Kijana huko uliko Ulaya tunakuongezea references za mambo ya Mipango Miji na Mengineyo yanayosulubu watu katika kushirikisha wananchi na kupanga Ujenzi wa Miji, Vijiji na Mafao ktk Miradi Miundo mbinu na uwekezaji. umeiona nayo inaripuka Butiama sio tu Mtwara artisana miners wasioelekea kujiunga katika vikampuni waweze kupata hata mikopo kampuni sikue waweze kufanya large scale mining. uchao kutegemea kuua albino, mauaji na kushukiana uchawi kuchomeana nyumba. kila mtu kuchimba kivyake kuchakachua mazingiwa. mito inakwisha, magogo ya miti kukatwa na maji kuchafuliwa na wenyewe kuchezea mercury ambayo ni deadly. Leo wanataka kuendesha large scale industrial mining site. watafufuaje mitambo ya meremeta/Stamico? mashine watawezaje kununua, kuajiri geologists, occupational health officers, kuweka umeme, mashine za uchimbaji na mikanda ya usafirishaji etc. kama tanzania One ya Mengi inaajiri mpaka wazungu kuja kusaidia kuendesha uchimbaji na mitambo na huyu millionea, jee huyu wa kihirizi na kigozi cha chuma ulete ataweza bila kukubali kubadilika kiutendaji, kielimu etc. Ni sawa na kusema-Swedish comapny inayomiliki Wazo Hill Cement Factory inahama sasa Mitambo ile ya kuchimba mawe na kuzalisha cement wapewe wachima kokoto wadogo wadogo wa Kuchuchi na salasala waliouza mashamba yao na sasa wamehamia ktk mashimo ya kokoto hapo Mbuyuni wanachimba kwa sululu na sepeto na vibanda mvua ikinyesha hapakaliki. maekeri ya customary land na waliyopewa na vijiji vya ujamaa wameuza na sasa ni kuvamia mashamba ya watu (hatuna ardhi) kisha wanauza (kilabuni) kesho wanavamia tena na kuuza na kuchimba kokoto mpaka chini ya milingoti ya umeme na kato ya barabara. fika huko Alexander ukaone, fika machimboni ukaone halafu uone kama tusipobadilika tutajikwamua. Mchina, Mwarabu wa Dubai atajenga kama NHC ilivyojenga na itakavyojenga. Jee, tutatii sheria za miji na za usafi? Hebu angalia majumba ya NHC popole pale hata pale ambapo wanakaa wafanyakazi na police, police wa usalama barabarani, JWTZ. Angalia kuta kwa nnje zilivyochafu kwa watu kumwaga maji machafu kutoka juu, magunia ya mkaa na makorogoro kibao. angalia madirisha ya maboksi na mapazia ya mikeka na vigenge vya biashara huko huko juu na mabanda ya mbuzi na kuku maeneo ya kucheza watoto. Tutaweza kuiiga hiyo Dubai hata wakitujengea tutatunza? Mtanzania, hata umshirikishe atasema hajui sijashirikishwa. Ndani ya familia atasema-sijaambiwa ili apate sababu ya kutokuchangia. Mungu atusaidie tuonage vingine kwa macho chanya ili tubadilike tupate maendeleo.\ Sio kila kijacho kibaya. Ina maana wataalamu wote wa wizara hawakukaa kujadiliana, mpaka kufika kutoa tender ifike kuwa hakieleweki. hata wale wenye viwanja na hati kariakoo wakiambiwa wawe wabia-wengi hawakubali. Nipe pesa zangu mie niondoke. Na baada ya muda bilioni moja-kabang na hajafanya kitu cha maana na bank hakuweka. Kama alilipiwa bang alizitoa zikaporwa, akaibiwa. walioenda China kuleta vicna siku hizi dawa ya viagra ya akina mama imepatikana-mbona wanaporwa kichizi!! --- On Tue, 28/5/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment