Sunday, 2 December 2012

Re: [wanabidii] POLISI MNATIA SHAKA MALI ZA SHARO MILIONEA-MMEIBA?

Josephat

Nakushukuru kwa kulishupalia suala hili ambalo kwa liasi kikubwa linalifanya jeshi letu la polisi kuonekana linafanya kazi kizamani sana wakati linategemewa kufanya kazi kisayansi na kiteknolojia katika zama hizi. Jeshi hili kwa sasa lina wasomi weng wa hali ya juu lakini utendaji wake wa kazi ni wakizembe kwa kiasi kukibwa na kukusa uwajibikaji kwa raia. Lakini ikitokea kuwa mmoja wao kapatikana kama ilivyokuwa kwa Kamanda Barow wanafnya kazi kwa majigambo makubwa. Sasa hii inaonyesha kuwa kumbe wana uwezo lakini hawataki kuutumia mpaka kuwe na maslahi yao kama jeshi hii ni hatari sana. Kwa mfano katika zama hizi za sayansi na teknolojia kazi ya jeshi lililo makini inakuwa rahisi sana lakini wao wanapodai kuwa mtuhumiwa kakimbia na hawakuweza kumkamata inatia kinyaa.

 Lakini pia kama nilimsikia vizuri kamanda wa polisi Muheza alisema kuwa baadhi ya vitu kama betri ya gari, tairi na begi likiwa na vitu vilikuwa wemetelekezwa mahali na watu walivikuta wakatoa taarifa kuwa vimeonekana kuachwa sehemu ila alisema pesa hazikuweza kurudi kwa kuwa ni viumu kuthibitisha kuwa fedha hii ilikuwa ya marehemu na hii siyo. 

Nafikiri kwa hatua hii ya kutia mkwara vitu vikarudi ni ya kupongezwa pia kwani watu wengi sana wanaopata madhara kama hayo wanappoteza kila kitu. Lakini nafikiri hili lisifanyike tu kwa watu maarufu inatakiwa lifanyike kwa watu wote.

Kwa mtazamo wa upande mwingine nafikiri jamii inatakiwa kuelimishwa kutokuwa na roho ya kikatili namna hii. Wakati ajali inapotokea watu wawe na utu kutoa msaada na siyo kutaka kujinufaisha kwa namna hii ya kinyama. Kwa kweli hata kama hali ya maisha ni ngumu kiasi gani kwa mtu mwenye utu na anayejiheshimu vitendo kama hivyo ni aibu tupu na kujiletea laana. Na kwa mtindo huu inawezekana kabisa kuwa watu wakamalia kumuua mtu ambaye amgeweza kupona katika ajali ilimradi walijiridhishe kupora mali zake. Mungu ainusuru jamiiyetu na tabia hii mbaya na ya kinyama. Sasa sijui suala hili litawezekanaje kushughulikiwa ili umma wa wakazi wa maeneo ya barabara kuu na nyinginezo waweze kuachana na tabia hii.

Napenda kuwasilisha

Ken


2012/12/2 Josephat Isango <joseisango@yahoo.com>

Jeshi la polisi, tungependa mjue kuwa ninyi mnaishi katika jamii. Sio vizuri sana kuiona jamii ni ya watu wajinga sana kwa kiasi kwamba mnabeza hata uwezo wa jamii kuelewa vitu kwa akili ya kawaida bila kusoma sana. Jeshi la Polisi jifunzeni kwetu tunapoandika makala. Tunapoandika na kuitoa, tunajua inasomwa na watu wengi, wenye maarifa mbalimbali, hivyo inatuwia vigumu kuandika kwa kukurupuka. Unapoandika kitu kwa jamii, ujue jamii inayosoma suala hilo ina wasomi, ina wakulima, ina madaktari, ina polisi wenye akili, ina wana jeshi nk.

Ukiandika tamko la polisi likawa la kipuuzi, unadhalilisha jeshi. Tunafikiri na wengine hawana akili, lakini kumbe pengine sio. Sasa kwanini wewe uliyepewa jukumu la kukaa mezani kuandika kwa niaba ya Polisi uchafue jeshi zima kwa sababu za fikra ndogo?. Watu wanatilia shaka kuwa uteuzi wa majaji hauzingatii sifa, je na polisi uteuzi hauangalii hayo? Ni hatari sana kuongozwa na watu wenye maono madogo.

Pengine hata tunaposema, mauaji, vitendo vya kikatili, na vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi vinazidi. Vitendo hivi vinazidishwa pamoja na utendaji na matamko ya polisi ya kizembe kama hili ninalotaka watu waelewe uwezo wa polisi ulivyo.

 Hivi majuzi tunatambua kuwa msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Mkieti 'Sharo Milionea' alipata ajali, ajali hiyo ilipelelekea kifo chake, na watuw asio waungwana wakamwibia kabisa na kila mtu mwenye maadili mema akasitikishwa na kitendo hicho.

Tarehe 30/12/2012, jeshi la polisi lilitoa taarifa kuwa vitu vilivyoporwa na watu wasiojuliana katika ajali ya msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Marehemu Hussein Mkieti 'Sharo Milionea' eneo la Songa Kibaoni wilayani Muheza mkoani Tanga, vimesalimishwa na wananchi wanaosadikiwa ni wezi. Hivi kweli wananchi ni wezi?, tunazumgumzia wananchi wenye hasira kali, kumbe ahta siku hizi tunaweza kusema wananchi wezi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, alithibitisha kupatikana vitu hivyo, ambako alisema upatikanaji wake ulitokana na msako mkali uliofanywa na uongozi wa serikali Muheza wakishirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo. Mpaka hapo hakuna shida, tunawapongeza kwa msako. Hii ni kazi nzuri

Kamanda alisema, baada ya kutokea kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Tanga, liliweka mtego na kutangaza kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya 'blackberry' ndipo moja kati ya wanaodaiwa vibaka waliohusika kwenye tukio hilo, alipojitokeza na kuipeleka kwa ajili ya kuiuza. Hii ni intelijensia nzuri, mliweka mtego, mwizi akaleta simu nako ni sawa. Tunamshukukru kachero aliyeweka mtego simu ikaletwea.

Kamanda alisema, wakati wezi walipofika eneo ambalo walikubaliana, walikabidhi simu hiyo kwa ajili ya kuikagua, lakini baadaye wezi hao walishtukia mtego huo na kukimbia huku wakiiacha simu hiyo. Hapo ndo huwa nakasirishwa na polisi. Walijua anayekuja ni mwizi, alipokimbia kwanini hawakumkamata? Kwanini hawakumfukuza? Hawakuwa na bunduki kumtishia? Kwanini mwizi amekimbia, na amekimbilia wapi? Polisi semeni vizuri kuondoa dhana kuwa mmehongwa kuwaachia watu wasio waungwana. Eti Mwizi amekimbilia kusikojulikana, kwanini wakati anakimbia askari hakukimbizana naye kwenda huko kusikujulikana ili kujulikane ni wapi? Kifalsafa nakataa

Kamanda hakuishia hapo ametaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo kuwa ni simu ya mkononi aina ya blackberry, Betri la gari, tairi la akiba, radio ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo ambazo alikuwa amevuliwa na vibaka wa eneo hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo. Mmesema Mwizi wa simu alikimbia, wa tairi la fari, na Yule wa betri, na Yule wa redio ya gari, na Yule wa begi la nguo. Wote hawa walikimbia, au  polisi kweli mtaaminika lini kwa utendaji wa aina hii? Inasononesha sana lakini matamko kama haya  yanazidisha hasira za wananchi, na kuongeza vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi. Badilikeni. Polisi kuvaa magwanda kuja kukaa kwa waandishi kuzungumza "hewa". Iwe mwisho.

 

 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment