Mfano wa SEA kabla ya mpango wa uwekezaji. Watendaji kazi wa Ujenzi wa Kinondoni walitakiwa kufanya kitu cha namna hii na studies nyingine nyingi kabla ya SEA ili kuweza kuamua kufanya walilofanya. participatory land use planning Mama Tibaijuka anaijua sana ndio Habitat yake na Sustainable Cities approach aliyotuletea Tanzania ikawika halafu ikazimia ikalala. Maana kunajengeka-tunaharibu. Ardhi wangehusishwa wananchi kama nilivyotolea mfano wa Mafia huko nyuma katika ujenzi wa International Airport (na pia kuna bandari inajengwa kukuza uchumi) kuunganisha kisiwa kukubwa chenye mali na miji mingine na coastal ports nyingine mambo yangekuwa poa. Ufuatiliaji wa utendaji unatakiwa kama mipango iliyopangwa na kufaidika wananchi kunatokea kweli-ajira, elimu, huduma na faida nyingine. Bila ya shaka Mh Tibaijuka akiwa kiongozi mmojawapo aliyejipatia sifa kwa kazi yake Un-Habitat amefanya hivyo lakini sharing ya walichofanya nasi wanaTZ wengine ni tatizo. Aweke wazi basi alifanyaje hiyo mipango ya Kigamboni, medium of communication gani alitumia, walishirikishwaje wananchi na viongozi wao na Idara mbali mbali za huko na za mawizara maana budi huduma huko wizara mbali mbali zitahusika. Majibu yatapatikana kama ilikuwa Top-Down au Bottom-up ili wengine au sekta nyingine sijufunze kutoka makosa haya ya ushirikishaji pungufu wa wananchi na viongozi wao yasirudiwe kama kweli hawakufanya. Muhimu ili moto wa mtwara usirukie kigamboni-itatugharimu wote kitaifa. Wananchi waone pia jinsi wanavyojifukuza wenyewe kwa kuuza maeneo yao wengine wanajenga maghorofa yanayozuka mpaka low income residential areas. anahama anahamia pondeni au anakwenda kwao, anamaliza hela bara kisha anarudi tena mjini anakuwa impoverishi kuliko kwanza. kwa sasa kote kunakopita barabara ya lami watu wameuza mashamba ni mlolongo wa bar na majumba ya vileo tu njia nzima. Tuelimishe familia na jamii zetu wasiuze`maeneo yote wanajifanya wakimbizi ndani ya nchi yao.Wanapogawana mauzo ya nyumba ya miradhi-wafanye vya maendeleo kwa kuzingatia sheria. Magendo utakamatwa na kupoteza bidhaa na hela ukawa burai/masikini maisha. --- On Tue, 28/5/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment