Sunday, 9 July 2017

[wanabidii] WAZAZI WASHAURIWA KUTUMIA AKAUNTI YA MTOTO

WAZAZI WASHAURIWA KUTUMIA AKAUNTI YA MTOTO NA CHIPUKIZI YA NMB 

BENKI ya NMB imewashauri wazazi na walezi kuwafungulia watoto wao akaunti mbili mpya ambazo zimeanzishwa na benki hiyo ya Mtoto Akaunti na Chipukizi Akaunti kwa ajili ya kutumia kuwawekea fedha watoto wao.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Elimu ya Fedha wa benki ya NMB, Ryoba Mkono baada ya kutoa elimu ya fedha kwa wazazi na watoto kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba yanayofanyika jijini  Dar es Salaam. Mkono alisema mzazi atakuwa na nafasi ya kuchagua akaunti gani inamfaa mtoto kulingana na umri wake na kwa kila akaunti mtoto atakuwa anapata riba ya asilimia tano kila mwisho wa mwaka kulingana na kiasi cha fedha alichonacho kwenye akaunti.

"Mtoto Akaunti inahusisha watoto wenye umri kuanzia miaka 0 hadi 17 gharama yake ya kufungua ni 5,000. Ni akaunti ya kuweka akiba na mzazi ndiyo anaweza kuweka na kutoa na mara nyingi tunashauri mzazi asitoe ili itumike kwa mtoto baadae."

"Kwa upande wa NMB Chipukizi Akaunti hii inahusisha watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 17 ni akaunti ambayo ina ATM Card na mtoto anaruhusiwa kutoa pesa hadi 50,000 kupitia ATM zetu au NMB Wakala kwa siku moja na kila akitoa pesa mzazi anapata ujumbe kuwa mtoto katoa pesa," alisema Mkono.

Pia Mkono alizungumza kuhusu faida za akaunti hizo mbili tofauti na akaunti zingine ambazo zinapatikana kwenye benki ya NMB, "Faida yake ni hazina makato ya mwezi kwa ajili ya uendeshaji, pia mtoto anapata riba ya asilimia tano ya kiasi alichonacho kwenye akaunti yake ya NMB."

Aidha Mkono aliwashauri wazazi kuwafungulia watoto akaunti hizo ili wapate huduma boa kutoka NMB lakini pia hata katika kipindi cha maonesho ya Saba Saba watoto wataweza kutumia kadi zao kununua vitu mbalimbali ambavyo wanahitaji.

"Wazazi wamekuwa wakiwapa watoto pesa mkononi wanapoenda kwenye Saba Saba lakini kama mtoto ana miaka 13 anaweza kuwa na ATM Card ni vyema wakawafungulia akaunti ili wazoee kutumia pesa kwa uadilifu na hata mwakani wakija kwenye Saba Saba wanakuwa wanaweza kutumia kadi zao kutoa pesa ili kufanya matumizi yao," alisema Mkono.


MAELEZO ya PICHA:-
Baadhi ya watoto wakionesha zawadi walizopewa ndani ya Banda la NMB Sabasaba. Kulia ni mmoja wa maofisa wa Benki ya NMB.

--
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment