Hii hainihusu.
em
2017-03-16 16:35 GMT-04:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Chama cha Mapinduzi kimerekebisha katiba yake kwa makusudi ya kukifanya kijitegemee badala ya kutegemea "wafadhili"; kiboreshe utendaji wake; kipunguzr garama za uendeshaji na kuondoa muingiliano; mambo ambayo yakifanikiwa yatarudisha chama mikononi mwa wanachama wa kawaida na kukiweka karibu na wananchi. Mambo haya yalitarajiwa kufanyika mwaka 2005 alipoingia madarakani rais mstaafu Jakaya kikwete. Nakumbuka kuandika makala kuonyesha tumaini la wanachama hilo. Kumbe hii ilikuwa haiwezekani mpaka kiongozi awe na uwezo wa kuwaambia wenye pesa waeleze kama kuna aliyemchangia hata shilingi katika kampeni za uchaguzi.
Jambo lolote likifanyika lazima likubalike na lipingwe. Kwa hiyo napenda kujadili mambo matatu; kufanikiwa kwa mabadiliko hayo; kukubaliwa kwa mabadiliko hayo na kukataliwa kwa mabadiliko hayo na athari zake hasi na chanya.
Mabadiliko haya yakubalike yasikubalike kwa wote lazima yatafanikiwa. Yatafanikiwa kwa sababu tayari yamepitishwa bila kuonekana kupingwa. Nasema kuonekana kupingwa kwa sababu kura za ndiyo zilikuwa nyingi na hakukuwa na sauti za hapana. Lakini baada ya sauti hizo, mtu angesambaza karatasi watu wapige kura ya siri ndipo tungeona tofauti. Kuna watu wangepiga kura ya hapana.
Chama Cha mapinduzi, kama vilivyo vyama vingine vya siasa hapa Tanzania, vimekuwa mbali sana na wananchi hasa wanyonge. Ukiondoa CHADEMA kilivyokuwa kati ya mwaka 2007 hadi 2015 kilipojiweka karibu na shida za wanyonge; lakini vyama vyote , (na CHADEMA ikiwemo baada ya kipindi hicho cha 2007-17) vyama vya siasa vimemilikiwa na matajiri na wafanyabiashara haramu. CCM iliwakumbatia ikafikia mahala vijiwe vya kuuzia bangi vinasimikwa bendera ya CCM au kufungua tawi la wakereketwa na kuendelea kwa uhuru. Rushwa zilitawala katika chaguzi mbalimbali za chama. Watu kwa mfano walitafuta nafazi za ujumbe wa halmashauri kuu ili iwe rahisi kwao kugombea ubunge ambao mavuno ya kiinua mgongo baada ya myaka mitano ni ya ajabu. Hivyo shida za wananchi zikawa ni kuzisikiliza na kuziacha hapohapo. Viongozi wakawa na matamshi kana kwamba hawaishi Tanzania. Mfano mmoja ni mbunge aliyesema Serikali ipandishe kodi ya Petrol kwa sababu magari yake ni ya anasa. Akasahau kuwa bodaboda wanatumia Petrol na wanabeba maskini. Madaktari wanatumia magari yao ya Petrol kwenda kuokoa maisha ya maskini. Hawajui kuwa magari ya Diesel ndiyo ya hanasa kuliko ya Petrol, ukiondoa magari ya mizigo na mabasi. Wananchi wakakosa jambo walilolizoea, kuwa na chama kilicho karibu nao. Kama nilivyosema hapo juu katika kipindi tajwa, CHADEMA kilijiweka karibu na wananchi kwa kuzitajataja shida za wananchi na namna ya kuzitatua. Wananchi wengi wakakiandama. wanaCCM wakiwemo viongozi wakahangaika wafanyeje kukirejesha chama karibu na watu. Moja kati ya mazoa ni uanzishwaji wa CCJ. Magufuli ni zao la msuguano huo. CCM ilibanwa, ikaona ikiendelea kuwakumbatia wenye fedha ndio mwisho wake. Kikamchagua Magufuli awe mgombea wa nafasi ya urais 2015. Tunakumbuka kigugumizi alichokuwa akikabiliana nacho kuitaja CCM katika kampeni zake. Ni kwa sababu CHADEMA ilitelekeza mwelekeo wake kwa kuwakumbatia watuhumiwa wa ufisadi; na CCM kumuweka mtu anayeuzwa na rekodi yake ya utendaji, la sivyo 2015 ulikuwa ni mwaka ambao CCM ingeondolewa madarakani.
Nakumbuka mwandishi mmoja wa makala kuandika kuwa Kama CCM haitaondolewa 2015 basi itachukua myaka mingine mingi upinzani kujipanga kuiondoa. Maana ya mwandishi huyo ilikuwa ni hiki kinachojitokeza kwamba CCM inajijenga upya na inakwenda kwa wananchi. Ikumbukwe kuwa CCM inao uzoefu wa kutosha. Inao watu wa namna zote; Viongozi wazuri wako CCM. Viongozi wabovu wako CCM. Kilichokuwa kinakosekana ni namna ya kuwaengua viongozi wabovu safu ya mbele na kuwasukuma nje au safu za nyuma.
Sasa ameingia fyatu. Hajui kuheshimu mtu labda kama mtu huyo anajiheshimu mwenyewe. Matamshi kama yaliyotamkwa na msukuma Bungeni hutayasikia tena, Kuwa bangi ni zao halali lihalalishwe? Hakuna. Nidhamu moja kwa mbele. Kila kiongozi atalinda nafasi yake kwa utendaji wake.
Matunda ya mabadiliko haya yanaweza kuishia kwa kupanuka CCM ikawa na wanachama na washabiki na wapenzi wengi. Matunda ya kazi yake yataonekana yatake yasitake. Kama viongozi watakwenda kwa wananchi na kuziangalia kero zao na kutoa maelekezo kwao au kwa uongozi wa serikali, hakutakuwa na kiongozi wa serikali anayelala. Kama alivyosema Mwenyekiti wa CCM katika mkutano maalum, kuwa mvua zinanyesha lakini viongozi wengine hawawahimizi wananchi kulima mazao ya muda mfupi. Kama viongozi wa serikali na wachama watalazimika kutoa taarifa walifanya nini katika tatizo Fulani, hapo wananchi watajikuta wana chama tawala na serikali vilivyo karibu nao.
Ikitokea hali ikawa hivyo na vyama vingine vikakosa kwenda na mabadiliko ndani ya CCM basin chi ya vyama vingi itageuka kuwa ya chama kimoja kwani wananchi watakuwa wanashiriki mikutano ya vyama vyote na kuichagua CCM kwa wingi na kuibakiza madarakani.
Upo uwezekano wa watu wengine kupinga mabadiliko haya. Kuna viongozi ambao kwa kupungua kwa ukubwa wa muundo wa chama au kupungua kwa wingi wa wajumbe kuna wanaoweza kujiengua ili kutafuta maslahi katika vyama vingine. Wengine wanaweza kuhama kwa kusudi la kwenda kutafuta uongozi maana wamezoea kazi za siasa. Lakini pia kutokana na marupurupu (kwa maana ya posho) kupungua watu wengine wataendeshwa na itikadi na sera. Naamini kuna watu wako CCM si kwa sababu ya mwelekeo wake wa ujamaa bali wanaongozwa na uwepo wa posho na maslahi mengine binafsi. Zikisha pungua kitakachowaongoza ni itikadi na sera za chama.
Kwa muhtasari Mabadiliko ndani ya CCM:
1 Chama Cha Mapinduzi kinatarajia kurudi karibu sana na wananchi hasa wale wa kawaida ambao kiliwatelekeza muda.
2 Kama vyama vingine havitaiga mabadiliko hayo basi taifa linaweza kujikuta likiongozwa na chama kimoja huku vingine vikiishi katika daftari la msajili wa vyama tu.
3 Kama Chama cha mapinduzi kikipoteza baadhi ya wanachama wake na wakajiunga na vyama vingine hasa ambavyo vitaenda na mabadiliko basi taifa litakuwa na vyama vya siasa ambavyo vitashindana kwa sera. Matokeo yake ni kuinufaisha CCM kwa muda vitakapokuwa vikijijenga upya na baada ya hapo ushindani wa kisiasa kupanuka sana nchini
Mwisho taifa litanufaika kwa sababu kukiwa na vyama viwili au vitatu vyenye nguvu vinavyoshindana kwa hoja ni manufaa kwa demokrasia ya nchi. Katika mazingira yoyote, lazima kila kundi lijitenge na watu wenye historia ya sifa mbaya. Vinginevyo vitadhoofika kama vinavyodhoofika vingine vilivyozoa hovyo.
Elisa Muhingo
0767 187 507
elisamuhingo@yahoo.com
--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@ googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting to this Forum bears
the sole
responsibility
for any legal
consequences of his or
her postings,
and
hence
statements and facts must be
presented
responsibly.
Your
continued membership signifies that
you agree to
this
disclaimer and pledge to abide by
our
Rules and
Guidelines.
---
You received this
message because you
are subscribed
to
the
Google Groups "Wanabidii"
group.
To unsubscribe from this group and
stop receiving
emails
from
it, send an email to wanabidii+...@
googlegroups.com.
For more
options, visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented
responsibly. Your
continued membership
signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules
and
Guidelines.
---
You received this message because you are
subscribed
to
the
Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
from it, send an email
to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/optout .
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her
postings,
and
hence
statements and facts must be presented
responsibly.
Your
continued membership signifies that you agree to
this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are
subscribed
to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout .
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment