TAMWA kutoa elimu kupambana na ulevi kupindukia
KITUO cha Usuluhishi (CRC) kinachofanya kazi chini ya Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) kimejipanga kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha kinapambana na matumizi ya pombe kupindukia kwa jamii suala ambalo limezidisha vitendo vya ukatili wa jinsia unaofanywa na watumiaji pombe kupindukia.
Akizungumza na wahariri wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka alisema utafiti uliofanywa na Shirika la IOGT International unaonesha kuwa kiwango cha unywaji pombe jijini Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake huku ikibainika kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya vitendo vya ukatili na matumizi ya pombe kupita kiasi.
Bi. Soka alisema takwimu zinaonesha kuwa wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha vipigo, kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77, huku kiwango cha ukatili kwa wanawake ambao waume ama wenzi wao hawanywi pombe ni asilimia 33.
"...Utafiti uliofanywa na shirika la IOGT International unaonyesha kwamba kiwango cha unywaji pombe katika jiji la Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake...lakini takwimu kutokana na utafiti wa Demographia na Afya Tanzania (TDHS) 2010...unaonesha wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha kipigo/kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77," alisema.
Aidha aliviomba vyombo vya habari kushirikiana na TAMWA kutoa elimu kwa jamii kupunguza matumizi ya pombe kupindukia kwani licha ya ukatili huo familia pia zimekuwa zikiathirika kiuchumi juu ya matumizi ya pombe huku baadhi ya watoto wakikosa huduma za msingi kutoka kwa baadhi ya wazazi ambao ni walevi kupindukia.
Alisema TAMWA inatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unaosababishwa na pombe huku lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha maisha ya wanawake na watoto yanaboreshwa kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia.
Hata hivyo alisema tayari chama hicho kimeanza kufanya utafiti mwingine katika Wilaya ya Kinondoni kuangalia madhara yanayotokana na unywaji wa pombe kupindukia ili kuangalia hali halisi ya matumizi ya pombe eneo hilo na madhara ambayo yamekuwa yakitokana na matumizi hayo.
Alisema malengo mengine ya mradi ni pamoja na kuboresha maisha ya wanawake na watoto kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe katika wilaya ya Kinondoni na pia kujenga uelewa miongoni mwa jamii juu ya madhara yatokanayo na unywaji wa pombe kupindukia.
Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA aliongeza kuwa mapambano hayo pia yatasaidia, kukabiliana na matumizi ya pombe na kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu ukatili dhidi ya wanawake unaotokana na matumizi ya pombe, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa jamii kukabiliana na ukatili unaosababishwa na unywaji wa pombe dhidi ya wanawake na watoto.
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment