Hivi wale waliosimamisha msafara wa Magufuli huko Magu na kumwambia wana njaa walikuwa wapinzani? Hivi rais akisema debe la mahindi liuzwe kwa ng'ommbe watatu je hiyo
si dalili kuwa kuna uhaba wa mahindi? Na kama kuna uaba wa mahindi hiyo inaashiria nini? Mpaka watu wafe kama ilivyotokea Ethiopia na Somalia ndio mkubaLI kuwa kuna njaa?
em
2017-01-17 12:50 GMT-05:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Nashangaa malumbano yanayoendelea kati ya viongozi waliochaguliwa na watanzania kuliongoza taifa kwa upande mmoja na waliokataliwa na watanzania na wapambe wao kwa upande mwingine; kuhusu kutokuwepo na kuwepo baa la njaa Tanzania.
Mtu anasimama mbele za watu na kusema atakwenda kuomba chakula cha kuwasaidia watanzania maana taifa linakabiliwa na njaa. Kiashilia ni kuwa mahindi yananunua bei kubwa! Kweli bei kubwa ni kiashilia cha njaa??? Kingine ni kwa sababu mahindi sehemu fulani yamekauka! Hii maana yake kuna njaa? Yaani mtu ataitisha mkutano wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao awaambie 'tunaomba chakula. Sababu mchele unanunua shilingi 2000/= kwa kilo. Uliwahi kufikia sh 2500/=.
Kwa nini tugawanyike kwa kitu kisichokuwepo badala ya kuungana kwa kitu kilichopo? Kama ndiyo siasa za multi-party-sm heri kurudi kule! Ala!?
Mgoja niwaunganishe wale wenye akili sawasawa.
1) Tanzania inanyemelewa na Ukame. Mvua zilizonyesha maeneo mengi zilikuwa chini ya kiwango kilichotarajiwa. Baadhi ya maeneo mazao hayakusitawi sawasawa na kuna uwezekanio mavuno yakapungua kwa asilimia 60-70.
2) Sababu kubwa inayosababisha hali hiyo ni ukataji holela wa misitu.
3) Matokeo ya hali hiyo ni upungufu mkubwa wa chakula mwaka wa mavuno ujao.
Mpaka hapo sioni mahala pa kubishana kwa sababu watu hawabishani kuwa leo ni jumatatu au jumanne. Jumatatu ni jumatatu kwa watu wote. Wanaweza kubishania cha kufanya siku hiyo.
Hatua za kuchukua:
Hapa ndipo pa kubishana na ndipo pa kuonyesha chama gani kina sera gani inayofaa au iliyo nafuu kwa watu.
Hatua za kuchukua za haraka (za muda mfupi) ni namna ya kuepusha balaa la njaa. Njia zilizopo ni nyingi. Hizi ni naadhi:
a) Matumizi mazuri ya chakula kilichopo kuanzia ngazi ya familia kwenda juu.
b) Kudhibiti kutoka chakula kwenda nje ya nchi.
c) Kutumia mvua kiasi zilizopo na zinazotarajiwa kulima chakula kinachokomaa haraka kama Mtama, Viazi na kadhalika.
d) Kulima mazao yanayostahimili mvua kidogo kama Mhogo, mtama nakadhalika.
Katika hayo manne bado tunahitaji kubishana kwa uangalifu la sivyo tukubaliane nayo na kuyasimamia. Kila anayejiona ni kiongozi ayapigie chapuo kuliko kuona fahari kutembeza bakuli kuomba chakula ili watu wakupende kwa sababu unadumaza akili zao za kufikiri kujitatulia matatizo yao.
Hatua za muda mrefu:
Ili kuepuka janga la ukame kazi kubwa ni kulinda mazingira yasiendelee kuharibika na kuyarejesha katika uoto yaliyoharribika. Hapa ndipo hasa panapohitaji mjadala mkali na kutofautiana kukubwa. Hapa ndipo mtu akitaka kuonyesha umahili wake wa uongozi anaweza (ili mradi histolia yake inaonekana kama anavyoseka).
Katika kulinda mazingira kunahitaji hatua kadhaa. Kuna watu wanakata miti na kuchoma mkaa kinyume na sheria zilizopo. Nakutana na watu maporini wanaonyesha kiatu au kanda mbili. Ukisimama ukamuuliza unauza viatu? Anasema hapana; nauza mkaa. Pitia pori la Burigi au kutoka Lusahunga kuja Biharamulo utaona ninachokisema. Kunyoosha kiatu ni 'lugha' wanayotumia kuwasiliana na wateja wa mkaa. Kwani watendaji wa maliasili wakipita wakaona hilo hawaelewei lugha hiyo? Wanachukua hatua gani? Ukipita usiku (tena wa saa mbili) utakutana na pikipiki zimebeba mkaa magunia yasiyopungua matano. Hukosi kukutanam na pikipiki 10 kati ya Kasindaga na Muleba. Hivi Mkuu wa Wilaya husika hajui/haoni hilo? Wilaya hazina maafisa maliasili na wakurugenzi watendaji? Hawaoni? Nani hajapita Nyakanazi kati ya viongozi wetu? Hata rais alikwenda Rwanda kwa barabara lazima alipita hapo. Fanicha zilizopo hapo hakuna mtu mwenye liseni ya kukata miti hiyo. Kamaa kuna anayebisha aniletee vielelezo. Kudhibiti ukataji holela wa miti yetu kwa ajili ya mkaa na mbao kunahitaji kuwakamata hao na kuwatendea kikatili. Kwa nini maafisa-Maliasili wasitembee usiku mmoja na polisi na hakimu. Wakimkamata mwenye pikipiki huyo amebeba mkaa wakamsomea shitaka hapohapo. Akikana anawekwa ndani na kuamua kesi yake kutajwa tena mwaka 2030. Akikubali kosa anafungwa myaka kumi na mitano na hakuna fine ila pikipiki na mkaa vinataifishewa. Mbao na samani vilivyotanda barabarani navyo hivyo. Ninaamini kesi tatu zinatosha kudhibiti hayo. Baada ya hukumu msafirisha mkaa na mwenye mbao anawapeleka alikovipata. Nao wanapata hukumu hizo hizo. Watu hao hawataonekana misituni tena badala yake watakuwa wanaikimbia miti kama wanaowakimbia tembo.
Serikali ikishaweka mazingira hayo inahitaji kufanya moja au mawili zaidi.
Kuna technology ya kutemgeneza mkaa bora kutokana na mitu ya kupandwa na takataka. Serikali iwekeze sana katika technology hizo kulinda mazingira. Serikali itengenezeshe majiko yanayookoa kuni na mkaa ili yapatikane kwa bei nafuu. Ni kutoa ruzuku katika technology hiyo. Serikali itoe ruzuku kwenye gas ili itumike mpaka vijijini ambako mkaa na kuni toka misitu vinaweza kuwa shida kuvidhibiti. Serikali itengeneze sera –rafiki kwa watu wanaopanda miti na kuilinda kwa muda wa kutosha. Haitoshi kupiga marufuku ukataji miti ambayo mtu aliipanda kwa kupenda. Watu wanaweza kuacha kupanda mingine.
Watu wanakata misitu ili kulima na kufuga. Mazao ya kupatikana katika ekari moja yanapatikana katika ekafri kumi. Nyama inayoweza kupatikana katika ng'ombe mmoja inapatikaana katika ng'ombe watatu. Makapi ya mazao kama ya maharagwe, Mpunga, Mahindi badala ya kulisha mifugo hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira, yanachomwa moto. Mfugaji ana ng'ombe elfu tano. Hana nyumba, watoto hawaendi shule, anapata wastani wa lita moja na nusu ya maziwakila ngombe wakati ng'ombe hao wanaharibu mzazingira. Robo ya ngombe hao wangeweza kutoa maziwa mengi zaidi na nyama nyingi zaidi na mazingira kubaki salama.
Niliwahi kumhoji bwanashamba mmoja kuwa kama aliingia kwenye kata wakati mkungu wa ndizi unapima kilo 20 badala ya 80 iweje myaka miwili akiwa kwenye kata hiyo bado mkungu wa ndizi una kilo 20 naye analipwa mshahara? Hapa panahitaji mipango mikali ya kuhakikisha eneo dogo linatupatia chakula cha kutosha na kuuza nje huku eneo kubwa linalosali linatunzwa kama misitu ya asili na kupanda miti. Mkulima wa punga mathalan anayelima zaidi ya ekari mbili, ahakikishe ana ekari moja au zaidi ya miti. Miti ni yake. Nakumbuka kumsikia Rais kagame akisema 'Eneo linaloweza kustawisha gunia 10 za mazao atavumilia likitoka 8. Chini ya hapo Mkulima mwenyewe ana la kujibu; Kiongozi wa eneo ana la kujibu; waziri wa kilimo ana la kujibu na Rais analo la kujibu. Ilikuwaje mkulima avune gunia 6 badala ya 10? Kumbe kama mipango ikiwekwa na kusimamiwa, hatuwezi kuogopa ukame wa mwakammoja. Wala hatuwezi kukosa chakula. Hatuwezi kukosa kuwalisha majirani zetu na mazingira yetu yatakuwa salama.
Sasa wanaotafuta cha kupinga wapinge katika hayo na yanayosaidia watu kwenda mbele. Sio kutegea matatizo ya wananchi na kutaka kuwaletea misaada ili waonekane wana maana. Watakuwa wa maana machoni pa wapumbavu ambao wanapungua kila siku. Tukifika hapo tutaanza kufaidi uwepo wa vyama vingi vya siasa.
Elisa Muhingo
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout .
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment