Friday, 4 December 2015

Re: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] Magufuli Anapotumia ' Dawa Chungu' Kwa Maslahi Ya Nchi.. [1 Attachment]

Falsafa ya Machiaevelli etc inakusaidia uelewa na maono/mtazamo lakini kubadilika kimawazo, kitabia au kimatendo iwe positive na hiyo issue na ufanye itakiwayo kwa output iliyotukuka-ni kitu kingine kabisa kwa sababu utakuwa unaangalia vigezo vingi vya mafao positive na negative vyako binafsi yale binadamu unayoyategemea ili ufanye kulingana na msimamo wako uliotokana na vigezo vyako. Change in behaviour/practice inakuwa ngumu kutokana na mitazamo na vigezo hivyo vya binadamu hata kama anaiona hatari wazi na bado mwingine habadiliki.

Kuna usemi wa Kiswahili usemao-"Mbio za Sakafuni huishia ukingoni!!" Hii ni kama hakuna cha kushika au kuegemea ujizuie usianguke.
Ina maana kwa usemi mwingine wa ufahamu wangu mdogo kuwa-unawahitaji viongozi walio chini yako na wananchi kwa ujumla wakusaidie wawe nguzo kwako usianguke. Kila mmoja atoe mchango wake afanye au kutimiza wajibu wake kikamilifu.

Ujuavyo-hakuna mabadiliko ya kweli kama sisi wananchi tunaoongozwa kukubadi kubadilika kila kona na kila mahala tulipo. Sio PMO na Rais pekee au mawaziri wachache, RC, DC kuwa wakali na kukagua kila kona. Ni sisi wote kujituma, kuchapakazi tukizingatia maadili na kutekeleza sera na sheria husika.

Huyo Mwanafalsafa Niccole Machiaevelli anayetaka watu kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia madarakani na hata wenye kumzunguka.Kwa
asiwajeruhi waliomsaidia kuupata utawala kwa Mwafrika na hasa Mtanzania-kuwa kigeugeu au nduma kuwili ni donda la kuzaliwa na ni donda ndugu. Anakusaidia akiwa na kakitu rohoni, akiona anaweza kukakosa-anaanza kuwa kinyonga kukufanyizia, kusema hili na lile. Huwa hatupendi kuambiwa ukweli na kujituma kwa maendeleo yetu ni Culture ya wachache. Na ndio maana mnaweza kukaa kikao Kichama au kiofisi ukayakuta ya Siri mliyoyaongelea yapo nje yameshavuja. Mara unaona gazetini kiongozi mmoja wa chama kingine anasema-ana taarifa za siri za suala hili au lile. Ana nakala kutoka confidential file! Kapataje? Kamata huyo akuambie kapataje taarifa kutoka kikao cha siri na confidential file funga wote. Na huyo aliyekuchagua akianza kukugeuka kwa vile alitegemea ataiba, kufisadi umuachie-geuza kibao-Hapa kazi tu. Urafiki wa ubadhilifu Mungu hapendi.

Kuwashughulikia sio wana siasa tu Viongozi wa juu mafisadi- hata wananchi wawekezaji wazawa na hao wa Tanzania Private Sector Foundation, wa migodini wachimbaji wadogo wadogo, wavuvi, wafugaji, wakulima, wapiga debe kwenye daladala, madalali wa tiketi za basi, madalali wa viwanja na nyumba etc. Sote tunastahili. Kila mmoja kwa wakati wake. Upo ushahidi mwingi wa wananchi kupewa maekari ya yaliyokuwa mashamba ya Katani na mengine ya mamlaka mbali mbali ili walime. Waliomba, kijiji kikapewa, wakagawiwa. Wameuza maeneo au badala ya kulima wamejenga nyumba za kupanga. bar, lodges. Kinachoendelea Jangwani ukianzia kinondoni Hananasifu/Mkwajuni kushoto na mpaka jangwani Mto msimbazi ni kujaza mchanga kwenye Wetland ambayo inatakiwa iwe protected na kma ni ujenzi sio kujaza udongo na kufukia taka ngumu. Ni kujenga barabara za juu na nyumba za kisasa zitakazoruwa juu maji chini yapite na yasiwe machafu kama sana. Angalia wananchi wafanyavyo na mazingira yalivyo mabaya hapo utasema wanaonewa lakini ukubali kuwa adui sio wa viongozi wabadilifu pia wananchi wa kima cha chini wenye SIKIO LA KUFA, wasioambilika na kujifunza kutoka mifano yao wenyewe wanavyoteseka na mafuriko yanapotokea kila mwaka. Umerasimisha makazi yao, wameuza, wamehamia hapo bondeni budi utafute tingatika, toa notice, bomoa na hakikisha JWTZ na JKT wanalinda mji waondoke kulinda afya zao na usafi wa mazingira ya miji na vijiji. Mkamate sio tu Afisa Ardhi aliyokagua wa kwanza na kuthibitisha ujenzi wa hiyo Hoteli/Ghorofa ndani ya Mto Msimbazi Jangwani kwa kufukia udogo ndani ya mto na kuithibitisha design hiyo. Utamuonea Waziri ukimfukuza kazi yeye kwani amepewa taarifa ya uongo na waliochini yake. Waziri hawezi kukagua kila file-anategemea walio chini yake. Yatakushinda ukiwafukuza wao tu.

TPSF wanapolalamika kuhusu wageni kushika uchumi wakati wenyewe hawawekezi, hawajiungi kuwa na a multinational corporation wakawekeza ktk utalii, madini, kufufua viwanda na wanajua serikali ilitakiwa na IMF na World Bank kuwa na PPP na kupunguza ukubwa na gharama za public sector? tatizo la kuacha kuwekeza serikali itaruhusu tu wawekezaji wageni ambao sisi wazawa tunaingia nao ubia na kuiibia serikali yetu. Au tukiwekeza-tunalipa wananchi mishahara midogo kuliko ya serikali. Hapa lazima ukague mpaka mishahara na mafao ya wafanyakazi ktk private sector na kama wanaofanyakazi hatarishi wana protective gear. Viwanda vyao kuchafua mazingira na kusababisha kwa mfano watu kuvunja miundo mbinu na kuwapelekea wao waya, nondo na mifuniko ya chuma wao wanazalisha raw materials za vyuma!??? Mbongo huyo. Si kazi ndogo kama hao wawekezaji wazawa nao wanasababisha uharibifu wa miundo mbinu, amli asili kusafirisha au kununua magogo yanayopatikana isivyoruhusiwa na wapo wanyonyaji kwa wananchi wenzao kama alivyokuwa mkoloni. Au wapo kufanya biashara rahisi rahisi za kuagiza rahisi na kuuza ghali-mitumba, soda za rangi, juice sio kuushika uchumi katika heavy industrial sectors na kufufua kiuhakika viwanda vilivyokuwa vya serikali; kushjika sekta ya utalii na kufufua/kujenga na majengo ya kihistoria yaliyoanguka na makaburi yanayoporomoka watu wanachukuwa mawe yake wanajengea baraza zao. Sote tubadilike tuipende nchi yetu na kuwa wakweli ktk sekta tulipo sio kulalama tu.

Wakandarasi za kuuza dawa, kununua mazao ambao ni wazawa wanauza dawa na mbegu zilizokwisha muda wakulima wanaathirika, Maduka ya ushirika yamekufa wao wanapata nafasi ya kuiba. Nilifanikiwa kufanya assessment ya Coffee Mbozoi miaka ya nyuma. Serikali ilitaka kufahamu kuna nini Kahawa TZ ya kutoka Mbozi inakataliwa na kurudishwa kimataifa. Nini kinaendelea? tukakuta hao wa private sector wanunuzi waliopewa mkataba na GVT wanawafundisha jinsi ya kuchanganya Kahawa nzuri na mbovu (fifi) na madawa yaliyokwisha muda na madeni wanayowaingiza wananchi kikanjanja. Wananchi nao wakishangaa kusema-mbona hawa wa makampuni wanatufundisha kinyumea na tulivyofundishwa na ushirika na serikali zamani? Kuna nini? Tumeikosea nini serikali yanatufika haya? Wanatuambia bei itakuwa 2000/= kwa kilo na anakukopa gari kwa vile kilo zako utaweza kulipa na ukabaki na pesa za matumizi gari pickup ya kukusaidia kubeba mazao shamba. Ukishakuvuna kahawa anasema bei imeshuka ni 1000/= kwa kilo. Anabaki kuwa mdeni na gari kutengenezwa anashindwa. Kahawa nayo inarudi mbichi na fisi zimekaangwa kuchanganywa. Ilitutia simamzi. Hiyo ndio private sector. Bei wanayopewa sio ile waliyoambiwa na serikali. Kwenye Korosho Mkuranga tulikuta hivyo pia. Kama kilo wapewe 1500 wao wanawapa shs 800. Turudishe Maduka ya Ushirika, kusimamia SACCOS vizuri na decentralization ifanyekazi sawasawa kote sekta zote wote tuwajibike. Extension staff na watumishi wa umma wapewe mkataba na uongezwe kwa ouput ya kazi yake. Ama sivyo-PMO na Rais mbio zao zitakuja kusimama. Budi kumshughulikia kila mmoja, pia kutoa elimu kuanzia mashuleni ili kutenga utaifa na utu zaidi. Kwani hata SACCOS utakuta viongozi wanajipa mikopo wao na wana madeni ya mamilioni.

Ni kawaida ya Mswahili kusema-haya ngoja tuwaone -watching it all! Kisha-Unawakamata-wao ndugu na marafiki wanahaha kuwawekea dhamana watoke, mawakili watawekwa kwa mihela mingi, muda na gharama za serikali unakuwa mkubwa. Tumwogope Mungu.Ndugu akubali asimuwekee Fisadi dhamana na lawyer? Anawekea mbakaji katoto dhamana itakuwa fisadi?

Tumbua jipu ila usaha usije ukakurukia ukakuchafua.
Tabia ya watu kuona kiongozi anakagua wakaiimbia kimbia akiondoka-wanaendelea kukaa na kusoma simu. Sawa na watoto au mtumishi wa nyumbani anaposikia unaingia wanakimbia kufunika chakula mezani. Lakini muda wote kilikuwa wazi inzi wakilamba. Kisha daily ni kulipia gharama za matibabu watoto wanaumwa na mwenyewe pia. Usaha umekurukia ukakuchafua. Unakamata na kufunga huyu na yule lakini bado wanaungana na kutenda kinyume kwa manufaa binafsi. Unakaa unaumia kichwa-Why hawabadiliki? Tuna matatizo ndani ya bongo na mioyo yetu hatuogopi Mungu. Angalia hiyo Map attached uone mashamba hayo ya katani walivyopewa wananchi wawekeze na panda Bus uende Ngerengere uone kama yanalimwa! Labda hilo la seriklai la LMU-Livestock Management Unit. Na hata hivyo-linavamiwa na wafugaji kutoka Mwanza, Monduli, Simanjiro-migratory pastoralists kulishia nyasi LMU inazopanda na mazingira yanayotunzwa. Pamoja na robo kijiji kuweka eneo la ufugaji-Mifugo daima ipo katikati ay kijiji mashambani ktk wetlands- Baweni na mashambani kulisha mazao mashamba na kesi za bakora watu kuchapwa ni kila siku. Rushwa nayo imekithiri katika kesi hizo-haziishi. Unakuta mpaka wenyeviti vijiji na kitongoji maeneo hayo ya Morogoro Rural Ngerengere Division wamechapwa bakora na wafugaji ktk kuamua kesi hizo. Na bado kuna ardhi inagombaniwa iliyorudishwa kwa Rais (wakati huo Kikwete) aamue. Na hilo shamba likigawiwa-watauza! Wakipewa wananchi na wawekezaji wa ndani ya Nchi-Ngoma droo-kutoitumia ardhi ilivyokusudiwa. Land use planning ya gharama, kutunga bylaws wenyewe zikapitishwa na halmashauri, mabaraza ya utatuzi migogoro na Baraza la Ardhi Wilaya na la Sheria la Kata yapo lakini-Uswahili na migogoro isiyokwisha na kupoteza muda na resources za serikali. Tusimamie ufufuaji viwanda lakini pia kusimamia kuwa-Wananchi hawauzi ardhi yao kiholela kwa manufaa ya muda mfupi. Uhuru wa kuhamahama, kuhamia popote utakapo ufanye lolote utakalo ndio unatufanya pia tuwe wazembe na waharibifu. Hapa kazi tu!! Kubali lawama lakini uhuru huo ukomeshwe. Ile ya kuogopa wapiga Kura kisiasa iishe ili kimazingira na kiuchumi tuendelee na tutaboresha afya pia.

Ni sawa na hizi mbio za usafi kwa sasa kuondoa taka ndani ya mitaro na kufagia barabara. Lakini mama ntilie bado anashuka bondeni anachota maji hayo yanayotiririka kutoka mitaro anakoshea vyombo anavyoweka chakula akalisha watu. Watu wanakufa kwa cholera, typhoid, kuhara damu tunazika, tunaona, tunashuhudia lakini bado tunaendelea na uchafu huo. Badho vyakula vipo wazi barabarani; wamepanga biashara ktk baraza ya kituo cha basi ambapo wananchi wanatakiwa kukaa wao wakali wanauza ubwabwa haop. Wamepanga mbao mpaka kwaenye mapito ya watu kwa miguu kuna magari yamepanga kupakia mbao au kusubiri wateja. Yote yapo wazi hatujirekebishi. Viti vya wanywaji bear na magari yao kwenye feeder roads za wapita kwa miguu tena kwenye main road? rais pekee na PMO ataweza kama hatutakubali kubadilisha bongo za vichwa vyetu. Viongozi wa Mitaa, ubalozi na kamati husika zipo-Rais ndio aje kurekebisha haya. Fanya biashara pale panaporuhusiwa na kwa usafi unaotakiwa lakini tatizo ni Sisi na Kuzingatia na kutekeleza sheria na kuzingatia maadili. Bila ya wote kubadilika tata.

Hata wanahabari nao wabadilike. wawe wanahoji vitu kwa kumtia akili wanaomuhoji. Sio kila wakati-Unaiambia nini serikali na tatizo hili wakati aliyejenga bondeni, aliyeunganisha choo mferejini, anayetupataka, anayetoa dhamana kwa kibaka ni huyo huyo mwananchi? Mwanahabari amuhoji TPSF-kwa nini hamuwekezi hapa na pale. Aende kwenye viwanda na mashamba waliyochukua yasiyolimwa. Mikopo waliyopewa baada ya kupewa hatimiliki wamefanyia mambo mengine ya kibiashara na mijengo ya majumba ya fahari.Maeneo hayo ya viwanda yamekuwa karakana ya kuuza magari, warehouses ni karakana za mitumba; nyingine ni hall za arusi. Walipe kodi iliyotakiwa kuanzia mwisho wa grace period ya ujenzi/ufufuaji viwanda. Watapata pressure na watu kufa hapa. Ukifika Morogoro unapoingia mjini Wetland wamepimiwa wenye uwezo na zoinafukiwa udongo wanaweka karakana. Watu wanajenga majumba ya fahari hadi juu milimali kusiko ruhusiwa. Viongozi wanaona. Eti leo hii ndio wanasimama kutoa matamko makali! Siku zote walikuwa wapi. Bwana ardhi awajibishwe kwa kutoa wetlands na milima mawe yavunjwe watu wajenge na pia kulima milimani bila ya makinga maji. Bwana mifugo awajibishwe na Diwani na MP wake kwa kuruhusu mifugo ihamie wetland areas na milimani na kuna maeneo waliyopangiwa sio huko na Village Land use Plans-hata kama si rasmi ila ni zile za mgawanyo kijijini ktk mpangilio wao informal ramani bado- zinaonyesha nani afanye nini mahala gani. Rushwa tupu unapokuta yanafanyika kinyume . Pita mtaa kila mtaa uonyeshe walivyoziba njia ukilinganisha na ramani, wazazi wanavyoweka video ndani ya majumba na kutoza hela vitoto na bar na watoto wamejaa wazazi hawajali na wanaojenga wetlands za bahari huko mbagala etc na kuwahoji-kwa nini unafanya hivi? Lakini angalia usalama wako-Watakugecha siku sio nyingi.

Wabongo tuna utata wa kutokupenda kuambiwa ukweli. Uwe mkweli na muwazi ndani ya familia-kiofisi na kwa jirani kisha kaa usikilize majungu utakayokuwa unasukiwa. Tumuombee Mungu Mh Mangufuli asije kugeukwa na waliochini na karibu yake!!




--------------------------------------------
On Sat, 5/12/15, 'bernard baha' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] Magufuli Anapotumia ' Dawa Chungu' Kwa Maslahi Ya Nchi.. [1 Attachment]
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 5 December, 2015, 1:35

Mwenyekiti Maggid, 
Huwa
twakuita hivyo huko Kijijini kwetu Mjengwa blog, mazingira
na mkitadha katika kumwongelea Machiaevelli sidhani kama
unahusika sana na mazingira tuliyokuwa nayo....nadhani
katika chambuzi zetu kwasasa yatupasa kuwa makini,binafsi
simsomi JPM kwa mwelekeo wa Prince aweza kuwa aelekea huko
ila nachelea kutaka kuwa mtabiri wa majanga. Isije kuwa
ajali za kisiasa tu zitakazo wakumba wachache, nipo nae
katika hatua azifanyazo ila sipo tayari wala hata kusema
mwelekeo ni huu ama ule. Mapinduzi ya Ufaransa yalikuwa na
mwelekeo sampuli hii sio? na kuna wengine wanasema Hitler na
Mussolini pia walifanya mambo ila baadae ikawa
majanga. 
Nadhani
atupe kwanza timu yake, kikosi cha kazi ndio tuanze kusema
is he a prince kwa mujibu wa Machiavelli ama? na je
tunahitaji aina ya Prince wa Machiavelli kweli? Sidhani
ulitaka kutuaminisha hapo nyuma kwa maana ya miaka 10
iliyopita tulikuwa na mtawala aliyekuwa mbali, huyu jamaa
tuliyemwamini kwa asilimia 80 na baadae tukazishusha akapata
bado 60+ alikuwa mbali kweli?.....falsafa za kale zatusaidia
kuyaona kwa urahisi haya mambo. Na je huyu anayaona sasa kwa
ukaribu? baada ya kuhakikisha kodi sawa sawia, je nitaona
sasa mashamba ya wawekezaji wasioendeleza yakipelekwa kwa
wanavijiji wanaoyazunguka?waliokuwa wakitumikishwa? etc
etc....haya wacha tuendelee shuhudia utumbuaji majipu, pia
baada ya kutumbua tusisahau yapaswa kuponywa yasijegeuka
vidonda na ama vidonda ndugu kisha kansa.
Wasalaam,Mwanakijiji
wako.
From:
"Maggid Mjengwa mjengwamaggid@gmail.com
[Wanazuoni]" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
To:
mabadilikotanzania
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>;
Wanazuoni@yahoogroups.com; wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
Sent:
Friday, December 4, 2015 9:13 PM
Subject:
[Wanazuoni] Magufuli Anapotumia ' Dawa Chungu' Kwa
Maslahi Ya Nchi.. [1 Attachment]


 









[Attachment(s)
from Maggid Mjengwa included below]



Ndugu
zanguKwenye
kitabu chake cha " The Prince", yaani, "Mwana
Mfalme", Mwanafalsafa Niccole Machiaevelli anamtaka
kiongozi kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia
madarakani na hata wenye kumzunguka.Kwa
mujibu wa Machiavelli, hutokea kwa Mwana Mfalme
"kuwajeruhi" waliomsaidia kuupata utawala. Hii ni
kwa kutowatimizia yote yale waliodhani kuwa ni haki yao
kutimiziwa.Badala
yake, Mwana Mfalme huwaingiza kundini wawe kama wengine.
Katika manung'uniko yao, Mwana Mfalme
hawezi kutumia dawa chungu dhidi yao kwa vile hujihisi ana
deni kwao. Lakini, cha msingi kwa Mwana
Mfamle ni kuzingatia ukweli, kuwa, hata kama
atakuwa na maadui
wachache, katika kuchukua
nchi, muhimu ni kuwaridhisha walio wengi, na
hapa ni wananchi.Huwezi kutawala kwa amani bila upendo na utashi wa
walio wengi. Ni kwa sababu hizi, Mfalme Louis XII wa
Ufaransa aliweza kwa kasi ya ajabu kuitwaa Milan na kwa kasi
ya ajabu kuipoteza Milan.Hakukidhi matakwa na matarajio ya
wananchi walio wengi waliomfungulia
milango.Mtawala aliye mbali na asiyejali maslahi ya watu wake
walio
wengi ni mtawala mwenye hofu. Na
mtawala mwenye hofu zaidi na watu
wake
kuliko adui wa nje, basi, hujijengea kasri ama ngome imara
ya
kujihifadhi ingawa hilo halitamsaidia
kuzuia nguvu za umma za
kumwondoa
madarakani. Kwa mtawala, kasri ama ngome iliyo imara ni
kuepuka kuchukiwa na wananchi, kuacha ubinafsi
na kujali maslahi ya
wengi.Tunaona,
katika kutanguliza maslahi ya wananchi walio wengi, John
Magufuli ameamua kutumia dawa chungu ya ' kutumbua
majipu' hata kwa wale waliodhani, kuwa hawangeguswa kwa
vile wamemsaidia katika kuingia madarakani. Maana, kuna
wanaodhani, kuwa kwa vile wamechangia kwenye hata kampeni za
kumwingiza Magufuli madarakani, basi, Magufuli hapaswi
kuhangaika na kuchunguza makandokando yao, kwamba
wanastahili kuwemo kwenye Serikali ya Magufuli.Na kwa
vile, Magufuli ana kila dalili za kufanya kinyume na
matarajio ya watu wa aina hiyo, basi, yumkini watu hao
watageuka kuwa maadui zake.
Na tusubiri
tuone.
Maggid,
Iringa.






__._,_.___

Attachment(s)
from Maggid Mjengwa | View
attachments on the web

1 of 1
Photo(s)





1.jpg










Posted by: Maggid Mjengwa
<mjengwamaggid@gmail.com>




Reply
via web post


Reply to sender


Reply to group

Start a New
Topic

Messages in this
topic
(1)






Check out the automatic photo album with
1 photo(s) from this topic.






















Visit Your Group


New Members
2






• Privacy • Unsubscribe • Terms of Use
























.







__,_._,___



#yiv1910494160 --
#yiv1910494160ygrp-mkp {
border:1px solid #d8d8d8;font-family:Arial;margin:10px
0;padding:0 10px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mkp hr {
border:1px solid #d8d8d8;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mkp #yiv1910494160hd {
color:#628c2a;font-size:85%;font-weight:700;line-height:122%;margin:10px
0;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mkp #yiv1910494160ads {
margin-bottom:10px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mkp .yiv1910494160ad {
padding:0 0;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mkp .yiv1910494160ad p {
margin:0;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mkp .yiv1910494160ad a {
color:#0000ff;text-decoration:none;}
#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-sponsor
#yiv1910494160ygrp-lc {
font-family:Arial;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-sponsor
#yiv1910494160ygrp-lc #yiv1910494160hd {
margin:10px
0px;font-weight:700;font-size:78%;line-height:122%;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-sponsor
#yiv1910494160ygrp-lc .yiv1910494160ad {
margin-bottom:10px;padding:0 0;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160actions {
font-family:Verdana;font-size:11px;padding:10px 0;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160activity {
background-color:#e0ecee;float:left;font-family:Verdana;font-size:10px;padding:10px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160activity span {
font-weight:700;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160activity span:first-child {
text-transform:uppercase;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160activity span a {
color:#5085b6;text-decoration:none;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160activity span span {
color:#ff7900;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160activity span
.yiv1910494160underline {
text-decoration:underline;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160attach {
clear:both;display:table;font-family:Arial;font-size:12px;padding:10px
0;width:400px;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160attach div a {
text-decoration:none;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160attach img {
border:none;padding-right:5px;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160attach label {
display:block;margin-bottom:5px;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160attach label a {
text-decoration:none;}

#yiv1910494160 blockquote {
margin:0 0 0 4px;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160bold {
font-family:Arial;font-size:13px;font-weight:700;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160bold a {
text-decoration:none;}

#yiv1910494160 dd.yiv1910494160last p a {
font-family:Verdana;font-weight:700;}

#yiv1910494160 dd.yiv1910494160last p span {
margin-right:10px;font-family:Verdana;font-weight:700;}

#yiv1910494160 dd.yiv1910494160last p
span.yiv1910494160yshortcuts {
margin-right:0;}

#yiv1910494160 div.yiv1910494160attach-table div div a {
text-decoration:none;}

#yiv1910494160 div.yiv1910494160attach-table {
width:400px;}

#yiv1910494160 div.yiv1910494160file-title a,
#yiv1910494160 div.yiv1910494160file-title a:active,
#yiv1910494160 div.yiv1910494160file-title a:hover,
#yiv1910494160 div.yiv1910494160file-title a:visited {
text-decoration:none;}

#yiv1910494160 div.yiv1910494160photo-title a,
#yiv1910494160 div.yiv1910494160photo-title a:active,
#yiv1910494160 div.yiv1910494160photo-title a:hover,
#yiv1910494160 div.yiv1910494160photo-title a:visited {
text-decoration:none;}

#yiv1910494160 div#yiv1910494160ygrp-mlmsg
#yiv1910494160ygrp-msg p a span.yiv1910494160yshortcuts {
font-family:Verdana;font-size:10px;font-weight:normal;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160green {
color:#628c2a;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160MsoNormal {
margin:0 0 0 0;}

#yiv1910494160 o {
font-size:0;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160photos div {
float:left;width:72px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160photos div div {
border:1px solid
#666666;height:62px;overflow:hidden;width:62px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160photos div label {
color:#666666;font-size:10px;overflow:hidden;text-align:center;white-space:nowrap;width:64px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160reco-category {
font-size:77%;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160reco-desc {
font-size:77%;}

#yiv1910494160 .yiv1910494160replbq {
margin:4px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-actbar div a:first-child
{
margin-right:2px;padding-right:5px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mlmsg {
font-size:13px;font-family:Arial, helvetica, clean,
sans-serif;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mlmsg table {
font-size:inherit;font:100%;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mlmsg select,
#yiv1910494160 input, #yiv1910494160 textarea {
font:99% Arial, Helvetica, clean, sans-serif;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mlmsg pre, #yiv1910494160
code {
font:115% monospace;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mlmsg * {
line-height:1.22em;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-mlmsg #yiv1910494160logo
{
padding-bottom:10px;}


#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-msg p a {
font-family:Verdana;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-msg
p#yiv1910494160attach-count span {
color:#1E66AE;font-weight:700;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-reco
#yiv1910494160reco-head {
color:#ff7900;font-weight:700;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-reco {
margin-bottom:20px;padding:0px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-sponsor #yiv1910494160ov
li a {
font-size:130%;text-decoration:none;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-sponsor #yiv1910494160ov
li {
font-size:77%;list-style-type:square;padding:6px 0;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-sponsor #yiv1910494160ov
ul {
margin:0;padding:0 0 0 8px;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-text {
font-family:Georgia;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-text p {
margin:0 0 1em 0;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-text tt {
font-size:120%;}

#yiv1910494160 #yiv1910494160ygrp-vital ul li:last-child {
border-right:none !important;}
#yiv1910494160





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment