kazi kweli, 2015 tutasikia mengi sana
On 6/27/14, MABADILIKO CHADEMA <mabadilikochadema@gmail.com> wrote:
> JORUM ABDALLAH MBOGO
>
> S.L.P 1110
>
> TABORA
>
> 25.06.2014
> MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA
> S.L.P 63010
> DAR ES SALAAM
> TANZANIA
>
> Ndugu,
> YAH: *MAOMBI YA UFAFANUZI WA KIKATIBA JUU YA* *UVUNJIFU WA KATIBA NA
> YA CHAMA UNAOFANYWA NA VIONGOZI*
> Mheshimwa Msajiri, Somo hapo juu la husika.
> Mimi ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,
>
> Kwa niaba ya wanachama wenzangu, tunaleta kwako malalamiko ya uvunjifu
> wa katiba ya chama Yanayotokana na matamko yanayoendelea kutolewa na
> viongozi wa kitaifa juu ya kuungana na UKAWA yenye tafsiri kwamba
> wataachiana majimbo ya kugombea ili waweze kuingia madarakani na kuunda
> serikali ya pamoja.
>
> kama hivyo ndivyo wanakiuka SURA YA TISA. IBARA YA 9.3.1 ya *KATIBA YA
> CHADEMA* inayosema ''*chama kinaweza kuunda mseto na chama au vyama
> vingine vyenye madhumuni na malengo yanayofannaili kuimarisha iwezo wa
> kushinda uchaguzi mkuu au wa serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda
> utawala wa pamoja''*
>
> Kwa kuwa viongozi wa CHADEMA na CUF na NCCR wameungana na kuunda chama
> kingine cha UKAWA kwa mujibu wa SURA YA TISA ibara ya 9.3.3 *''chama
> kinaweza kuungana na chama ama vyama vingine kuunda chama kipya'' *hivyo
> wamevunja *SURA TISA*, *Ibara ya 9.3.4* inayosema *''Uamuzi kuhusu
> vipengere 9.3.1, na 9.3.3 utafanywa na mkutano mkuu wa Taifa na kuhusu
> kipengere 9.3.2 na Baraza KUU''.*
>
> Na hivyo sisi kama chama hatujakaa BARAZA KUU ili kupitisha AGENDA za huo
> mkutano mkuu na wala MKUTANO mkuu haujaitishwa kujadili maamuzi hayo
> yaliyofikiwa na viongozi wetu.
>
> Mheshimiwa Msajiri, Tunafahamu kwamba KANUNI za chama SURA YA TISA kuanzia
> ibara ya 9.0 Mpaka ibara ya 9.7 zinatoa uhuru wa chama kuungana na kufanya
> ushirika na vyama vingine kwa kadri itakavyoona inafaa.
>
> Ila kanuni hizi zinaweka mkanganyiko wa kitafsiri, na hivyo zinazuiwa na
> kuuliwa nguvu na Ibara ya *9.2.3 *ya*KATIBA YA CHAMA* Inayosema
> *''kukitokea
> migongano kati ya kipengele cha katiba na kile cha kanuni, kipengele cha
> katiba kitatawala''. ** Hivyo kanuni zinazotoa uhuru huo haziwezi kutumika
> hapa.*
>
> Mheshimiwa msajiri, kwa kuwa wewe ndio mlezi na msimamizi wa vyama vyote
> vya siasa, na kwa kuwa hakuna chama cha siasa kilicho juu ya katiba yake,
> hivyo tunakuomba uingilie kati mgogoro huu wa uvunjifu wa katiba unaofanywa
>
> kwa makusudi na viongozi wa chama.
>
> Tunakuomba pia uuagize uongozi wa kitaifa uitishe haraka kikao cha baraza
> kuu, kwani tumeshapitisha miezi mi nne sasa ya kisheria ambayo baraza kuu
> lilipaswa kukaliwa, mara ya mwisho tulikaa kikao cha baraza kuu mwezi
> febryary mwaka 2013, hivyo tulitakiwa tena tukae baraza kuu mwezi February
> mwaka huu. Hatujaitwa, wala hatujapewa sababu yoyote yenye mantiki.
>
> Vile vile tunakuomba uwaagize viongozi wa chama waitishe chaguzi halali za
> zhama na waache kuchomeka watu wao wanaowataka kwa hila, kwa mujibu wa
> ratiba tulizozipitisha uchaguzi ulupiswa kuwa umeshafanyika kufikia
> December 2013, na baadae june 2014, lakini mpaka tunavyokuandikia leo,
> hakuna lililofanyika.
>
> Tunakutakia kila la heri katika kutusaidia ufafanuzi huu.
>
> Tunatanguliza shukrani za dhati na tukiamini swala letu litafanyiwa
> linavyostahili.
>
> Wako katika ujenzi wa Taifa.
>
>
> JORUM ABDALLAH MBOGO
>
> ………………………………………..
>
> *+255785054539 <%2B255785054539>*
> *jorummbogo@gmail.com* <jorummbogo@gmail.com>
> MWANACHAMA WA CHADEMA
> MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
> MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
> MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
>
> Nakala :- Vyombo vya habari
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment