Mkurugenzi wa Mawasiliano Chadema John Mnyika amemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kujiandaa kupokea maandamano ya maelfu ya wafuasi wa Chadema watakaokwenda kumueleza ukweli kuhusu chama chao.
Mnyika alisema hali hiyo imesababishwa na ofisi ya msajili wa vyama wiki iliyopita kuamua kupokea maandamano ya wahuni na vibaraka wa wasaliti waliofukuzwa Chadema mapema mwaka huu.
Mnyika amesema ofisi ya msajili inapaswa kuwa makini sana ili isipoteze hadhi yake kwani haiwezekani mhuni yoyote kuvamia ofisi ya msajili na kujiita kiongozi wa Chadema na ofisi hiyo ikampa heshima bila kuuliza vielelezo vyovyote vya kuthibitisha uongozi wake ndani ya Chadema.
Ni hivi karibuni baadhi ya watu waliofukuzwa ndani ya Chadema walifanya maandamano haramu kwenda ofisi ya msajili na kupeleka mashtataka dhidi ya viongozi wakuu wa Chadema huku wakijiita ni viongozi wa Baraza Kuu la Chama.Hata hivyo baadhi ya nyaraka kutoka ofisi hiyohiyo ya msajili zinaonyesha baadhi ya watu hao ni viongozi wa chama kimoja kipya cha siasa hapa nchini kilichopata usajili hivi karibuni.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment