Sunday, 2 December 2012

[wanabidii] POLISI MNATIA SHAKA MALI ZA SHARO MILIONEA-MMEIBA?

Jeshi la polisi, tungependa mjue kuwa ninyi mnaishi katika jamii. Sio vizuri sana kuiona jamii ni ya watu wajinga sana kwa kiasi kwamba mnabeza hata uwezo wa jamii kuelewa vitu kwa akili ya kawaida bila kusoma sana. Jeshi la Polisi jifunzeni kwetu tunapoandika makala. Tunapoandika na kuitoa, tunajua inasomwa na watu wengi, wenye maarifa mbalimbali, hivyo inatuwia vigumu kuandika kwa kukurupuka. Unapoandika kitu kwa jamii, ujue jamii inayosoma suala hilo ina wasomi, ina wakulima, ina madaktari, ina polisi wenye akili, ina wana jeshi nk.

Ukiandika tamko la polisi likawa la kipuuzi, unadhalilisha jeshi. Tunafikiri na wengine hawana akili, lakini kumbe pengine sio. Sasa kwanini wewe uliyepewa jukumu la kukaa mezani kuandika kwa niaba ya Polisi uchafue jeshi zima kwa sababu za fikra ndogo?. Watu wanatilia shaka kuwa uteuzi wa majaji hauzingatii sifa, je na polisi uteuzi hauangalii hayo? Ni hatari sana kuongozwa na watu wenye maono madogo.

Pengine hata tunaposema, mauaji, vitendo vya kikatili, na vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi vinazidi. Vitendo hivi vinazidishwa pamoja na utendaji na matamko ya polisi ya kizembe kama hili ninalotaka watu waelewe uwezo wa polisi ulivyo.

 Hivi majuzi tunatambua kuwa msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Mkieti 'Sharo Milionea' alipata ajali, ajali hiyo ilipelelekea kifo chake, na watuw asio waungwana wakamwibia kabisa na kila mtu mwenye maadili mema akasitikishwa na kitendo hicho.

Tarehe 30/12/2012, jeshi la polisi lilitoa taarifa kuwa vitu vilivyoporwa na watu wasiojuliana katika ajali ya msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Marehemu Hussein Mkieti 'Sharo Milionea' eneo la Songa Kibaoni wilayani Muheza mkoani Tanga, vimesalimishwa na wananchi wanaosadikiwa ni wezi. Hivi kweli wananchi ni wezi?, tunazumgumzia wananchi wenye hasira kali, kumbe ahta siku hizi tunaweza kusema wananchi wezi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, alithibitisha kupatikana vitu hivyo, ambako alisema upatikanaji wake ulitokana na msako mkali uliofanywa na uongozi wa serikali Muheza wakishirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo. Mpaka hapo hakuna shida, tunawapongeza kwa msako. Hii ni kazi nzuri

Kamanda alisema, baada ya kutokea kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Tanga, liliweka mtego na kutangaza kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya 'blackberry' ndipo moja kati ya wanaodaiwa vibaka waliohusika kwenye tukio hilo, alipojitokeza na kuipeleka kwa ajili ya kuiuza. Hii ni intelijensia nzuri, mliweka mtego, mwizi akaleta simu nako ni sawa. Tunamshukukru kachero aliyeweka mtego simu ikaletwea.

Kamanda alisema, wakati wezi walipofika eneo ambalo walikubaliana, walikabidhi simu hiyo kwa ajili ya kuikagua, lakini baadaye wezi hao walishtukia mtego huo na kukimbia huku wakiiacha simu hiyo. Hapo ndo huwa nakasirishwa na polisi. Walijua anayekuja ni mwizi, alipokimbia kwanini hawakumkamata? Kwanini hawakumfukuza? Hawakuwa na bunduki kumtishia? Kwanini mwizi amekimbia, na amekimbilia wapi? Polisi semeni vizuri kuondoa dhana kuwa mmehongwa kuwaachia watu wasio waungwana. Eti Mwizi amekimbilia kusikojulikana, kwanini wakati anakimbia askari hakukimbizana naye kwenda huko kusikujulikana ili kujulikane ni wapi? Kifalsafa nakataa

Kamanda hakuishia hapo ametaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo kuwa ni simu ya mkononi aina ya blackberry, Betri la gari, tairi la akiba, radio ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo ambazo alikuwa amevuliwa na vibaka wa eneo hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo. Mmesema Mwizi wa simu alikimbia, wa tairi la fari, na Yule wa betri, na Yule wa redio ya gari, na Yule wa begi la nguo. Wote hawa walikimbia, au  polisi kweli mtaaminika lini kwa utendaji wa aina hii? Inasononesha sana lakini matamko kama haya  yanazidisha hasira za wananchi, na kuongeza vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi. Badilikeni. Polisi kuvaa magwanda kuja kukaa kwa waandishi kuzungumza "hewa". Iwe mwisho.

 

 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment