Kwa nini kamati zisibaini hayo? Huenda walipewa kitu kidogo wakamezea. Kuna tabia kwamba ukiona tume imeundwa kuja kukagua au accountant wanatumwa kuja kufanya auditing kwenye mradi kama kunautata-wanapokewa vizuri na kupewa malazi mazuri na mafao hata kama walishalipwa posho. Mkaguliwa anaandaa mazuri na zawadi kiasi kwamba mnaona soni kumuandika vibaya na kumtolea taarifa ya mahesabu mbaya.Lakini, wapo wale ambao-watakula posho na hongo yako na wataandika taarifa ya ukweli bila ya woga. Hapo ndipo utakapozimia. Umepoteza hela na umeandikwa vibayaunavyostahili.
Kwani haya anayoyafanya Mh Mangufuli sasa nani hakuyaona huko nyuma. Kuna mawe au beacons za barabara, za mito na bahari. Hata kama beacons au mawe hakuna lakini Bwana Ardhi anafahamu sheria ya mita 60 za ufukwe na mita 30 hadi 60 za barabara (Right of way) inategemea na barabara kuu au ndogo. Wanajua pia sheria ya Mazingira ya 2004 na inavyozungumzia Wetlands-maeneo Oevu na semina wanakwenda kila mara na posho juu za semina kuongelea ulinzi wa mazingira, misitu ya hifadhi na mingineyo. Wanarudi na michele, mkaa, mahindi etc majumbani kwao wakienda semina. Lakini Bwana ardhi anapima viwanja vya nyumba kwenye ardhi oevu mfano Morogoro mjini ambako wananchi wamezoea kulima nyanya, kabichi, mchicha. Wanaacha mashamba makavu ya katani yasiyolimwa wanariuhusu wajenzi kufukia wetlands na kujenga magereji, majumba na magodown. Nani pamoja na Diwani na Mbunge haoni jinsi wetlands za Bagamoyo za mito iingiayo baharini maeneo ya Ukuni, Magambani, Bong'wa na unapoingia mjini yanavyopimwa viwanja maeneo ambayo wakazi wa huko karne hawakujenga nyumba bali wakilima mpunga. Vizee vinavyojitegemea vitapata mchele wapi. Hata Hoteli hiyo ya Kiromo imejengwa kwenye mapito ya Mto na ikafunguliwa na Mheshimiwa. Nani haoni???? River Basin Authorities (Ruvu, Rufiji, Rukwa etc) zipo lakini zilipo ofisi zao nje yake watu wanajenga katika wetlands! Ndenda Iringa Mjini-Rufiji River Basin ukaone ujenzi ktk wetlands wala sio mbali na basin offices. Watu wanapelekewa vinoti-muache ajenge au mtoe huyo hapo polisi kolokoloni! Uswahili wetu unatumaliza-udugu, kujuana, usiasa kuliko kuzingatia sheria. Hata Kamati za Bunge zinaingiza masuala haya.
Kwani nani haoni mjini DSM vituo vya basi kibaraza cha kukaa watu wakisubiri gari kuna watu wamepanga biashara au mama ntilie anapikia ugali anauza? Kwani hizi taka zinazotakiwa kuondolewa na usafi ufanyike tulikuwa hatuzioni? Mfumo wa kufagia, kukusanya na kuzoa taka kwa magari kupeleka dampo upo decentralized. Viongozi wa mitaa wanakusanya hela, wanajaza matumbo. Health officer anaona anayetiririsha maji machafu anapewa kijisenti anamuachia. NEMC, DAWASA waliona yote haya ya watu wa majumba makubwa na madogo waliounganisha vyoo na septic tanks zao kwenye open water drainage system. Viongozi wa mtaa wanakusanyakodi kutoka mauzo ya vyakula wazi barabarani na samaki mbichi zilizozungukwa na inzi. Tunaona muuza chips na kuku alivyowacha kabati la vyakula hivyo wazi na zimejaa inzi lakini tunakula. Ni sisi sote na akili zetu za ajabu ajabu. Nani haoni Kariakoo watu wanavyouza biashara barabarani kiasi kwamba gari kupita ni tatizo? Tatizo ni kuingiza SIASA katika Utendajikazi. Daima ni kuogopa kukosa KURA-Waache wapigakuwa Wetu!!
Kwani nani haoni kuwa mashamba waliyopewa kuwekeza wamegeuza magulio ya mitumba na chuma chakavu? Nani haoni kuwa Kiwanda kinachotumia Chuma Chakavu ndio kinasababisha watu wan'oe miundo mbinu ya mifuniko ya mitaro, vyuma vya madaraja na akaamua kukifunga kiende kununua au kuchimba chuma Mtwara? Vipofu?
Ukienda Kilosa Mjini maeneo ya Railway utaona magodown toka ukoloni na baada ya uhuru yanavyoporomoka. Halafu tuna Matajiri nchini ambao hulalamika uchumi kushikwa na wageni. Serikali ina wafungwa ambao zamani wakitumiwa na mafundi wa serikali kujenga na kukarabati nyumba za serikali za DC, RC, hospitali/zahanati, ofisi nyingine pia. Leo hii utafika katika makazi ya askari utaona kuta za nyumba zimepasuka, paa juu zimeshikiliwa na mawe ay tofari zilizowekwa juu. Nyumba zilizokuwa za Railway waliokuwa wafanyakazi wamekaa hapo miaka na kuamua kujenga ktk eneo hilo la serikali majumba binafsi ya kisasa. Viongozi wa Kata, Tarafa, Wilaya wanaona hawakemei. Nenda Nyumba za Police na za Railway Mikumi utaona haya. Hapa DSM unaona nyumba ya ghorofa ya NHC hapo Fire-Jangwani, Upanga mtu amegeuza design amejenga frame na vyumba vya biashara atakavyo? Hapa mjini kila mtu anaona. Uwanja umekuwa garage watoto wanakosa pa kucheza? Tanzania-Kichwa cha Mwenda wazimu. Bila ya shata nyumba za Taasisi nyingi waliokaa miaka ambazo zinatakiwa ukarabati zimeuzwa kwa wenye hela wamejenga magorofa. Hao wa jangwani wanaendelea kurudi na kujenga kama kawa. Unapoachia viende kombo nawe upo-sheria ya Kimataifa unatakiwa umlipe fidia kwani uliona, sheria ipo ulitakiwa umkemee umpe muda abomoe achukue chake. Wewe ukampa kibali kinyemela au rasmi, ukamuacha ajenge na awepo hapo karne-MLIPE!! Nawe U MKOSA!!
Hivyo hao wa Bandari etc walibebwa na hizo board na viongozi wake kwa kuangalia udugu na urafiki hawakuadhibiwa. Kwa somo kunaliwa na kwa mwali. Nao washughulikiwe. Watu wengi sasa watakufa njaa kwani milango ya rushwa inafungwa. Nasi watanzania tukubali kuwa usafi wa 9 Decemba ni wa kudumu. Tuanze kuondoa maunganisho ya vyoo kwenye mitaro wazi; kubomoa frame za biashara tulizojenga katika feeder roads na kuziba barabara na zilizochukua maeneo wazi. Tusingoje kuja kubomolewa halafu tuone tunaonewa. Maofisini unakuta mtu amemuweka Project Officer wa elimu ndogo ameacha wa elimu kubwa na ujuzi. Hawezi hata kuandika taarifa. Ukiomba aondolewe awekwe mwenye uwezo inashindikana na kazi za maana zinakuwa mbovu hata wakati mwingine donors wanatushangaa. Tumboni na Chupi street; udugu na ukabila, kujuanaism na usiasa vimetutawala ambavyo ni kansa katika utendaji na maendeleo ya nchi yetu.
--------------------------------------------
On Tue, 8/12/15, 'Paulo lunyalula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Kamati Za Bunge Nazo Zilishindwaje Kubaini Madudu Haya?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Tuesday, 8 December, 2015, 14:35
Maggid,sio kwamba
hawakubaini, ila walichukua chao ndio maana hawakuwa na hoja
za kuyaona madudu hayo.Paulo.
On Monday, December
7, 2015 9:52 PM, Maggid Mjengwa
<mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
Ndugu
zangu,Ninapozidi
kusikia uoza wa bandari na reli, na huko kwengine
najiuliza;
Hivi zile Kamati Za Bunge nazo zilikuwa zianafanya '
Ziara Hewa' kukagua utendaji wa mamlaka hizo. Kwamba
zilishindwaje kubaini madudu haya yanayobainishwa sasa? Nini
hasa kazi za Kamati za Bunge?
Maggid,
Iringa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment