Monday 21 August 2017

[wanabidii] Timu ya Polisi Tanzania yapokea vifaa vya michezo toka NMB

Timu ya Polisi Tanzania yapokea msaada wa vifaa vya michezo toka NMB  

 

Na Mwandishi Wetu

 

BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya mchezo kwa Timu ya Mpira wa Miguu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara. 

 

Vifaa hivyo ni pamoja na mipira, mabegi ya wachezaji, viatu, tracksuit na jezi mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13, vilikabidhiwa kwa jeshi la polisi na Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB - Ally Ngingite kwa Kamishna wa Polisi - Adrian Magayane.

 

Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, bwana Ngingite alisema NMB inaamini msaada huo kwa Timu ya Jeshi la Polisi utakuwa chachu ya kufanya vizuri zaidi katika michuano mbalimbali iliyopo mbele yao hususani Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inayotarajia kuanza hivi karibuni.

 

"Vifaa tunavyokabidhi leo ni pamoja na jezi, track suti, mabegi, mipira, viatu vya kuchezea na vifaa vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13," alisema bwana Ngingite

 

Msaada huo kwa timu ya jeshi la polisi ni mwendelezo wa kusaidia kukuza sekta ya michezo nchini huku benki hiyo ikijinasibu kuwa imekuwa mshirika mkubwa sana katima maendeleo ya michezo nchini. Mbali na kuisaidia timu ya polisi, NMB pia inaidhamini timu ya Azam MC ya Ligi Kuu Tanzania Bara na imekuwa ikisaidia timu mbalimbali kuendeleza michezo.

 

Bwana Ngingite alizitaja timu nyingine ambazo NMB imetia Mkono wake hapa nchini ni pamoja na clabu ya Gofu ya Lugalo, Singida United na Clabu ya jeshi ya Gymkana.

 

Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo, Kamisha wa Polisi - Adrian Magayane alishukuru kwa msaada na kusema kuwa utaongeza chachu ya ushindi na kuhakikisha kuwa wanatinga ligi kuu msimu ujao.

"Tunawashukuru sana NMB, benki hii imekuwa mshirika wetu mkubwa sana katika nyanja mbalimbali, tunaimani tutabeba nembo yao vizuri kwa kufanya vyema kwenye mashindano ya ligi daraja la kwanza." Alisema Kamishna Magayane.




MAELEZO PICHA

IMG_6487, IMG_6489, IMG_6497, IMG_6487, 
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) akimkabidhi baadhi ya vifaa vya michezo Naibu Kamishna wa Polisi, Adrian Magayane (kulia) vilivyotolewa na NMB kwa ajili ya Timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Daraja la Kanza Tanzania Bara. Wengine katikati kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mwandamizi Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada wa NMB, Stephen Adili na Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmada Khamis wakishuhudia tukio hilo.

IMG_6457, IMG_6476, IMG_6477
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya mchezo wa mpira wa miguu kwa ajili ya Timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Daraja la Kanza Tanzania Bara. Wengine kushoto kwake ni maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania walioshiriki kupokea vifaa hivyo vya msaada.

IMG_6515, IMG_6518
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB (kushoto) pamoja na wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lililofanyika leo jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya Benki ya NMB. Vifaa hivyo vimetolewa na NMB kwa ajili ya Timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Daraja la Kanza Tanzania Bara. 

NMB 1, 
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya mchezo wa mpira wa miguu kwa Timu ya Polisi Tanzania inayotarajia kushiriki Ligi Daraja la Kanza Tanzania Bara. Kulia ni Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmada Khamis wakishuhudia tukio hilo.

IMG_6468
Sehemu ya Maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.

___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

Virus-free. www.avast.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment