Saturday, 18 March 2017

[wanabidii] AGGRESSIVE CHRISTIANITY MISSIONS TRAINING CORPS (ACMTC)

AGGRESSIVE CHRISTIANITY MISSIONS TRAINING CORPS (ACMTC)
Na. Maj. Frank Materu – ACMTC TANZANIA   0715 350 752
Kwanza  kabisa "AGGRESSIVE CHRISTIANITY "HAIHUSISHI VURUGU AU MATUMIZI YA SILAHA ZA KIMWILI (ona maelezo ya Mtume Paulo katika 2 Wakorintho 10:3-6 ambapo amewalenga maadui wa  Kristo na Wakristo; kadhalika angalia Waefeso 6:12). "Aggressive Christianity" au "ACMTC"  ni jina, ni njia ya uzima inayoilinda imani ya Kikristo (Yuda 3). Kama vile Yesu ALIVYOZIPINDUA MEZA  NA VITU VYAO  Hekaluni ( Mathayo Mtakatifu 21:12-13) na kuwaita watu WEZI (mst.13) ndivyo "Roho ya Aggressive ya Kikristo" iletavyo mtikisiko.
Mungu alituinua kama mwili wa waumini, kufundisha kwa ajili ya utume-"Kumpeleka Yesu Duniani Kote" KATIKA KITABU CHA (waraka wa) Yuda, tunapata neno "mwishindanie imani" "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu". (Yuda 1:3). Hiyo ndiyo "Roho ya Aggressive" . Kuhusu uanajeshi katika Agano Jipya fungua mistari inayosema "Ushiriki taabu pamoja nami, kama ASKARI mwema wa Kristo Yesu". (2Timotheo 2:3) Na tena tunaiona hiyo katika 1 Timotheo 6:12 – "PIGA VITA vizuri vya imani…".  Kwa kweli ASKARI anahitaji silaha za vita( ona Waefeso 6:10-18).
JINSI ACMTC ILIVYOANZA – Kwa kifupi sana
Mara zote Mungu amekuwa akitukumbusha kutodharau siku zile za mwanzo ndogo.  "Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo?….." (Zekaria 4:10). Kama tukiangalia katika maisha, mchakato wote unaanzia katika mbegu, kitu kidogo kabisa, ndipo kinaota na kukua na kuzaa matunda. Ni muhimu kiasi gani kumwamini Mungu na kuendelea kuzitii amri zake kwetu. Marekani mwanzoni mwa miaka ya 1980's Majenerali Jim & Deborah Green walifungua huduma, walikuwa na mzigo sana  wa kushuhudia kwa kutumia machapisho ya injili.  Kwa hiyo, kwa msaada wa watu wengine wachache wakachukua rasilimali walizokuwa nazo na kuaza machapisho ya injili sebuleni kwao. Mungu akasema nao kwa njia ya unabii akawaambia kuwa ataizidisha sadaka yao, na kwamba machapisho hayo atakayotaka wayafanye  baadaye yatasambaa duniani kote kwa makumi ya mamilioni. Na mpaka sasa Mungu amelitimiza neno lake na machapisho ya injili yamesambaa duniani kote tena na tena.
Muda ulipokuwa unakwenda, Mungu akawambia anataka wafanye huduma ya ukombozi na kufunguliwa. Jumbe za vita vya kiroho zikawa dhahiri zaidi kwa jinsi walivyoanza huduma kwa kukemea mapepo kwa Wakristo wengi waliowaendea wakiwa na hitaji kubwa la msaada. Tangu siku za awali hadi sasa, kazi za huduma na usambazaji wa vifaa vya mafundisho na machapisho ya injili dunia nzima ni bure  na ukubwa wa ACMTC unatisha.
Sasa hivi wana wasambazaji na maaskari wa mstari wa mbele na maktaba kila mahali hata  sehemu za vichochoroni duniani. Kanda za video zinaonyeshwa vijijini, mitaani, kwenye mabasi, popote na kwa namna yeyeote ujumbe unavyoweza kufika.  Kadhalika Mungu amezibariki jumbe za Aggressive kwa njia ya redio.
HATUWASHAURI WATU WA MUNGU KUFIA KWENYE KANISA LILILODUMAA, bali kusonga mbele na kumpiga vita adui ili kuwaokoa wanaopotea na kwenda jehenamu. ACMTC  ni watu wanaomwamini Mungu na kuzitii amri zake.  HADITHI YA ACMTC NI RAHISI: MWAMINI MUNGU, TAFUTA HEKIMA YAKE, TII AMRI ZAKE, NA UMWONE AKIFANYA.   Mungu anawainua watu wa Rohoni ambao watamtii na kuona ni kwa jinsi gani alivyo mkuu, jinsi asivyo na mipaka, jinsi awezavyo: Mungu wetu.
JINSI ACMTC ILIVYOINGIA TANZANIA
Hatimaye machapisho ya ACMTC yalifika hadi Tanzania. Ilikuwa ni kama, Wagalatia 4:4 inavyoeleza: "hata ilipowadia utimilifu wa wakati".    "ROHO YA AGGRESSIVE YA KIKRISTO" itafanya hivi – "watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako" (Matendo ya Mitume 17:6).
Mwanzoni mwa mwaka 1994, Maj. Frank na Elina Materu waliyasoma machapisho ya ACMTC na kuonyesha HAMU NA NIA YA DHATI YA KUTAMANI MASUALA YA KIROHO. Walianza kupokea machapisho ya ACMTC, VHS Videos, DVDs, CDS, na Cassettes na KUPATA SHAUKU ya kujiunga na ACMTC.
NENO LA MUNGU LA UNABII KWAO LILIWAAMBIA HIVI:  "Je, si Mini Bwana Mungu wako nionaye hamu ya moyo wako?, na je, sitakukirimia kwa jinsi unavyohitaji?, Ili uweze kunitumaini, na kuniamini kwa maana ninaweza. Endelea kuwa na kiu ya maji yangu yaliyo hai nami nitakunywesha, endelea kutamani mkate wangu wa uzima nami nitakulisha. Usifie katika dini, bali endelea kufuata kunijua Mimi".
KUJIUNGA NA ACMTC- TANZANIA ILI KUWAFIKIA WATU WENGINE
Mungu anawaita wanaume na wanawake kujiunga na JESHI LAKE LA KIROHO, pamoja na Mwanaye kama Amiri-Jeshi Mkuu. Hili jeshi la wapiganaji wa AGGRESSIVE -  haliui wala kumharibu mtu yeyote, bali badala yake linaleta furaha, utimilifu, huduma za ujenzi, na uzima wa milele kwa askari  mwaminifu na wa hiari. Kujiunga huja kwanza!  Kwa sababu adui, Shetani, mara zote anamtafuta mtu ili ammeze na kumharibu, kujiunga kunahitajika haraka!
VIGEZO NA MASHARTI ya kujiunga inatakiwa kuwa mhusika ni lazima AMWAMIMI Amiri-Jeshi wake Mkuu, YESU KRISTO, Mwana wa Mungu, na ni lazima amtumaini kikamilifu (Yohana Mtakatifu 5:24, 6:29, 8:24). Ni lazima atoe tamko na KUMKIRI Yesu kwa kinywa chake ( Waruni 10:9,10). Ni lazima amjeukie Mungu katika TOBA (Matendo ya Mitume 2:38, Marko 16:16, Wagalatia 3:26,27). Askari wa Kristo wana adui mwovu anayetisha – Shetani. Kwa hiyo wanaume na wanawake wa na Mtume Paulo katika Waefeso 6:10-17. Jiunge na huduma maalumu kutoka kwa Mungu.
KUANZISHA TAWI LA ACMTC MAHALI ULIPO
Je, unapenda KUANZISHA KIKOSI CHA ASKARI WAPIGANAJI kwenye vita? Uwe AGGRESSIVE! Jiunge nasi katika vita kwa ajili ya nafsi za watu kwa kuunda kikosi cha kusambaza Neno  la Mungu. Idadi haijalishi. Makao Makuu watakusambazia vifaa vinavyohitajika – vipeperushi, CDs, DVDs, nk.- kwa maelekezo kwako na kwa kusambaza kwa wingi. Kinachohitajika ni MOYO UNAOCHEMKA kwa ajili ya Yesu, shauku ya moto kwa ajili ya kweli, na HAMU ya kuona nafsi zikikombolewa. CHUKIA KURIDHIKA! Anzisha vikosi kwa ajili ya Jeshi la Mungu, na eneza Neno leo!
KANISA LA KWANZA
Kila mtu anasema, "kanisa la kwanza, kanisa la kwanza, kanisa la kwanza" Kila mtu anasema, "na turejee katila kitabu cha Matendo ya Mitume" lakini hakuna hata mmoja atakaye yatoa maisha yake. Wale waliotembea na Kristo mwanzoni waliyatoa maisha yao. Ni kwamba hawakulinda haki zao katika maisha, hawakutafuta kuishi katika starehe na anasa  na wala kukubaliwa na watu. Mioyo yao ilijikita kwenye kusudi moja ambalo liliwasukuma hadi kifo.
TATIZO LA KANISA LA SASA
Tatizo ni hili; na mara zote limekuwa hili: mtu hamruhusu Mungu amtawale kikamilifu. Lakini Mungu ampatapo mwanaume, wakati ampatapo mwanamke ambaye atajinyenyekeza mwenyewe na kumruhusu Yeye ayatawale maisha yake kikamilifu, Mungu hatakuwa na mipaka katika  kutembea, kwa maana anapenda kutembea, na anapenda kuonyesha utukufu wake, na anapenda kuionyesha nguvu yake.
JIBU LA KANISA LA SASA
Hakuna mtu awaye yote ajuaye jibu la kanisa kwa sababu jibu haliko kwa wanadamu. Jibu linapatikana kwa kumtumikia Mungu. Ni katika Bwana watu watahifadhiwa katika saa ya uovu, hiyo ni kwamba wakaweze kuongozwa katika nuru Yake, kuelekezwa na kuomgozwa naye. WATU WOTE KILA MAHALI WANAOLITAJA JINA LAKE, WANAHITAJI TOBA KWA MUNGU.
SIKIA NENO LA BWANA: NINYI NI WATU WANGU AGGRESSIVE
"Msiogope kwa ajili ya jina aggressive. Msiwe na hofu wala msiliogope. Kwa maana ninyi ni silaha yangu ya vita. Na ninyi ni watu wangu shupavu. Na hilo ndio jina langu ambalo mara zote limekuwa hivyo. Na nimewaiteni ninyi katika vita vya kudumu na vita havitasimama. Kwa hiyo wala msirudi nyuma katika hilo, wala kuliogopa lile jina ambalo nimewapeni ninyi - AGGRESSIVE"
 
Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam. Simu 0715 350 752, 0754 350 752. Barua pepe: materufrank@yahoo.com

0 comments:

Post a Comment