Monday, 26 May 2014

Re: [wanabidii] KUONDOA SHILINGI NI MCHEZO WA KUIGIZA!

Ryoba, katika point yako ya pili unayosema sio kweli, walikuwepo akina tuntemeke sanga mbunge wa makete walikuwa wakiondoa shilingi ki ukweli acha hawa wanafiki.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: 'Gikaro Ryoba' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "Mabadiliko" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>,"wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, May 26, 2014 12:27:42 PM GMT-0700
Subject: [wanabidii] KUONDOA SHILINGI NI MCHEZO WA KUIGIZA!

Katika
hili bunge la bajeti linaloendelea sasa hivi, pamoja na kwamba limekosa mvuto
kutoka kwa jamii ya watanzania, kuna mambo matatu nimeyagundua. Kwanza, huu
utaratibu wa kuondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri ni kama mchezo wa
kuigiza kwa kuwa wabunge wanaoshika hizo shilingi hatimaye huziachia na vifungu
vya ovyo vya bajeti hupitishwa.
 
Pili,
kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge hili nimeshuhudia wabunge wa CCM
wakiondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri wa chama chao. Nadhani ni muendelezo
ule ule wa kuleta mzaha na kuwakoga wananchi wanaowatazama ili waone kwamba wana
uchungu na maendeleo yao wakati si kweli. Lakini pia wanafanya hivyo ili
kufuata mkumbo wa wabunge wa UKAWA ambao tangu mwanzo walitahadharisha kushika
shilingi za mishahara ya mawaziri ambao wameshindwa kuleta maisha bora kwa kila
mtanzania. Kinachowaponza wabunge wa UKAWA ni uchache wao kwani hata kama
wakishika shilingi, mwisho wa siku wabunge wa CCM watapiga kura za
Ndiyooooooooooooooo ili kuwaokoa mawaziri wao wa CCM.
 
Tatu,
nimegundua kwamba mle bungeni kuna wabunge wa CCM ambao wao kazi yao kubwa
wanayoijua ni kusema NDIYOOOOOOOOOOO kwa sauti kubwa ili vifungu vya bajeti,
hata vile vibovu, vipite bila kupingwa. Kundi hili huwa halichangii chochote
bungeni. Wakishaingia bungeni wakasaini kwenye kitabu cha posho, hukaa mezani na
kusubiri kugonga meza. Hili ni suala la kustaajabisha sana kwani wabunge hawa wametumwa
na wananchi waende kuwawakilisha lakini wamegeuka kuwa wachumia tumbo na
watetezi wa ukandamizaji wa serikali dhidi ya wananchi. Na kwa kuwa moja ya
kazi ya wabunge ni kuibana serikali iwahudumie wananchi, wabunge hawa wa CCM ni
wasaliti wa wapiga kura wao na hawafai kurejeshwa bungeni tena msimu ujao. Inasikitisha
sana kuona kwamba wabunge hawa wa CCM wapo bungeni kwa lengo la kuwakandamiza
wananchi badala ya kuwatetea!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment