaka rangi za
bendera ya
Tanganyika hazitishi sana kama maneno niliyoyasikia Zanzibar
katika
mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Kwa kiasi
kikubwa, na kwa
tafsiri yangu, viongozi wa UKAWA huko Zanzibar walijikuta
wakipigania uhuru
wa Zanzibar na Tanganyika badala ya kupigania Serikali
tatu.
Sijui viongozi hawa kama walikusudia kufanya jambo hili au
walijikuta
wakilifanya tu kutokana na mazingira na mihemko ya kisiasa
iliyokuwepo pale
Zanzibar. Ili kuweka vizuri hoja yangu, naomba niwanukuu
viongozi wawili wa
juu wa UKAWA.
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA na UKAWA katika mkutano
wa Aprili 30,
2014, pamoja na mambo mengine, alinukuliwa na gazeti la moja
la kila siku
la Mei mosi, 2014 akiwaeleza wananchi wa Zanzibar kuwa:
"Ni jambo la hatari
katika mchakato wa Katiba ya wananchi kuwa na woga au
hofu…Lazima tuwe
tayari kuwaonyesha watawala kuwa tuna umoja imara,
tunapigania mataifa huru
ya Tanganyika na Zanzibar".
Katika mkutano huo huo, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na
mjumbe muhimu wa
UKAWA, Tundu Lissu, alinukuliwa na gazeti jingine la kila
siku la Mei mosi,
2014 akiwaambia wananchi kuwa: "Kwa sababu Zanzibar
haijawa huru na
Tanganyika haijawa huru na ukitaka kujua ukweli wa hili
angalia vitabu,
kuna jina Tanganyika limefutwa ili kuitawala Zanzibar, sasa
inabidi tuseme
ili kuleta uhuru wetu". Lissu aliendelea kusema;
"Zanzibar inatakiwa kuwa
mamlaka kamili".
Baada ya kutafakari maneno haya na muktadha mzima wa
mikutano ya UKAWA huko
Zanzibar nimejiuliza swali moja muhimu: Je, UKAWA
wanapigania uwepo wa
Muungano wa Serikali tatu au uhuru wa Tanganyika na
Zanzibar?
Pamoja na kuunga mkono umoja wa vyama vya upinzani kwa
ujumla wake hasa
katika muktadha wa kuimarisha upinzani nchini, jambo ambalo
tumeliombea
miaka mingi, nalazimika kuhoji dhamira ya UKAWA katika
mazingira ya Katiba
mpya. Ukichunguza kwa makini maneno ya Mbowe na Lissu
unaanza kupata jibu
kwa nini CHADEMA na CUF waliokuwa maadui wa kisiasa hadi
juzi kiasi cha
kushindwa kusimamisha mgombea mmoja wa ubunge huko Chalinze
dhidi ya
mgombea wa CCM, ghafla wamegeuka marafiki wa kisiasa bila
hata makubaliano
rasmi yenye ajenda ya wazi.
Kimsingi CHADEMA sasa wanapigia debe sera ya CUF, ya
Zanzibar huru yenye
mamlaka kamili pengine bila wao kujua. Inajulikana enzi na
enzi kwamba CUF
hawataki Muungano uliopo; wanataka tu ushirikiano wa
kijirani wa kawaida
kama ulivyo katika nchi zingine za Afrika kama vile Jumuiya
ya Afrika
Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC)
au ile Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS). Lakini
zote hizi ni
ushirikiano tu na wala sio Muungano. Ndio maana CUF wanataka
Zanzibar iwe
na mamlaka kamili kuhusu mambo yote nyeti, ikwemo uraia,
uhamiaji, fedha,
bandari, mambo ya nje na kiti Umoja wa Mataifa na wanajua
fika kwamba
ukishayatoa mambo haya katika Muungano huna haja ya kuwa na
Muungano tulio
nao.
Kwa hiyo wenye akili tunajua kwamba CUF hawataki Muungano
kwa sababu huwezi
ukataka Muungano na hapo hapo ukataka mamlaka kamili. Hakuna
Muungano wa
namna hiyo duniani bali ni ushirikiano wa kijirani.
Sasa kama hivyo ndivyo, je CHADEMA nao sasa hawataki
Muungano? Na je, huu
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni umoja wa watu
wasiotaka Muungano?
Kama hivyo ndivyo, kwa nini wasiweke wazi matakwa yao ili
waweze kujulikana
hivyo na wapate wafuasi kwa sababu hizo? Vinginevyo,
viongozi wa UKAWA wana
wajibu wa kutuelimisha wanamaanisha nini wanaposema
wanapigania uhuru wa
Tanganyika na Zanzibar? Uhuru huu wanaupigania kutoka koloni
gani?
UKAWA wanasema kwamba wanapigania Rasimu ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba.
Lakini Rasimu ya Tume hiyo inapendekeza Muungano imara na
kwa maoni ya tume
pengine imara zaidi kuliko hata huu uliopo. Rasimu
haiongelei uhuru wa
Zanzibar au Tanganyika na wala haiongelei habari za mamlaka
kamili ya
Zanzibar kama walivyohubiri wao huko Zanzibar. Hivyo basi
UKAWA hawawezi
kutafuta uhalali wa ajenda yao kwa kujificha katika rasimu
ya tume kwa kuwa
wanajua rasimu hii inaungwa mkono na walio wengi.
Kwa hiyo wasiwasi wangu ni kwamba, kupitia ndimi zao huko
Zanzibar, ni wazi
kwamba UKAWA wanataka uhuru wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa
maneno mengine
hawataki Muungano au wanataka Muungano lege lege utakaojifia
wenyewe mbele
ya safari.
Wosia wangu ni kwamba UKAWA wanawajibika kuweka msimamo wao
wazi na kututoa
wasiwasi baadhi yetu tunaopenda Muungano imara bila kujali
aina ya muundo
na ambao tunaanza kutishwa na kauli zao.
- See more at:
http://www.raiamwema.co.tz/ukawa-wanapigania-uhuru-wa-tanganyika-na-zanzibar#sthash.W1y6hDst.dpuf
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment