Mkutano Mkuu Wa Umoja wa Watanzania Ujerumani 2017 watingisha Essen
Umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V watingisha jiji la Essen nchini Ujerumani baada ya kufanya mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba ulioandamana na sherehe za ushindi wa viongozi wapya. Hapo jijini Essen katika ukumbi wa Bob's Cafe, watanzania zaidi ya 75 ambao wanaishi nchini humo walihudhuria mkutano huo ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wao, katika safu ya uongozi mpya Mhe Mfundo Peter Mfundo alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa umoja huo baada ya kukosa mpinzani. Makamo mwenyekiti mpya ni Mhe Salim Malumbo Jr. Katibu mkuu ni Julieth Myn, muweka Hazina ni Bi Nashe Mvungi, Mkaguzi wa mahesabu namba 1 ni Mhe Bi Jovither Mushashu, Mkaguzi wa mahesabu namba 2 ni mhe Bi. Lilian Sorogo. Mjumbe namba Moja ni Mhe Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja na Mjumbe namba 2 ni Mhe Vanessa Lymo. pamoja na mengi yalioongelewa kwenye mkutano huo azma ya umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V ni kuwaendeleza watanzaniawanaoishi hapa ujerumani na hata kuwaletea maendeleo watanzania wanaoisho Tanzania, umoja ni Nguvu na utengano ni Udhaifu
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment