Ikiwezekama watoe kipaumbele kwa kutoa leseni za biashara za uzalishaji badala ya za uagizaji. kwa sasa kila mmoja biashara ni malori ya kubeba na kusambaza mitumba hadi chupi na magagulo, nguo kutoka Uarabuni, China badala ya kuzalisha hapa nchini kwa pamba ya kutoka usukumani na coastal villages zamani walilazimishwa kulima pamba. Kila anayepewa leseni aambiwe pia inadani ya ajira kwa wananchi. Kuleta magunia ya nguo, mitumba, mabasi ayabiria ni kujaza tu madalali mitaani badala ya wafanyakazi viwandani. Libaba kifua cha miraba minne kutembeza nguo, vipodozi kukaa barabarani na spare za magari, midoli, mazuria imetuchosha. Huyu msuli wote huo na kutembea kilometa 20 kwa siku, kuuza midoli used toka ulaya, beseni kajaza mabararani na jeki za magari-tunataka akae kiwandani au shamba la katani, la mazao lenye processing factories. TPSF wanaiona hii mbona hawachukui hatua? Ukitoka mwenge kituo cha ITV au mwenge Mataa kuelekea NACTE hebu angalia viwanda vya Wazawa humu nchini vinavyotiririsha maji machafu ktk mitaro wazi , mazingira machafu na hao wanaelewa madhara yake. Kwa nini sio mfano wakaunganisha maji yao machafu kwenye underground stormwater sewerage system?
Wasiilaumu serikali inapowapa wageni uwekezaji maana waliowengi wa wawekezaji wazawa au matajiri waenyekuwekeza nchini wanapenda easy come easy go (Soda za rangi unga kuagiza kutoka ulaya-Prof Muhongo) badala ya kununua maembe, mananasi yanaoza vijijini kufanya processing ya juice za matunda halisi hapa nchini.
Management ya Masoko TZ ina kamati na uongozi maalum. Wanaaweka kiasi cha % ya kodi wanayokusanya na kulipa kodi sereikalini. Lakini viongozi wanakuwa madarakani kujaza vitambi sio kufanya independend development ya soko. Huachia uchafu ukajazana. Unakuwa soko linavuja mvua ikinyesha, bati juu wazi, hakuna cold storage facilities sokoni na stores za kuhifadhi biashara. Hygiene sio priority sio Soko la Buguruni, Manzese, Mabibo, Makumbusho pamoja na maeneo yao makubwa au nafasi waliyonayo. Kituo cha bus cha Simu 2000 kimejenga Soko lakini Raia hawakai. Wapo wanauza chakula barabarani kwenye vumbi la mchanga na moshi wa risasi wa kutoka magari. Raia unawaona wanakula hapo mavumbini wanajilamba na wenye kuta za nyumba zao wamepata hela za kupangisha wachoma nyama na chips mavumbini. Uongozi wa Mtaa unapata pesa za kujilamba za kodi kimyaaa badala ya kutumia mgambo kuwazoa hao wafanyabiashara waingie kituo cha bus cha Ubungo Simu 2000-mawasiliano. Pia, Bwana Maendeleo na Ushirika hayupo kuwashauri jinsi gani Viongozi wa Soko wanaweza wakachukua mkopo Bank CRDB Mr Kimei ni mtu wa maendeleo mwelewa. Waweke mfuko wao bank utune waombe mkopo. Kisha kumuomba Kiongozi wa NHC the brightest guy ever in NHC Mr Mchechu kuwajengea soko la kisasa lenye good storage facilities including cold storage chambers, ghorofa hii ni ya restaurants, juu kabisa lodging kwa wafanyabiashara waletao mizigo kutoka mbali, section ya nyama, samaki, na vyakula vya mashamba mfano floor hii mihogo, viazi magimbi, floor nyingine vya bustani-nyanya, nyanya chungu, matango, kabishi etc. Floo nyingine nazi tupu na madafu, floor ingine ni nyama tupu-ng'ombe, mbuzi, vichochoroni-nguruwe. Architects wapo wanasomeshwa nchi hii UCLAS na wapo wa makampuni binafsi-Kitu gani kinashindikana kufanya organization ya masoko kuwa ya kisasa na yanatazamika. Watu hata watalii kwa mfano watafika Soko la Mwenge baada ya manunuzi ya vitu soko la utalii watafika mwenge sokoni kula ugali wa muhogo na sato; magimbi na mihongo ya kuchemsha na mchemsho wa kuku wa mnavu! Hatupo innovative kazi ni majungu, story za simba na yanga, michepuko dili ya ukimwi, bangi na viroba ndio dili.
Wafanya biashara matajiri hawayaoni haya au potentials hizi? Hata mmoja wao au kundi lao kununua kisiwa kama Kilwa, Baadhi ya vya Mafia kukarabati majengo ya karne ya 6-9 na kuboresha utalii, kutoa ajira na hjuko gas imepatikana, taa ziwake kila kona na milo ya samaki hotelini na kutoa ajira.anafungua kiwanda cha kuzalisha kuku wa mayai na kulisha kuku na mayai hotelini? Kuna visiwa havikai watu lakini ni potentia kwa kujenga Majumba ya utalii itakayoondoa vituo vya siri vya madawa ya kulevya, kusafirisha wahamiaji haramu na ukataji mikoko kisiri.
Wamelala wafanyabiashara bado hawajaukamata uchumi mkuu seriously. Wanasubiri vishuke kama mvua, lawama daily kwa serikali. Ninaomba Mungu asaidie serikali ikague viwanda, mashamba yote waliyopewa na hayafanyikazi-watozwe kodi kisha waporwe wapewe hata wawekezaji wageni wate ajira. Huyo mwekezaji mgeni kama hao wachina wanaopanga nyumba na kufungua kiwanda kisha kutupa kinyesi na uchafu nje hovyo. Akihojiwa anajifanya hajui Kiingereza na Kiswahili-Wapewe masaa 24 kuhama nchi na kufirisiwa vifaa vyao!! hii itawatisha wajao kama matapeli au wawekezaji makanjanja!!
Aibu kwa hao ambao wanaona shida za wananchi za maji, hospitali, vitanda na mabenchi shuleni. Lakini hawachangii mpaka Rais aonyeshe tatizo ndio wannunua vitanda na kupeleka. Lakini wanaona ktk TV, magazeti au waishipo hawajali. Hii ni mtoa kitu kwa kutaka kitu.
Wananchi pia tushughulikiwe kwani kila kona sekta zote wananchi tuna utata. Viongozi na watumishi ugani ndio kabisaaa!
Ikiwa tupo vijijini na hapo tunafyatua matofari tunachoma na kuuza, kuna mafundi ujenzi pia, kuna uongozi na watumishi wa ugani-inakuwaje shule haina choo au madarasa yameanguka kuta wanafunzi wanasoma nje chini ya miti na ofisi ya kijiji ni chini ya mti au imeporomoka (ona picha attached ni ofisi ya kijiji ya Mkulazi). hapo Bwana Afya, Bibi Maendeleo anakwenda. Huyo ni pumba-fukuza kazi. anashindwa community mobilization in cash and inkind? Hawajibiki pamoja na kufundishwa ethics za kazi yake. Akakae nyumbani!! Diwani na Mbunge walambe kibano nao hawahamasishi wananchi wao kufanya yanayoonekana-hata kukandisha kwa tope jengo la ofisi ya Kijiji? ambapo mtu unaweza ukapita kikazi kwa mwezi tu ukaweza kuhamasisha ujenzi wa choo cha shule au darasa. AIBU
On Fri, 4/12/15, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Tukumbushane: Magufuli Na Wafanyabiashara...
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, Wanazuoni@yahoogroups.com, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, 4 December, 2015, 8:20
"
Kama kuna mfanyabiashara humu aliyenichangia fedha kwenye
kampeni zangu anyoshe mkono!'- John Magufuli, Jana
Alhamisi.Ndugu
zangu,Jana kupitia runinga tumemwona
Rais John Magufuli aklizungumza na Wafanyabiashara. Ilikuwa
ni hotuba muhimu kwa Rais wa nchi kuonyesha maono yake
inapohusu mahusiano ya Serikali na Wafanyabiashara.Kuna wakati, kwenye kipindi cha
kampeni, niliandika yafuatayo kwenye Raia Mwema; "John
Magufuli anayekuja, atakuwa na nafasi ya kipekee inayofanana
na ya Mwalimu Nyerere kwa kuweka rekodi ya kuingia
madarakani kwa kufanya kampeni ambazo hazikuhusisha sana
matumizi makubwa ya fedha ambayo mara nyingi huambatana na
michango ya wafanyabiashara wakubwa. Hivyo, John Magufuli
hatakuwa na wadeni wake wa kuwalipa fadhila, isipokuwa,
kuwahakikishia wafanyabiashara hao, uwepo wa mazingira
mazuri ya kufanya biashara zao na walipe kodi ili zisaidie
maendeleo ya wananchi wengine walio wengi. Kuna haja ya
kutenganisha biashara na siasa, kuwa hata watendaji wakiwamo
mawaziri, mbali ya Magufuli kuwasainisha mikataba, lakini
umma ungetaka pia kwenye mikataba hiyo mawaziri na watendaji
wakuu wawe tayari kutenganisha uongozi wa kisiasa/utendaji
wa kiserikali na shughuli zao za kibiashara.Na kwa kweli hili za kampeni za
urais kuchangiwa na wafanyabiashara wakubwa lina mifano hai
ya athari hata kwa wenzetu walioendelea kidemokrasia mfano
wa Marekani.Kwenye kampeni za
kuwania Urais wa Marekani mwaka 1996, ambapo, mbali ya Bill
Clinton kupambana na George Bush ( Baba) alikuwepo mgombea
binafsi bilionea Ross Perrot aliyegharamia kampeni za urais
wake kwa fedha za mfukoni mwake. Wamarekani hawakuwa tayari
kutawaliwa na Rais bilionea Ross Perrot, na pamoja na
ushindi wa Bill Clinton, Wamarekani walitilia shaka pia
michango aliyopewa Bill Clinton na wafanyabiashara wakihofia
kuwa wafanyabiashara hao wangenufaika zaidi kwa misamaha ya
kodi. Katika hili, Bill Clinton mwenyewe, mwaka ule wa 1996,
alikiri udhaifu huo kwa kutamka;" Mistakes were made in raising money for my
re-election campaign, but contributors did not buy influence
with me and the system is not corrupt.." ( Mwandishi,
The Guardian, Juni 30, 1996)"- Maggid Mjengwa, Raia
Mwema.Na John Magufuli
amewaambia wafanyabiashara jana, kuwa fanyeni kazi yenu ya
biashara, lakini, ya Kaizari mwachieni Kaizari, akimaanisha
anachotaka walipe kodi.Maggid, http://mjengwablog.com
Iringa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment