Monday, 16 January 2017

Re: [wanabidii] MABADILIKO HAYAEPUKIKI: Nakubaliana na Lowasa kwa asilimia zote:

Pole sana.
Huenda ni kwa sababu siyo uliyotaka.
Mabadiliko haya yanatokea katika mawazo ya watu. Walitegemea kupewa sasa wanalazimika kutafuta.
Wakishaona kutafuta ndio msingi wa maisha wataanza kutafuta viongozi watakaotetea misingi ya uchumi na maisha yao badala ya kushabikia wachaguliwa.
Mwisho watadai katiba. katiba itakayokuwa inatetea maslahi yao sio ya vyama vya siasa.
Hapo wachaguliwa watalazimika kuwajibika kwa wachauaji badala ya kuwajibika kwa rushwa waliyoitoa. Mfano: kama mbunge hatatetea maslahi ya wakulima waliomchagua wataweza kumtimua. Katiba itakayodaiwa kwa msingi huo ni ya swatu kuliko inayopigiwa chapuo na vyama vya siasa.
Ndiyo mabadiliko ninayoyaona
--------------------------------------------
On Mon, 1/16/17, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] MABADILIKO HAYAEPUKIKI: Nakubaliana na Lowasa kwa asilimia zote:
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, January 16, 2017, 3:06 AM

Sijaelewa
mabadiliko unayoyazungumzia.em
2017-01-15 12:09 GMT-05:00
'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Zaidi ya
mara nyingi vyombo vya habari vimemkariri mwanasiasa mwenye
historia ya kipekee hapa Tanzania, Ndugu Edward Lowasa kuwa
'Mabadiliko Tanzania hayaepukiki'.

Ninaanza kumuelewa Lowasa na maana yake anaposema na
kulirudia neno hili. Ameona bila shaka kuwa wapo mahafidhina
ndani ya jamii yetu ambao wanashindwa kwenda na mabadiliko.
Yeye kama mwanasiasa mwenye ushawishi hana budi kuwaandaa
wale mahafidhina kuhakikisha hawabaki nyuma ya mabadiliko
ambayo hayana budi kutokea.

Mabadiliko yenyewe anayoyapigia chapuo Lowasa, yameanza
kitambo na zaidi kipindi cha uchaguzi. (Na kama siyo
anayoyaongelea basi ana matatizo makubwa). Kuna watu
walikuwa wanaamini kuwa lazima rais wa Tanzania atoke CCM.
Tena kuna walioamini kuwa Rais wa Tanzania lazima atokane na
Mtandao. Siasa zilizotangulia uchaguzi zilibadilisha hilo.
Watu walichoshwa na ufisadi, rushwa, ukosefu wa uwajibikaji,
na kadhalika. Kelele zilizopigwa zilionyesha kuwa kwa sasa
sio lazima Rais atoke CCM au mtandaoni. Tayari watu
walishaonja machungu. Walitaka mtu atakayeyashughulikia hayo
yanayowaudhi au kuwasumbua. Wakaangalia sera za chama na
watu wanaozitangaza sera hizo.



Baada ya uteuzi wa wagombea urais kuna watu (wahafidhina)
walitaka kuchanganyikiwa. Hawakuamini kuwa nchi inaweza
kupata rais kutoka nje ya CCM na nje ya mtandao. Kumbe CCM
yenyewe ilikuwaa imeliona mapema kuwa si kila atakayeteuliwa
na CCM lazima achagulike. Ikahakikisha inamteua mtu ambaye
hatapita kwa sababu katoka CCM, bali kwa sifa zake za
kiutendaji. Kumbe walisoma alama za nyakati na wakapatia.

Wakati wa siasa ya ujamaa na kujitegemea; ujamaa ulikazaniwa
na kujitegemea kukasahaulika na kwa kweli kukafutika.
Kujitegemea kulifutika miongoni mwa jamii na viongozi wao
pia. Watu na viongozi wakazoea misaada. Kila kitu watu
wakategemea serikali ifanye. Serikali ikatarajia kila kitu
kutegemea wafadhili. Nakumbuka kumsikia jamaa yangu mmoja
akilalamikia bei ya madawa. Anasema kupiga picha (X-Rays)
shilingi 30,000/= hospitalini ni nyingi. Nikamuuliza mboja
juzi ulibadilisha injini ya gari lako kwa hela nyingi na
sasa unalalamikia bei ya kurekebisha afya yako mwenyewe?



Watu wakazoea. Ukame kidogo ukitokea wanasubiri chakula cha
serikali. Huo ni ukame wa msimu mmoja. Kwa watendaji wa
serikali hiyo ikawa neema maana sehemu kubwa watachukua.
Watu wakilima mazao wanasubiri serikali iwatafutie, masoko
na kwa kweli wako tayari kulaumu kwa nini serikali
haijawaletea bei nzuri. Kukuta mtu amelima ekari kumi za
mahindi na kuvuna gunia hamsini na anachekelea likawa ni
jambo la kawaida. Hana haja ya kuhakikisha anapata mazao
mengi katika eneo dogo. Serikali ipo. Nakumbuka wakati wa
awamu ya kwanza uliwahi kutokea ukame. Watu wakalazimika
kusaidiwa chakula. Ukiondoa wazee wasio na waangalizi, watu
walipewa mbegu ya mihogo na mazao mengine yanayostahimili
ukame kama msaada. Ilipolazimika kuwapa chakula utaratibu
ulikuwa "Food for Work". Unafanya kazi ya kulima shamba
lako mwenyewe na kupewa chakula.

Tunamkumbuka aliyeilalamikia serikali kwa sababu ngombe wake
wamekufa kwa maelfu. Hakuchukua hatua alipoona ng'ombe
wanakonda, wanashindwa kutembea mpaka kufikia hatua ya kufa
mmoja, mamia mpaka maelfu anasubiri tu kwa sababu anajua
kuna msemaji wa upinzani ataitukana serikali apige makofi
basi. Katika mabadiliko yasiyoepikika ikitokea atauza mifugo
mingine ili kupata mal;isho ya michache inayosalia.

Watu wakasahau na sababu ya uchaguzi. Wakawa na tabia ya
kuchagua mtu kwa sababu anatoka chama fulani bila kupima
uwezo mgombea huyo; uelewa wake katika matatizo
yanayowakabili au hata tabia yake katika maswala
anayoyazungumzia katika jukwaa la siasa. Mtu anatoka Dar Es
Salaam na kuja kuwanunulia pombe kesho wanampa ubunge.
Hawajiulizi atawasaidiaje kwenye bei ya kahawa au pamba yao
au mifugo. Havijui na hawajui kuwa wanayemchagua lazima awe
anavijua na awe mshirika kwa maana mkulima wa zao
wanalolitegemea.



Mabadiliko yakaanza. Baadhi ya walioamini rais lazima
atokane na mtandao kwa kuona CCM imemteua mtu asiye na
mtandao wakahama ili kuhakikisha mtandao unajitokeza na
kutoa rais. Nakumbuka kusoma mahala mtanzania mmoja akisema
Sangara hawezi kuishi akishatoka majini na kuonja hewa.
Mwisho wa uchaguzi taifa lilimpata rais ambaye hakuwa
mwanantandao na hata kama alitoka CCM lakini hakuchaguliwa
na watanzania kwa sababu hiyo bali kwa jinsi walivyompima
yeye binafsi. Mabadiliko ya kwanza.



Rais akaingia madarakani. Akaanza kutumbua. Wauza unga
(madawa ya kulevya) waliokuwa wanafanya kwa uhuru sasa
wanajificha. Wamo lupango na wengine wamekimbia. Watu
waliozoea kutegemea rushwa sasa wana tahadhali kubwa. Bado
wapo na wanaiomba. Lakini si kwa uhuru. Waliozoea kuweka cha
juu na kufanya kwa uzembe wakashughulikiwa. Lakini angalau
serikalini kuna nidhamu hata kama ni ya woga, huo woga
utaisha nidhamu itakuwa tabia. Mabadiliko hayo.



Mabadiliko mengine ndiyo haya tunayoanza kuyashuhudia.

Rais alipotangaza kuwa Mkoa utakaokumbwa na njaa mkuu wa
mkoa huo hana kazi watu walishangilia. Hawakujua kuwa maana
yake ni wao watakaowajibika kuhakikisha mkoa hauna njaa, na
si mkuu wa mkoa.



Watu wachache walimuelewa rais aliposema Misaada iliyotolewa
kufuatiwa tetemeko la Kagera itatumika kutengeneza miundo
mbinu kama shule na vituo vya afya. Kuna waliojipanga
kuifaidi wakati wa usambazaji hata kama hawakuathirika. Sasa
wengi wameishajiweka sawa na wamejenga nyumba wanazoweza.
Kumbe inawezekana?! Shule ambazo wananchi lazima
watazifaidi; zimejengwa. Najua kuna wajinga wachache bado
hawajaona na wanaweza kutarajia iwe hoja katika chaguzi
zijazo

Watu wachache wanamuelewa rais anaposema limeni muuze kwa
uhuru bila vikwazo. Mabadiliko hayo.



Si mbali sana watanzania wataanza kuwahoji wabunge na
madiwani kuhusiana na barabara ili mazao yao yapite salama.
Si mbali sana mkulima atagoma kuuza mpunga kwa sababu
anaweza kuuza mchele. Si mbali sana hatutaona mahindi
mijini. Utafika unga na mahindi yaliyokobolewa. Hapo hakuna
atakayekuwa anauliza viwanda maana vitakuwa vinaonekana. Na
huo ndio msingi wa viwanda vya kati na vikubwa. Waliochukua
mbegu za mawese yetu walianzia huko.

Fikra za watu sasa zitakuwa kujitegemea badala ya kutegemea
kupewa. Usishangae baada ya myaka kumi Magufuli; kama
alivyosema Obama; akajitokeza kuwashukuru watanzania kwa
kusimamia mabadiliko yao.

Ninaamini Lowasa anaposema mabadiliko anamaanisha hayo. Kama
hamaanishi hayo basi ajiandae kulalamika 2020.

Elisa Muhingo

0787 187 507



 --



 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



  



 Kujiondoa Tuma Email kwenda



 wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com  Utapata Email ya

 kudhibitisha ukishatuma



  



 Disclaimer:



 Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility

 for any legal consequences of his or her postings, and
hence

 statements and facts must be presented responsibly.
Your

 continued membership signifies that you agree to this

 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.



 ---



 You received this message because you are subscribed to
the

 Google Groups "Wanabidii" group.



 To unsubscribe from this group and stop receiving
emails

 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.



 For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma



Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment