Thursday, 8 May 2014

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] SERIKALI INAWADHIHAKI WAFANYAKAZI!

.........................................
..................................................................................................................................


On Saturday, May 3, 2014 12:42 AM, 'LINGONET Lindi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
mfumo wa wakusajili walimu ndio unaowatesa,kuchukua waliofanya vibaya katika mitihani na kuwafanya walimu ni vigumu kutetea haki ya na kujenga umoja kwa sababu wanaona wameingia kwa fadhila za utawala ndio chanzo cha kukosa umoja na mgawanyiko miongoni mwao leo hii.walimu walioingia kwa uwezo wao wanashindwa kuwashawishi walimu walioingia kwa fadhila za viongozi kujenga umoja na mshikamano wa kweli
--------------------------------------------
On Sat, 3/5/14, 'george ramadhani' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] SERIKALI INAWADHIHAKI WAFANYAKAZI!
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 3 May, 2014, 8:35

Ryoba,Msipofundisha
kabisa mtakuwa mnawakomoa watoto wa wakulima na watumishi wa
umma wa kima cha chini wakiwemo walimu! Wataendelea
kutawaliwa milele kwa sababu ya ujinga!Watoto
wa wakulima na watumishi wa umma wa kima cha chini
wanahitaji kufundishwa kwa bidii, ndipo watakapopata ufahamu
wa kujitambua wao ni nani na wanapaswa kufanya nini ili
kuondokana na utawala
  wa kifisadi! Mtu anapokuwa mjinga inakuwa rahisi
kutawaliwa kwa sababu hakuna anachojua kuhusu uendeshaji wa
serikali kifisadi. Kashfa kama za EPA, Richmond/Dowans,
Rada, Twiga hai, biashara ya pembe za ndovu, madawa ya
kulevya, Mabilioni yaliyofichwa Uswis nk,
zisingeweza kuibuliwa na watu wajinga.Endeleeni
kupigania haki zenu kama walimu na watumishi wa umma kwa
ujumla lakini msiache kuwafundisha watoto wetu, mtakuwa
mnawajengea mazingira ya kutawaliwa milele.

  

    On Friday, May 2,
2014 7:25
  PM, 'Ambokege Benard M' via Mabadiliko Forum
<mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:
   
 


Kaka Ryoba napingana na wewe
kuwa mbele za Mungu makosa yote yako sawa. Si kweli,
kilicho  sawa ni adhabu za makosa hayo.

Nawasilisha!



From:
'Gikaro
Ryoba' via Mabadiliko Forum
Sent:
‎5/‎2/‎2014 0:40
To:
wanabidii@googlegroups.com;
Mabadiliko
Subject:
[Mabadiliko] SERIKALI
INAWADHIHAKI WAFANYAKAZI!



Katika biblia hakuna kosa lililo dogo wala kubwa
kuliko lingine. Makosa yote ni sawa mbele za Mungu. Jambazi,
mchawi, fisadi, kibaka na mzinzi, wote watapata hukumu iliyo
sawa sawa. Dhana hii ni tofauti na jinsi tunavyoichukulia
hapa duniani ambapo kila mtu huadhibiwa kulingana na uzito
wa kosa alilotenda.
 
Kosa kubwa kuliko yote hapa Tanganyika ni kuendelea
kuikumbatia serikali dhaifu na ya kifisadi inayoongozwa na
CCM. Serikali hii 'sikivu' imeshindwa kabisa kuboresha
maisha ya wafanyakazi katika nchi hii. Kila mwaka tunaambiwa
serikali haina fedha huku tukishuhudia ufisadi wa kutisha,
matanuzi ya kipuuzi ya viongozi wa serikali, kulipana posho
kubwa kubwa, misamaha ya kodi, ufisadi na maovu mengine kama
haya yakitendwa na serikali ya CCM kila kukicha. Yote haya
yanafanyika kwa gharama za wananchi na mwisho wa siku
wananchi wameendelea kuishi maisha ya kusikitisha wakati
nchi ikiwa imebarikiwa kuwa na rasimali kedekede kama vile
almasi, misitu, tembo, twiga, dhahabu, tanzanite na utajiri
mwingine chekwa!
 
Kitendo cha serikali ya CCM kugoma kuongeza
mishahara ya watumishi kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 ni
uhaini, ugaidi na uuaji ambao haukubaliki hata kidogo.
Watumishi wa umma wamekuwa wakiishi kama yatima katika nchi
hii huku kikundi kidogo cha mafisadi wasiozidi 50
wakiendelea kutumbua rasimali za taifa na kuishi kama vile
wako peponi. Ni lini hasa serikali hii ya kijangili itaacha
kuwadharau, kuwanyonya na kuwaonea wafanyakazi katika nchi
hii kwa kuthamini mchango wao katika maendeleo ya
taifa?
 
Mwaka wa jana tumeshuhudia serikali hii ikigoma
kupunguza kodi ya mishahara na badala yake ikapunguza kwa 1%
tu, kiwango ambacho ni sawa na bure. Tumeshuhudia wajumbe wa
Bunge Maalum la Matusi (BMM) wakilipwa mamilioni ya shilingi
kwa ajili ya kutukana tu na kazi hiyo ya kutukana wameifanya
kwa muda mrefu hadi imebidi waongezwe muda mwingine wa
kuendelea kutukana na kukejeli maoni ya wananchi. Pesa kama
hizi zinazopotea bila sababu ya msingi, zingepaswa zitumike
kuboresha mishahara ya walimu. Walimu tumekuwa tukiishi kama
wakimbizi. Huwezi kuamini kwamba mshahara wa mwalimu mwenye
shahada hauzidi Tsh 300,000 kwa mwezi. Kila mtu ni shahidi
kwamba wajumbe watukanaji wa bunge la katiba wanalipwa zaidi
ya kiasi hicho cha pesa kwa siku wakati mwalimu
anayeeelimisha taifa hulipwa chini ya kiwango hicho kwa
mwezi na wakati mwingine
  kukaa zaidi ya miezi 6 bila kulipwa mshahara. Jamani, usawa
wa binadamu upo wapi katika nchi hii?
 
Natoa wito kwa wafanyakazi wote, hasa walimu,
kujitahidi kuwahi kufika kazini. Mkifika kazini tieni saini
kwenye vitabu vya mahudhurio, kisha endeleeni kupiga soga
mpaka muda wa kazi unapoisha mrudi majumbani kwenu. Ndio.
Hatuwezi kila siku tuwe tunatumiwa na mafisadi kama ngazi ya
kupandia na kuning'inia madarakani huku sisi tukiendelea
kuishi maisha ya dhiki. Ifike wakati walimu tujitambue na
tukatae kunyonywa na mafisadi ilhali tunao uwezo wa kukataa
unyonyaji huu. Mkakati huu wa kutofundisha utasaidia
kuzalisha wajinga na wajinga wakishakuwa wengi itakuwa sio
rahisi kutawalika. Hapo ndipo sasa wafanyakazi tutakapoanza
kuthaminiwa. Malipo yetu yataboreshwa na tutakuwa
hatucheleweshewi mishahara. Ule utaratibu wa kufundisha
chini ya kiwango umeonekana kwamba haulipi tena. Kufundisha
chini ya kiwango huzalisha watu wenye elimu
  nusu ambao ni rahisi kutawalika. Ni bora sasa tuanze
mapango mpya (BRN) wa kutokufundisha kabisa ili tuzalishe
vilaza halisi wasiotawalika tupate
kuheshimiana.
 
SOLIDARITY FOR EVER!



     


--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment